Exclusive Interview: Waulize maswali Nape Nnauye na Ruge Mutahaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive Interview: Waulize maswali Nape Nnauye na Ruge Mutahaba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makutano Show, Aug 17, 2012.

 1. Makutano Show

  Makutano Show Verified User

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana-JF

  Kwenye Makutano Jumamosi hii atakuwepo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye na baadae mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

  Moja ya vitu atakavyoiongelea Nnape ni kuhusu kauli yake ya kuwa CHADEMA ina wafadhili nje ya nchi na kuwa harambee ya M4C Jumamosi Serena hoteli ilikuwa ya kisanii. Pia atazungumzia mambo mbalimbali ya ndani ya chama.

  Ruge Mutahaba ambaye nilifanya nae kazi wakati nikiwa Clouds FM atazungumza kuhusu maisha yake binafsi na ya kazi na changamoto walizokutana nao hadi kuufikisha Muziki wa bongo hapo ulipo.

  Kama kawaida nitapenda kupata maswali toka kwa wanajamvi hapa ambayo watayajibu moja kwa moja kwenye kipindi.

  Na pia sasa tutapatikana online kupitia
  http://www.ustream.tv/channel/makutanoshow kuanzia saa tisa hadi kumi na mbili jioni na kipindi kitakuwa www.youtube.com/makutanoshow saa moja jioni.

  Karibu.
   
 2. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Muulize Nape what is his Job description? Na anatoa wapi maelekezo na ana report kwa nani?

  Kwa sababu mara nyingi kauli zake na za mwenyekiti wa CCM zimekuwa zikikinzana; mfano ni kuhusu watuhumiwa wa ufisadi ambao alizunguka nchi nzima kuwataja na akidai wajivue gamba na mwisho wa siku mwenyekiti alitamka hadharani akiwa anaongea ana wahariri wa vyombo vya habari last month kwamba hakuna kashfa ya Rushwa kwenye manunuzi ya RADAR.
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Ok.
  1) Nape ni nini kimekusibu, badala ya kukieneza chama chako cha CCM unakuwa katibu mwenezi wa CHADEMA isivyo rasmi, hii inatafsiriwa huku mitaani kuwa chama tawala kinatapatapa na kimekosa grip ya kuongoza nchi. Jitetee!!!!

  2) Kabla ya kuishupalia CHADEMA kuhusu kuingiza fedha unazodai ni chafu, serikali ya chama chako imechukua hatua gani kufuatia taarifa za kuaminika kuwa kuna maofisa waandamizi wa serikali wametiliwa kwenye akaunti zao uswisi zaidi ya bilioni 300 na makampuni yanayojihusisha na gesi hapa nchini!?

  3) Nape tueleze, mkataba wa ujenzi wa jengo mnalodai ni la Vijana wa CCM pale Lumumba uko shwari? Hakuna harufu ya rushwa pale? Kumbuka tuhuma ulizozitoa wakati ukigombea nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM. Majibu yako ya-reflect tuhuma zile kama hukuwa sahihi ama ulinyamazishwa kwa kupewa ukuu wa wilaya.

  4) Angalau kwa sentesi sita unamuelezeaje Lowassa kisiasa na kijamii?
   
 4. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Muulize Nape anaichukuliaje dhana ya kujivua gamba? Je, imefanikiwa kwa kiasi gani na ime-fail kwa kiwango kipi? Anamuelezeaje Andrew Chenge kama Kiongozi wa Maadili ndani ya CCM?
   
 5. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,899
  Likes Received: 4,751
  Trophy Points: 280
  Muulize Ruge ilikuaje Zamaradi alirusha kipindi kuhusu yule mtoto bila privacy hakuona kama amemdhalilisha?
   
 6. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Muulize Ruge vp mwenendo wa Clouds FM, maana imeshatokea mara kadhaa baadhi ya watangazaji wake kuweka ushabiki wa vyama vya siasa hususani chama tawala wakati wa matangazo; yao mfano Kibonde katika kipindi chake cha Jahazi. Ndio msimamo wa redio?
   
 7. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Kwanza nakupa BIG-UP sana kwa kufunguka na kuwa member wa JF katika real terms, I wish siku moja nami niwe kama wewe.

