Exclusive Interview: Waulize maswali Nape Nnauye na Ruge Mutahaba

Exclusive Interview: Waulize maswali Nape Nnauye na Ruge Mutahaba

Amwambie Ruge mimi ni mpenzi sana sana wa clouds wa vipindi vyote kasoro Jahazi ya Kibonde, na yafaa jahazi kiitwe CCM time.

Maswali kwa Nape:

Alitueleza kuwa wanaotoka CCM ni oil chafu je, wale mapacha watatu ni oil safi?
Anakubaliana na maelezo ya serikali kuwa kashfa ya rada hakuna mtanzania aliyehusika na mjadala umefungwa?
 
Hii ''mixture ratio'' ya Nape na Ruge haijakaa sawa.

Jitahidi next time uwakutanishe watu walio katika tasnia moja. Kwa mfano hapa walipaswa kuwa Nape na Mnyika, au Nape na Mtatiro, au Ruge na Kipanya, au Ruge na mtu mwingine yeyote wa entertainment industry!
 
Muulize Nape:

Kwa uelewa wake anadhani ni kwanini kundi kubwa la vijana hivi linaipinga CCM na linaona upinzani ndio mkombozi pekee aliyebaki? Ni juhudi gani chama kinafanya kurudisha imani yake kwa vijana hapa nchini?
 
Swali langu la mwisho, namwomba mwulize mheshimiwa Nape:

Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji vitu vinne watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Je yeye anadhani uongozi bora ni tatizo katika nchi yetu? Na kama jibu ni ndio, kwa nini wananchi waendelee kukichagua chama ambacho kimeshika hatamu kwa zaidi ya miongo mitatu sasa?
 
Kaswali kadogo kwa NAPE:

Je, yeye kama katibu mwenezi amesaidia kuleta mafanikio au anguko kwa chama chake toka yeye awe katibu mwenezi?
 
Dada yangu inabidi ungalie sana aina za watu wa kutuletea humu, mtu kama Ruge ni mjasiriamali wa kawaida sana tena mwenye mlengo flan. Hana mamlaka kitaifa so he is just like any businesman anayemiliki kituo cha mafuta kule Ngara so you better stop this maana utafanya kipindi chako kiwe ni kijiwe cha vijana flani flani kuja kupiga porojo.

Nape ni sawa maana ni mtu ambaye tunahitaji kuongea naye na matamshi yake yana impact kubwa kitaifa! Kwangu mimi ni bora zaidi kama ungeleta mmachinga yeyote hapo toka mtaa wa kongo au kwingineko atueleze changamoto wanazokumbana nazo na anadhani wanahitaji kusaidiwa vipi ili atoke kimaisha!

Yaani kumualika Ruge hapo haina tofauti sana na kumualika Papaa Msofe aje atueleze mafanikio yake!
 
Nnape:-

Anajisikiaje kukosoa utaratibu wa CHADEMA, wakati yeye aliteuliwa(hakuchaguliwa) kuwa katibu mwenezi akiwa hana kadi chama na hadi sasa hajawahi kuwa nayo!!?
 
Wana-JF

Kwenye Makutano Jumamosi hii atakuwepo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye na baadae mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Moja ya vitu atakavyoiongelea Nnape ni kuhusu kauli yake ya kuwa CHADEMA ina wafadhili nje ya nchi na kuwa harambee ya M4C Jumamosi Serena hoteli ilikuwa ya kisanii. Pia atazungumzia mambo mbalimbali ya ndani ya chama.

Ruge Mutahaba ambaye nilifanya nae kazi wakati nikiwa Clouds FM atazungumza kuhusu maisha yake binafsi na ya kazi na changamoto walizokutana nao hadi kuufikisha Muziki wa bongo hapo ulipo.

Kama kawaida nitapenda kupata maswali toka kwa wanajamvi hapa ambayo watayajibu moja kwa moja kwenye kipindi.

Na pia sasa tutapatikana online kupitia
MakutanoShow on USTREAM: Magic FM test. kuanzia saa tisa hadi kumi na mbili jioni na kipindi kitakuwa www.youtube.com/makutanoshow saa moja jioni.

Karibu.


Swali kwa Nape Nnauye Jr:

1. Hakuna shaka kwamba CCM ipo katika siku zake za mwisho za kuishi. Anaizungumziaje kauli ya marehemu Horace Kolimba kwamba 'CCM imepoteza mwelekeo"? Ni unabii unaotimia?

2. Chadema tumejipanga kuchukua nchi mwaka 2015. Anajiandaaje?
 
naomba nitoe angalizo kwako ''mtangazaji'' nape ana tabia akiulizwa swali huwa anazunguka sana mbuyu ..yaani anaanzia mbali sana katika kujibu..lengo likiwa ni kupoteza mda...naomba usimpe air time ya iana hiyo .. hakikisha anakuwa specific kwenye majibu....kuna member humu tayari wameshauliza maswali niliyotaka kuyaauliza
 
Naamini sijachelewa, nina swali 1 kwa kwa kila mmoaja wa hawa wahusika.

