Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Mnakuja jukwaa hili kufanya nini kama uwezo wa kuchangia ni mdogo,kwanini usikae kimya tu na kuwa msomaji zaidi ili ujifunze kwa wengine.Unatia aibu,rudi kwenye Jukwaa la siasa ukachangie kwa style hiyo ya vijimaswali vya "unalipwa shilingi ngapi?" Huku waachie real GT .
Jifunze kusoma mtiririko wa post vizuri, ndio ukoment.
Umedandia treni kwa mbele, ona unavyojidhalilisha sasa!
unajua maana ya propaganda lakini?
 
..lakini mimi HRC kanishangaza sana jinsi alivyojitumbukiza ktk matatizo haya ya e-mail server.

..kuna Republicans, kwa miaka mingi,wanafuatilia kila anachokifanya, na wanatumia kila mbinu kumuangamiza kisiasa.

..Sasa sijui kwanini HRC alishindwa kutambua kwamba hiyo private e-mail server itamletea
matatizo ktk harakati zake za kisiasa.

..misukosuko anayoipata HRC ni ya kujitakia mwenyewe, hakuna mwingine wa kumlaumu.
 
Mkuu JokaKuu siyo kwamba kajitakia huo ndo udhaifu alionao. Wapinzani wake wanaposema haaminiki hiyo ndo maana yake.
 
Mkuu JokaKuu siyo kwamba kajitakia huo ndo udhaifu alionao. Wapinzani wake wanaposema haaminiki hiyo ndo maana yake.

..unaweza kusema haaminiki ikiwa ana tabia ya kutenda uhalifu.

..huyu mama angekuwa mhalifu, kwa jinsi Republicans wanavyomchimba, tena kwa miongo kadhaa, basi lazima angepatikana na hatia ktk kosa fulani.

..HRC siyo waziri wa kwanza kuwa na private e-mail server. Lakini HRC alipaswa kutambua kwamba hao waliomtangulia hawawindwi na wapinzani wao kama inavyofanyika kwake.

..kwa hiyo mimi kwa mtizamo wangu HRC hakupaswa kuwa na private e-mail server.

..Tatizo lingine la HRC ni kwamba she is TOO TOUGH and TOO SMART.

..Sifa hizo mbili zinamfanya akose ile huruma na heshima ambayo wanawake hupewa.

..kwa mfano ungetegemea wapiga kura wawe excited kumpigia kura mgombea mwanamke wa kwanza ktk historia ya Marekani. lakini hali ni tofauti kwasababu HRC is being judged/treated as HRC first and foremost and rarely as a female politician or woman.

..
 
..jambo lingine linalonifurahisha ni TRANSPARENCY/UWAZI ktk zoezi zima la uchaguzi wa Marekani.

..vyombo vya habari na taasisi mbalimbali wanafuatilia uchaguzi kwa karibu na kutoa uchambuzi wao.

..sasa turudi hapa Tanzania. Kwanini hatuigi mazuri toka kwa wenzetu wenye uzoefu wa muda mrefu?

..labda tungeanza kwa kudai uchaguzi wetu uendeshwe kwa uwazi zaidi. Hilo likifanyika kutapunguza yale mabishano ya kusimama mita 100 toka kutoa cha kupiga kura kusubiri matokeo.

..lingine linaloharibika chaguzi zetu ni ushabiki na propaganda. Kuna upotoshaji mkubwa unafanyika ktk siasa zetu.
 
..lakini mimi HRC kanishangaza sana jinsi alivyojitumbukiza ktk matatizo haya ya e-mail server.

..kuna Republicans, kwa miaka mingi,wanafuatilia kila anachokifanya, na wanatumia kila mbinu kumuangamiza kisiasa.

..Sasa sijui kwanini HRC alishindwa kutambua kwamba hiyo private e-mail server itamletea
matatizo ktk harakati zake za kisiasa.

..misukosuko anayoipata HRC ni ya kujitakia mwenyewe, hakuna mwingine wa kumlaumu.

Mkuu JokaKuu uko sahihi kabisa.

Lakini kwa upande mwingine nafikiri FBI ndio walichemsha kutoka mwanzo walipokuwa wanachunguza sakata hili. Mara ya kwanza walifanya uchunguzi na kufikia hitimisho kwamba ijapokuwa kulikuwa na uzembe fulani kuhusiana matumizi ya server binafsi lakini hakukuwa na kosa lolote la jinai la kumshitaki Clinton... na hii ndio iliyompa Clinton uhai kwa kiasi kikubwa na ndicho amekuwa akisisitiza kwenye kampeni kwamba ameshachunguzwa na hajakutwa na hatia yoyote. FBI wangefanya uchunguzi wa kina wakati ule na wakakuta Clinton ana hatia basi uchaguzi huu ungekuwa na mwelekeo tofauti kabisa.

Kitendo cha FBI kuanzisha uchunguzi kwa mara ya pili huku zikiwa zimebaki siku chache tu kabla ya uchaguzi ndio imeleta maswali mengi kwa kambi ya Clinton wakimuona Comey kuwa amefanya hivi kwa shinikizo la wanasiasa kutoka Republican. Mbaya zaidi FBI wenyewe sasa wamekiri kwamba uchunguzi huu hauwezi kukamilika kabla ya uchaguzi kitu ambacho kambi ya Hilary wamekuwa wakishinikiza kwamba uchunguzi ukamilike haraka ili kumsafisha mgombea wao once and for all.
 
Ki-msingi FBI walimbeba clinton ktk uchunguzi wa awali ule uchunguzi wa awali ulikuwa unamuondoa moja kwa moja kuwa mgombea wa urais. Obama anataka kuwachagulia wamarekani Rais mwingine atakayefanya kazi km yeye. Trump amemshangaa kuendelea kuhangaika kumpigia kampeni HC wakati ana majukumu ya kitaifa. FBI wamegundua walifanya makosa na pengine walitaraji Democrat wasingemteua na badala yake angeteuliwa Bernie senders. HC na Obama dhambi waliyoifanya kwa Bernie senders haitawaacha na Urais hataupata!

Ataweka historia tu ya kuwa mshindani mkali,lkn kupewa majukumu ya white house hilo asahau huyu bibi. Rais ni DT piga ua...!!
 
Taratibu ndugu yangu tupunguze kidogo ushabiki... Sijui una ushahidi gani kwamba FBI walimbeba Clinton uchunguzi uliopita. Usiwalinganishe FBI na wa huku kwetu kwamba wanafanya kazi kienyeji kwa kubeba watu.

Kwenye uchunguzi huu wa FBI lazima ufahamu kwamba kinachochunguzwa sio matumizi ya email server pekee bali ni kama server hii ilitumika kufanya mawasiliano nyeti ya kiusalama kinyume na taratibu. Na ndio maana walipofanya uchunguzi mara ya kwanza walifikia conclusion kwamba ndio email server binafsi imetumika na sio sahihi lakini baada ya kuchunguza email zilizopitia mle hawajaona taarifa zozote zinazoweza kumtia hatiani Clinton.... Sasa sijui hapo FBI wamembeba vipi Clinton? Uchunguzi mpya ulioanzishwa unahusiana na emails za washirika wa Clinton kina Anthony Weiner na wanataka kuona ikiwa kama kilichomo mle kinaweza kumtia hatiani Clinton au la. Uchunguzi bado unaendelea na tayari FBI wamesema kwamba hawawezi kumaliza uchunguzi kabla ya uchaguzi! Ikiwa walimbeba Clinton mwanzoni kwa nini wasimbebe hata sasa kwa kumaliza uchunguzi haraka na kusema kwamba hana makosa?
 
Mkuu Mwalimu

Usinishambulie mimi,walioanza kulalamikia maamuzi ya FBI ya awali ni Bernie senders na Republican. Unaweza kuanza kuwalamikia hao ambao walitaka HC ashitakiwe. Mpaka leo wapenzi wa Bernie senders wanaamini hicho nilichoandika. Unachosema ww ndicho kinachosemwa na wafuasi wa HC,wanaona km James comey ameingilia uchaguzi. Alichokifanya james comey ni kitu chenye madhara kwa kampeni ya clinton lazima wa upande huo wakitetee. Pengine na ww mwalimu upo upande huo..!!
 
Bado unazidi kupotea mkuu, hapa hatuko kupiga debe upande wowote isipokuwa kuchambua hoja zilizopo mezani kutokana na matukio yanayoendelea kwenye uchaguzi. Sio kila anayepingana na wewe basi anakushambulia au ni mfuasi wa HC hapo utakuwa unapotea njia sana.

Nimekwambia FBI walifanya uchunguzi wakaona hakuna kosa linalostahili kushitakiwa. Maadamu sasa wameamua kuanzisha upya uchunguzi basi ni mpaka pale watakapomaliza kazi yao na kutoa ripoti ndipo tutakapojua ikiwa HC ana hatia ama la na si vinginevyo. Hatuwezi kuchukulia kuibuka upya kwa uchunguzi huu kwamba lazima HC atapatikana na hatia la hasha! Na ndio maana hata HC mwenyewe amesema angependa uchunguzi ukamilike haraka ili hatimaye mjadala ufungwe.
 
Mwalimu, tatizo la magode ni kwamba analeta ushabiki wa Kitanzania kwenye mambo ambayo maoni ya Mtanzania hayawezi kuleta athari zozote kisiasa nayo. Pamoja na hilo sidhani kama anapotaja neno establishment kwa nchi kama Marekani anajua anaongelea kitu gani kwa siasa za huko.

Donald Trump anapojieleza kama anti-establishment ana maana ya Washington lakini kwa magode, picha unayopata ni serikali ya shirikisho inayoongozwa na Obama. Asichojua ni kwamba Obama hana mamlaka ya mwisho Marekani kama ilivyo hapa Bongo ambapo kauli ya Magufuli moja kwa moja ni sheria.

Mathalan Obama alipoingia madarakani, yapo mengi alipanga kuyatekeleza kuendana na ahadi zake wakati wa kampeni iliyokuwa na kaulimbiu ya mabadiliko. Hata hivyo toka siku yake ya kwanza ofisini, parallel establishment iliapa kutompa ushirikiano na kuanza kufanya mipango ya kuhakikisha hafanikiwi.

Juzi tu hapa Bunge limebatilisha hatua alizochukua kwa kutumia madaraka aliyopewa kikatiba likidai aliyatumia madaraka hayo visivyo. Na hivi sasa bunge hilo limekataa kumpigia kura za kumthibitisha Jaji aliyeteuliwa na Rais Obama kuziba nafasi iliyo wazi kwenye benchi ya mahakama Kuu ya nchi hiyo.

Mfano wa pili ni juzi ambapo Mkurugenzi wa FBI Jame Comey kukataa mwongozo wa bosi wake, Mwanasheria Mkuu wa serikali aliyeteuliwa na Obama. Hivyo tunapoongelea establishment Marekani ni lazima tukiri kwanza kwamba hakuna aliye juu ya sheria nchini humo na hii ni pamoja na Rais mwenyewe.

Kama hata Rais Obama na serikali yake hawana maamuzi ya mwisho, naomba nichukue nafasi hii kumuuliza magode swali moja tu; ni mamlaka ipi anadhani inambeba Clinton? FBI inayoongozwa na Republican? Senate inayoongozwa na Republicans? House inayoongozwa na Republicans? Au Mahakama?

Kuna mambo mengine hata kujaribu kuyadai tu kuaonesha udhaifu katika kufikiri na Donald Trump anajua sana kutumia huu upungufu kupata mashabiki wasiofikiri ukiacha wachache wanaotetea mkate wao. Kwa mfano anapodai uchaguzi utakuwa "rigged" na watu wenye akili wanaitikia hewala; ni maelezo gani yanaweza kutosheleza imani hii?

Katika majimbo yote 50 ya Marekani Republicans wanaongoza majimbo 31 na Democrats 18 na jimbo moja la Puerto Rico liko chini ya chama kinachoitwa Popular Democratic Party of Puerto Rico. Sasa mtu lazima ujiulize hizo kura zitachakachuliwa na nani wakati kila jimbo lina sheria zake za uchaguzi!

Wengine tumejaribu sana kuwaeleza ndugu zetu hali halisi ilivyo Marekani lakini badala ya shukhrani tunashutumiwa eti tunatumiwa kumtetea Clinton...ili iweje? Mkuu Nguruvi3 katuhumiwa kulipwa kumtetea Clinton. Kwa kweli Watanzania kwa mtindo huu tusitegemee kuendelea maanake ni wazi hatujielewi.

Nachoka...!
 
Mwalimu, Kama hata Rais Obama na serikali yake hawana maamuzi ya mwisho, naomba nichukue nafasi hii kumuuliza magode swali moja tu; ni mamlaka ipi anadhani inambeba Clinton? FBI inayoongozwa na Republican? Senate inayoongozwa na Republicans? House inayoongozwa na Republicans? Au Mahakama?

Wengine tumejaribu sana kuwaeleza ndugu zetu hali halisi ilivyo Marekani lakini badala ya shukhrani tunashutumiwa eti tunatumiwa kumtetea Clinton...ili iweje? Mkuu Nguruvi3 katuhumiwa kulipwa kumtetea Clinton.Nachoka...!
Mkuu umeongea mengi ya msingi. Nianze kwa kusema kinachofanyika hapa hakina influence ya aina yoyote hata tone la maji baharini.

Tunachokifanya hapa ni kuangalia uchaguzi wa wenzetu, kutafsiri maeneo yenye utata wa kueleweka na kujifunza ili nasi kwa utaratibu wetu tuweze kujua tupo wapi na tunaelekea wapi
Nadhani wengi wanasimama na hilo.

Kuhusu establishment uliyosema, yupo mwenzetu kasema Marekani nao wana Jecha.
Nikajiuliza Marekani ipi? Marekani inaweza kuwa na tatizo katika mfumo lakini si kiwango cha Jecha

Umezungumzia kuhusu uchunguzi, mwenzetu angejua kuwa house committee chini ya Republican walichunguza na kusema hawakuona kitu chochote cha ''indictment''

Tatizo la kuangalia mambo kwa ushabiki linapelekea baadhi yetu kutoelewa nini hasa kinazungumziwa. Kama utakumbuka hapo nyuma tumeeleza tofauti za emails zinazochunguzwa
Sasa mtu anaposema emails tu bila kujuani zipi ni tatizo

Tumesema, kauli ya James Comey ambayo sasa ndiyo gumzo kwa wenzetu ina utata
Hakuna aliyesema kwanini FBI wanachunguza,bali timing ya kauli yake isiyo na conclusion ilikiuka mambo mengi.

Moja, ile norms kwamba within 60 days hakuna mfanyakazi wa federal ku interfere election
Hili tukalieleza kwa nukuu ya Hatch Act ambayo Magode kasema hajaisoma

Kauli ya Comey imekuwa na effect kubwa sana katika uchunguzi.
Clinton anasema ashinde au ashindwe emails zote zifutwe kwa takribani miaka 2

Kwasababu ya kauli ya Comey, Trump na Republican wanaitumia kama tayari kuna 'crime' na kwamba Clinton anachunguzwa.

Ukiangalia tangazo lao la leo, kwa mtu asiyejua lazima akubali Clinton ametenda kosa.

Anatumia kauli ya Comey kwamba Clinton yupo katika uchunguzi wa uhalifu ingawa Comey mwenyewe kasema hajui emails zina nini na kama ni relevant

Kosa la Comey si kufanya kazi, bali namna gani amefanya kazi na athari zake

Trump anatumia ku hype, ni mzuri kwa kueleza hata emails zilizopatikana zina siri za nchi

Haya tunapoyaeleza technically tunaambiwa tunalipwa.

Ukimuuliza Magode kwanini 'vita' imehamia N.Carolina na Florida, atakwambi una upande

Hata hivyo wengi wanaelewa, tusonge mbele
 
Ukimuuliza Magode kwanini 'vita' imehamia N.Carolina na Florida, atakwambia una upande. Hata hivyo wengi wanaelewa, tusonge mbele
Ni kweli, si wengi humu wanaofuatilia hii ya vita kuhamia N. Carolina na Florida lakini tupo wachache tunafuatilia hasa. Clinton anahitaji tu mojawapo lakini Trump anazihitaji zote pamoja na mengine mengi tu ili kuzidi kuwepo mwanga katika tumaini lake la kuingia Ikulu. Kauli aliyoitoa James Comey wa FBI tayari moto wake unafifia na sasa kuna hatari ya mambo kuigeukia FBI na hivyo kumpa Clinton ahueni kwa kiwango fulani. Someni hii...! Something is brewing...;

'The FBI is Trumpland': anti-Clinton atmosphere spurred leaks, sources say

“The FBI is Trumpland,” said one current agent.