  Pili nadhani una kazi sana ya kumoderate hiyo discussion kwani wote wanaonekana wanavaa jezi moja... maswali yangu ni haya yafuatayo, tena naomba kama wanweza wajiandae tu kujibu
  1. Ni kitu gani Ruge na Nape wanadhani wanacho in common?
  2. Ruge na Nape wote wametokea familia bora, je kuna nini wanachoweza kuwafundisha watoto wao kuhusu ukweli, uwazi na kupinga matendo ya kutochukulia shida za masikini wengi serious? Mfano kunyonya maskini, kuwatumia maskini kwa faida binafsi nk
  3. Swali la mwisho.... Kutokana na walichokwishapanda hapa nyumbani, je wanaona any sustainable future kwao na vizazi vyao kwa mfumo huu-huu tulio nao sasa?
   
 8. m

  mbishi Member

  #8
  Aug 18, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Muulize Nape, ni nini faida ya hili vuguvugu la kufungua matawi ya chama ughaibuni? Yanasaidiaje vyama hivyo kuwa na wanachama katika pande hizo za dunia?
   
 9. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Muulize Ruge vipi anashirikiana vipi na Wadau wa sanaa ya Muziki ktk kuongeza pato la wasanii wa bongo fleva ambao Clouds ndo wateja wake wakubwa?

  Vp anamuelezeje Sugu kama Muasisi wa Hip Hop Tz?
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Muulize Nape:

  CCM sasa ni chama cha Habari Maelezo? Kwanini wanavizia Chadema wakifanya chochote wao kesho yake wanakimbilia kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari na kuzungumzia kilichofanywa na Chadema? Mbona wanakuwa kama wao ndiyo wapinzani na Chadema ndiyo watawala?

  Muulize pia katika siku chache zijazo M4C itakuwa na harambee kubwa Mwanza huenda kubwa kuliko ile ya Dar, anaizungumziaje?
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tunawaomba nyie waandaji wa Makutano Show mumlete John Mnyika msemaji rasmi wa Chadema....
   
 12. J

  JBK Member

  #12
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mpe swali hili Nape:

  Unajisikiaje unapoona watu wanakuwa na vyeo zaidi ya viwili kama ubunge na ukuu wa mkoa vilevile kama uenezi wa chama na ukuu wa wilaya wakati nchi hii ina wasomi wengi wanaozunguka barabarani?

  Muulize Nape:

  Utajisikiaje pindi itakapotokea Lowassa kuchaguliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM?
   
 13. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Maswali kwa Nape:

  1. CCM inafanya biashara au wanatarajia kuingia ubia na wawekezaji?
  2. Anaelezeaje ujio wa Bilionea wa Kinaijeria ambaye anajenga kiwanda cha saruji Mtwara ana uhusiano wowote binafsi na CCM au biashara yake?
  3. CCM wameshawahi kueleza umma mchanganuo wa misaada wanayopata kutoka kwa wahisani?
  4. Anauzungumziaje ufisadi na rushwa ndani ya serikali na CCM kwa ujumla? Mwizi akiiba then akabainika anaambiwa arudishe chenji?
  5. Nape huoni kama kadri siku zinavyokwenda una loose focus...? Ni lipi ambalo unaweza kuwaambia watu kuwa umefanikiwa? Kuvua gamba, ufisadi mkataba wa ujenzi jengo la UVCCM, chaguzi ndani ya chama, mvuto wa chama mbele ya umma...
  6. Nini lengo la mikutano ya Jangwani, Rukwa na Kigoma? Na gharama za kuandaa hiyo mikutano zinalingana na matarajio?

  Asante Fina Mango nitashukuru kama Nape atayapata haya maswali na kuyajibu bila kupepesa macho
   
 14. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  MUHIMU: Muulize Ruge kuhusu Kibonde, kwanza ni mjua vyote wakati hajui, pili ule ukada wake wa Ccm ambao hata akiongelea mpira lazima atangulize maslahi ya chama chake kwa kweli inaboa sana.

  Je Ruge haoni umuhimu wa kuanzisha kipindi cha comedy kitakachoongozwa na Kibonde na Jahazi amuachie kijana mwenye upeo na mpenda kujifunza Anold Kayanda?
   
