Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

LEGAL PERSPECTIVE

Kuna mwanasheria Paul Callan ameandika Makala kuhusu sakata hili linaloendelea
Callan anasema, FBI wamevunja utaratibu wa kufanya uchunguzi kwanza na kuja kwa umma na conclusion

Kitendo cha Director wa FBI kusema hana uhakika kama email zina impact au hazina katika uchunguzi unaondelea hakikuwa sahih. Alichotakiwa ni kuja na conclusion kuhusu uchunguzi ambao kwa muda mrefu umeendelea

Ameandika kuwa kuhusu siku 11 kabla ya uchaguzi na kwamba kauli ya 'Dir hajui kama kuna impact au la' inasumbua katika mtizamo wake.

Clinton ameendelea na kampeni Florida. Hili suala lime derail kampeni yake iliyokuwa inaendelea vema hadi jana
Kwa sehemu kubwa, tuhuma hizi zina impact katika maeneo haya

1. Kwa early voter, hili halina impact kwani kura zimeshapigwa
2. Kwa wafuasi wa Dem halina impact kwani watapiga tu kwa Clinton
3. Kwa wasiompenda Trump nao watapiga kura tu kama hivyo. hata hivyo hili linaweza kuwa put off kwavile tayari wana struggle kati ya kuacha chama chao na haya yanayotokea

4. Kwa independents inategemea ni wa aina gani
a) Kwa independents wenye weledi watafutalia kupata ukweli
b)Kwa independents waliokuwa wanasubiri muda hili litakuwa limewa move

Tatizo: Tatizo kubwa ambalo Comey amelisababisha kwa kampeni ya Clinton si kuhusu emails ambazo hajasema impact yake. Tatizo kwa kampeni ya Clinton ni Trump ambaye amelichukua suala hili na kulitolea hukumu

Tayari anasema kuna classified information, kuna illigal server,ame link masuala yote pamoja na emails zote tulizoeleza hapo juu

Trump ni mzuri sana wa ku hype na hili impact yake ni kubwa katika electoral map

Swali linabaki FBI wataweza kutoa matokeo katika siku 10 za uchaguzi? Hapa ndipo Comey anapojikuta katika wakati mgumu

Tunafuatilia
 
Hii kashfa ya emai ya Hillary Clinton ina impact kubwa sana hvyo usijaribu kumtetea hata kidogo, maana ninajua kabisa wewe unampigia kampeni HC mitandaoni.
Japo unajifanya mchambuzi lakini hauko fair

Swali;
Hivi unalipwa sh. Ngapi na HC?
 
Hii kashfa ya emai ya Hillary Clinton ina impact kubwa sana hvyo usijaribu kumtetea hata kidogo, maana ninajua kabisa wewe unampigia kampeni HC mitandaoni.
Japo unajifanya mchambuzi lakini hauko fair

Swali;Hivi unalipwa sh. Ngapi na HC?
Jamani mbona mnakuwa hivyo? Nimeeleza source ya nani kasema nini, sijasema.

Pili nimefanya analysis na hapo nimeweka wazi scenario zote zenye positive na negative

Tunachokifanya si kupiga kampeni kwasababu hatusikiki Marekani wala hatupigi kura

Hapa tunafanya analysis ya nini kinaendelea.

Please naomba uzi uwe kama ulivyo na si simba na yanga

Hebu rudi usome kwa makini ili uelewe kwanini nimeandika

Kwa mfano, nimesema Comey ametoa taarifa isiyo na conclusion.
Hayo si maneno yangiu ni barua ilivyo ambayo haikusema kama kuna conclusion yoyote na ndivyo watu wote wanavyoiangalia

Nikasema FBI wapo katika wakati mgumu. Hili ni kutokana na ukweli kuwa Democrat na Republican wametoka kwa pamoja na kusema ukweli uwekwe wazi

Halafu kasome pia, nimesema Trump ka hype story. Haya kayasema Colarado muda mfupi uliopita. Alichosema hakimo katika barua ya FBI kwa bunge kama inavyosomeka

Na nikaeleza impact ya suala hili kwa kusema wazi lina athari
1. Wale waliopiga kura tayari hawana namna wamepiga tayari iwe kwa Trump au Hillary
2. Wale watakaompigia Hillary watabaki hivyo kama wale watakaompigia Trump.
4. Nikaenda mbali na kusema kuna independents, nao nikawagawa

Mwisho nikasema suala hili lina impact katika electoral map.

Nadhani wanaosoma between the lines with no prejudice wanaelewa hilo lina maanisha nini. Kuna impact gani haijulikani

This is how we discuss, na inaweza ukawa na maoni tofauti na hayo.

Ni vema ukachukua hoja ukaonyesha upande wa pili wa hoja hiyo na si kama ulivyochangia kwa hasira , ghadhabu na kupoteza maana
 
Hii kashfa ya emai ya Hillary Clinton ina impact kubwa sana hvyo usijaribu kumtetea hata kidogo, maana ninajua kabisa wewe unampigia kampeni HC mitandaoni.
Japo unajifanya mchambuzi lakini hauko fair

Swali;
Hivi unalipwa sh. Ngapi na HC?
Duh, Nguruvi3 alipwe kumtetea HC hapa JamiiForums ili iweje? Ili Wamarekani wanaosoma JF wampigie kura? Pamoja na hayo, hiyo impact unayoongelea ni kwa nani...Clinton, Trump au Comey (FBI) Je ni positive au negative?
 
