Elon Musk hana ujuzi wa maswala ya mitandao ya kijamii

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,125
1,922
Elon Musk hana ujuzi wa maswala yote yanayohusiana na mitandao ya kijamii kwasababu amekuwa na tabia za childish tangu awe mkurugenzi wa kampuni ya Twitter.

Kwa kawaida mtu anaponunua kampuni yeyote ile anatakiwa kuboresha huduma zilizokuwa zikitolewa hapo awali na sio kuharibu huduma.

Bwana Elon tangu amiliki kampuni ya Twitter, malalamiko yalianza kwa watumiaji wake wakichukizwa na mfumo mpya wa uendeshaji ikiwemo masharti mengi kwa watumiaji pamoja na nembo mpya ya X ikishutumiwa kuwa inatambulisha ngono jambo ambalo limeharibu kabisa mtandao huo wa Twitter na hivi sasa kuonekana kama mtandao wa kipuuzi

Elon Musk ana fedha nyingi lakini hana taaluma ya maswala ya mitandao ya kijamii hivyo basi ni vizuri angejiondoa katika nafasi ya mkurugenzi wa kampuni hiyo na kumwachia mtaalamu aliyebobea katika maswala ya mitandao ili anusuru kampuni hiyo ya X kwasababu ipo mbioni kuondoka machoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii
 
Kwanza siyo mkurugenzi wa X bali ni Linda Yaccarino. Pili Elon kanunua mtandao wa X kwa ajili ya ku feed data katika kampuni ya XAI.
Elon Musk, mwenye maono nyuma ya makampuni kama Tesla na SpaceX, tena ameweka macho yake kwenye uwanja wa akili bandia (AI). Mradi wake wa hivi karibuni, xAI, una lengo la kuongeza hazina kubwa ya tweets ili kufundisha algorithm yake. Katika mazungumzo ya hivi karibuni ya sauti ya Twitter Spaces, Musk alishiriki maono yake ya kujenga AI ya uchunguzi na ya kweli, akiibua maswali kuhusu faragha ya data na changamoto za kisheria.

Kwa hiyo hayo masuala ya hajui yeye hayamhusu anacho focus nacho kwa sasa ni kuhakikisha XAI inafanikiwa kama SpaceX na Tesla motor.

Na anaenda kuifanya mtandao wa X kuwa mtandao bora kabisa.. Kwa takwimu mwezi huu wameweza ku record watumiaji million 500+ kwa mwezi ni rexord ya juu kabisa ya watumiaji toka kuanzishwa kwake.
Saiv content creators wanalipwa.

Na sasa mtandao wa X unaenda kuwa kama WeChat ambapo services zote za kifedha zinapatikana ndani ya mtandao mmoja.
 
Elon Musk hana ujuzi wa maswala yote yanayohusiana na mitandao ya kijamii kwasababu amekuwa na tabia za childish tangu awe mkurugenzi wa kampuni ya Twitter.

Kwa kawaida mtu anaponunua kampuni yeyote ile anatakiwa kuboresha huduma zilizokuwa zikitolewa hapo awali na sio kuharibu huduma.

Bwana Elon tangu amiliki kampuni ya Twitter, malalamiko yalianza kwa watumiaji wake wakichukizwa na mfumo mpya wa uendeshaji ikiwemo masharti mengi kwa watumiaji pamoja na nembo mpya ya X ikishutumiwa kuwa inatambulisha ngono jambo ambalo limeharibu kabisa mtandao huo wa Twitter na hivi sasa kuonekana kama mtandao wa kipuuzi

Elon Musk ana fedha nyingi lakini hana taaluma ya maswala ya mitandao ya kijamii hivyo basi ni vizuri angejiondoa katika nafasi ya mkurugenzi wa kampuni hiyo na kumwachia mtaalamu aliyebobea katika maswala ya mitandao ili anusuru kampuni hiyo ya X kwasababu ipo mbioni kuondoka machoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii
Ungesema kuhusu JF na maximo mkuu wao hata sekunde Uzi wako ungeondolewa
 
Wewe ujuzi wako ni upi bwashee 🤣
Anasikiliza haters w kimarekani. Wazungu sio wote wema kuna wenye chuki ya ajabu. Elon alianza kuchukiwa USA mapema tu alipoanzisha miradi yake na kupingwa kuwa ni ya kijinga leo ni LIDUDE LILILO NA MOMENTUM YA AJABU hakuna kenge anaweza kumsimamisha huyu mtu kwa sababu miradi yake anafadhili mwenyewe pamoja na watu wenye maono ya mbali
Ni mtu atakaekuja kusomwa ktk vitabu miaka na miaka. Mtu amegusa mpaka akili ya binadamu kiiunganisha na mifumo ya electronics. Ni blessed of blessed of blessed! Kwa kizazi chetu hakuna kama Elon, ameweza kujua kila kitu ktk technolojua, he us alien. Propagabda za kijinga zitakwama dhidi yake.
Elon anafaa kuwa role model sio viceversa!
 
Elon ni mtu na nusu, hakuna kama yeye dunia hii, huyu ndio Isaac Newton wa kizazi hiki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom