Fahamu mashirika ya ujasusi yenye uwezo mkubwa duniani

Vincenzo Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2020
12,132
25,370
 Ujasusi ndio 'kiini tete' cha kila nchi na ujasusi wake wa nje na wa ndani unazingatia masilahi na usalama wa kitaifa.

Shirika la Kitaifa la Ujasusi ndilo ulinzi wa kwanza wa taifa, na ndilo shirika linalohusika na kupata taarifa za siri, na dhana za udukuzi zinazofanywa na nchi, lakini si nchi zote zinazoweza kuwa na nguvu sawa za kiuchumi na kijasusi.


1.Shirika la ujasusi la Marekani CIA
CIA ilianzishwa mwaka wa 1947. Ni bora kitaalam kuliko mashirika mengine mengi ya kimataifa na inajua mengi kuhusu matukio ya kimataifa.

CIA ina jukumu la kukusanya taarifa za kigeni, wakati mwingine Marekani. Idadi ya maafisa wa ujasusi katika shirika hilo haijatangazwa rasmi, lakini wanaaminika kuwa miongoni mwa watu wenye nguvu na walioendelea kifedha duniani. CIA inaongozwa na William J. Burns
_123167948_7305b50d-e555-4353-b143-4af6881b733f.jpg

2. Shirika la kijasusi la Israel Mossad
Mossad ilianzishwa mwaka 1949, mwaka mmoja baada ya kuundwa kwa Israel. Israeli ni taifa la Kiyahudi katikati ya nchi tano za Kiarabu. Kwa kawaida, walihitaji wakala kama Mossad kuweka jicho ili kuwachunguza adui zake.

Ni shirika muhimu sana kwa Israeli na linafanya shughuli nyingi katika sehemu nyingi za ulimwengu.

Utamaduni wa Mossad ni kujiandaa kwa hatari kubwa, ambayo zinatokana na hali ngumu iliyokuwepo wakati wa kuanzishwa kwake.

Katika historia ya Israeli mara kwa mara imejikuta katika vita na ulimwengu wa Kiarabu au katika hali ya migogoro. Leo, Israeli ni nguvu kubwa, lakini utamaduni wa Mossad haujabadilika.

3. Shirika la ujasusi Uingereza MI6
Likiwa na makao yake makuu huko London, lilianzishwa mnamo Julai 4, 1909.

Wakala huu hukusanya taarifa zinazohusiana na usalama wa taifa ndani na nje ya nchi.

MI6 ni mojawapo ya mashirika ya kijasusi yenye nguvu zaidi duniani, na linaongozwa na Richard Moore.

4: Shirika la ujasusi la Pakistan ISI
ISI ni wakala wa kitaifa wa kijasusi wa Pakistan na ndio kiini cha usalama wa kitaifa wa nchi hiyo.

ISI ina makao yake makuu mjini Islamabad na ilianzishwa mwaka 1948 na kwa sasa inaongozwa na Nadeem Anjum.

Inasemekana kuwa chombo chenye nguvu zaidi nchini Pakistan na ndicho chombo kinachoaminika zaidi nchini humo

5. Shirika la Ujasusi la Urusi GRU
GRU ni shirika la ujasusi la Urusi lililoanzishwa mnamo 1992.

Ilianzishwa baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti mwaka 1990 na nafasi yake kuchukuliwa na KGB yenye nguvu.

Taasisi hii iliimarishwa na ujio wa rais Rais Putin. By BBC
 
Back
Top Bottom