TANZIA: Thomas Mollel maarufu 'Askofu' afariki dunia jijini Dodoma akihudhuria kuapishwa kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,781
5,205
Mfanyabiashara maarufu wa madini nchini Tanzania, Thomas Mollel maarufu kwa jina la Askofu amefariki dunia jana usiku Jumatatu Mei 20, 2019 jijini Dodoma.

Alikwenda Dodoma kushuhudia kuapishwa kwa mbunge mteule wa Arumeru Mashariki (CCM), Dk John Pallangyo.

IMG_20190521_135308.jpg

Mollel ambaye mwaka 1995 alipata umaarufu baada ya kugawa fedha akiwa ghorofani huku wananchi wakiziokota chini, amefariki dunia saa tano usiku, muda mfupi baada ya kutoka kuoga akiwa na mkewe.

Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Meru, Joshua Hungura amesema kabla ya kifo chake, Mollel alikuwa mzima na jana saa nne usiku walikula pamoja chakula cha jioni.

Amesema Mollel ambaye pia alikuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Meru na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya wilaya hiyo, siku za nyuma alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu.

"Lakini tulitoka salama Arusha alikuwa mzima kabisa akifurahia kuja kuapishwa mbunge wetu na alifariki ghafla akiwa ametoka kuoga baada ya kudondoka mlangoni,” amesema

Amesema mwili wa Mollel unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Arusha baada ya Pallangyo kuapishwa.

"Tumeshauriana ni vyema sote kama tulivyokuja turudi na mwili wa mpendwa wetu na taratibu za mazishi zitatolewa baadaye,” amesisitiza.

Enzi za uhai wake, Mollel alikuwa pia mchimbaji maarufu wa madini ya Tanzanite na aliwahi kumiliki timu ya mpira wa miguu ya Pallson iliyowahi kushiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Pia, amewahi kuwa diwani wa Mbughuni.
 
Yeah neh wote sisi tutaonja mauti,ILA utakumbukwa kwa ulichokifanya katika siku zako za uhai,huyu mh.wakati moto wa mageuzi mwaka 1995 unawaka naye alijiunga na moto huu,mh.AL Mrema alikubalika sana na marehemu,wapi na why aliamua kugeuka yeye mwenyewe anajua na ilikuwa haki yake,ila pamoja na haki hii kuna kitu kinachoitwa USALITI ni vema ukakiogopa sana,but time ni mwamuzi wa haki,jirani zetu hapo Angola wamekubaliana kuwa nchi ile ni yao wote na moja ya mambo yanayofanyika sasa ni kuufukua mwili wa shujaa Jonas Savimbi(kwangu mimi ni shujaa)na kwenda kuzikwa kwa heshima nyumbani kwake,sisi bado tumo kwenye wimbi la bado kutokuzikana,kuchafuana,kutekwa na kuumizwa,kuuliwa,kisa TOFAUTI zetu za kiitikadi,but ipo siku nasi tutakuwa kama Angola now.
 
Ok kumbe alikuwa mjumbe kamati kuu ccm arumeru.....okkk

Ova
Bila kuwa Chukua Chako Mapema utamilili mgodi au chochote? Niliiashaulizwa nikiwa NY wakati najiandaa kurudi home kwamba vipi una kale kakaratasi ka kijani? Nilijibu sina chama na sitakuwa na chama ila nitatetea ukweli sababu kazi yangu hainiruhusu kuwa na itikadi. Nilishasepa tena maana nisingehimili vishindo vya huko.
 
Sema wameanza kulamba matapishi baada ya binti wa kiongozi wao kuwekwa lupango.
 
Bila kuwa Chukua Chako Mapema utamilili mgodi au chochote? Niliiashaulizwa nikiwa NY wakati najiandaa kurudi home kwamba vipi una kale kakaratasi ka kijani? Nilijibu sina chama na sitakuwa na chama ila nitatetea ukweli sababu kazi yangu hainiruhusu kuwa na itikadi. Nilishasepa tena maana nisingehimili vishindo vya huko.
Mzee unaongea na cm? Au ndoto?
 
Huyu jamaa namfahamu mmiliki wa Pallson hotel Arusha. Alisumbua sana Arusha enzi hizo na pesa za madini.
Sijui kwa nini aliamua kuiacha hotel hiyo ya Pallsons iwe katika hali iliyonayo bila hata kuiboresha. Haivutii kabisa.
 
Back
Top Bottom