eti 'HAKUNAGA'..

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
48,427
110,668
hii nyimbo itachangia mno kuharibu kiswahili.....

sio kiswahili fasaha kusema hakunaga.....
 
Inakera sana watu wanaojidai na kujiita waswahili wanaposhindwa kuandika kiswahili na wanachafuwa mazingira wanapoongea"ga". Sijui hizi "ga" "ga" zimetokea"ga" wapi?
 
Inakera sana watu wanaojidai na kujiita waswahili wanaposhindwa kuandika kiswahili na wanachafuwa mazingira wanapoongea"ga". Sijui hizi "ga" "ga" zimetokea"ga" wapi?

kingereza hatujui kiswahili nacho hatujui. Watu wengine wanaokera wanaochanganya r na L
 
Hakunaga ni neno sahihi tu la kiswahili na maana yake ni ''hakuna kitu kama hiki'' mfano ''hakunaga Rais mzuri kama Kikwete''
 
Inakera sana watu wanaojidai na kujiita waswahili wanaposhindwa kuandika kiswahili na wanachafuwa mazingira wanapoongea"ga". Sijui hizi "ga" "ga" zimetokea"ga" wapi?

tembelea unyaluni "ga" "ga" za kumwaga
 
Nijuavyo mie ni kwamba kuna Kiswahili cha kuongea na Kiswahili cha kwenye tenzi/mashairi, katika Kiswahili cha kuongea ndipo hasa mtu anatakiwa kuwa makini kwa kuandika/kuongea lugha sahihi/fasaha!!

Kiswahili cha kwenye tenzi/mashairi sasa, hapa mtunzi hulazimika kubadilisha neno (hasa herufi za mwisho) bila kupotosha maana halisi ya neno ili mradi tu kufuata vina!!! Kama wewe ni msomaji mzuri wa mashairi utakuwa umekutana na hivi vitu mfano vina vya mstari wa kwanza viliishia na neno `wabaya` utalazimika kumalizia na `ya` kwa mistari yote sasa ndiyo pale mtunzi anajikuta anatumia maneno kama tembeya, chekeleya, kubaliya na n.k.!!!

Hivyo, simlaumu Suma Lee hata kidogo kwani alikuwa anafuata vina vya `ga` na hii ni kutokana na kuona labda kama angemalizia na herufi tofauti tofauti wimbo usingekuwa na utamu kama ulionao hivi sasa mpaka watu wanasema amerudi tena!!!

Ni hayo tu waungwana wa JF!!!
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom