Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki

Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki

Kaaya unahangaika nini, ulipata kura zako 205, ungerudi zako Mwanza kuendelea na kazi zako, ona sasa na unadhifu wako wote umeishia lumande.
Mbona Lowana na huyo freddy hawaitwa na takukuru ili wahojiwe, kesi gani hii ya upande mmoja?
 
Mh! Sidhani. Hauna "mandate" ya kutusemea WATANZANIA woote. Halafu, AruMeru wana vigezo vyao kwenye mambo haya ya kuchaguana. Chama gani mgombea anatoka sio mojawapo ya vigezo hivo.
Na sidhani vile vile kama una Mandate ya kuwapangia vigenzo vya aina ya mgombea wanayemhitaji watu wa Arumeru.
 
Nilishasema, hakuna uchaguzi unaowashirikisha wanaCCM wasihonge. Na huu ni uchaguzi wa wao kwa wao. Vipi ule wa kupambana na wapinzani!?
 
Tupatieni kidogo WASIFU wa Joshua Nassari.
Waulize wanachama wa CHADEMA waliompitisha kwa kura nyingi ndio wanaojuwa wasifu wake, au kama tume ya Uchaguzi ina data base nzuri basi wasifu wake uko pale.
 
Bila shaka unamzungumzia Papa King mmiliki wa Tripple A,Mwarusha mjinga huyu ndiyo mweka hazina na mchangishaji mkuu wa fedha za rushwaa hasa wakati wa uchaguzi.Papa King alimponza Dr Batilda na sera za ukabila eti Arusha ni ya waArusha.(umenikumbuka Ditopile kipindi kile Temeke Dr Mrema aliwasumbua CCM wakaja na mipasho ya alo alooo mara Mrema hajuia kula chapati mwisho wa siku mgombea wa CCM akaangukia pua)

Na wale masai wa Tripple A hawapo kwenye hiyo grupu?
 
Nduguyetu joseph Peter, inaonekana wewe umebobea upotoshaji na umebobea Kabisa. Mimi naomba ni toe facts Kama zilivyo na nipo tayari kuwa challenged na mtu yoyote. Kwa sasa hivi nipo nje ya ukumbi wa mkutano wa kupigia kura na wajumbe wameshaingia wote wakiwa wamependeza na mashati yao ya kijani na njano na nimefurahia Sana kumuona kamanda wangu Elirehema Kaaya akiingia ukumbini kwa nyuso ya furaha kabisa hata baada ya kupigwa msukomsuko na maafisa wa takukuru.

1. Elirehema Kaaya alikwenda Dsm kushirki vikao vya secretariat na kamati kuu akiongozana na ndugu Kisali sarakikya ambaye name anapigiwa kura leo, walikaa wote Dsm na baada ya kikao wakafanya safari ya kurudi wote arusha. Ni mjumbe halali wa mkutano wa leo na Jana wakati amekamatwa alikuwa amekaa kwenye grocery na wapiganaji wake wakibadilishana mawazo, hakukuwa na mambo yoyote ya pesa. Elirehema anajimudu kiuchumi na ninategemea ana uwezo Kabisa aw kulipia nauli zake, lakini Kama kuna wa kumtuhumu kumsaidia usafiri labda iwe sarakikya, lakini bado siamini hivyo.

2. Ezekiel Mollel ni katibu wa vijana wa uvccm monduli na ni mkazi na mwenyeji wa wilaya ya arumeru, uvccm mkoa kwa kupitia katibu wake wa mkoa Mpokwa wanashiriki marudio haya ya kura Kama jumuiya zingine zote za mkoa kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu tar 1 april. Huyu alishikwa akiwa peke yake anapanda pikipiki na inasemekana maafisa walikuwa na kijani anaitwa ammo akiwaonyesha watu wa kukamata, kwenye kundi hilo hilo walikuwepo makatibu wa wilaya zote za mkoa na katibu mwenyewe wa mkoa, napa unaona u-monduli ulitumika ili kwa Mara nyingine tena tuliingize jina la lowassa kwenye midahalo ya CCM. Mawasiliano yake na simu siwezi kuwa na uhakika, ila ukiniambia alikuwa anawasiliana na lowassa, hiyo ni PUMBA.

Tukirudi kwenye mchakato wenyewe wa kura za leo, inasikitisha na inatia aibu kubwa sana, ningekuwa mimi ndiyo Huyo kijana anaitwa sioi ningejitoa. Jana Mkuu Wa wilaya aliwaita madiwani wote wa arumeru mashariki na kuwaambia msimamo wa serikali ni ssarakikya, na ikatokea vurugu kubwa na polisi wakaweka madiwani wengine chini ya ulinzi. Tujiulize kwanza kwanini huu uchaguzi unarudiwa Leo? Hamna Majibu ya kuridhisha, na ukijiuliza tena ni watu gain walipinga matokeo ya sioi kwenye vikao? Unapata majibu ni wateule wote wa serikali na chama, sishangai kusikia haya ya takukuru leo ila inasikitisha Sana. Demokrasia ya Kweli iko wapi? Ningefikiri kazi ingekuwa kusimamia uchaguzi wa kweli na haki, na wananchi wapate fursa ya kuamua wawakilishi wao.

Namalizia,baada ya kamati kuu kuamua uchaguzi kurudiwa, wazee wawili wa kamati kuu walimfuata Sioi kumshauri ajitoe kwasababu sababu za yeye kukatwa jina hata Kama akishindwa zimeshaandaliwa na Sioi akawajibu kwamba sivyo ambavyo nimelelewa na wazazi wangu, nilifanya sala Kuomba baraka za marehemu baba, ningependa huko aliko alone kijana wake sikumuangusha na nilismamia ninachokiamini mpaka mwisho whether win or lose.

Tusubiri tuone cinema hivi inaishia wapi.

Mkuu KGBtz, na wadau wengine,

Mimi nadhani Joseph Peter si mtoposhaji kwa bandiko lake aliloliweka hapa jukwaani, kwani kwa kiasi kikubwa taarifa iliyo kwenye bandiko lake imethibitishwa na Afisa Mwandamizi wa TAKUKURU katika taarifa ya habari ya saa 7 mchana huu.

Source: TBC1 Habari [Dira ya Mchana]
 
Tatizo lililopo ndani ya makundi ya CCM; Ni sawa na wachimbaji wawili ndani ya shimo la choo wanachafuana ndani kwa ndani baada ya mmoja kumchafua mwenzake anafikiri yeye akitoka nje ataonekana msafi.

Badala ya kundi moja kujisafisha ili adui wao aonekane mchafu, wanamchafua adui ili wao waonekane wasafi bila kwanza wao kujisafisha hivyo kuendelea kuonekana wachafu nje ya CCM.
 
Takukuru Leo wameamua kumgeuka Edward Lowasa na vibaraka wake katika marudiano ya uchaguzi wa Arumeru. Katika sakata Hilo katibu wa UVCCM wilaya ya Monduli ndugu Ezekiel Mollel ametupwa rumande Mara baada ya kukamatwa na simu yake ilipo pekuliwa na kukutwa na mesej alizokuwa Akiwasiliana na Lowasa kuhusu kuchukua hela kwa askofu na mathius manga kwa Lengo la kwenda kuwahonga wajumbe wa arumeru Mashariki.

Katibu huyo amekiri kupewa maelekezo hayo na Lowasa na kuomba asamehewe kwa kuwa Lowasa ni kiongozi mkubwa yeye asingeweza Kuwa na ujasiri wa kumkatalia. Hadi wakati huu Ezekiel Mollel na Askofu wapo rumande.

Pia katika tukio lingine Fred Lowasa amethibitika kumhonga ticket ya ndege Elirehema kaaya ili amsaidie Sioi aweze kushinda. Kwenye simu ya elirehema Kaaya zimekutwa mesej Kuwa nakulipia ndege pamoja na kukupa lile fungu la kuwapelekea wajumbe. Kwa ushahidi huu hadi sasa elirehema Kaaya yupo rumande.

Wakati wowote mambo haya yatapelekea wahusika kupelekwa mahakamani.

Wana Arumeru mashariki wafanye uchaguzi kwa amani na utulivu na tena wasiwe na hofu yoyote.

Undugu wenu utawaponzeni enyi Lowassa senior na Junior!
Mkwe na shemeji...mnataka taifa zima mlitawale? Huyo Sioi si ni mkwe wenu ..inatosha.
Waachieni wengine nao washiriki katika uongozi.
Diversity ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
 
Kama kweli taarifa hizi zina mashiko then nakubali kwamba JK is the silent killer. EL out of the game.
 
Hapo kwenye RED ndipo watu wengi humu huwa wanakutilia mashaka, kama swala ni mtu wa kaskazini kuwa Rais, hakuna hata mmoja mwenye sifa zaidi ya Dr Wilbroad Slaa, kwahiyo basi kama shida yako ni mtu wa kaskazini kuwa Rais nakuomba rasmi kuanzia sasa uanze kumfanyia kampeni shujaa wetu Dr Slaa. CCM ni chama ambacho kimeshakufa hakina tena uhalali wa kuendelea kuitawala Tanzania, miaka 50 waliyopewa sasa imetosha.

inatia hasira sana mkuu matola, mi nadhani mashabiki wa Lowasa wanapewa zaidi ya pesa, pengine jamaa anawapa vitamu zaidi ya tunavyodhani, haiwezekani ukawa na roho chuma kiasi hiki
 
Pamoja JF kujulikana kama Home of Great Thinkers lakini nasikitika sana inapotumiwa kama sehemu ya propaganda
Sitaki kusema mengi lakini sijona hata mtu mmoja kujaribu kudadisi hii habari inaukweli kiasi gani, kila mtu anrukia kwenye hitimisho tu
 
Hii ni kama kawaida Chama cha Wasanii na afanyaye usanii zaidi ndiye anayeonekana bora zaidi.Msanii bora kati ya wasanii na Chairman Msanii then sera zote ni usanii
 
sasa kama watu wanahonga hivyo kwaajili ya kuupata ubunge inakuwaje Anna makinda na Makinda yake wanasema ubunge ni umaskini?
Wana Arumeru nawapa uashauri wa bure mkihongwa chukueni wakati wa kuchagua chagua ambaye hajatoa rushwa.
 
Afu uyo katibu wa uvccm monduli ezekiel mollel ni darasa la saba mkazi wa ngaramtoni,chadema 2songe mbele wacha magamba wajizike.mamvi ameisha
 
Ezekiel huyo katibu wa uvccm jimboni kwa mamvi ni darasa la saba
 
Back
Top Bottom