Eti uchochezi, uchochezi gani?

Eti uchochezi, uchochezi gani?

Na
Hizi habari za uchochezi mimi sizielewi kabisa.

Hao watu wanaotuhumiwa sijui kuchochea, wamechochea kitu gani?

Kumpindua Magufuli?

Huyu jamaa asipoangalia anaweza kutumia muda wake mwingi kupambana na watu wenye maoni na hisia ambazo zipo kinyume na atakavyo au apendavyo yeye.

Katika viongozi ambao Tanzania imewahi kuwa nao tokea tuanze kutawaliwa na CCM huyu jamaa atakuwa anaongoza kwa kutokuwa na busara wala hekima.

Hovyo kabisa!

Sitashangaa JF nayo ikifungiwa kwa kupromoti uchochezi wa akina Ngabu😉.
Naogopa!
 
[HASHTAG]#hapakazitu[/HASHTAG] Mwaka huu mtanena kwa lugha zote lakini lazima mnyooke...hakuna maigizo hapa ni kazi tu.


MADIKTETA WOTE DUNIANI HUFANANA

Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.

b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.

c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!

d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!

e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi).

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?

2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)

3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.

4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)
 
Ata yule bwana mdogo Nape naye ni dikteta hataki kuckia chombo chochote cha habari kinamkosoa MAgufuli atahakikisha kinafungiwa, tuukemee huu Udikteta.
 
Unaogopa nini kaka?
Naogopa kukamatwa! Nyani kuna attachment nimeiweka humu kuonyeha kuwa sedition is no longer a preferred law! It is condemned by any civilized society! Please take you precious time to read it! Nakuwekea wewe particularly here! Definitely hakuna uchochezi, ni huko kuwasumbua watu tu. Sheria iko wazi kuwa kuwakosoa viongozi sio kosa/sedition. Uganda supreme court imeifuta sheria hiyo! Nitakuwekea case hiyo baadaye
 

Attachments

Hapa kwa Mwanakijiji nadhani bado kidogo atamuita mtukufu rais kuwa ni Mungu wake
 
H

Huyu jamaa asipoangalia anaweza kutumia muda wake mwingi kupambana na watu wenye maoni na hisia ambazo zipo kinyume na atakavyo au apendavyo yeye..
Hoja yangu na yako zinashabihiana kwenye hiyo sentensi niliyonukuu. Kwamba, anaweza kujikuta anatumia rasilimali nyingi sana (rasilimali watu, rasilimali fedha na rasilimali vifaa), kupambana na wapinzani badala ya ku deal na maendeleo. Kuja kushtuka anakuta 2020 iko mlangoni, hana cha kuwaambia wananchi.
 
Hoja yangu na yako zinashabihiana kwenye hiyo sentensi niliyonukuu. Kwamba, anaweza kujikuta anatumia rasilimali nyingi sana (rasilimali watu, rasilimali fedha na rasilimali vifaa), kupambana na wapinzani badala ya ku deal na maendeleo. Kuja kushtuka anakuta 2020 iko mlangoni, hana cha kuwaambia wananchi.

Halafu mwishowe yatakuwa yaleyale ya maisha bora kwa kila Mtanzania!

Baada ya Kikwete kumaliza muda wake ni Watanzania wangapi walio na maisha bora?

Na hapo kuna idadi kubwa tu ya watu walionunua hizo ngonjera zake mwaka 2005.
 
I guess uchochezi is whatever the government doesn't like hearing/seeing on that day
I think its time sheria zispecify kabisa uchochezi ni nini? Huu mtindo wa kuweka certain sections vague, ndo hiyo mtu anapachika meaning yake halafu anakusweka ndani.smh
umesemaje hapaaaa?????.... ni kisukumaaa au kisengerma?
 
Hizi habari za uchochezi mimi sizielewi kabisa.

Hao watu wanaotuhumiwa sijui kuchochea, wamechochea kitu gani?

Kumpindua Magufuli?

Huyu jamaa asipoangalia anaweza kutumia muda wake mwingi kupambana na watu wenye maoni na hisia ambazo zipo kinyume na atakavyo au apendavyo yeye.

Katika viongozi ambao Tanzania imewahi kuwa nao tokea tuanze kutawaliwa na CCM huyu jamaa atakuwa anaongoza kwa kutokuwa na busara wala hekima.

Hovyo kabisa!

Sitashangaa JF nayo ikifungiwa kwa kupromoti uchochezi wa akina Ngabu😉.
Big up Leo umenipa burudani Sana mkuu
 
Wacheni uchochezi! Mlimtukana sana baba yake Ritz mkiamini mswahili hawezi uongozi ni dhaifu. Kwa kuwa naye "mswahili" akawajibu kwa kiswahili nawaletea mkali asiye mswahili. Sasa mnalalama nini?
 
Tanzania ambayo Africa nzima tuliheshimika tumegeuka mara hii kuwa kichekesho. Nchi inaendeshwa na matamko ya viongozi tu. Taratibu za kila siku zimeshindikana. Jamani huyu mtu hana watoto wa kumwambia. Tafadhali wasanii wamtungie wimbo kama ule wa "Riziwan ongea na mshua......."
Msanii yupi ambae hajipendi amtungie nyimbo
 
Baada Ya africa kusini na Botswana Tanzania ndiyo inayofuata kwa kuwa na demokrasia bora barani Africa.
 
Teh teh teh teh kwa hali hii inayoendelea ya ukandamizaji wa serikali dhidi ya vyombo vya habari kuna siku watatamani kufunga jukwaa letu. Maana linatoa uwanja mpana wa kuikosoa serikali hii ya mtukufu malaika asiyependa kukosolewa
 
Back
Top Bottom