Ephraim Kibonde asema kutotaja walioficha hela ni ujinga

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,133
1,250
kushindwa kuwataja walioficha Hela Uswisi ni Ujinga,asema Kibonde. Akizungumza katika kipindi cha Jahazi leo tarehe 22.11.2012, bila kutaja jina, Kibonde amedai kuwa yeye anashangaa hata waandishi walioshindwa kumuuliza ukweli kuhusu madai ya kuwepo kwa watanzania wenye fedha nje ya nchi. Yeye anaona yule anaedai kuwa ana ushahidi wa kufichwa mabilioni nje ya nchi bila kuwataja wahusika ili kurahisisha kazi ya uchunguzi hana akili na ana nia ya kujitafutia umaarufu tu. Watangazaji wenzake akina Kayanda na Wasiwasi Mwabulambo wameonekana kukubaliana na mawazo ya Kibonde! na kusema huyu ambae anaropoka tu kuwepo kwa walioficha hela Uswisi bila kuwataja ni "MPUMBAVU"

Kwa tafsri ya moja kwa moja na bila kupinda ukweli, kwa kuwa hoja ya kuwepo kwa watanzania wenye akaunti USWISI ilitolewa Bungeni na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Chadema, kauli hii ya Kibonde itakuwa inamhusu sana mtoa hoja huyo (Mhe. Zitto) na sio mwingine.
 

Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,238
2,000
Nakubaliana na kibonde kabisa. Huu wala siyo ujinga bali ni upumbavu!
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
35,793
2,000
Amesema kutowataja majina ni upumbavu!. Akasema "Mpumbavu wewe wataje kama huwataji kaa kimya!.

Akimaanisha anayejidai anawajua huku hawataji ni mpumbavu!.

Kusema ukweli japo Kibonde ni rafiki yangu ila kiukweli jamaa yangu huyu sii mzima kichwani!. Kuwa kichaa sio lazima mpaka mtu aokote makopo!.
 

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,451
1,170
Sikuhizi vyeo vinatafutwa kwa njia tofauti ukizingatia kuwa upepo wa waandishi wa habari umefunguliwa....... Hakika tutawasikia wengi tu!
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
Pasco, Nyani Ngabu,

..I would never call Zitto mpumbavu, nadhani Kibonde amekwenda mbali.

..sidhani kama Kibonde anaweza kumuita kiongozi yoyote yule wa CCM mpumbavu.

..kwa upande mwingine, nashauri Zitto ajilipue tu na hayo majina.

..mbona Dr.Slaa alijilipua pale Mwembeyanga na ile orodha ya mafisadi na mpaka leo bado anapeta tu??

..au, Zitto amkabidhi Dr.Slaa mikoba yote uone mmang'ati atakavyoshughulika.

NB:

..Dr aliniacha hoi alivyowalipua Mkapa na Ole Njolay kwamba walijaribu kumhonga post kwenda ubalozini UN.
 

Heavy equipment

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
951
500
Kibonde nakukumbusha kuwa wakuu wa wilaya walishateuliwa suburi awamu nyingine, mbona JK alizuia pesa za hayati KIGOMA MALIMA kwanini hizi zishindikane? Kibonde nakuomba unipe interviews kwenye clouds radio nikudadavulie zaidi..
 

swrc

JF-Expert Member
Jun 17, 2012
442
0
huyo kibonde ndiye mpumbavu kwani serekali haijui kinachoendelea? Ni mabo mangapi yanayofanyika ya hovyo lakini serekali bado inakaa kimya na kukanusha? Si walisema kuwashitaki walioiba pesa za epa kunaweza kuhatarisha amani ya nchi? Waache zao huko na huyo anayetaka zito ataje majina. Na zaidi si tumeona jinsi wanajiundia kamtandao kao ka ulaji kama walivyouza mahoteli yote (ndani ya hifadhi za taifa) yaliyokuwa ya serekali kwa bei poa?
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,411
2,000
Pasco, Nyani Ngabu,

..I would never call Zitto mpumbavu, nadhani Kibonde amekwenda mbali.

..sidhani kama Kibonde anaweza kumuita kiongozi yoyote yule wa CCM mpumbavu.

..kwa upande mwingine, nashauri Zitto ajilipue tu na hayo majina.

..mbona Dr.Slaa alijilipua pale Mwembeyanga na ile orodha ya mafisadi na mpaka leo bado anapeta tu??

..au, Zitto amkabidhi Dr.Slaa mikoba yote uone mmang'ati atakavyoshughulika.

NB:

..Dr aliniacha hoi alivyowalipua Mkapa na Ole Njolay kwamba walijaribu kumhonga post kwenda ubalozini UN.
Asipowataja mimi nitamuona hana courage of his convictions!
 

Faru Kabula

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
12,558
2,000
Katika hali ya kushangaza, radio ya Clouds FM jioni hii ya leo 22/11/2012 kupitia mtangazaji wake Efraim Kibonde, imemuita Zitto Kabwe kuwa ni mjinga kwa kile walichokiita kutotaja majina ya waliojilimbikizia mali Uswisi !

