Exclusive Interview: Waulize maswali Nape Nnauye na Ruge Mutahaba

nape amepwaya katika nafasi yake hiyo yeye binafsi analizungumziaje hilo ,na kuwajibika haitoshi kwanini asitumie nafasi hiyo kuwaomba radhi wana ccm kwa yote aliyofanya ama kwa kuelekezwa au kujituma
 
u stream inakwamakwama sana, am sure network yangu iko bomba, sijui wengine kama wanaipata vizuri!!!
 
Naomba umuulize ruge ni kitu gani kipo kati yake na vinega? na ni nini mtazamo wake kwa siku za mbeleni kuhusu uhusiano wake na kundi la mziki wa bongo(vinega)?. mia
 
swal kwa nape! Alitembelea chuo cha udom anacho kiita mradi wa ccm na kubain majengo mengi ambayo hata miaka 3 hayana yamepasuka pasuka na mengne yamepinda na kukaa kimia..sijui alimaansha nn
 
Swali kwa nape moses nnauye.Kwanini katika ccm ni vigumu vijana wadogo kupata nafasi kugombea nafasi za ubunge?ukiacha wa kuteuliwa kupitia uvccm.tunaona upinzani vijana wanafanya vizuri mfano nasari,yule wa mbozi cdm na akina machali na mkosamali wa nccr,
 
Nape ni miongoni mwa wanasiasa wazuri, namshauri aachane na propaganda/siasa za maji taka hizo ni siasa za kizamani enzi za chama kimoja. Sasa hivi ni siasa za kisasa zinazoenenda na utafiti, ukweli, utashi wa kisiasa na uzalendo wa kweli kwa taifa na watu wake ndicho kilichomfanya awe katika nafasi aliyonayo sasa. Kuanziasha chama kingine ni namna nzuri aloionyesha kuchukizwa na siasa sizizo za kimaadili. "nape Usijichafue jitazame, urejee ktk misingi yako ya awali, daima utakuwa ni tunu ya taifa la Tanzania" .
 
muulize nape mbona maagizo yake anayoyatoa kwa watendaji wa serikali hayatekelezwi na kuna maana gani kuendelea kutoa maagizo au ni kuwahadaa wananchi?
kwa mfano,
1.huko iringa aliliagiza jeshi la magereza kufungua njia waliyokuwa wameifunga ili wananchi wasizunguke umbali mrefu lakini mpaka leo wannchi wanalalamika
2.Huko singida aliagiza hospitali ya mkoa inayojengwa ianze kutumika hata kama haijakamilika lakini watendaji wamempuuza
3.huko kigoma yeye na mwanri waliigiza manispaa ya kigoma waache mara moja kuwatoza ushuru wafanyabiashara wadogo kwenye masoko ya manispaa lakini juzi tulimuona mbunge wa kigoma mjini akilalamika bungeni kuwa ushuru unaendelea kutozwa.
 
Wana-JF

Kwenye Makutano Jumamosi hii atakuwepo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye na baadae mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Moja ya vitu atakavyoiongelea Nnape ni kuhusu kauli yake ya kuwa CHADEMA ina wafadhili nje ya nchi na kuwa harambee ya M4C Jumamosi Serena hoteli ilikuwa ya kisanii. Pia atazungumzia mambo mbalimbali ya ndani ya chama.

Ruge Mutahaba ambaye nilifanya nae kazi wakati nikiwa Clouds FM atazungumza kuhusu maisha yake binafsi na ya kazi na changamoto walizokutana nao hadi kuufikisha Muziki wa bongo hapo ulipo.

Kama kawaida nitapenda kupata maswali toka kwa wanajamvi hapa ambayo watayajibu moja kwa moja kwenye kipindi.

Na pia sasa tutapatikana online kupitia
MakutanoShow on USTREAM: Magic FM test. kuanzia saa tisa hadi kumi na mbili jioni na kipindi kitakuwa www.youtube.com/makutanoshow saa moja jioni.

