04 February 2024
Dakar, Senegal
RAIS WA SENEGAL AFANYA MAPINDUZI YA 'KIKATIBA' KWA KUFUTA UCHAGUZI MKUU
Rais wa nchi tulivu iliyokwepa Mapinduzi ya kijeshi ya Africa Magharibi ya Senegal imeigia katika mtihani mkubwa toka ipate uhuru wake. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo uchaguzi mkuu kalenda ya uchaguzi kufutwa kwa muda usiojulikana.
Uchaguzi mkuu ulitegemewa kufanyika tarehe 25 February 2024, lakini kwa kutumia madaraka yake wachunguzi wa kisiasa wanasema haya ni mapinduzi ya kikatiba kwa rais Macky Sall kuahirisha uchaguzi mkuu.
Rais Macky Sall asema sababu ya hatua yake ni baada ya mahakama ya kikatiba kukata majina ya wagombea baada ya kudai majaji walikula rushwa kuondoa majina ya watia nia wa kugombea uongozi ktk uchaguzi wa baadaye February 2024
Rais Macky Sall asema sasa ataitisha mkutano wa kitaifa wa maridhiano ili mchakato wa mazingira ya uchaguzi huru wa haki yapatikane, ni baada ya kukutana na waziri mkuu, spika wa bunge na tume ya uchzguzi katika ikulu ya mjini Dakar Senegal.
Rais Macky Sall aliingia madarakani kupitia uchaguzi mwaka 2012 na kuchaguliwa tena 2018 huku akitangaza kuwa hatagombea tena urais 2024.
Viongozi wa upinzani akiwemo kinara wa upinzani Bw. Ousmane Sonko walaani hatua hiyo ya kufutwa uchaguzi mkuu kwa kisingizio cha rais Macky Sall aliyepo madarakani kuokoa taifa toka Mahakama ya Kikatiba anayodai imekosa sifa kutokana na rushwa kusimamia uchaguzi huru na wa haki
Upinzani wanadai hatua hiyo ya rais Macky Sall ni njama zake za kuendelea kubakia madarakani kwa kufanya mapinduzi ya 'kikatiba' tofauti na nchi jirani za Afrika magharibi kutumia mapinduzi ya kijeshi kuingia mafarakani.
Wachambuzi wa siasa za Senegal wanasema rais Macky Sall amefanya mapinduzi hayo ya kikatiba kutokana na woga kuwa akiingia rais mwingine madarakani ataingia katika matatizo kutokana na ufisadi wa utawala wake toka mwaka 2012 utamuwekea mazingira ya kushitakiwa kama rais aliyemtangulia, rais Abdoulaye Wade alifunguliwa mashitaka na kubidi kukimbilia uhamishoni Ufarasa kuepuka kifungo.
Picha maktaba : Rais mstaafu Abdoulaye Wade wa Senegal