The currently serving FBI agent said Clinton is “the antichrist personified to a large swath of FBI personnel,” and that “the reason why they’re leaking is they’re pro-Trump.”

There are ties between Trump surrogate Rudy Giuliani, the former New York mayor, and the FBI’s New York field office, which reportedly pressed the FBI to revisit the Clinton server investigation after beginning an inquiry into Weiner’s alleged sexual texting with a minor.

Yako mengi nyuma ya pazia.
 
HALI YA UCHAGUZI SIKU 4 KABLA YA UCHAGUZI

Tulieleza uwepo wa states ambazo ni safe kwa wagombea na battleground
Battleground kwasasa ni Nevada, AZ, Colorado, FL, North Carolina, Iowa, New Hampshire, na Ohio.

Kuanzia Ijumaa Comey alipotoa kauli tata, kura za maoni zinaoonyesha kubadilika sana
Zipo zilizofanyika zikionyesha kuwa independents, 51% ni less likely ku vote kwa Hillary

Hii inatokana na ukweli kuwa kuna uncertainty.
Wapo wanaojiuliza je ikiwa kuna tatizo miezi 3 au mine nini kitatokea Hillary akishinda?

Pili, kauli hiyo ime invigorate hata Republicans waliokuwa demoralized na Trump

Colorado imerudi upande wa Trump kutoka real toss up kama ilivyo Arizona
Nevada ambayo ilitakiwa iwe safe kwa Democrat inaonekana ku slip away

Hili linatoa path kwa Trump kufikia 270 kama na endapo atashinda Ohio, Florida,NC,Penn

Hapa ndipo mtinange ulipo kwasababu hizi

Trump anatakiwa ashinde Nevada, Colorado na Arizona, asipoteze state yoyote kati ya hizi;
Florida, Ohio , Pen state, na North Carolina

Kwa kutambua udhaifu huo, Clinton kampeni inakwenda mahali alipo vulnerable.

Ndiyo maana Obama, Sanders, Hillary, Kaine wapo Florida, North Carolina na Jumatatu siku ya mwisho Pennsylvania.

Lengo lao ni moja, Trump akipoteza jimbo moja tu njia inakuwa ngumu

Trump kwa kuelewa udhaifu naye kapiga kambi Florida, Pen, North Carolina

Kati ya leo na Jumanne mchezo unachezwa Florida, Ohio, North Carolina na Pennysl

Lakini pia kuna hesabu. Clinton ana target Latino na Blacks akijua ana share kwa white wasiompenda Trump.

Donald Trump anategemea blue color people na wale wasio na college educ

Concern iliyopo;
Clinton: Idadi ya watu wa constituent's ya Latino na black imepungua ukilinganisha na 2012

Ndiyo maana Obama amerudi ili kuleta msisimko wa kinachoitwa Obama coalition

Concern ya Hillary kule Nc ni voters suppression ambayo ni systematic kutoka Republican.

Je, kuna tofauti na rigged election aliyosema Trump? Jibu ni yes na tutafafanua bandiko lijalo

Trump: ana tatizo na Latino na blacks. Hata hivyo tatizo hilo la Latino halionekani Florida na hapo ndipo kuna concern Zaidi kwa Clinton kampeni

Tayari watu milioni 30 wameshapiga kura, na tracking zipo kuonyesha nini kinaendelea
Hawa early voters ni kama 40% ya wapiga kura wote

Habari kutoka WSJ zinaonyesha Georgia sasa ni 45 kwa 44 in favor of Trump. Hizi ni habari mbaya kwa Republican kwasababu hiyo ni red state.

Tutaendelea..
 
''RIGGED ELECTION VS VOTER SUPPRESSION''

Rigged election ni uchaguzi ambao kuna mfumo maalumu wa kuhujumu au ku influence au kuvuruga uchaguzi huo. Hili mara nyingi linahusisha vyombo vinavyosimamia uchaguzi

Katika nchi kama zetu, kura hukusanywa na kuhesababiwa bila uhakiki wa watu wengine
Tume zikifanya kazi bila uhuru na hata kufuata maagizo na wasimamizi wakiwa makada n.k.

Uchaguzi unaweza kufutwa, matokeo kubadilishwa kwa nguvu n.k. kwa kutumia system
Kwa ufupi ni kuwa kunakuwepo na systemic corruptions

Kwa Marekani uchaguzi unasimamiwa katika county na matokeo yanatolewa hapo kukiwa na wahusika na independent observers. Ndiyo maana leo tunajua North Carolina early voter ni 2M+

Democrat wana kura 887, 619 na Republican 644,425.
Data hizo zipo kwa state kama Ohio, Florida n.k. Penn hairuhusu early voters ina tartibu zake

VOTER SUPPRESSION

Huu ni mfumo wa kuwakatisha tamaa wapiga kura kwa mbinu za wagombea na au wasimamizi

North Carolina kilichotokea ni watu kupelekewa mkaratasi ya kura katika address tofauti na kurudishwa kwasababu hayakupokelewa.

Kimantiki yametumwa, ukweli ni kuwa yametumwa katika wrong address makusudi

Kuna tangazo linalohusu kupiga kura kwa text kwa Clinton.
Hili limetengenezwa katika mtandao ili watu wapige kura kwa Clinton ambazo ni feki.

Au inaweza kuwa vituo vya kura vinawekwa mahali pasipofika kurahisi.

Kwa maneno mengine ni kuwatisha tamaa wahusika bila wao kujua nini kinaendelea

UTAH KAMA BATTLEGROUND

Katika sehemu za kuangalia Jumanne Utah ni mojawapo. Hili ni jimbo la GOP, yaani ni Red state

Kura za maoni zinaonyesha Trump akiwa na 37%, Hillary 31 na Evan Mcullin 24

Hapa kuna tatizo kwasababu hili ni jimbo salama la Republican. Haieleweki nini kitatokea kwa Evan
Kuna uwezekano asishinde lakini akapunguza kura za Trump kwa sehemu kubwa

Kama ikitokea hivyo, hilo litakuwa tatizo kwa Republican. Ukimuondoa Evans linabaki kuwa Red state. Akiwemo Democrat wanapanda kwa kura.

Kwasasa wanaliita new battleground state
 
'The FBI is Trumpland': anti-Clinton atmosphere spurred leaks, sources say

“The FBI is Trumpland,” said one current agent.

The currently serving FBI agent said Clinton is “the antichrist personified to a large swath of FBI personnel,” and that “the reason why they’re leaking is they’re pro-Trump.”

There are ties between Trump surrogate Rudy Giuliani, the former New York mayor, and the FBI’s New York field office, which reportedly pressed the FBI to revisit the Clinton server investigation after beginning an inquiry into Weiner’s alleged sexual texting with a minor.

Yako mengi nyuma ya pazia.
Mkuu habari hii sasa imepata nguvu.
Rudi Gillian alihojiwa na Fox News siku 13 zilizopita na kusema 'something big is coming, we can go down without a fight' alipoulizwa ana maana gani akasema 'just wait'

Leo amehojiwa na Wolf Blitzer wa CNN. Kwanza amekiri kuwa aliongea na rafiki zake wa FBI wa zamani waliomweleza kutoridhishwa na maamuzi ya Comey ya July.

Halafu akasema habari nyingi alizosoma magazeti na hakuwa na knowledge

Guliian akasema alipoulizwa na fox na kusema kuna jambo linakuja alimaanisa matangazo ya kushtukiza. Wolf akamuuliza, wakati anahojiwa na radio Waltson alisema ameambiwa na active FBI member. Gullian akasema kama alisema hivyo alikosea

Wolf akamzungusha tena kwa kumuuuliza kama aliongea na wastaafu wa FBI, Gullian akasema ndiyo hao ni rafiki zake wa zamani aliofanya nao kazi.

Wolf akamuuliza, hivi hao si wamekula kiapo cha kutoa toa siri maisha yao yote ilikuwaje wakamwambia yaye. Gullian akakwepa na kusema hawakuongea na wastaafu

Hii inakuja baada viongozi wawili wa Dmeiocrat kumwandikia inspector wa FBI kuchungua leak ya habari hizo kabla Comey hajazitoa.

Kwa mtazamo huo, Gullian anaonekana kujua nini kinaendelea. Tatizo ni kuwa uchunguzi ukifanyika ima utamwekea mahali pagumu au utawaweka FBI wastaafu mahali pagumu

KURA ZA MAONI
Kura za maoni zinaonyesha mabadiliko.
New Hampshire imetoka lean Dem na sasa ni toss up

Utah imetoka toss up na sasa ni lean Republican. Arizona ni lean Republican

Kwa mujibu wa CNN hadi sasa Clinton ana electoral vote 268, s shy of 270. Donald Trump ana 204, 64 shy of 270.

Kwa mtazamo huo, Trump anatakiwa kushinda Ohio, Florida, NC, New Hampshire, Iowa , Nevada na Colarado ili kufikisha 268.

Kura mbili zitapatikana kwa state of maine na Nabraska.
State hizi hazitoi electoral vote kwa winner take all bali kwa congressional district

Congressiona district zina maana wanagawanya viti kutokana na nani kashinda kwa wingi eneo gani. Hapo kuna possibility ya kupata 2 na kufanya 270

Kwa upande wa Clinton anachotakiwa ni kushinda state moja tu hata yenye lectral vote chache kama New Hampshire. Ndio maana team ya Clinton imegawanyika, North Carolina, NH na Florida

HABARI ZA KUVURUGA UCHAGUZI
Kuna taarifa za serikali ya Marekani kuwa Russia itafanya hacking ya system za uchaguzi

Hili ni ku undermine uchaguzi wa Marekani na kuthibitisha kauli ya uchaguzi ni rigged

Vyombo vingi vya habari vinaonyesha wasi wasi na azma ya Russia ya kuingilia uchaguzi

Concern hii inatokana na WikiLeaks, kuna msemo wa kiingereza unosema 'Chicken are coming home to roost'

Tunafuatilia zaidi
 
Mkuu Nguruvi3, hii habari ni kubwa sana ila kwa timing yake muda haupo kwani bado siku tatu tu kura zinapigwa na Clinton hana muda wa kufuatilia. Wachunguzi wa mambo tayari wanajaribu kuunganisha dai la Trump la rigged election kutumika kama boya tu katika kupoteza lengo. Tetetsi zinasema kwamba hata wikileaks inahusishwa kwenye huu mpango ambao ulisukwa kwa muda mrefu kuhakikisha Clinton hawi Rais baada ya Obama.

Pamoja na hayo matokeo ya huu uchaguzi ndio yataamua Marekani inaelekea wapi kuhusiana na chombo kama FBI kuhusishwa na njama za kuingilia mchakato wa uchanguzi. Baada ya uchaguzi nina hakika FBI itaundiwa tume ya uchunguzi na hapo ndipo ukweli utajulikana wa mbivu na mbichi. Wakati Trump anamtuhumu Clinton kubebwa kumbe yeye ndiye muda wote alikuwa anabebwa na chombo kinachotakiwa kutoegemea upande wowote.

Habari za ndani zinasema Democrats wameamua kufuatilia hili jambo kimya kimya huku ikijikita zaidi na kampeni ambazo sasa zinafikia ukingoni. Kama habari hizi zingevuja mapema, hivi sasa tungekuwa tunaongelea mambo mengine kabisa na yawezekana hii ndiyo sababu kampeni imeonekama kuwa ngumu kwa Clinton. Hii inaeleza kwa nini Trump pamoja na kuona dalili ya ushindi ukiwa mdogo anayo imani kwamba Wamarekani wengi bado watampa kura.
 
Mkuu Mag3

Kosa alilofanya Rudi Gullian ni kwenda katika vyombo vya habari na kueleza hayo

Wana habari wanafuatilia kwa umakini kauli zake na tayari wameshapata hoja.
Kwanza, alisema habari hizi kapewa na marafiki zake wa zamani wa FBI. Ipo katika rekodi

Hilo tu linawaweka 'maafisa' hasika mahali pagumu sana kwasababu wana kiapo

Pili, kama atadai amesoma magazeti, kauli za kuambiwa na wastaafu wa FBI amezitoa wapi?

Kama FBI wamegawanyika kama inavyosemwa sasa, kutakuwa na tatizo baada ya uchaguzi

Safari ya Comey kikazi ipo katika wakati mgumu
 
Back
Top Bottom