Karibu.

urgently-matangazo yamekatika ndugu.fina mbna mwatunyima uhondo,mtulipe dk. zetu bhana
 
vipi mbona radio imetoweka hewani baada ya kuanza kujibu kuhusu kauli yake kuhusu pesa chafu za CHADEMA kama anavyodai yeye,ambapo ameanza kwa kujikanyaga baada ya kuulizwa kama alishaurian na uongozi wa juu wa CCMkabla ya kutoa kauli hiyo,amejibu ya kua anaomba asijibu swala hilo kama alishauriana au la!!!!
 
Muulize Ruge vp mwenendo wa Clouds FM, maana imeshatokea mara kadhaa baadhi ya watangazaji wake kuweka ushabiki wa vyama vya siasa hususani chama tawala wakati wa matangazo; yao mfano Kibonde katika kipindi chake cha Jahazi. Ndio msimamo wa redio?

MUHIMU: Muulize Ruge kuhusu Kibonde, kwanza ni mjua vyote wakati hajui, pili ule ukada wake wa Ccm ambao hata akiongelea mpira lazima atangulize maslahi ya chama chake kwa kweli inaboa sana.

Je Ruge haoni umuhimu wa kuanzisha kipindi cha comedy kitakachoongozwa na Kibonde na Jahazi amuachie kijana mwenye upeo na mpenda kujifunza Anold Kayanda?



Muulize Nape:

1. Kama akipata nafasi ya kuzungumza na Dr steven Ulimboka mazungumzo yake yatakuwa juu ya nini???
2. Kama akipewa nafasi ya kumuuliza maswali mawili tu mwandishi mahili wa habari za kiuchunguzi ndg Kubenea,atauliza maswali gani??

Amwambie Ruge mimi ni mpenzi sana sana wa clouds wa vipindi vyote kasoro Jahazi ya Kibonde, na yafaa jahazi kiitwe CCM time.

kwa ruge-naomba mtwange swali mbna anawalea watu wanaoharibu clouds fm kama kina kibonde.

Kweli huyu Mnyakyusa anawaumiza kichwa sana wanazi wa CHADEMA.
 
Katika mahojiano yake na majibu yake ni kinyume na matarajio yetu tuliokua tunafuatilia katika maswali aliyotumwa kupitia JF.Hakuna chochote cha maana alichojibu au kuzungumzia mbali na porojo NAUJUTIA MUDA WANGU!MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Katika mahojiano yake na majibu yake ni kinyume na matarajio yetu tuliokua tunafuatilia katika maswali aliyotumwa kupitia JF.Hakuna chochote cha maana alichojibu au kuzungumzia mbali na porojo NAUJUTIA MUDA WANGU!MUNGU IBARIKI TANZANIA.

hicho kipindi hamna kitu mkuu,kinaboa tu..
 
ndio naungana na wadau hapo juu,fina kaanza boa mapema maana anaomba maswali jamvini lakini anauliza maswali yake ya kichwani inakera kweli kweli,hasa kaboa alipokuwa ana muhoji ruge wa klauz as if alikuwa anaogopa kuuliza maswali yanayolenga moja kwa moja kumfukuzisha kazi kibonde na mengneyo,ngoja wiki ijayo ifikapo ijumaa mtamuona tu anaomba maswali halafu hayaulizi,inaboa aaaarghhhh...
 
fina umeniangusha. ndo maana mara ya kwanza tulikuuliza;
utaweza kuuliza maswali ya jf? ukasema ndiyo. Sasa kulikoni leo? Wewe bado rongorongo. kesho saa mbili kaangalie wenzako startv wanavyo endesha kipindi. Waweza kujifunza. Jipange. mia
 
Muulize ruge
1. Vipi makubaliano yake na sugu na vinega? Nini kipya?
2. Haoni kama kibonde anazidi kupunguza idadi ya wasikilizaji wake?

Kwa nape
1. Vp wale mafisadi na siku zao 90?
2. Hajashtuka kuwa chama chake kimepoteza mvuto?
 
Back
Top Bottom