Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki

Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki

Hizi ID mpya ambazo zinaonesha pasi na shaka yeyote kwamba mwenye ID hii tunaye hapa muda mrefu kwa ID nyingine huwa nakosa majibu ya malengo ya watu, na nyingi ya ID hizi zimefunguliwa mwezi Februaly, na jinsi ya kugunduwa malengo halisi ya watu hawa hutoweza hata siku moja kukutana nao jukwaa lingine zaidi ya hili jukwaa la siasa!! why?....

user-online.png
Mussa Wangota

Today 15:44
#229
Junior Member Array


Join Date : 27th February 2012

Posts : 6
Rep Power : 302


Kaka Matola usiwe na wasi wasi juu ya uwepo wangu hapa. Ni kweli mimi ni mzoefu hapa jukwaani na kwa kuwa huu ni wakati wa kujivua gamba na langu pia nimelivua ili kusogea hatua moja mbele katika mapambano.

Usifunge milango kwa watu kujivua gamba mkuu, kuna haja ya kuibadili jamii forum ili tukutane ana kwa ana kama walivyo akina Zitto Kabwe, Slaa, Mwigulu, Nape, Mnyika na n.k. .Vile vile si lazima ama haijalishi kumpata Matola halisi ama nick name hapa jamvini ila uzito wa hoja mkuu.

Kuhusu kutokuonekana kwenye sehemu nyingine nadhani hapa hujawa sahihi, kila mtu ana jukwaa lake kama ambaye anapenda kuwa jukwaa la "mapenzi", "udaku" ndivyo hivyo na sisi wengine tunapatikana hapa Mkuu.
 
Iwapo yaliyosemwa ni kweli basi hali ya nchi ni tete. Askofu gani huyu anayetajwa? Kwa nini wasiwakamate watoa fedha sawa na wasambaza fedha? Hawa takukuru ni genge jingine la uhalifu nchini. Sina imani nao hata kidogo kwani baada ya mida mtasikia waliokamatwa wameachiliwa kwa uchunguzi au ushahidi wa takukuru haujitoshelezi. Wizi mtupi!

Kweli hakuna atakayeuona ufalme wa Mungu, kama wale wanaojiita watumishi wa Mungu ni mawakala na makuwadi wa ufanisi.
 
Mkuu Mkandara binafsi mimi naheshimu sana michango yako hapa jamvini, wewe ni sehemu ya watu makini hapa JF, lakini hili la kwamba Rais ajae ni lazima awe mkristo halina mjadala ndani ya CCM na Lowasa analijuwa hili vyema, labda vyama vya upinzani ndio havitoendeshwa na utashi huu, lakini Mwislamu yeyote mjanja na anaeona mbali tayari ameshaujuwa ukweli huu na ndio maana katika sarakasi za urais ndani ya CCM husikii majina ya kiislamu, hili liko wazi, na ndio maana hata Bernad Membe baada ya kugunduwa kwamba haesabiki kama mkristo bali Mwislamu nae ameshanawa mikono mapemaaa!!
Nakuomba unisome vizuri, nimesema hivi sielewi sababu za Lowassa kuyatumia makanisa ktk kampeni zake -pengine blaa..blaa, hili ni swala la wakristu kulishtukia kwamba huyu mtu sio binadamu ni nusu mnyama.

Hili sio swala la vyama, CCM hawana Udini wala Chadema hawana udini isipokuwa wamo watu wenye dini zao na wanatanguliza dini zao mbele ya mahusiano kisiasa. Kama katiba isemavyo Nchi haina dini bali watu wake na ndivyo hivyo ukiona watu wanatofautiana ktk maswala na kuleta udini haina maana nchi nzima ama vyama ni vya kidini.

Kuhusu nani atasimama CCM hatujui wala sio hoja isipokuwa tunayemzungumzia hapa ni Lowassa na anafanya nini na pengine nikwambie kwamba kuna baadhi ya vitu navifahamu. Kama kweli wewe unaheshimu michango yangu nakuomba unisome vizuri, jiulize imekuwa vipi Mkandara siku hizi kamshikia bango Lowassa na Udini, ukiweza kunielewa na kwa nini napiga vita watu wanaomshabikia Lowassa basi hutatatizwa na hoja zangu.

hili, sio swala la waislaam/Wakristu hata kidogo, isipokuwa kumshabikia Lowassa bila kujua malengo yake na itakuwa makosa kwangu kuto watahadharisha. Nayajua malengo yake na ndio maana naandika hapa.
 
