Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Jul 19, 2016.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi Marekani

  UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI

  Baada ya kumalizika chaguzi za ndani ya vyama, kilichopo ni uchaguzi mkuu wa Marekani
  Wagombea ni Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democrat

  Uzi huu utakuwa mwendelezo hadi uchaguzi utakapomalizika.

  Kabla hatujaendelea na mijadala, tuangalie lililopo mbele kwa sasa.

  Mkutano mkuu wa Republican ulioanza leo
  Mkutano ni wa kumtihibitisha mgombea kiutaratibu wa vyama, na kuweka sera za vyama mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu.

  Mkutano mkuu wa GOP upo Cleveland
  Kwasasa mkutano umeanza na wazungumzaji kadhaa wameshaongea.

  Agenda kubwa ya leo ni ulinzi na usalama wa Taifa.

  Hii ni nguzo katika chama cha Republican. Kwamba, huitumia katika katika chaguzi.

  Katika waongeaji wa leo, mmoja ni Lt Gen mstaafu Michael Flynn, Director of Intelligence Agency kabla. Mwingine ni Joni Ernest seneta wa Iowa, ambaye naye pia ni mstaafu

  Mayor wa zamani wa New York, Rudi Gulian aliongea akiambatanisha hotuba yake na mambo ya ulinzi wa ndani, akiwazungumzia Polisi na walinzi wengine.

  Wiki moja iliyopita Rudi alihoji mauaji ya askari kutokana na kile kinachoitwa black lives matter. Gulian alisema, iweje kundi lisisimame kwa mauaji ya vijana kule South Chicago.

  Rudi Gulian anaonekana kama alama ya 9/11 kutokana na kuwa meya wakati huo.
  Hivyo kuongea kwakwe kunafungamishwa na suala la ulinzi na usalama.

  Kinachoonekana kwa siku ya kwanza, ni suala la ulinzi hasa ugaidi.

  Hili linafungamanishwa na Hillary Clinton na emails(Benghaz).

  Kuna wakati Lt Gen Michael alimshambullia Obama kwa uwepo wa ISIS na Osama.
  Gen alikosea kwani kuingiza Osama na Obama ni kutoa point kwa Democrat

  Mkutano mkuu ulianza kwa kupingwa na makundi nje, hata hivyo hali imetulia.
  Jambo moja ni kuonekana kwa baadhi ya watu mashuhuri kama Gav wa Texas Rick Perry

  Hata hivyo, safu kubwa ya viongozi nguli kama Familia ya Bush, Mitt Romney, John McCain haipo katika mkutano mkuu na kupunguza hamasa kwa kiasi Fulani

  Mbinu wanayotumia GOP ni kutisha Wamerekani kuwa hawapo salama.

  Mbinu ya pili ni kumshambulia Clinton, wakitambua kumshambulia Obama ambaye approval rate yake ipo katika 50% italeta tabu.

  Tutaendelea kila wakati kutokana na yanayojiri
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #2
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Republican na hoja ya usalama

  Hii hoja ina nguvu kwa wakati huu ambapo matukio ya ugaidi yamezidi duniani.
  Rep wanaitumia hoja hiyo kuonyesha kuwa Taifa lao haliko salama.

  Katika kufanya hivyo, wanagusia baadhi ya mambo kwa kumwacha Obama na kufungamanisha hoja zao na Hillary Clinton.

  Kuna msemaji mmoja ambaye mtoto wake aliuawa katika shambulio la Benghaz.
  Mama huyiu alivuta hisia kwa kueleza kuwa kifo cha mwanawe anamlaumu Clinton

  Inafika mahali baadhi ya wasemaji wanaunganisha suala la email na Benghaz.

  Haya ni mambo mawili tofauti, hata hivyo kwa mbinu za kisiasa,yanafungamanishwa kuonyesha udhaifu wa Clinton uliosababisha shambulio la Benghaza na emails!

  Tukumbuke kuwa suala la email linatumiwa na Republican kwa maaana moja kubwa. Bernie Sanders alilitumia wakati wa uchaguzi wa Democrat na lilimsaidia katika kampeni.

  Hata baada ya chaguzi bado Bernie Sanders alitumia mbinu za kushawishi ili suala hilo limuondoe Clinton

  Baada ya taarifa ya FBI ambayo kwa kiasi kikubwa ilimfungua Clinton, kura za maoni zinaonyesha kumpunguzia 'kura' kwa kile kinachoonekana ni kutokuwa mwaminifu

  Kwa mantiki hiyo GOP wanatambua suala limefika mwisho, hata hivyo kisiasa lina nguvu kwa kuangalia mafanikio ya Sanders na na kura ya maoni baada ya taarifa ya FBI

  Uchaguzi wa 2008, hoja kubwa ilikuwa kumfungamanisha George Bush na matatizo.

