Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA | Page 28 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Jul 19, 2016.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi Marekani

  UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI

  Baada ya kumalizika chaguzi za ndani ya vyama, kilichopo ni uchaguzi mkuu wa Marekani
  Wagombea ni Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democrat

  Uzi huu utakuwa mwendelezo hadi uchaguzi utakapomalizika.

  Kabla hatujaendelea na mijadala, tuangalie lililopo mbele kwa sasa.

  Mkutano mkuu wa Republican ulioanza leo
  Mkutano ni wa kumtihibitisha mgombea kiutaratibu wa vyama, na kuweka sera za vyama mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu.

  Mkutano mkuu wa GOP upo Cleveland
  Kwasasa mkutano umeanza na wazungumzaji kadhaa wameshaongea.

  Agenda kubwa ya leo ni ulinzi na usalama wa Taifa.

  Hii ni nguzo katika chama cha Republican. Kwamba, huitumia katika katika chaguzi.

  Katika waongeaji wa leo, mmoja ni Lt Gen mstaafu Michael Flynn, Director of Intelligence Agency kabla. Mwingine ni Joni Ernest seneta wa Iowa, ambaye naye pia ni mstaafu

  Mayor wa zamani wa New York, Rudi Gulian aliongea akiambatanisha hotuba yake na mambo ya ulinzi wa ndani, akiwazungumzia Polisi na walinzi wengine.

  Wiki moja iliyopita Rudi alihoji mauaji ya askari kutokana na kile kinachoitwa black lives matter. Gulian alisema, iweje kundi lisisimame kwa mauaji ya vijana kule South Chicago.

  Rudi Gulian anaonekana kama alama ya 9/11 kutokana na kuwa meya wakati huo.
  Hivyo kuongea kwakwe kunafungamishwa na suala la ulinzi na usalama.

  Kinachoonekana kwa siku ya kwanza, ni suala la ulinzi hasa ugaidi.

  Hili linafungamanishwa na Hillary Clinton na emails(Benghaz).

  Kuna wakati Lt Gen Michael alimshambullia Obama kwa uwepo wa ISIS na Osama.
  Gen alikosea kwani kuingiza Osama na Obama ni kutoa point kwa Democrat

  Mkutano mkuu ulianza kwa kupingwa na makundi nje, hata hivyo hali imetulia.
  Jambo moja ni kuonekana kwa baadhi ya watu mashuhuri kama Gav wa Texas Rick Perry

  Hata hivyo, safu kubwa ya viongozi nguli kama Familia ya Bush, Mitt Romney, John McCain haipo katika mkutano mkuu na kupunguza hamasa kwa kiasi Fulani

  Mbinu wanayotumia GOP ni kutisha Wamerekani kuwa hawapo salama.

  Mbinu ya pili ni kumshambulia Clinton, wakitambua kumshambulia Obama ambaye approval rate yake ipo katika 50% italeta tabu.

  Tutaendelea kila wakati kutokana na yanayojiri
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #541
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  COMEY AANDIKA BARUA NYINGINE

  Director wa FBI kaandika barua nyingine akisema wamemaliza uchunguzi wa email katika laptop ya Anthony Weiner mumewe Huma Abiden.

  Conclusion ni kuwa hakuna kilichoonekana kipya kinachobadilisha uamuzi wa July

  Hii imekuja siku 2 kabla ya uchaguzi na siku 11 baada ya kuandika barua ya kwanza

  Kwa mtazamo barua hii haimsaidia Clinton baada ya uharibifu uliofanyika wiki mbili zilizopita.

  Tayari kuna maeneo yamefunga early voting ambazo definite zina makundi yaliyokuwa na misimamo kwa mtazamo wa indictment, corrupt na kila aina ya kauli

  Wiki mbili Trump ametumia kauli ya Comey katika matangazo na katika mikutano.

  Ilifika mahali watu wakasema kutakuwa na impeachment Clinton akichaguliwa.

  Kwa ufupi damage aliyofanya Comey kwa Democrat na Clinton ni kubwa katika uchaguzi huu

  Saga la Comey halijaisha kwani Dem wanaonekana kulivalia njuga na hasa baada ya barua ya pili

  Wakati huo huo Trump anamlaumu Comey kwa kubadili msimamo.

  Lakini hili haiwezi kulinganishwa na uharibifu alioufanya.

  Kwa haraka tulikuwa tunaangalia Wachambuzi na wanasheria, Comey yupo katika wakati mgumu sana
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #542
  Nov 7, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nguruvi3 kwa Kiingereza wanasema the damage has been done and what has been done cannot be undone. Ni katika msingi huo, Democrats wamemshauri mgombea wao kutogusia hiyo issue na badala yake ajikite tu katika kampeni na kusonga mbele.
   