Mkuu siku hizi mawazo makubwa kama haya hapa sio mahali pake, mmetengewa ukumbi wenu maalum unaitwa FIKRA PEVU.

Hapa habari zinazotakiwa siku hizi ni Lowasa Fisadi, Chadema gogoro lanukia, n:K, lakini mambo uliyoyaongea ni mazito kiasi kwamba hawajui kama tawala za duniani zinapangwa na Freemassons, so what if kama Lowasa ni Agent wao? who to stop? Na kwa nini Dr Slaa mpaka leo haijulikani alipata kura ngapi! na hata Kikwete mwenyewe kama kweli aliongoza kwa kura halali nae hajui alipigiwa kura ngapi!!

Ni kwa nini Kikwete awe Rais wa kwanza kutoka Africa kuonana na Obama? na nina uhakika mavuvuzela mengi humu hajajui kwamba Richmond sasa hivi ndio Symbion Power mali ya Wamarekani, je kuna kiherehere yeyote aliwahi kuhoji uharari wa mkataba huo?
Aiseeeh ! Mie nilipomuona Hilary Clinton anafungua Symbion, aka Dowans aka Richmond, nikajua kilichobaki nikuvaa mabomu !
 
Mtoto wa Marehemu Sumari nasikia kashinda kwa kishido Chadema-Kata JF vichwa vinauma.
 
Mkuu Matola,

Mbona nilishamsifu sana.

[1] Nilimpongeza aliposhinda ubunge wa Arusha.

[2] Nilimpongeza kwa kununua kiwanja kwaajili ya ujenzi wa Hospital.

Mkuu wangu tafuta hizo threads utakumbana na pongezi zangu kwa Mheshimiwa Lema lakini akifanya ujinga sichelewi kusema,kulalamika,kukemea na kuelekeza.


Kama maelezo yako haya yote yanatoka ndani ya nafsi yako je uko tayari siku kumsifia Godbless Lema kwa jambo zuri atakalofanya?
 
Mtoto wa Marehemu Sumari nasikia kashinda kwa kishido Chadema-Kata JF vichwa vinauma.
Huu ni ushindi mkubwa kwa Lowasa na ni onyo kwa wale wote wanaounderestimate nguvu za Lowasa ndani ya CCM. acha kukurupuka hili haliwahusu CHADEMA bali ilikuwa ni vita kati ya kamati kuu ya CCM dhidi ya Lowasa na amewagaragaza, sasa ni wakati muafaka wa JK kujiandaa kumuachia uenyekiti wa chama Lowasa. many more to come!!
 
Mtoto wa Marehemu Sumari nasikia kashinda kwa kishido Chadema-Kata JF vichwa vinauma.
Kama ungelijua tu yanayotayarishwa kwa Taifa la kesho sidhani kama ungekuwa na fursa hata ya kusema uloyasema kwa shangwe.
 
simshangai lowasa maana naishangaa zaidi ccm maana hata mr presdent ana kasha ya rushwa na kumsingizia mahalu.
sasa wanaumbuana au wanashushiana heshma!
 
Hii serikali na TAKUKURU yake ilishakiri kumshindwa EL.
Huyu jama ni hatari sana kwa hii nchi.
 
Hivi mpaka dakika hii bado kuna uhalali wa hii Thread kuitwa eti Lowasa aumbuka Arumeru Mashariki?
Kama ni habari za uhakika zilizopatika kwamba Sioi Sumari Ameshinda kwa kishindo, basi hii thread isomeke hivi:
LOWASA KIDUME, AIGARAGAZA KAMATI KUU YA CCM, MSEKWA ATOKEA MLANGO WA UWANI, CHILIGATI AGOMA KUTOA PRESS RELEASE, HUKO FACEBOOK NAPE NNAUYE NAE AGOMA KU UPDATES STATUS ZAKE ZA MBWEMBWE.
 