  Ilifika mahali wagombea wa Republican walijitenga na Bush ambaye approval rate yake ilikuwa chini sana.

  Kwasasa approval rate ya Obama at least kwa muda huu ipo juu kwa kulinganisha na watangulizi wake katika kipindi kama hiki.

  Ndio maana Republican hawamshambulii sana bali kumhambulia Hillary kama Hillary
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Katika bandiko la 2 Mkuu Mag3 ameeleza kuhusu demokrasia kwa wenzetu.
  Kwa kufuatilia mkutano mkuu utaona jinsi hoja zinavyowekwa hadharani na kujadiliwa

  Hata askari wastaafu wamepewa nafasi za kueleza uzoefu wao hadharani. Hawakujificha kama ambavyo baadhi ya viongozi wa nchi yetu walivyotushangaza wakati wanachukua fomu za Urais

  Kwa upande wa vyama, wanachama wapo huru kusema wanachokifikiri.

  Wapo akina Romney na McCain wanaompinga Trump hadharani.
  Kumpinga mgombea wa chama si kosa la jinai au madai, ni matumizi ya haki ya kila mtu

  Utaweza kuona siasa zao hazina mizengwe na kila jambo linazungumzwa bila kuwa na mawaa
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  VYOMBO VYA HABARI

  Navyo vinaendelea na kazi zake.
  Uchambuzi wa hotuba ya mke wa Trump Bi Melanie Trump imeonekana na matatizo.

  Kuna mistari aliyobeba kutoka kwa Michelle Obama ya 2008

  Katika mizania ya siasa za Marekani, hili linaweza kuleta mjadala utakaohamisha ujumbe aliokusudia Bi Trump.

  Wapo wanaomlaumu mwandishi wa hotuba kwa kuchukua kauli ya Michelle.

  Siyo big deal, lakini Melanie ni mke wa mgombea hivyo wapinzani wao Democrat wataigeuza hoja kufunika hoja nyingine.

  Tayari wanaisema ni 'plagiarism' na kuhoji ule uaminifu wanaousema upo wapi?

  Haya ni makosa ya kifundi ambayo kwa siasa zilizokomaa yanatumika.

  Kwa nchi zinazoendelea, kusema mke wa mgombea 'kaibia' utalala mbali na nyumbani

  Waandishi wa habari wanaitafuta timu ya Trump ya mawasiliano kueleza jambo hilo.

  Melanie kama mke alikuwa akimwelezea mumewe dunia imfahamu.

  Kwa hili, ile message yake inapoteza nguvu kwani vyombo vya habari vinatafuta habari kwa kile wanachosema 'habari si mbwa kumg'ata binadamu bali binadamu kumg'ata mbwa'
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kauli mbiu ya GOP katika siku ya kwanza ya Convention imekuwa to make America safe again wakitaka kuonesha kuwa kwa ulinzi na Usalama wako bora kuliko Democrats. Mkewe Trump naye kaelezea ubora na umahiri wa mumewe kama mtu anayeaminika na asiyekubali kushindwa. GOP imetumia vifo vya Bengazi katika kuonesha kuwa Clinton alihusika moja kwa moja.
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kwasasa timu ya kampeni ya Trump inafanya kazi ya 'damage control' kutokana na 'desa' la Melanie Trump kutoka kwa Michelle Obama 2008

  Theme ya mkutano wa leo kama inavyosemwa ilikuwa 'make America safe '

  Kosa la Melanie linaweza kufunika ujumbe wa leo ambao kwa kiasi kikubwa sana ulilenga kumuonyesha Clinton kama mtu hatari katika nafasi ya Urais.

  Hivyo Trump team ina kazi mbili mbele
  1. Kutoka na kuomba radhi kwa kosa hilo
  2. Kutangaza kumfukuza aliyeandika hotuba hiyo

  Tatizo moja kubwa ni kuwa baada ya hotuba, Melanie alihojiwa na waandishi na kukirialiandika hotuba mwenyewe. Kampeni itamchukulia nani hatua ikiwa mwenyewe keshasema ameandika?

  Tayari hii ni habari inayozungumzwa katika vyombo vya habari wakiweka wasemaji wote wawili kwa kuwalinganisha. Political pundits wa Trump wanakiri kuwa ni kosa

  Unaweza kuona nguvu ya vyombo vya habari katika kutafuta, kutafuna na kutathmini maneno ya wasemaji.

