Pascal Mayalla, hakunaga National Sovereignty kwenye kutenda uhalifu!

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
39,788
Reaction score
92,287
Hamjambo!

Mkuu Pascal Mayalla Kwa heshima yako. Ni muhimu kujua japokuwa najua unajua kuwa hakunaga national sovereign kwenye kutenda Uhalifu.

Wale wafuasi wa sijui nchi huru, lazima wajue ni Uhuru katika haki na utu.
Kinyume na hapo utaingiliwa utake usitake.

Kama vile serikali inavyoweza kuingilia familia yako pale ambapo Baba au mama au mtoto anapotenda uhalifu. Ndivyo hivyohivyo nayo inaweza kuingiliwa inapofanya dhulma, uhalifu, na kuonea watu wake.

Haiwezekani wewe Pascal kama Baba umpige mkeo, umuonee, uwaumize watoto wako alafu ujitambe hapa uko huru, sijui familia yako hutaki Sisi tukuingilie tutakuingilia tuu.

Tena mkeo na watoto wataungana na watu wanje kukunyorosha, kukushikisha adabu.

Pascal Mayalla unataka usiingiliwe na familia zingine mtendee haki mkeo na watoto wako. Full stop.

Hao watoto wako sio magari, midoli, au mbuzi kwamba unaweza kuwachinja muda wowote unaotaka.

Serikali yoyote kama haihitaji kuingiliwa itende haki. Kama inavyojipa umuhimu kuingilia wananchi wahalifu ndivyo nayo ikifanya uhalifu itaingiliwa vilevile.

Kwako Pascal Mayalla na watu wenye mitazamo ya namna hiyo.

Karibuni kwa mjadala
 
Paschal saa ingine anajitoa ufahamu. Hivi yeye akinyanyasa au kuuwa watoto wake anadhani majirani zake watamnyamazia. Lazima washughulike naye kwa njia zozote zile, hatasema hapa ni kwangu sasa nafanya unyama kama ninavyotaka. Nadhani pia paschal anaidanganya CCM.

Ni kweli Kabisa
 
Mkuu @Pascal Mayalla Kwa heshima yako. Ni muhimu kujua japokuwa najua unajua kuwa hakunaga national sovereign kwenye kutenda Uhalifu.

Wale wafuasi wa sijui nchi huru
, lazima wajue ni Uhuru katika haki na utu.
Kinyume na hapo utaingiliwa utake usitake.
Mkuu hili wanalijua vizuri, ila sijui wamepatwa na jambo gani hadi wanaposema wanasema vice versa.

Ujinga sometimes ni kama kifo, tuliowazunguka ndio tunaumia. Ila wao wanaona Fresh tu.

UHURU una mipaka yake, kuanzia ngazi ya Familia, Mtaa, kijiji hadi ngazi ya Taifa na Dunia kwa ujumla.
 
Kuna kosa kubwa la kifikra kudhani mateso, mauaji au ukandamizaji ndani ya mipaka ni internal affairs.

Uhalifu unapovuka mipaka ya utu, unakuwa global concern, kama ambavyo dunia inaruhusu kuingilia kati wakati wa genocide, ndivyo ambavyo msingi wa haki za binadamu unavyokataa national sovereignty kama kisingizio cha kutenda unyama.

Nchi ambayo haiwezi kuheshimu haki za watu wake, haina haki ya kuheshimiwa na mataifa mengine.
 
Shida ya shemeji yangu Pascal Mayalla ni kupenda kuuma na kupulizia. Hakuna sovereignty kwenye mauaji ya wananchi wasio na hatia, utekaji, uonevu, dhuluma, ukandamizaji wa haki za kiraia, wizi, ubadhirifu, ufisadi, nk.

Serikali inayojiingiza kwenye hayo matukio, hupoteza sifa ya kuwaongoza wananchi. Na hata ikitokea shinikizo kutoka nje, wananchi wataungana na wageni kuikataa hiyo serikali.
 
Uko sahihi Kabisa
 
Sahihi Kabisa
 
Eeh elezea hii yakuitana shemeji
 
Wanafahamu sana wanajitoa ufahamu tu… hiyo ndio narrative wajinga waCCM wameona waiuze.

Wenyewe tumecompliy na sheria za kimataifa za haki za binadamu, tujiondoe kwanza kwenye mikataba yote ya international laws ili tupate uhuru wa kuua “raia wetu wenyewe” bila kubughudhiwa.

Takataka hawa watu 🚮
 
Nimemshangaa sana mayalla uue watu maelfu alafu useme wasikuingilie!?
Ili uendelee kuua kwa uhuru!!
Ingawa tukipigwa spana itatubana sie wa kawaida lakni walau ujumbe uwafikie

Halafu kufananisha mazingira ya siku na nyakati za Nyerere na huyu mama ni kumuonea kabisa
Naomba Pasco awe serias japo kidogo
 
Back
Top Bottom