Mkandara neno zito sana hili, ila/but/lakini;
....

In other words tukiingia ndani zaidi Kikwete kwekwa pale na wamarekani piga ua atakayekuja atawekwa na hao hao wamarekani ambapo Kikwete hatakuwa na ubavu wa kumfanya lolote

Food for thought! Nimeisikia sana kauli ya aina hii. Kwa Waafrika wenzetu wanaozungumza kifaransa inasemekana hakuna anayepata urais au hata uwaziri bila Paris kuweka "tiki". Hivyo, yaelekea mijadala yote tunayoendesha hapa kuhusu hatma ya uongozi wetu tunachangamsha bongo tu; hatuna uwezo wa kuamua "matokeo halisi". Binafsi siamini sana katika hili. Nachojua wakishindwa kumweka mtu wao, basi hutafuta kumtumia yeyote aliyefanikiwa kukalia kiti. Atatumika kiasi gani itategemea na jeuri yake na mikakati yake ya kucheza na wakubwa wote (super powers).

Nikirudi kwenye mada, hao wote: JK, EL, RA, BM, n.k. ni waarabu wa Pemba. Hivyo, hakuna cha kusherehekea (no joy) katika kuanguka au kufanikiwa kwa yeyote katika genge hilo. Mjadala halisi ni kuhusu sisi wenyewe kwa ujumla wetu. Hivi kweli tu wakweli kwa nafsi zetu? Si kwamba tumegubikwa na unafiki angamizi kwa taifa? Tunajidai tunaka watu safi, wazalendo na wenye nia ya dhati ya kuendeleza nchi, lakini kwenye sanduku la kura wengi tunaishia kuangalia maslahi binafsi tena ya muda mfupi. Wako wenye kuishia kwenye pilau, t-shirts na vitenge, wengine kwenye vyeo, tenda na kukwepa kodi, na waliokubuhu kwenye kuuza nchi kabisa (migodi, ardhi, uraia ...).

Huwa naamini sana katika kauli inayohusishwa na Alexis de Tocqueville kwamba "people get the government they deserve"! Kule tu kuipa CCM "gerentii" ya kuwa madarakani miaka yote hii ni kielelezo cha uhakika kuhusu utashi wetu kwa ujumla. Kwamba mtu kama Lowasa anapata kurasa zote hizi za mjadala kuchambua ubora wake (au la) kama rais mtarajiwa ni changamoto jingine jinsi tulivyobanwa kifikra kuhusu machaguo tuliyo nayo. Eti JK ameamua kupambana na mafisadi kwa dhati! Hata hao marekani wenyewe huwa wanatusaidia tu kukamilisha ujinga wetu katika kuchagua viongozi!
 
Matokeo ya mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM huko Arumeru yanaonyesha jinsi mtu huyu alivyo hatari pamoja na ushahidi wote kama huu -Na bado!
 
Masters of dirty deals and ploys at WORK against Arumeru people!!!! To the Arumerus... Vote for what you stand FOR if you don't want to regret in future!
 
Hivi mpaka dakika hii bado kuna uhalali wa hii Thread kuitwa eti Lowasa aumbuka Arumeru Mashariki?
Kama ni habari za uhakika zilizopatika kwamba Sioi Sumari Ameshinda kwa kishindo, basi hii thread isomeke hivi:
LOWASA KIDUME, AIGARAGAZA KAMATI KUU YA CCM, MSEKWA ATOKEA MLANGO WA UWANI, CHILIGATI AGOMA KUTOA PRESS RELEASE, HUKO FACEBOOK NAPE NNAUYE NAE AGOMA KU UPDATES STATUS ZAKE ZA MBWEMBWE.
Watu walikuwa wakishangilia Lowassa kaumbuka nikawambia labda hawamjui Lowassa, kuna mwingine simkumbuki akaongeza Lowassa anaweza kuongoza CC kwa remote control na kweli imejidhihirisha jamaa hata hayuko kwenye ukumbi lakini ameugaragaza uongozi karibu wote wa juu kasoro m/kiti wake.
 
Back
Top Bottom