  Tunahitaji kupanua demekrasia yetu ifike mahali pa kuwawezeha wanahabari kutumikia taaluma yao si kuwatisha
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Trump na mkewe Melanie
  Mkuu uliona ulinzi na heshima wanayopewa wagombea wa vyama vyote, huwezi kujua yupi ni mgombea wa chama tawala au chama pinzani. Bila shaka umemuona hata Sheriff Clarke (mweusi) anavyowaponda Rais Obama na Senator Clinton na kuwalaumu kwa kutokemea kauli ya Black Lives matter akidai hata Blue Lives matter akimaanisha polisi. Hapa Tanzania hata askari wa kawaida tu anaweza akamtisha mgombea Ubunge na hata mgombea Urais mradi tu anatoka Upinzani...inasikitisha!
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2016
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Wakuu Mag3 & Nguruvi3 naendelea kusoma bayana zenu Mungu awabariki si kila mtu ana nafasi ya kufuatilia siasa za USA lakini kupitia mabandiko yenu tunajikuta tuko karibu na taifa hilo kubwa duniani.

  Sijui kama wagombea tayari wameshatangaza wagombea wenza wao au bado.Naamini wagombea wenza wana nafasi kubwa ya kuongeza chachu ya ushindi kwa wagombea urais.Itakuwa jambo la afya iwapo mtajadili nafasi za wagombea wenza na jinsi gani wana weza kusaidia ushindi wa wagombea URAIS.
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Tayari Trump keshamtangaza mgombe mwenza,Gavana wa jimbo la Indiana Bw Mike Pence

  Mr Pence ni mzaliwa wa Indiana,wazazi wake ni wa Irish wakatoliki

  Alikuwa mbunge wa congress kabla ya kuwa Gavana wa Indiana 2013

  Ni mwanasheria kitaaluma,mwenye kuheshimika katika Republican

  Katika harakati Pence ni kundia la GOP 'Tea Party' lengo mrengo wa kulia zaidi

  Amefanya kzi kubwa katika jimbo lake na anasifiwa kwa hilo

  Tatizo ni kuwa yeye ni mwanasheria, mtu makini kwa kauli zake.

  Je ataweza kwenda na kasi ya Trump ya kusema sema bila mpangilio?

  Tunasema hivyo kwasababu Pence ni zao la wahamiaji ambao Trump 'hakubalia' uwepo wao.

  Pence kama Hillary alipiga kura ya vita ya Iraq , Je, msimamo wa Trump kuhusu poor judgement ya Hillary utabaki katika nafasi gani?

  Kutangazwa kwa Pence kulifunikwa na tukio la Nice,ilibidi Trump atangaze uteuzi wake kwa njia ya Tweeter.

  Siku mbili baadaye ali mu introduce katika hali iliyoleta utatanishi sana

  Tukio lilipaswa kuwa kubwa kama kawaida, Trump akalichukua kuwa sehemu ya hotuba zake. Ilimchukua zaidi ya dakika 20 kuzungumzia uteuzi wa Pence akisema 'now back to Pence'

  Hili lililondoa ladha ya kumtambulisha mgombea mwenza

  Alipopewa nafasi ya kuongea, Pence alionekana mtu makini kuliko Trump. Wasi wasi umetanda kama hatamfunika Trump katika kampeni.

  Uteuzi huu umeacha ukakasi kwa Spika wa zamani wa Bunge Bw Newt Gingrich aliyetarajiwa sana. Pia mtiifu gavana wa New Jersey Christie Christie

  Na katika mbinu za kisiasa, mkutano mkuu wa Republican utamalizika Alhamisi kwa Trump kukubali uteuzi rasmi.

  Tunatarajia , katika kipindi hicho Hillary Clinton atatangaza mgombea mwenza ili kufunika hoja zote za mkutano mkuu wa Republican

  Kati ya kesho na Ijumaa mgombea mwenza wa Democrat atatangazwa.
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Ulinzi wa Trump na Hillary ni sawa na ungharamiwa na Taifa.Wakati wa kampeni, Trump alipotoa kauli za 'maudhi' ilibidi aongezewe 'secret service' kumlinda
  Mkutano mkuu unalindwa kwa gharama zote bila kujali chama gani kipo madarakani nani
  mpinzani. wagombea wanapewa haki sawa

  Kwasasa Trump na Clinton wamepewa access ya classified information ili kuwawezesha kujenga hoja kutokana na hali ya nchi, kiulinzi , usalama na kiuchumi.

