johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,035
- 142,137
Mwenyekiti wa Chadema na KUB Mh Freeman Mbowe anazungumza na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuhusu Corona.
UPDATE
Tangu WHO ilipotangazwa ugonjwa wa Corona kuwa ni janga la Kidunia, sisi kama CHADEMA tumeendelea kuamini katika ushirikishwaji wa kila mmoja katika nchi hii kwa pamoja kwenye mapambano
Janga hili linahitaji dunia kupambana pamoja kwa kushauriana na kusaidiana. Watawala wasiotambua hili ni janga kubwa kwa watu wao sasa na siku za usoni, hakika wanajitayarishia na wanastahili anguko kubwa la kisiasa.
Ushirikiano unahitajika kwa kiasi kikubwa, mfano nchi ya Syria kulikuwa na vita kali lakini hivi sasa pande zote mbili zimesimamisha vita ili kupambana kwa pamoja. Huu ndiyo ushirikikiano ambao sisi CHADEMA tunatamani kuuona katika nchi yetu
Tulitii kwa Serikali na tukasitisha mikutano yetu ambayo ilikuwa tuifanye mwezi Aprili, nimezungumza na Mhe. Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha na Spika wa Bunge nimewapa moyo na mawazo kwa niaba ya chama ili tushirikiane kupambana na COVID-19
Nimezungumza Bungeni na hapa tunatoa mapendekezo kwa Serikali ilete hoja ya dharura Bungeni, tuache mambo mengine yote na tujadili janga hili kwa kina. Pia ifanye marekebisho makubwa ya bajeti ya mwaka 2020/21 kwani ikibaki iliyo haitatekelezeka
Tunashauri Mhe Rais asione aibu juu ya janga hili, halikuanzia Tanzania na watumishi wake hawapaswi kuficha chochote, bajeti kubwa itengwe katika kupambana na janga hili haraka iwezekanavyo
Njia kuu ya kisayansi ya kupunguza au kuzuia maambukizi ya Covid-19 ni kuvunja mwingiliano wa watu (breaking the cycle of human interaction) . Wengi wanatambua mfumo huu kama "Lock down" ni njia ngumu na yenye gharama kubwa za kiuchumi hususani kwa nchi masikini
Ni ujinga uliopitiliza kwa nchi yoyote kufikiria ina uwezo wa kukabiliana na janga hili la #COVID19TZA kwa utaratibu wake wa ndani, iwe kwa misingi ya kiuchumi, kisayansi, kitabibu ,kiutamaduni, kwa imani za kidini na mbaya zaidi hata kwa imani za kishirikina"
Ni ujinga zaidi kutokujifunza kwa uzoefu kutoka kwa nchi zilizotangulia kupambana na janga hili la #COVID19, janga hili linahitaji dunia kupambana pamoja kwa kushauriana na kusaidiana
Serikali iunde 'COVID-19 Task Force' na iwashirikishe watu wengine nje ya Serikali na kamati hizo ziwe katika kila ngazi na viongozi wa kamati hizo wachaguliwe kwa kuzingatia uwezo wao na si vyeo vyao
Mimi binafsi, ni Mhanga wa janga hili kwani mwanangu alikuwa miongoni mwa wahanga 10 wa kwanza. Aliambukizwa na kupelekea familia nzima kuwa chini ya karantini huku kijana akiendelea na uangalizi na matibabu hadi leo ikiwa ni takribani wiki zaidi ya 5
Kwa nyakati mbalimbali, binafsi nimezungumza suala hili na namna bora ya kushughulika kwa pamoja kupambana nalo. Nimezungumza na Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Spika wa Bunge na Naibu wake, Mawaziri kadhaa moja kwa moja au kupitia Kamati mbalimbali za Kibunge.
Tunatambua vile vile juhudi zinazofanywa na vyama vingine vya siasa vya Upinzani, hususan Chama cha ACT Wazalendo na CUF, Taasisi mbalimbali za Dini, Taasisi mbalimbali za Kiraia na Kitaaluma, vyombo vya habari, makundi ya wawekezaji na umoja wa wafanyabiashara.
Nchi nyingi duniani zimeimarisha mahusiano na umoja wa Kitaifa kupitia janga hili, msingi mkubwa ukiwa ni kuweka tofauti zao zozote pembeni, kisha kushikamana na kunia pamoja
Hapa kwetu Tanzania, umoja wetu wa Kitaifa unaelekea kuparaganyika zaidi kwa namna Serikali ya Rais John Pombe Magufuli ilivyolipokea na inavyoratibu mapambano dhidi ya Janga hili. Madaraka na Mamlaka yao yatambue wakati wote kuwa Mamlaka Kuu na ya mwisho hapa Tanzania ni Umma wa Watanzania wenyewe.
Kwa msingu huu, sasa tunaamini pasipo shaka kuwa njia bora zaidi ya kuisaidia Serikali na hatimaye wananchi ni kutokukaa kimya. Tunapotoa ushirikiano kwa kusema ndani ya vikao, Serikali haionyeshi kujali vya kutosha na inapunguza kasi ya mapambano katika vita hii.
Sasa tumeamua kuisaidia zaidi serikali kwa kuanika kwa uwazi maeneo mbalimbali ambayo tunaamini ikiyafanyia kazi itaweza kuthibiti kwa kiwango kikubwa janga hili.
Aidha, tunawasihi wananchi wote sasa wajifunze zaidi kupaza sauti zao katika kutetea uhai wao. Kila mmoja apige kelele kwani ukimya na Upole wa Watanzania ndiyo unaowapa CCM na Serikali yao jeuri ya kupuuza maoni yao.
Sisi kama Chama Kikuu cha Upinzani hatuoni Serikali ikipokea na kutambua ushauri wetu. Tunaamini hali hii iko vilevile kwa vyama vingine na makundi mengine yaliyo nje ya Chama cha Mapinduzi na Serikali yake. Nina vielelezo kadhaa vya ni kwa nini tunaamini hivyo.
Kwa ukubwa wajanga hili, ungetegemea Bunge makini hadi hatua ya sasa,lingekuwa limeshaiamuru Serikali kuleta taarifa rasmi Bungeni ili kuwapa Wabunge,kwa niaba ya wananchi fursa ya kupata taarifa rasmi ya serikali, kuijadili na kuishauri na au kuielekeza hatua za kuchukua.
Katika mazingira ya kutatanisha na kushangaza, Bunge halijatekeleza wajibu huu licha ya kuwepo maombi mara kadhaa toka kwa wabunge hususan wa Upinzani kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji Bunge.
Rai hii ya Upinzani, nimeifikisha binafsi kwenye vikao vyote mahsusi vya Kamati za Kiuongozi za Kibunge, bila kupewa kipaumbele chochote. Hii ni pamoja na Kamati ya Uongozi, Kamati ya Bajeti na hata Tume ya Utumishi wa Bunge.
Zaidi, soma: FULL TEXT: Hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA (T) na KUB kwa Umma wa Watanzania kuhusu COVID-19 - JamiiForums