Eti uchochezi, uchochezi gani?

Eti uchochezi, uchochezi gani?

Wacheni uchochezi! Mlimtukana sana baba yake Ritz mkiamini mswahili hawezi uongozi ni dhaifu. Kwa kuwa naye "mswahili" akawajibu kwa kiswahili nawaletea mkali asiye mswahili. Sasa mnalalama nini?
Jaman najuta Mie, namkumbuka mbaya, mambo yako hovyo hovyo sahivi
 
Huyu jamaa asipoangalia anaweza kutumia muda wake mwingi kupambana na watu wenye maoni na hisia ambazo zipo kinyume na atakavyo au apendavyo yeye.
Duuuuh kuwa kwako ng'ambo kunakuziba macho na masikio...
Mbona JPM anafanya kazi zake kila siku za kutuletea maendeleo, ndege zinakuja, mafisadi hawana amani, nizamu imerudi katika Utumishi.. Bilion 18 kila mwezi za Elimu bure..

Sijaona wanapo mfanya Magu asifanye kazi yake... Wanaoleta fujo watakutana na Polisi ambao ndio kazi yao kutunza amani

Wizara ya habari inafanya kazi yao..

Wizara ya Utumishi inafanya kazi yao

Wizara ya uchukuzi na Mawasiliano inajenga barabara za juu, reli ya kati.. Serikali inapiga kazi kila jambo linashughulikiwa
 
Ss hv ukitaka kutoa maoni mtandaoni lazima uwaze cha kuandika
Hawakawii kutukamata
Na JF yetu ikibaki salama sijui nadhani wanaitamani sana.
Wacha niendelee kusubiri Sept Mosi nkaandamane mie
Aisee Mie ntakuwa mmojawapo, really am tired
 
Mutoto mazuri kama malaika namuomba namba ya simu amejibu huo ni uchochezi.
 
Huyu naye anadai eti ana anatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi! sheria na katiba ipi ya nchi ambayo inampa nguvu yeye ya kutoiheshimu katiba ya nchi!?


Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Dodoma

Kamanda ajiapiza kudhibiti Ukuta

KAULI za vitisho bado zinaendelea ambapo sasa viongozi wakuu wa jeshi hilo, wanaeleza dhamira ya kutumia nyembo mbalimbali kuhakikisha operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) inazimwa, anaandika Dany Tibason.

Operesheni hiyo ilitangazwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Julai mwaka huu baada ya kufanyika Kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho.

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi amesema, atatumia kila nyenzo kuzima Ukuta.

Kauli hiyo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari mjini hapa, ikiwa ni siku moja tangu Mbowe, atangaze msimamo wao kwamba, maandamano hayo yatafanyika kama ilivyopangwa.

Amesema, jeshi hilo lina majina ya wanachama wa Chadema wanaopita nyumba kwa

nyumba kuhamasisha watu washiriki maandamano hayo.

Na kwamba, wengine wamejipanga kushambulia polisi hivyo amewataka kutambua kuwa, jeshi hilo lina uchungu wa kuondokewa na askari wenzao walioshambuliwa na baadhi kupoteza maisha hivyo hawako tayari kuendelea kuchezewa.

Hata hivyo, alipotakiwa kutaja majina ya watu hao Mambosasa amesema, yatatajwa baada ya kuwakamata kwasababu, angeyataja wangeweza kutorokea mikoa mingine.

“Serikali siyo polisi pekee, vyombo vya usalama ni pamoja na Ofisa Mtendaji wa Kata, viongozi wote wa serikali za mitaa, wakaguzi wa

tarafa na polisi kata ambao wanategemewa kukusanya na kutoa taarifa za

kiintelijensia, tutatumia nyenzo zote kuhakikishia wananchi usalama

wao na mali zao,” ameseleza Mambosasa.

Wakati Mambosasa akisema hivyo, Jerad Mambo, Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Dodoma amesema, mikakati yao imekamilika na vijana wana ari ya kutetea haki yao.

Geofrey Mwakiseyo, Katibu wa Chadema wa Jimbo la Mpwapwa amesema, mpaka sasa watu wa kada tofauti katika vitongoji 39 wapo tayari kwa maandamano hayo.

Kuhusu zuio lililotolewa na Kamishna Mambosasa, Mwakiseyo amesema, anatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Nchi kama ambavyo na wao watatekeleza majukumu yao ya kisheria na Katiba hiyo hiyo, kupitia Ukuta.

