Nduguyetu joseph Peter, inaonekana wewe umebobea upotoshaji na umebobea Kabisa. Mimi naomba ni toe facts Kama zilivyo na nipo tayari kuwa challenged na mtu yoyote. Kwa sasa hivi nipo nje ya ukumbi wa mkutano wa kupigia kura na wajumbe wameshaingia wote wakiwa wamependeza na mashati yao ya kijani na njano na nimefurahia Sana kumuona kamanda wangu Elirehema Kaaya akiingia ukumbini kwa nyuso ya furaha kabisa hata baada ya kupigwa msukomsuko na maafisa wa takukuru.
1. Elirehema Kaaya alikwenda Dsm kushirki vikao vya secretariat na kamati kuu akiongozana na ndugu Kisali sarakikya ambaye name anapigiwa kura leo, walikaa wote Dsm na baada ya kikao wakafanya safari ya kurudi wote arusha. Ni mjumbe halali wa mkutano wa leo na Jana wakati amekamatwa alikuwa amekaa kwenye grocery na wapiganaji wake wakibadilishana mawazo, hakukuwa na mambo yoyote ya pesa. Elirehema anajimudu kiuchumi na ninategemea ana uwezo Kabisa aw kulipia nauli zake, lakini Kama kuna wa kumtuhumu kumsaidia usafiri labda iwe sarakikya, lakini bado siamini hivyo.
2. Ezekiel Mollel ni katibu wa vijana wa uvccm monduli na ni mkazi na mwenyeji wa wilaya ya arumeru, uvccm mkoa kwa kupitia katibu wake wa mkoa Mpokwa wanashiriki marudio haya ya kura Kama jumuiya zingine zote za mkoa kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu tar 1 april. Huyu alishikwa akiwa peke yake anapanda pikipiki na inasemekana maafisa walikuwa na kijani anaitwa ammo akiwaonyesha watu wa kukamata, kwenye kundi hilo hilo walikuwepo makatibu wa wilaya zote za mkoa na katibu mwenyewe wa mkoa, napa unaona u-monduli ulitumika ili kwa Mara nyingine tena tuliingize jina la lowassa kwenye midahalo ya CCM. Mawasiliano yake na simu siwezi kuwa na uhakika, ila ukiniambia alikuwa anawasiliana na lowassa, hiyo ni PUMBA.
Tukirudi kwenye mchakato wenyewe wa kura za leo, inasikitisha na inatia aibu kubwa sana, ningekuwa mimi ndiyo Huyo kijana anaitwa sioi ningejitoa. Jana Mkuu Wa wilaya aliwaita madiwani wote wa arumeru mashariki na kuwaambia msimamo wa serikali ni ssarakikya, na ikatokea vurugu kubwa na polisi wakaweka madiwani wengine chini ya ulinzi. Tujiulize kwanza kwanini huu uchaguzi unarudiwa Leo? Hamna Majibu ya kuridhisha, na ukijiuliza tena ni watu gain walipinga matokeo ya sioi kwenye vikao? Unapata majibu ni wateule wote wa serikali na chama, sishangai kusikia haya ya takukuru leo ila inasikitisha Sana. Demokrasia ya Kweli iko wapi? Ningefikiri kazi ingekuwa kusimamia uchaguzi wa kweli na haki, na wananchi wapate fursa ya kuamua wawakilishi wao.
Namalizia,baada ya kamati kuu kuamua uchaguzi kurudiwa, wazee wawili wa kamati kuu walimfuata Sioi kumshauri ajitoe kwasababu sababu za yeye kukatwa jina hata Kama akishindwa zimeshaandaliwa na Sioi akawajibu kwamba sivyo ambavyo nimelelewa na wazazi wangu, nilifanya sala Kuomba baraka za marehemu baba, ningependa huko aliko alone kijana wake sikumuangusha na nilismamia ninachokiamini mpaka mwisho whether win or lose.
Tusubiri tuone cinema hivi inaishia wapi.