Nimeshangaa sana kwa ujasiri wa Kibonde, kwani hakustahili kumuita mtu msomi kama Zitto kuwa mjinga, tena usomi usio na shaka, wakati inajulikana wazi yeye Kibonde tangu alipofeli Form Four, amekwisha re-seat mtihani wa kidato cha nne mara tatu bila ya kufanikiwa kuongeza credit ya somo hata moja!

Redio hii inafanya makosa makubwa kuwapa vipindi vya uchambuzi watangazaji wasio na upeo wa kutosha juu ya mambo mbalimbali katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Hivi kuna hata haja ya kuuliza Kibonde na Zitto nani ni mjinga?

Sifahamu ni nani hapa nyumbani aliyetune katika frequency za hii radio leo, huwa sitaki kuisikiliza. Tatizo mahouse girl nao wanapenda sana kusikiliza umbea
 

chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,937
1,195
Kwani akiwataja alafu, mbona wa madawa ya kulevya wanajulikana lakini ndo yameshika kasi, mbona Dr.Slaa alipeleka majina kwa DPP na ushaidi mpaka leo kimya, Mbona Jk alisema anawajuwa wanaovuruga Bandari ,je wameacha? Je akitaja tuwafukuze au tufute TISS maana wao wakipewa habari ni kuchunguza. ZITTO ASITAJE,TAIFA LIFANYE KAZI YAKE
 

mwimbule

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
559
250
Kwani kuna shida gani katika kutaja majina ya watu wenye pesa Uswisi. Nafikili ilikuwa jambo jema kuwafahamu wabaya wetu kama kweli anawafahamu kwanini anawaficha.Dr Slaa aliwataja mafisadi kumi na moja kwa majina yao tukawajua pale mwembeyanga. Nakubaliana na Kibonde zitto awataje kwa majina, ili tuwasute na wengine wafe kihoro.
 

Keen

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
618
195
Nakubaliana na kibonde kabisa. Huu wala siyo ujinga bali ni upumbavu!
Katika nyakati tofauti tofauti watu (mainly wanasiasa) wamekuwa wakitaja watu mbali mbali kuhusika na tohuma mbali mbali. Kwa mfano, orodha ya mafisadi, kutekwa kwa ulimboka kama ambavyo mchangiaji mwingine ametukukbusha. Ni action zipi serious ambazo zimechukuliwa dhidi ya wahusika? Penye nia pana njia, kama kweli serikali ina nia ya kushughulikia hizi tetesi za kuficha mabilioni ya dollar, sidhani kama inahitaji majina ili kulifanyia kazi hili swala. Alivyouawa kamanda barlow, majina ya wauaji iliyapata wapi? Kwa sababu nia ilikuwepo, njia ilipatikana. Wahusika wasitafute sababu, wameshaambiwa wapi pesa zilipofichwa, vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake na siyo kusubiri majina. Wanao-insist kutajwa majina ndo wafanye kazi ndio, kwa mtizamo wangu nawaona wajinga!!
 

Mzawa Halisi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
610
500
Kusema ukweli japo Kibonde ni rafiki yangu ila kiukweli jamaa yangu huyu sii mzima kichwani!. Kuwa kichaa sio lazima mpaka mtu aokote makopo!.
Mkuu Pasco,

Msaidie kumpa ujumbe, nafikiri kwenye comedy anafit zaidi kuliko kuwa mchambuzi wa mambo, na kuwa siyo watangazaji wote ni wachambuzi.
 
Last edited by a moderator:

humphg

Member
Apr 20, 2011
56
0
Kibonde yuko sahihi kabisa. Kama mtu hauko tayari kuyataja hayo majina basi usifungue mdomo wako! Kaa kimya.
Mjinga we kama kibonde! mmekutana pipa na mfuniko! Kwanza jina "Kibonde" tu! maana yake huna akili na uwezo wa kufikiri mambo kama wengine, wa mwisho kabisaa! pia na wasiwasi na elimu yenu!

wananchi tunalipa kodi selikali ili iweze kulinda mali zetu watanzania! Kama malizetu zanaibwa na yenyewe yenye dhamana ya ulinzi (Selikali) iko hapohapo na haijui nani kaiba!!? kunahaja ya kuendelea na selikali hii zembe!! yenyewe kwa miaka takriban mitano sasa tangu mambo ya VIJISENTI yaanze hadi leo haina hata jina moja!!!!

Basi na itoke hapo akae mwingine atakae tulindia malizetu kiuhakika bila magumashi! au tusilipe kodi kabisaa maana hawezi na kashindwa kuzilinda malizetu zaibiwa tu, na sio kusingizia wananchi wataje majina si kazi yao!! Ni kazi ya selikali kubaini mwizi sababu ndie mwenye dhamana ya ULINZI wa malizetu! Kwa hili naona selikali haina dhamira ya dhati kuhusu suala hili la USWIS, wanataka kulipotezea tu!! na kuzuga wananchi eti hakuna alie tajwa lipite!!!
 
Top Bottom