eti 'HAKUNAGA'..

Nyimbo gani?

Hakunaga'' Siipendi! kila redio station hakunaga hakunaga, watangazaji wetu nao malimbukeni sana, ndo sababu huwa nasema watangazaji walishaenda karibia wote wamabaki madj's tu
 
Mie pia huo wimbo hauniingii kabisa moyoni, unaudhi, HAUNA MAADILI KABISA, NASHANGAA REDIO ZA UCHOCHORONI WANAVYOUPIGA WANA LENGO GANI?
 
Mie nachukizwa na watangazaji wa redio wanaotumia 'L' nafasi ya 'R' na kinyume chake . Inafundisha vibaya watoto.
 
kumbe hata jf kuna wanafiki.nyimbo zote za bongo fleva hakunaga ndo momeona mbaya?mnashindwa hata kuzungumzia movie.mwacheni msanii wetu apete.alivyo imba ule wimbo wa chungwa mbona hamkusemaga?achanegi hizo bana.mia
 
huu wimbo unavyonikera natamani wanaojiita chombo cha kucontrol hii mambo wangeupiga burn tu ...HAKUNAGA? mtu akishapuliza mabange yake tu anaingia studio HAKUNAGA? inamaana hata hizi redio hazichuji cha kucheza hewani au ndo wakishapewa chenchi wanapiga tu?
 
kisanii inakubalika kutumia lugha isiyo rasmi katika baadhi ya maneno ili kuonyesha msisitizo au kuburudisha.........lugha ya kisanii tu tusijitie ujuaji wa kukosoa kila kitu!
 
Ni kweli inaweza kuwa inakela maskioni kusikia hilo neno, lakini katika sanaa inaruhusiwa.
 
Ni nani anayewapima na kusema lugha zenu ni sahihi au la, maana ya kiswahili ni lugha ambayo maneno yake yametoholewa kutoka lugha nyingine, neno fulani kuwa sahihi katika lugha fulani ni makubaliano tu yanaweza kutungwa maneno na yakakubalika, hakunaga ni neno sahihi inategemeana na mtizamo wako, hayo ni maneno ya mpito, kumbuka neno kama kasheshe, maneno mengi ya kiswahili yametoholewa kutoka kwenye lugha za pwani mfano pakacha, kumbi, msala,mbachao na neno meza, ilhali ni maneno ya kiarabu kwa tafsri yenu basi hayo si maneno ya kiswahili, lugha inakuwa jamani sio kitu ambacho miaka yote itakuwa vile vile. Ukitaka kutafuta kiswahili ni nini kwa mujibu wa tafsri zenu hutapata lugha ya kiswahili. Suma lee hoyee.
 
Acha lugha ijieleze yenyewe lkn co ww m2miaji wa lugha uielekeze lugha. Kuna mambo mengne japo hayakubaliki lkn hayapingki ndo km hlo neno hakunaga, kitoto, jitu, bonge nk.
 
Wana jamvi hili ni eneo la great thinker hivi hamjaona maneno mengine ila hili tu HAKUNAGA kuongeza "ga" si tatizo mbona kuna maneno mengi yameongezwa hamsemi mfano kuna maneno mengi yanaongezwa "ni" hamsemi, mfano wa maneno kama hayo ni sebuleni, chumbani, nyumbani, mtoni, uwanjani, harusini, gengeni, sokoni, barabarani, barazani n.k lakini hayo mnaona yapo sahihi, maneno vile vile yanaweza kutumika bila kuongezwa ni na yakaleta maana.
 
dah..hii nayo ni kero sana kwangu mim binafsi....sasa maana yake ni nini...hivi mtunzi anapotunga wimbo lengo ni kuelemisha jamii, kuifikishia jamii ujumbe fulani...sasa huu wimbo maudhui yake hasa ni nini....eti Dushelele....hakunaga...aaagrrrrhhhh
dah dushelele...
 
Wana jamvi hili ni eneo la great thinker hivi hamjaona maneno mengine ila hili tu HAKUNAGA kuongeza "ga" si tatizo mbona kuna maneno mengi yameongezwa hamsemi mfano kuna maneno mengi yanaongezwa "ni" hamsemi, mfano wa maneno kama hayo ni sebuleni, chumbani, nyumbani, mtoni, uwanjani, harusini, gengeni, sokoni, barabarani, barazani n.k lakini hayo mnaona yapo sahihi, maneno vile vile yanaweza kutumika bila kuongezwa ni na yakaleta maana.
kha!! Ina maana neno "nyumbani" sio sahihi??
 
mifano yako inaashiria hukwenda shule.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom