Mzee acha kutapa tapa tuko kwenye vitendo vinavyoashiria rushwa ambavyo vimenaswa na taasisi yetu ya kupambana na rushwa tanzania,taasisi ambayo lowassa akiwa nguvu iliwahi kujaribu kumsafisha alipopata ile "ajali" yake ya kisiasa na ni taasisi hiyo hiyo ndio imewadaka watu ambao baada ya mahojiano jina la lowassa limejitokeza kuwa maarufu miongoni mwa waliohojiwa...
Kuhusu kumfanisha jz na lowassa naona unachanganya mambo,lowassa tunaweza kumfananisha na julius malema ambae juzi kamati kuu cc ya ANC Imemvua uanachama;
Kwa nini lowassa wanafanana kimtindo na Malema?
Ni hivi,Julius Malema na genge lake ndio waliofanikisha JZ kuwa pale alipo,yani rais wa nchi na mwenyekiti/rais wa ANC,kutokana na hilo Malema licha ya umri wake mdogo aliogopwa na kila mtu ndani ya ANC na serikali,Malema akavimba kichwa akajiona mkubwa kuliko chama,mkubwa kuliko rais.Kila mtu ndani ya chama akamlaumu sana JZ kwa kumuendekeza malema.
Baada malema kuhisi zuma anamuogopa akaanza kutishia eti kumng'oa uenyekiti ANC,akaanza kubishana nae na kumkosoa hadharani,zuma akaona huu sasa upuuzi akaamua kupambana nae ka tika mpambano uliomalizika juzi kwa malema kufukuzwa uanachama na cc ya nec.
Nikirudi kwa lowassa huyu na genge lake ndio inasemakena wamemfikisha jk hapo alipo,lakini baadae lowassa akataka awe mkubwa kuliko rais awe mkubwa kuliko mwenyekiti wa chama,yakampata yaliyompata kwanza akaondoka serikalini bila kupenda,baada ya hapo lowassa akataka kuitikisa serikali,akataka kukitikisa chama jk akalaumiwa na kila m2 ndani ya chama kwa kumuendekeza lowassa ikasemekana eti mwenyekiti anamuogopa yeye na genge lake.Lowasa kichwa kikavimba akaanza kufikiria kumuondoa mwenyekiti madarakani kama malema alivyojaribu kufikiria kwa zuma,mwenyekiti akaona huu u.p.u.u.z.i. huyu mtu nambeba kwa mbeleko ya chuma ananiona mimi m.ji.n.g.a. sio???akaanzisha msamiati kwa kujivua gamba...kwanza yakafanyika mabadiliko makubwa kwenye sekretariet yalimzoa mzee makamba na timu yake wakaingia kina nape,kama hiyo haitoshi Lowassa akangolewa cc na sasa saula lake la kuvuliwa gamba liko ndani ya cc ambamo yeye hayumo,ikumbukwe ni cc ya ANC ndiyo iliyomvua gamba Juliua Malema mtu amabae ndio anafanana fanana na lowassa katika style yao ya kufanya siasa.
J e cc itamfanya nini lowasa??tusubiri tuone wakati huo huo lowassa anatakiwa kupima kati ya ubunge na u nec kipi kinamfaa ili aachia kimojawapo....