Eti hatujui... kipimo gani kinatumika?

mkuu kloro.....
Kwa mujibu wa majibu haya....hata la kununua gunia la mkaa linahusika hapa...
Ndio mahaba yenyewe
lol

....ohoooo,....sasa wewe ndio umeharibu kabisa, au unatania?

usiponunua wewe hilo gunia la mkaa atanunuliwa na nani?
tusichanganye wajibu na majukumu yako kama mume, na mahaba.

...
no wonder wengine ati baada ya kuachana na wake zao wanasitisha hata matumizi kwa watoto wao.
...ni ujinga wa 'mwafrika'

Kisha mmechunguza mwanamme wa Tanzania anaedekesha sana mkewe watu wakamuona anaitwa 'zoba'

p(^_^)q

...spot on, utapewa majina yote ya maudhi, ikiwamo umelishwa kipapai, ....na wanawake wasiojua 'kupendwa' hufikia hata
kujitapa mbele ya wajinga wenzake ati "nimemuweka kiganjani, hafurukuti!"...
 
Lol naona pasinipite....................Shemeji mwanamke mwenye kijiaibu ndo anakuwaje? Anaruhusiwa naye kuwa mtundu kidogo wakati wa ,Njenje, au ataonekana mcharuko? Hebu nijibu haraka nisije nikaachika shemeji yako nikafa kwa njaa!

Kwa uchokozi sikuwezi,

Unataka wazee wazima tuanze kuuza data...

Ila kwa kweli binti kama hana kiabu anakufanya upoteze mzuka...Na yule mwenye aibu aibu na haiba ya kiwizi wizi (sorry, simaanishi kibaka au jambazi!!), anayekuangalia kwa kuku-avoid kama vile anaungama dhambi zake kwa Padri anaweza kusababisha mauji ya kutokukusudia,

Turudi kwenye mada......Hadi sasa tujipe matumani kwamba kwa romance na sisi tupo au tumekuwa tukivumiliwa tu???
 
nataka nyie mnaojifanya wa zamani (mtoa mada akiwemo) mseme zamani mlionyeshaje mahaba?
 
Aaawww Bee thanks :]

You go girl put your romance on fyah !

thanks gurlie!!

Gee ngoja kwanza, hivi end result/s za kuwa romantic au romance zenyewe ni nini? unategemea nini unapoonyeesha mahabat ya nguvu kwa waubani wako?
 
hilo limejivika vazi ndo maana....
Hivi wewe bosi gunia la mkaa na kuku hai vinaongezaje mahaba? Hapo hata hakuna cha uzungu wala uafrika bana, hebu nieleze nielewe

hapa kloro anaweza saidia kutengeneza the best romantic picture itakavyokuwa lol

nakupa mfano......

Wewe bee ndo wife wangu....umekaa kibarazani unapiga story na wenzio...
Mimi nakuja kwa mbaali...kulia nimeshika kuku na kushoto kuku...wanalia lia...
Unaniona.....unawaambia watoto...kampokeeni baba enu nyi watoto...lol
watoto wanakuja huku wanaimba 'baaba kaleta kuukuu...'majirani wanakuonea wivu.....

Hiyo sio romantic?????? Kumbe je????????lol
 

Sasa wewe Mbu umeamua kuturudisha nyuma.....

Mimi kama mwanamume wa Kitanzania na Mwafrika origino (tena dume la mbegu), kama hayo mahaba hayahusiani na sex au hayatanisaida kupata sex nafanya ya nini???


Haki ya nani sina sababu ya kuyafanya kama mwisho wa siku naondoka patupu?? May be ninazeeka vibaya!!!
 

Dah! mkuu The Boss naomba nikutangaze rasmi kuwa starring wa hii thread.
Yaani huu mfano hai kabisa tena vere romantic llakini still bht ,gaijin na mj1 watabisha.
 

siku nyingine usinitolee mfano......

daaah Bosi kwa hiyo kuwa romantic kunategemeana na mtu na mazingira pia. mimi ukileta hivyo naona ni sehemu tu ya wajibu wako kama baba wa familia. lakini kuna vijimambo tu vidogo bana ukifanyiwa unajihisi uko ahera wallah tena...

kwa mfano akicheza na jina langu na kuja na jina lingine (yaani hakuna mtu mwingine alishawahi niita hila jina...its so unique) kwa kweli najiskia raha sana, au akinisifia sifia hivi kama nimefanya kitu vizuri au nimeonyesha maendeleo kwenye mambo fulani fulani, that is soo romantic to me!!!!
(does anyone need money to be romantic in such a case?)
 

Ubarikiwe mstaafu.
Hoja yako hata bungeni haiwezi kupingwa achilia mbali JF.
 

....wakati nikikutayarishia jibu, nami naomba nikuulize swali la kizushi ewe mkuu mstaafu....baada ya kupata hiyo kitu roho inataka, aka 'great' sex....romance/mahaba yanaishia hapo?
 

Loh Mzee DC swali langu mie umelifukia wataka lako nilianike sawa hiyo kweli?
Wewe mwenyewe ushasema kuwa wanaolalamika hivyo kuwa 'hamyajui/hamko romantic ni wake zenu majumbani' ilhali wale mnaokutana nao mara 2 kwa mwaka wanawasifia na kuwaganda. Sasa si ina maana mnajijua na sababu mwaijua??

Mie nlishasema moja, ukasema utajitetea kisha ukakimbia
 
waiiii gunia la mkaa? nipishe mie....hata ukiongeza na manumbu sitaki, bado sijashtuka.

hahahaha umenikumbusha mbali kweli...enzi hizo na chai ya asubuhi......hii thread cjui niianzie wapi mackini!
 

Mbu

Nilishawaambia kuwa kuna definition ya mume anavyotakiwa kuwa kimsingi

Romance ni zile extras ambazo si wajibu ila zikifanywa zinaongeza ladha ya mapenzi.

Anikande miguu hivi tukitoka safari (si mnajua mchuchimio na adhabu zake)....na mengineyo madogo madogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…