  Wote wanasimama sawa mbele ya sheria ya uchaguzi

  Ndio maana tulihoji sana, ilikuwaje mzee Warioba akashambuliwa na wahuni pale Ubungo plaza ambao wengine tunajua walizawadia.

  Mzee Warioba aliongoza tume kubwa nchini na alistahili ulinzi mkubwa

  Kwavile tu wakati huo hakupendeza wahusika kwa maoni ya tume, suala la ulinzi likapewa kisogo huku wakisema '..naomba mungu aniepushe na adha iliyompata mzee Warioba' Halikuwa suala la ulinzi tena bali siasa za mtaroni

  Wanasiasa wanamshambulia Obama perfect and square, rekodi inawekwa wazi hoja zinadadavuliwa. Siyo suala la kumfanya Obama mtukufu.

  Wenzetu kiongozi amebeba dhamana na anachukuliwa kwa uzito huo​
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Taratibu za uchaguzi wa Marekani

  Mwaka 2008 mkutano mkuu wa kwanza kufanyika ulikuwa Democrat
  Mwaka 2012 mkutano mkuu wa kwanza kufanyika ulikuwa Republican
  Na mwaka 2016 mkutano mkuu wa kwanza ni Republican

  Haya haytokei tu kwa chama kuamua kupanga. Ni utaratibu uliokubalika na vyama kwamba chama pinzani ndicho huanza mkutano mkuu kikifuatiwa na chama kilichopo madarakani

  Hivyo, Rep kufanya mkutano wao sasa hivi ni sehemu ya utaratibu na utamaduni uliokubalika katika siasa za Marekani

  Ni kama ilivyo uchaguzi mkuu. Huu hufanyika Jumanne ya kwanza inayofuatia Jumatatu ya kwanza ya mwezi November.

  Hapa ieleweke kuwa si lazima iwe Jumanne ya kwanza ya mwezi November ambayo inaweza kuwa ni tarehe 1, bali Jumanne ya kwanza baada ya Jumatatu ya kwanza ya November

  Kwa mantiki siku ya uchaguzi wa Jumanne hiyo ni kati ya tarehe 2-8 November.

  Haya ni mambo yapo tu yanasubiri muda kutokea kila msimu
  Hayahitaji tangazo la tume yoyote, ni utamaduni wa siasa zilizokomaa

  Katika kipindi hiki, wagombea hupewa taarifa na Rais 'briefed' linapotokea jambo lolote lenye masilahi ya Taifa hasa dharura

  Swali litakaloulizwa, mbona watu hawasikii tume ya uchaguzi ya Marekani?

  Nani anakusanya matokeo na kujumlisha kama Tume yetu ya NEC?

  tutajadili
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nguruvi3, leo kaulimbiu ya GOP itakuwa make America work again lakini kinachojadiliwa hadi sasa ni purukusani iliyogubika Convention katika siku ya kwanza. Ilianza kwa baadhi ya wajumbe kutomkubali Trump na kutaka sheria zifanyiwe marekebiso, ikafuatiwa na hotuba aliyotoa Mama Trump ambayo imekuja kugundulika ni plagiarism ya ile ya Mama Obama mwaka 2008.

  Kwa kweli Convention ya GOP imeanza vibaya na leo watu wanasubiri kuona mabadiliko katika ukomavu kiuendeshaji. Wengi wanajiuliza inakuwaje mtu ambaye amekuwa akijitamba na kuwaita mahasimu wake wa siasa wajinga anashindwa kuwapata watu makini wa kumsaidia. Je atazungukwa na watu wa aina gani wataokuwa washauri wake wakuu serikalini akishinda Urais?

  NB: Hiyo ya Tume ya Uchaguzi Marekani ni habari nyingine kabisa ha ha haa...!
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #14
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Aliyekuwa kampeni meneja wa Trump aliyefukuzwa June Lewandowski amesema aliyehusika wajibishwe.

  Chair wa RNC Priebus akizungumza 'pengine' angemfukuza aliyehusika

  Trump kampeni imekataa kumwajibisha mtu au kuomba radhi

  Habari ya 'desa' imebeba uzito 'over shadow' ujumbe mzima uliotolewa jana.
  Haionekani kama itapotea muda mfupi na imefungua uchunguzwaji zaidi

  Hii itaondoa confidence kwa wale wanaotegemea kusoma.
  Haitakuwa na tatizo kwa wazungumzaji wa 'asili' kama Rudi Gulian

  Rudi Gulian alifanya kazi nzuri ya ku move audience kwa hamasa kubwa.

