Nape ashauri TCRA iunde kanuni ya kusimamia na kukuza maudhui ya ndani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Kikao hiki kimefanyika kwa siku mbili ambapo jana Septemba 15, 2022 wadau walilalamikia baadhi ya sheria kuminya uwanja wa ubunifu na utengenezaji wa maudhui shindani.

kwa upande mwingine, wadau wa maudhui walieleza kutokuwa na uwezo wa kulinda kazi zao, kutafuta vyanzo vya mapato na kuziweka kwenye soko kazi zao pamoja na uwepo wa adhabu na cencorship kuwa ni mambo yanayo kwamisha ufanisi wa kazi.

Maudhui ya ndani kwa ujumla hayana ubora wa kushindana kwenye soko la kimataifa mbali na kuwa na vitu vingi ambavyo vinaweza kusaidia kuboresha maudhui ya ndani.

Elimu ilitajwa kuwa changamoto ya vijana wengi. Vyombo vya habari vilitajwa kuigana hivyo kutokuwa na diversity katika maudhui ya ndani. Mfano wa redio, baada ya clouds redio nyingine zimeiga namna ile ya utangazaji.

Wadau walifahamu uwepo wa maudhui mengi ya mapenzi kwenye filamu na miziki, aidha hakuna chaneli ya katuni za watoto, katuni iliyopo ni kipindi tu.

Hoja nyingine iliyozungumziwa ni kutawala kwa mijadala ya mapenzi ambayo huchukua hadi 68% ya maudhui yaliyopo(muziki na filamu) ambapo mdau wa filamu Ndugu Kimela Bila alisema filamu za kisiasa zinazuiwa akitolea mfano filamu yake ya Pingu ambayo ilioneshwa ZIF pekee.

=======

Septemba 16, 2022

Nape Nnauye - Waziri wa Habari na Mawasiliano
Jamii yetu inachangamoto ya kulishwa maudhui kutoka sehemu mbalimbali yanayochangia kuharibu utamaduni wetu, kwa kufabya hivi unaweza kumtawala mtu huyo kwa kila kitu.Taifa ambalo halina utamaduni limefikufa!

Waandaaji wa maudhui mna jukumu la kusimamia maudhui na kuhakikisha mila zetu hazipotoshwi, na kuacha kutegemea maudhui ya kigeni ambayo hayaakisi utamaduni wetu.

Ushauri kwa TCRA, ianzishe tuzo maalumu ya mzalishaji bora wa maudhi ya ndani pamoja na Kanuni za kusimamia wazalishaji binafsi wa maudhui nchini ili kazi zao ziweze kutumiwa na watangazaji.

Tukiwa na mawazo mazuri mfano filamu ambayo itatrace maisha ya wapigania uhuru wapi tunaweleza kupata content itayodumu vizazi na vizazi, kutengeza content kama hizi inaweza kuwa bisashara nzuri kuongeza mapato.

Wote kwa pamoja tuwalinde watoto wetu la sivyo vizazi vijavyo vitaaharibiwa na tamaduni ambazo si zetu. Tulinde na kupenda vya kwetu na kulinda utamaduni wetu kwa kuzalisha maudhui na kupeleka kwengine na kuacha kukumbatia vitu vya nje.

Uzalishaji na uandaaji wa maudhui ufanyike kitaalamu, ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti ili kuweka maudhui yanafaa, mfano TCRA inaweza kuandaa scholarships kwa watu kujifunza. Rai kwa vyombo vya habari kuwekeza katika utafiti utakao enda kuleta maudhui yenye tija.

TCRA inaweza kuwa na scholarships ili watu wajifunze kutoka nje kuhusu namna bora ya kutengeneza maudhui. Katika zile tuzo za watengenezaji wa maudhui, moja ya zawadi inaweza kuwapeleka nje ya nchi ili kujifunza kutengeneza maudhui yenye ubora.
 
Back
Top Bottom