 4. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #543
  Nov 7, 2016
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #544
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mjadala umehamia kwa Dir Comey

  Kinachosemwa ni gross misconduct ya Comey iliyompa Trump nafasi ya kujadili , kutoa matangazo na kuzungumzia barua yake kama agenda.

  Swali ni jinsi alivyokiuka kanuni za investigation kwa kutoa conclusion kabla ya hata kuona emails. Pili, ku interject hoja siku 9 kabla ya uchaguzi na tatu kuandika barua siku 2 kabla ya uchaguzi

  Wachunguzi wa mambo wanasema kama aliweza kuchunguza in less than a week, nini kilimshinda kusbiri kama ilikuwa ni lazima ili zichambuliwe? Je, hakuona madhara kwa Clinton

  Madhara

  Wamarekani milioni 40 wameshapiga kura baadhi katika battle ground states kama Florida na NC
  Hakuna anayejua ni wangapi walivurugwa na barua ya Comey hasa kundi la Independents

  Independents kama ni 5,000 waliobadili msimamo idadi inatukumbusha nini kilitokea kwa Al Gore.

  Pili, kampeni ya Clinton ilikuwa na point nyingi kwamba Hillary alikampeni kwa maseneta/congress Baada ya emails kampeni ilipoteza focus

  Ukiangalia polls, Clinton hakupoteza lakini Trump ali gain sana na ku close the gap

  Ahueni

  Kampeni ya Clinton ina ahueni kutokana na damage kwa kuzingatia kuwa baadhi ya wapiga kura wana agenda zao na kutovutwa na emails.

  Latinos is all about Ukuta na Trump. Kwao kura ni kuzuia Ukuta habari zilizopo wamepiga kura more than 100% ya 2012

  Pili, kama kuna independent aliyekuwa anasubiri dakika za mwisho, uamuzi wake utakuwa umezuiwa na barua ya pili ya Comey, na utatoa fursa kwa yeye kufikiria upya kuhusu kura yake

  Tatizo ni kuwa katika siku 2 wangapi watapata ujumbe huo ikiwa miaka 7 bado kuna wanaoamini Obama si Mmarekani kutokana na kauli za Trump na birth cert!

  Kampeni yakataa kujadili
  Kampeni ya Clinton imetumia busara kuliacha suala la barua ya pili ya Comey.
  Hili kisiasa ni kuua hoja ya emails ambayp imemdhuru mara nyingi.

  GOP wanataka iendelee kuwa agenda na ku derail focus ya Dem si kwasababu ya Trump bali kutoa fursa ya seneta na wabunge wao

  Tunafuatilia
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #545
  Nov 7, 2016
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  FBI naoana kama wanazidi kuchemka nadhani Mkurugenzi angeachia ngazi baada ya uchaguzi.
   
 7. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #546
  Nov 7, 2016
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Comey tayari anaanza kuhesabu siku lazima kibarua chake kiote nyasi.

  Wamejichanganya wenyewe kwa kufanya uchunguzi mara ya kwanza na wakatangaza kuwa hakuna kosa la jinai. Then wiki moja kabla ya uchaguzi wanatangaza kuitisha upya uchunguzi kinyume na taratibu... bora hata wangefanya uchunguzi wao kimya kimya na kutoa tamko baada ya kumaliza uchunguzi kuliko walivyoamua kutangaza kuanza uchunguzi halafu wanaambulia mikono mitupu.

  Trump sasa amewageuzia kibao FBI kwamba nao ni sehemu ya "rigged system" sababu haiwezekani kwamba wamemaliza kuchunguza maelfu ya emails kwa muda mfupi hivypo.
   
 8. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #547
  Nov 7, 2016
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Yaani akishinda HRC, ushindi wake hautanoga!! Maana tuhuma nyingi za kubebwa kwake bado ni mbichi mno. Na kibaya zaidi, huyu 'mama ' ana visasi, si mtu wa kuomba msamaha... kwa vyovyote lazima atawashughulikia wale wote anaodhani walimsumbua kwenye kampeini, endapo atabahatika kuingia ikulu. Na kuwashughulikia huko ndiko kutatimiza wasiwasi wangu wa kuiporomosha US kwa mwendokasi wa kutisha. Chakwanza kabisa atata ku'supress' Russia! Hili litaleta mtafutano na EU au hata NATO!!! Wananchi wengi wa Ulaya wanaumizwa na vikwazo dhidi ya Russia. Ndiyo maana dalili za mtafutano huo, ulikwamisha vikwazo vya' ziada ' dhidi ya Russia.
   