  Tatizo kwa Rudi ni hisia kuwa ameifanya 9/11 yake, na mtaji kisiasa

  Ndio hasa kilichopelekea akagombea Urais mara 2 zote akishindwa vibaya

  Kwa theme ya leo, Rep wanatakiwa wawe waangalifu sana.
  Kushambulia rekodi ya employment itawasumbua katika fact checks

  Hali ya ajira ni mbaya,rekodi inaonyesha miezi 75 mfululizo kuna tengenezo la ajira.

  Zipo baadhi ya rekodi zinazosemwa Obama anamkaribia Reagan kitakwimu
  Tutafuatilia kupata ukweli wa hili

  Ajira za mwezi June zinaonyesha kutengenezwa ajira 250,000 taofauti na matarajio.
  imeamsha hamasa katika masoko ya mitaji yaliyodorora kutokana na Brexit

  Republican wanapoweza kumbana Clinton ni katika trade kama NAFTA

  Tatizo ni kuwa mgombea mwenza Mike Pence yupo katika rekodi akitetea trade.

  Wanachoweza kufanya ni kuchukua maudhui ya 'B.Sanders' na kumshambulia Clinton.

  Hapo watakuwa na rekodi ya kujitetea kuwa hata Dem wamesema hayo.

  Inatosha kusema, plagiarism imetibua siku ya kwanza ya mkutano

  Imefunika habari zote na kuwa mjadala.
   
 15. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  Plagiarism at its best but then Trump gets away with almost everyhting!​
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2016
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Breaking News!
  Donald J. Trump is no longer the presumptive nominee for President of the United States but the GOP official nominee. He reached the threshold of 1237 delegates at 7:12 pm Eastern Time with votes cast by delegates from his home state of New York.
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Jul 20, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Lile kundi la never Trump safari imekwisha, Trump ndiye nominee

  Sasa hivi anaongea Speaker Paul Ryan aliyekuwa mgombea mwenza wa Mitt Romney
  Anaongea kuhusu uchumi. Huyu ana degree ya uchumi (Ohio)

  Katika mchakato Spika Ryan ali criticize hoja kadhaa za Trump kama ya kuondoa Muslim, na hata Immigration. Uwepo wake unatokana na hadhi kama Spika hata hivyo kimoyo yupo na akina Romney.

  Ryan ni potential candidate kwa miaka ijayo.

  Convention inaendelea
   
 18. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #18
  Jul 20, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Donald Trump Jr amemaliza kuongea. Ameongea fluently pengine kuliko baba yake
  Ilikuwa ni powerful speech ikiwa na substances ukiacha misinformation za hapa na pale

  Amemuelezea baba yake na kueleza baadhi ya hoja dhidi ya Clinton ambazo baba yake anasimamia. Kuna risk ndani yake lakini ameeleza kwa weledi

  Kwakweli hotuba yake imefunika mauza uza ya mama yake ambayo ni talk kwa siku nzima
   
 19. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #19
  Jul 20, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Dr Ben Carson

  Kwasasa anaongea Dr Ben Carson ambaye sehemu kubwa anamshambulia Clinton
  Anazungumzia one nation under God akizungumzia mahusiano ya Clinton, Saul Olinsky na kitabu cha Lucifer. Hapa anawavuta evangelical

  Dr Ben Carson alikuwa mgombea na hadi anajitoa alikuwa na wajumbe takriban tisa
  Kampeni yake ali ielekeza katika kuwapata evangelical hata hivyo hakufanikiwa

  Dr Carson ni paediatric suregeon na si Dr of Divinity kama wengine wanavyoweza kuelewa kwa neon Dr na kauli zake
   
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #20
  Jul 20, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Kimberlin Brown (actress)

  Huyu ni celebrity wa 'the young and resless' ambaye ni businesswoman pia
  Anongelea wanawake na suala zima la business.

  Kimberlin anaongelea Obamacare ilivyoathiri business zake akiwahusisha vijana.
  Hapa anasema, hao vijana walioathirika ndio watampigia kura Trump aondoe Obamacare

  Anazungumzia Clinton foundation kwa kusema, wanaume wanalipwa vema kuliko wanawake.
  Hoja yake hapa ni kuwavuta akina mama kwa kuonyesha foundation ina ubaguzi dhidi ya wanawake. Tutafuatilia fact check

  Kimberlin anaongelea trade na jinsi inavyoathiri trade na business za watu

  Anazungumzia Clinton kama mwanamke aliye attack wanawake wenzake.
  Kwamba comments zake zimewadhalilisha wanawake. Hivyo, anasema wanawake wapo katika bunge na seneti siyo Clinton.

  Amemaliza
   
Loading...