 15. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #15
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Muulize Mh. Nape:

  1. Kwanini viongozi wengi wa CCM na serikali (akiwemo yeye mwenyewe) wanapigana na rushwa, ufisadi katika majukwaa na vyombo vya habari wakati wengi wanaojihusisha na vitendo hivyo wamo ndani ya chama na serikali na wanafahamika mfano zoezi la kujivua gamba. Kwanini CCM inawalinda Wakati vyombo vyote vya dola polisi, serikali, jeshi, takururu mahakama na sehemu kubwa ya wabunge viko chini ya chama tawala?
  2. Katika kauli yako ya majuzi kuhusu "CHADEMA kusafisha pesa chafu" Kama una ushahidi kwanini hukuufikisha katika vyombo vinavyohusika na badala yake kutishia ya kua wasipo vitaja vyanzo vya pesa chafu utavitaja, kama ilivyokuwa katika katika kauli yako kuhusu kujivua gamba,uliposema ya kua katika siku 90 wasipojivua gamba mtawafuza?.
  3, Je kimaadili sio tu kwako wewe bali hata mtanzania wa kawaida inakuwaje mtu anapokua na ushaidi kwa uvunjifu wa sheria asiufikishe vyombo husika vya sheria nakuishia kutishia kuwataja katika vyombo vya habari? Je ni viongozi wangapi na wa ngazi zipi wameisha chukuliwa hatua ndani ya CCM katika zoezi la kujivua gamba?
   
 16. D

  Determine JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tatizo lako wewe Mango unakuja jf kutuomba maswali halafu tunakupa huyaulizi,unaishia kuchagua maswali mepesi mawili au matatu yasiyo kuwa na hadhi ya jf kama tank la greater thinkers, niseme tu usipobadilika jf tutakunyima ushirikiano

  Muulize Nape:

  1. Kama akipata nafasi ya kuzungumza na Dr steven Ulimboka mazungumzo yake yatakuwa juu ya nini???
  2. Kama akipewa nafasi ya kumuuliza maswali mawili tu mwandishi mahili wa habari za kiuchunguzi ndg Kubenea,atauliza maswali gani??

  Mwambie Ruge

  1. Awahimize sana watangazi wake umuhimu wa kuheshimu masilahi mapana ya watanzania na kuacha mara moja utangazi wa kipuuzi na kishabiki wanaofanya sasa, make kuna hatari ya wao (Clouds) kuanza kupondwa mawe muda wowote kama watu kama akina kibonde hawatabadilika
  2. Clouds inazidi kuchukiwa na wananchi kila siku kwa sababu yeye (Ruge) amekubali kutumiwa na wanasiasa,akumbuke kuwa clouds haina uwezo kwa kutulazimisha sisi tupende chama wanachoshabikia ambacho ni CHAMA CHA MAFISADI


   
 17. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #17
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Swali kwa Ndugu Ruge Mutahaba:

  Nini mtazamo wako kuhusu baadhi ya vipindi ambavyo watangazaji wake wanapwaya - yaani uendeshaji wake hauendani na mantiki ya kipindi
  [Mfano baadhi ya watangazaji ambao sitaki kuwataja wa Kipindi cha jahazi na power breakfast hawaendani na kipindi chenyewe hasa inapohusu habari nzito za kitaifa (siasa) Wakati mwingine wanaleta utani au ushabiki. Kwanini watangazaji hawa wasiwachiwe vipindi vya burudani? Ukiisiliza power breakfast on Sutarday vikiendeshwa na Steven Mwihava au Macharanga-sijui sasa amepotelea wapi? Na timu yao nzima vinaendeshwa kwa umahili, umakini na nidhamu tofauti kabisa na vipindi dada vya jumatatu-ijumaa.]
   
 18. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Muulize Ruge kwa nini ameruhusu Radio yake kugeuka kuwa mouthpiece ya chama tawala?
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Muulize Nape:

  CCM kina uongozi uliokamilika kuanzia nyumba kumi, tawi, kata, wilaya hadi taifa. Inakuwaje wote hawa hawaonekani wakifanya siasa matokeo yake CHADEMA ambayo haina mtandao kama huo inakifunika chama chake?
   
 20. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Naomba pia umuulize Ruge Clouds FM walilipa kodi kiasi gani mwaka jana?
   
Loading...