 9. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #548
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Wakuu JokaKuu Mag3 AG J.Reno amefariki asubuhi hii baada ya ku battle Parkinsonism kwa muda mrefu
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #549
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #550
  Nov 7, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  RIP Janet Reno, hakuna ajuaye siku wala saa...Amina.
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #551
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa kuna large turnout Florida ambayo ni 103% ukilinganisha na early voters 2012

  Florida ni diverse sana na hapa kuna hoja

  1. Je, ni effect ya Walatino kwa Trump kwamba 'wanamwadhibu
  2. Kuna Latinos Cubans ambao ni loyal kwa Trump kutokana na uhusiano mpya wa Cuba-USA
  3. Kuna Latinos Puerto Rico ambao ni loyal kwa Hillary

  Turn out bado inawachanganya wachunguzi wa mambo, nini hasa kinaendelea.
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #552
  Nov 7, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  Latest Fox News poll!
  7/11/2016  [​IMG] [​IMG]

  Democratic Nominee Hillary Clinton 48%... Republican Nominee Donald Trump 44%

  Kila mtu anajua msimamo wa Fox News, je hapa wanatoa picha gani?
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #553
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Turnout Nevada

  Kulikuwa na watu wengi waliopiga kura hadi saa 4 usiku wakati vituo vimefungwa saa 1
  Nevada kuna Latinos na ni state inayo lean Democrat

  Trump na Republican mmoja wa Nevada wakasema kufungwa vituo na kura kuendelea kupigwa kunaonyesha system ilivyokuwa rigged.

  Ukweli
  Sheria zinasema mtu akiwa katika mstari na kituo kikafungwa, ataruhusiwa kupiga kura
  Anayekatazwa kupiga kura ni yule anayekuja baada ya muda kufunga kufika

  Hili limetokea NC ambapo mama mmoja alifika kituoni muda wa kufunga ukiwa umefika.
  Hakuruhusiwa kupiga kura, ila mumewe aliyetangulia kama dakika 5 alikuwepo wakati kituo kinafungwa na aliruhusiwa kupiga kura

  Update zinaendele
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #554
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  UCHAGUZI NA UCHUMI

  Katika siku 9 zilizpita soko maarufu la mitaji la S&P lilipoteza thamani katika streak ndefu kwa miaka takribani 40. Dow J haikuwa katika hali nzuri iki trade below 18K

  Wachunguzi wanaangalia barua ya Comey ya jana kama kichoche cha masoko kufura siku ya leo
  Kwa sasa Dow ipo 341, NAS 116 S&P 43 Points.
  Mwisho wa siku tutaangalia point za mwisho za masoko.

  Hili linaeleza ukubwa wa siasa za Marekani na jinsi zinavyogusa maeneo mengi yawe ya kijamii, kiuchumi au kisiasa.
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #555
  Nov 7, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Pamoja na yote kuna mambo ya kuangalia katika majimbo ambayo miaka yote imeitwa battle ground states kwa sasa vita vimeelekezwa kwa yale majimbo ambayo ni crucial states. Kwa hali ilipofikia hivi sasa, siku moja kabla ya upigaji kura, mgombea wa Democrats, Hillary Clinton yuko vizuri kwa sababu moja tu, hana jimbo ambalo ni crucial kwa maana ya ulazima wa kushinda ili aweze kuwa Rais. Kwa mgombea wa Republicans, Donald Trump, mambo ni tofauti kidogo kwani karibu kila jimbo katika battleground states limekuwa crucial kwake ili aweze kushinda Urais.

  Majimbo ambayo ni crucial kwa sasa kwa Donald Trump ni North Carolina, Nevada, Florida, New Hampshire, Arizona na Nebraska. Majimbo haya yote ni crucial kweli kweli kwa Donald Trump na anatakiwa ayashinde yote huku Clinton akitakiwa ama kushinda moja tu na hata asiposhinda matokeo chanya kwenye battle grouns states zingine nje ya hizi yanatosha kumpa ushindi katika uchaguzi huu. Ni kwa sababu hii anafanya kila jitihada aweze kupenya ngome ya Democrats kwenye yale majimbo ambayo kwa kawaida nafasi ya Republicans kushinda ni finyu.
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #556
  Nov 7, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kuna factors nyingine za kuangalia. Kwanza, blacks wamepungua katika early vote ukilinganisha na 2012. Kuna explosions ya Latinos ambayo haijaweza kuwa defined clearly
  Kwa mfano, Nevada Trump anaongoza kwa point 6 kukiwa na Latinos wanaopiga kura kwa wingi, haileweki ni kwa Dem au ni kwa Trump lakini the surge is there

  Jambo jingine, Democrat wameathirika na Comey kwa sehemu kubwa.
  Hata hivyo, wameruhusu Trump acheze katika uwanja wao.
  Michigan ni mfano mmoja ambapo kuna EV 16.

