Eti uchochezi, uchochezi gani?

Eti uchochezi, uchochezi gani?

Anaweza akawa Rais wa awamu moja.

Watu kama akina January usione wapo kimya, waswahili wanasema ukiona Kobe kainama ujue anatunga Sheria.

Miezi 10 madarakani, kaharibu kila kitu. Wananchi, Wanasiasa, Wafanyabiashara hata Watumishi hawana amani na huyu jamaa!!
Mkuu tulia zamu yetu ni 2020 tutamchetua kwenye sanduku la kura
 
Tulishakosea kumchagua.kumpa madaraka makubwa mtu ambae hajatulia ni matatizo na mabalaa nchini.
 
Hakuna cha uchochezi hapo! Ni hofu tu na rahana za gori la mkono. Kibaya zaidi hawa waliopewa Rungu (nape, chemba) to mention a few wana roho za visasi dhidi ya upinzani. Sioni mwenye busara kati ya hawa kwa kutenganisha majukumu yao ya ukada wa ccm na shughuri za serikali.
 
Naogopa kukamatwa! Nyani kuna attachment nimeiweka humu kuonyeha kuwa sedition is no longer a preferred law! It is condemned by any civilized society! Please take you precious time to read it! Nakuwekea wewe particularly here! Definitely hakuna uchochezi, ni huko kuwasumbua watu tu. Sheria iko wazi kuwa kuwakosoa viongozi sio kosa/sedition. Uganda supreme court imeifuta sheria hiyo! Nitakuwekea case hiyo baadaye
I will also read the doc. thanx
 
Ni upumbavu mtupu, kurupuka ya kapuku
Uzamivu wa wivu, uza mbivu kwa saba buku
Baba kakaba LUKU, siasa kahaba shuku
Sio Wamakonde Maraba lakini kwa mahaba ya kuku
Tutakula mpaka panya buku chukuchuku
Dukuduku, OSS, aliye juu mpandie, usimngoje hukuhuku
Chai kwa pipi, sukari kiki
Elimu bure vipi huku redio unafungia?
Misukule pipi wenzio unatuungia?
Idi Amin asiye makini, nyama la baharini
Majina manne ubini, diva kwini, kingi wa magirini
Pol Pot, Ze Comedy Joti, baba mkusanya noti
Gusa shoti, samasoti, mwendo wa speedboti
Baba bwabwaja, jinga la haja, baja kaja
Paji kaa paja, Opobo Jaja, Black Maharajjah
Bwabwa kiporo, watu kihoro, limelala doro
Chini godoro, Dar mpaka Moro, twapitia Muhoro?
Serikali kali, bila uhalali, kwa mtaji wa shari
Hii manuwari, itenda muhali, vipi hadi dahari?
Chama mrama, ndama kapama, maziwa yahama
Hili drama la karma kama Obama na Osama
hii itakuwa hip hop hii
 
Chama chetu kipi? Sina mahaba ya kipumbavu kwenye chama chochote cha siasa.nasapoti nachokiona ni sahihi .nilimpigia kura Magufuli na kwa upande wa utekelezaji wa Sera zake nakubaliana nao kama kuzuia rushwa, kupunguza matumizi ya serikali n.k . Lakini hili la kuwakamata wanaomkosoa, kuzuia mikutano ya vyama vya siasa sikubaliani nae.

Unatuzuga.........hisia na mahaba.........
 
Hizi habari za uchochezi mimi sizielewi kabisa.

Hao watu wanaotuhumiwa sijui kuchochea, wamechochea kitu gani?

Kumpindua Magufuli?

Huyu jamaa asipoangalia anaweza kutumia muda wake mwingi kupambana na watu wenye maoni na hisia ambazo zipo kinyume na atakavyo au apendavyo yeye.

Katika viongozi ambao Tanzania imewahi kuwa nao tokea tuanze kutawaliwa na CCM huyu jamaa atakuwa anaongoza kwa kutokuwa na busara wala hekima.

Hovyo kabisa!

Sitashangaa JF nayo ikifungiwa kwa kupromoti uchochezi wa akina Ngabu😉.

Magufuli anachokifanya yeye anakaba njia tu,hakabi mtu.Kibaya zaidi anacheza namba mbili kwa mpigo half back four (4)na(5).
 
Natabili baada ya miaka miwili Tanzania itakua na wafungwa million 20
 
Guys we have to be patient, presidaa yashamuwia magumu ndio maana anasema tumwombee.Tuweni watulivu tu pengine mabo yatanyooka ingawa sina uhakika.

Hapana ,tusijichoree mstari wa kuuliza.Hilo neno 'pengine' halifai kutazamia kwa aina ya Mtawala wa sasa...
 
Ukinitukana hadhari si tu umenivunjia heshima pia umeingilia uhuru wangu. Haki yangu ni kukushitaki Mr. Nyani Ngabu.

Kwa kiongozi wa kitaifa ni UCHOCHEZI. Unamdharirisha mbele ya jamii iliyomchagua pia kwatafsiri hiyo, umedhihaki waliompa kura. Wewe uliyemdharirisha kiongozi huyo ni mhaini.

HABARI NDIYO HIYO Nyani Ngabu
 
Muhimu tu uwe na passport na hela ya akiba ndani ya kutoshamaana direction sio nzuri,kama hapa hata mwaka haujamalizika ndo mambo yako hivi,sasa sjui 2020 itakuwaje
Ngabu ntakuwa mgeni wako hapo atlanta na mie niwe kwenye chama la USA baby
 
kuna haja ya mahakama kutuweka wazi kwa hilo nini maana ya uchochezi na matendo au uchochezi wa aina gani ni kinyume cha sheria na sheria ipi kifungu kipi hasa kinavunjwa na vile vile ni adhabu ipi kifungo au fine au vyote kwa pamoja mana tumekumbwa na woga hatujui tuchangie kipi tuache kipi kila kitu ni............
 
Back
Top Bottom