Kamishna Mambosasa amewataka wanahabari kutohofia usalama wao na kufanya kazi zao hususan kuhusu hali itakavyokuwa siku hiyo ya Septemba Mosi.

SOURCE: MTANZANIA
 
Mwaka sasa unapita toka awepo madarakani Rais Magufuli
Sijaona la maana zaidi ya kuendelea kutoa ahadi
Utawala wa kulipeleka jeshi barabarani kupambana na wapinzani
Ahadi zake ZOTE hata moja haipo hata kwenye maandalizi
 
Mkuu, huu utawala ni mbovu na haijawahi kutokea nchi hii. Jamaa ni pretender na mwenye wivu na mtu yeyote anayezani amempita kimaendeleo. sijui tuna mkosi gani Tz?
 
Haijawahi kutokea Tanzania kupata kiongozi mbovu....toka uhuru kama huyu ngosha..a.k.a MFALME J.U.H.A. Mimi nimeanza mfungo rasmi ili Mungu atende mema na kuokoa jahazi....maana katika kondoo mia akipotea mmoja wakabaki 99 salama ni heri zaidi kuliko hii kadhia ambayo watanzania wanaipata kwa sasa. Poteleaaa mbali...kuanza upya sio ujinga.....MUNGU POKEA SALA ZANGU!

Lazima ulikuwa unaishi kiujanja janja.Nyufavzimezibwa mnaanza kulilia.JK alivyokuwa madarakani nyote mlimtukana sanaaaa tu.Kwamba ni Dhaifu.Mkaomba mpate dicteta.
Sala zenu za kupata dikteta zimekubaliwa bado mnalia.Mnatakani nini nyie?
 
Wacheni uchochezi! Mlimtukana sana baba yake Ritz mkiamini mswahili hawezi uongozi ni dhaifu. Kwa kuwa naye "mswahili" akawajibu kwa kiswahili nawaletea mkali asiye mswahili. Sasa mnalalama nini?

Mkuu umenena vyema kabisa.JK "muswahiri asie jua kutawala" Dua zao zilikubaliwa tukapata "mtendaji" sio muswahiri badoooooo Na huyu sio.Bado wana lalama.
Hapa ni kazi tu Na hajaribiwi
 
Hahahaa kuna watu waliwahi kusema huyu ni 'chaguo la Mungu'

Na bado tunaamini ni chaguo la Mungu.
Maisha ni Magumu Na sio ya kawaida Kwa wale walio zoea maisha ya kuigiza Na kuwa Na uhuru wa kufanya watakavyo.
Maisha yana songa.Pesa yangu ya hongo inachangia kodi.Sina haja ya kumjua mtu ili nipigiwe muhuri kwenye taasisi yeyeto.Heshima imeongezeka.Kwa kweli naishi Tanzania ninayo itaka.Hata kama JPM angetoka upinzani Na akafanya anayo yafanya bado ni chaguo la wengi.
 
Sahau Mkuu kuhusu Tanzania ya viwanda, sasa hivi tuna Tanzania ya vitisho chini ya fisadi dikteta uchwara Magufuli. Unategemea viwanfa kweli Mkuu na hizi sera za kukurupuka mwendo kasi? Saa zote wako busy kupanga mikakati ya kupambana na vyama vya upinzani ikiwemo kutoheshimu katiba, kupandikiza mamluki (CUF), kuratibu mazoezi ya polisiccm uraiani ili kutuweka roho juu Watanzania. Saa ngapi watapata muda wa kupanga mikakati ya Tanzania ya viwanda? Ni Majanga tu Mkuu tena makubwa sana.

Me naisubiri Tanzania ya viwanda
 
Inavyoonekana uchochezi hapa ni ni kukinzana na mipango iliyopo sasa.nimeona watu wanapinga ununuzi wa ndege mbili,wanapinga kufufua viwanda vya zamani n.k
 
Mwaka sasa unapita toka awepo madarakani Rais Magufuli
Sijaona la maana zaidi ya kuendelea kutoa ahadi
Utawala wa kulipeleka jeshi barabarani kupambana na wapinzani
Ahadi zake ZOTE hata moja haipo hata kwenye maandalizi
Kweli ujaona la maana mpaka sasa alilofanya Magu? Kweli kabisa unaongea toka rohoni? Kwa roho ya namna ukipewa kichapo kwa ukaidi utasema unanyanyaswa?
 
Back
Top Bottom