Nape:

Jengo la UVCCM - Nakumbuka ulilipigia kelele haswa mwanzoni mwa mradi; je, kuna marekebisho yalifanyika kulingana na mapendekezo yako na tume iliyoundwa? Kama ndiyo, umeridhika na marekebisho hayo? Watu walidhani ulipinga mradi mzima, una nafasi leo, wafafanulie!

Ruge:
Kuna taarifa kwamba Clouds imeuzwa kwa 'wafanyabiashara flani' wenye tuhuma za ufisadi, una kauli yoyote kuhusu hili?
Aidha, kuna taarifa kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Bima ndg Octavian Temu ana hisa katika kampuni yenu, ni kweli?

Yangu ni haya kwa sasa
 
kwa kuwa baba yake alikuwa katibu mwenezi ccm enzi za nyuma awaeleze watanzania alipataje nafasi ya katibu mwenezi ccm .
 
Muulize Nape...
Haoni kama serikali yake ni dhaifu kutokana na migomo isiyo kwisha???

Ruge:
yeye anawapaje support wasanii wanao ibiwa haki zao kupitia ring tone???
Halafu kwa nini clouds hawapigi nyimbo za sugu wakati bif lilisha kwisha???
 
kwa kuwa baba yake alikuwa katibu mwenezi ccm enzi za nyuma awaeleze watanzania alipataje nafasi ya katibu mwenezi ccm .

Jibu simple-like faza,like san...hyo ndo s.s.m bhana kama huamini cheki mjengoni utaona majina yale yale ya mashujaa wa tz tunaowasoma ktk history ndo wamejaa
 
muulize ruge je kuna ukweli kiasi gani juu ya tuhuma huku mtaani kwamba vituo vyao(clouds fm n tv) vimejaa mashoga??
 
kwa nape-naomba aulizwe analichukuliaje swala la mtanzania mmoja kuwa na vyeo viwili,anaweza akawa mbunge wakati huo huo ni mkuu wa wilaya ?je hapo kuna ufanisi wowote?
kwa ruge-naomba mtwange swali mbna anawalea watu wanaoharibu clouds fm kama kina kibonde.
 
kwa kuwa amepata nafasi hiyo kwa mgongo wa baba yake brigedia nape nnauye anawaeleza nini watanzania anawatumikiaje na anajisikia vipi kuendeleza yale mzazi wake aliokuwa ameacha
 
kwa kuwa ameshindwa majukumu yake kama katibu mwenezi haoni ni aibu kuchafua jina la mzee wake aliyetumikia taifa hili kwa unyenyekevu mkubwa akiwa ndani ya chama na serikalini kwa ujumla .
 
ruge vipi ile studio ya wasanii umeshawarudishia au bado usanii unaendelea na nini kilikuvuta hadi ukaikumbatia ni tamaa za pesa au nini
 
Naomba uulize haya maswali yafuatayo:

Nape
1. CCM tuluyoijua sisi toka inaanzishwa 1977, ilikuwa na sera ya ujamaa na kujitegemea (na hili halikuwa na ubishi wa aina yoyote). Kutokana na mabadiliko yaliyojitokeza toka mwanzoni mwa mika ya 1990, sera ya CCM (kinadharia na vitendo, theoretically and practically) ni ipi?
2. Alama za bendera ya CCM zililenga kuonesha wigo wa wanachama na wamiliki wa chama (wakulima na wafanyakazi. Je, Nape anaamini bado hao ndio wamiliki wa chama?
3. Ndugu Nape, siku zote muungwana uhukumiwa kwa maneno anayaoyasema (especially anapotoa ahadi) na huokolewa na matendo yake...Kwa ahadi zako kuhusu kauli mbiu ya kujivua gamba, Nape haoni kwamba umeshapoteza uhalali wa kuendelea kuwa Katibu mwenezi wa chama? Do you think you still have any piece of moral authority to sit on this Nobel post?

Ruge

Kila chombo cha habari hutakiwa kutangaza ama kwa kutoa maelezo rasmi au kwa mfumo wa uendeshaji wake mrengo ambao kinauunga mkono (ama ni partial au impartial) katika kushirikiana na serikali iliko madarakani pamoja na chama tawala. Je anaweza kutueleza kama Clouds ina mrengo (wa kisiasa) ambao kinauunga mkono? Na je, Clouds ina sera gani katika kuhudumia vyama vya siasa? Inaweza kuacha milango wazi kwa chama chochote iwe ni CCM, CHADEMA, TLP, NCCR-MAGEUZI au CUF? Kama jibu ni hapana, kwa nini? Kama jibu ni ndiyo, je Clouds haijawahi kutoa habari kwa ushabiki wa wazi kwa chama chochote cha siasa nchini?

Natanguliza shukrani!
 
Je Nape ana lolote la kuzungumza kuhusu vijisent vilivyofichwa uswis na kwingineko na watu ambao bila shaka ni makada wa CCM?
 
Back
Top Bottom