  Hata kama Dem watashinda kama wanavyotarajia, bado wame attract wapinzani wao kuja eneo lao

  Tatu, Dem wame miss opportunity. Georgia ni Red lakini inaonyesha wangekuwa competitive kama wangewekeza huko. Ndivyo ilivyo kwa Arizona na Utah.

  Utah, Dem wanasaidiwa na Evans Mcmullin wangeweza kuweka kambi ina maana Trump angevuta nguvu kutoka maeneo mengine kwasababu hapasi kupoteza Red state achilia mbali ku sweep the board.

  Pamoja na hayo Clinton anahitaji state moja tu bila kujali ukubwa wake.
  Trump anahitaji battle ground state zote pamoja na ku flip up blue moja. Hapo ndipo pana ugumu
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #557
  Nov 8, 2016
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,773
  Likes Received: 4,990
  Trophy Points: 280
  ..Trump made it too dificult for himself.

  ..kwanza alipaswa kuacha kuwanyanyapaa jamjj ya Wahispanik. Hili ni kundi kubwa kuliko weusi. Wahispanik wakikupenda uwezekano mkubwa utashinda Uraisi wa Marekani.

  ..pili alitakiwa awe na mahusiano mazuri na Republican national party. Hawa wangemsaidia kifedha na ku-organise kampeni yake kuwa more conventional.

  ..sasa hivi Trump yuko peke yake lakini analeta shida namna hii. Vipi kama angekuwa na chama kizima cha Republicans nyuma yake?
   
 19. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #558
  Nov 8, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  SURA YA UCHAGUZI

  Tukumbushe uchaguzi si idadi ya kura, bali viti (Electral vote) au EV katika state
  Kuna solid and Red Sates ikimaanisha zinajulikana zitakuwa Republican au Democrat

  Kuna state zitakazoamua nani awe Rais kwasababu hazitabiriki, hizo ndizo swing au battle states

  Macho kesho yatakuwa katika state zifuatazo (Kundi 1)
  Nevada EV 6
  Florida EV 29
  Ohio EV 18
  NC EV 15
  Hampshire EV 4
  Pen state EV 20
  Iowa EV 6

  Halafu kuna state ambazo hazieleweki kutokana na hali ya uchaguzi
  Utah EV 6 Hii ni kutokana na kuwepo kwa mgombea binafsi Evans M
  Arizona EV 11 Kutokana na kuwa na Latino
  Maine EV 2 Kutokana na kuwa na congressional district
  Georgia EV 16 Kwasababu hii ni red state lakini kura za maoni zipo karibu sana
  Michigan EV 29 , lead ya Clinton imepungua 11 hadi 4, ambayo ni within margin of error

  Hizi zinaweza kuwa chafuzi tu kwa wagombea ingawa ni unlikely zinaweza kuwa na impact hiyo
  Muhimu ni kundi la kwanza kwasababu hizi

  Kwa mujibu wa track poll (si lazima ziwe sahihi) Magic number inayogombewa ni 270
  Hillary Clinton anasimama na EV 268 na Trump 204

  Kwa minajili ya mjadala the EV baseline ni 204, hivyo wagombea wanatakiwa kufikia 270
  Kama polls na uchambuzi ni sahihi bila mishaps kutoka kundi la 2 hapo juu, then

  Clinto akiwa na 268 atahitaji EV 2 kutoka popote kama New Hampshire EV au Iowa
  Donald Trump 204 atahitaji EV 66 na hizo lazima zipatikane kutoka kundi la 1 hapo juu

  Inaweza kuonekana ni mlima mrefu kwa Trump kupanda, lakini huu ni uchaguzi lolote laweza kutokea. Ingalikuwa rahisi kiasi hicho Clinton asinge kampeni

  Kwa mfano, BREXIT ilibashiriwa ushindi UK kubaki EU. Kilichotokea kila mmoja anakijua
  Kwanza, wengi hawakujitokeza kupiga wakiamini kambi ya Remain itashinda.
  Kambi ya exit ikapiga kura na mwisho ikashinda

  Pili, katika primaries Hillary Clinton alikuwa anaongoza kwa asilimia 9-11 Michigan. Kwa mshangao Bernie Sander akashinda

  Tatu, hakuna aliyetarajia 2004 George Bush angerudi madarakani kwa kumshinda Kerry

  Nne, kuna factors nyingi zinafanya kazi katika uchaguzi tutajadili bandiko lijalo

  Inaendelea
   
 20. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #559
  Nov 8, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kampeni zimeisha...Donald Trump kamaliza saa 7:06 usiku (sawa na saa sita mchana Tanzania) na Hillary Clinton kamaliza saa 7:10 na kilichobakia sasa ni upigaji wa kura. Wote wamewaomba wapenzi wao wapate usingizi mfupi kabla ya kuamka na kuelekea vituo vya kupiga kura.
   
 21. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #560
  Nov 8, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
Loading...