Ephraim Kibonde asema kutotaja walioficha hela ni ujinga

Kuna kiongozi alituambia kuwa anayo majina ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya. Hiyo orodha mbona haitoki mpaka leo! Naye kutotaja ni mpumbavu kweli?
 
mjinga akielimishwa anabadili ila mpumba hata umtoboe ubongo hataelewa kibonde umewapa jina thuri sana hao ni WAPUMBAVU tena ukiwa waangali ni watu umri unasoma saa 12.30 baada ya kuwazika wao 2taiza mabilioni ye2 jamani hebu watajeni na picha zao zibandikwe km za move za kanumba
 
Mimi naona kutoboana macho nani mjinga nani mwerevu ni sawa tu na wafungwa kunyang'anyana bakuli la uji wakati mkuu wa gereza anajulikana. Zitto atapataje majina ya wahujumu nchi serikali na vyombo vyake vinavyotafuna mabilioni ya walipa kodi yenyewe isipate? Wote wanajulikana, na ni haki yenu kama mnataka majina ya hao, ishinikizeni serikali iyataje. Mnamwandama Zitto mmemwajiri kwa kazi hiyo? yeye katumia gharama zake kayapata, amewasilisha hoja kwa mpangilio anaojua yeye utaleta matunda, nyinyi mnataka mumtoe kwenye plani yake afate ya kwenu, si na nyie mkatafute hayo majina kwani yeye kayapataje. Huyo Kibonde katoa maoni yake lakini nadhani ulimi uliteleza kwakuwa hauna mfupa.
 
ukiangalia utaona kwa wepesi tu kuwa alikua akimlenga ZITTO,na nadhani kilichomtisha zaidi,si kibonde bali aliemtuma na kumfadhili,ni jinsi Mhe Zitto,alivyomudu kwa ufanisi kuweka wazi mambo yote yenye utata kuhusu yeye kwenye mdahalo ulioendeshwa hapa JF leo....kama Zitto alivyosema,Njia Pekee ya kumaliza Majungu na Uzushi ni Uwazi,leo amekua muwazi na mkweli na imewagusa wengi...
Pasco naona umenipa like ya post ya miaka saba nyuma...anyway R.I.P Kibonde
 
Back
Top Bottom