Kwa Hillary Clinton
 
Nguruvi3
nimekuelewa.. nadhani uchaguzi wa U.S.A hauna tofauti na wa Tanzania. Maana hawako fair hata kidogo na chama kilichopo madarakani kinatumia kila njia kibaki madarakani, mfano mpaka Michelle Obama naye eti anakuja kukinusuru chama
uchaguzi uliopita Obama alimuita H. Clinton kuwa ni kiongozi dhaifu, why sasa anampigia kampeni namna hiyo?

Na hizo poll za marekani hazina utofauti na zile tafiti za TWAWEZA, ni uzushi mtupu tu
 
Ndugu yangu, afadhli umesema

Vyombo vyote vya habari vinasema barua imesema kuna 'email pertinent' kwa maana hakuna anayejua ni relevant au irrelevant. Hakuna chombo chenye details, wenzetu wengine hawaelewi hilo

Tuliozungumzia electoral map, electoral process n.k. hatuna maana nyingine bali kufanya information simple ili wanaofuatilia waelewe kwa undani nini kinaendelea.

In the end kila mmoja akijua process ana uwezo wa kusema hili right lile wrong. That's the objective ya uzi

Kuna mchangiaji 'x' ka pm na kusema hakuelewa kwanini Rais anaweza kuchaguliwa na watu 'popular vote' nyingi na bado asiwe Rais.

Anasema ilikuwa concept inayochanganya hadi aliposoma kuhusu uchaguzi unavyofanyika

Kama kuna mtu anaelewa jambo huyo ni bora kuliko washabiki ku criticise kwa hoja bali feeling au kutafuta typo error. That's not all about this thread

Kama tulivyoahidi, Tarehe 8 tutakuwa na uzi 'election night in America' tukileta matokeo in real time
Hatuna uwezo wa kuzuia matokea achilia mbali ku influence uchaguzi kwa njia yoyote!
 
Nguruvi3
nimekuelewa.. nadhani uchaguzi wa U.S.A hauna tofauti na wa Tanzania.

Maana hawako fair hata kidogo na chama kilichopo madarakani kinatumia kila njia kibaki madarakani, mfano mpaka Michelle Obama naye eti anakuja kukinusuru chama

uchaguzi uliopita Obama alimuita H. Clinton kuwa ni kiongozi dhaifu, why sasa anampigia kampeni namna hiyo?Na hizo poll za marekani hazina utofauti na zile tafiti za TWAWEZA, ni uzushi mtupu tu
Uchaguz wa US na Tz ni mwanga na giza.

Unashangaa Michelle, mbona Obama , Biden wanakampeni?

Polls zinafanywa na institutions zenye reputations zake bila kujali hali ya kisiasa
Zipo zinazofanya za kisiasa ,na hapa unatakiwa kujua zipi unaangalia

Kwa hoja zako hapo you need to be calm and composed while learning
 
Hii kashfa ya emai ya Hillary Clinton ina impact kubwa sana hvyo usijaribu kumtetea hata kidogo, maana ninajua kabisa wewe unampigia kampeni HC mitandaoni.
Japo unajifanya mchambuzi lakini hauko fair

Swali;
Hivi unalipwa sh. Ngapi na HC?
Ulikuwa na hoja nzuri tu,sema umepanic sana. Kuwa upande fulani si tatizo la nguruvi3 au mag3 peke yao ni tatizo la watu wote Duniani..!! Hata angekuwa mchambuzi gani,lazima atakuwa na upande. Iwe kwenye uchaguzi,michezo etc.

Wewe mwenyewe unasema hivyo kwa sababu una upande. Yote haya mwisho wake ni maamuzi ya wamarekani wenyewe. Najua wewe tupo kundi moja,we ni shabiki wa trump km mimi. Nataka nikuondoe shaka,wamarekani hawawezi kumpa huyo bibi urais wa US.

-Kwanza Haaminiki na suala la Emails limethibitisha hilo.

-Pili Chama chake kimepata nafasi ya kuongoza vipindi viwili mtawalia,hapa wamarekani huwa wanahitaji mabadiliko na hiki ndo kipindi cha mabadiliko.

-Tatu kumchagua HC ni kumrudisha ikulu Bill clinton,hili halisemwi kwenye majukwaa,na hata likisemwa vyombo vya habari havilisemi. Lkn ukweli ndo huo,wamarekani hawawezi kufanya huo ujinga! Rais ajaye pamoja na makandokando yake ni DONALD J.TRUMP. mark my words!
 
Update

Kuna habari kuwa DOJ (idara ya sharia ya Marekani) ilimshauri FBI Dir asiandike barua ile kama alivyofanya
Inaonekana Dir aliomba ushauri wa kisheria kutoka katika serikali

Kuna kanuni inayosema katika muda wa siku 60 vyombo visiingile au ku influence uchaguzi kwa namna yoyote

Na ni kawaida uchunguzi wa FBI kukamilika kabla ya kutoa conclusion. Lakini pia, FBI haina role ya prosecution, hiyo ni kazi ya prosecutor au crown. Inapotokea kuna mgongano wa kisheria basi hutafutwa private prosecutor

Barua iliyoandikwa haikuwa na conclusion isipokuwa ilisema kuna 'pertinent' information

Inawezekana ipo link au hizo pertinent zinaweza kuwa kweli au si kweli.

Kwa hali yoyote GOP na Dem wamemtaka aweke wazi uchunguzi huo

Hii ina maana gani?

Kwanza, atakuwa ame influence uchaguzi kwa namna yoyote matokeo yake yatakavyokuwa na kukiuka kanuni inayokataza hilo katika siku 60 kabla ya uchaguzi

Pili, akitoa hoja za kushtakiwa uchaguzi mzima utakuwa umevurugika.

Njia aliyo nayo Dir
1. Kuacha suala hilo hadi uchaguzi upite. Challenge itakayomkabili ni 'rigged' election kama Trump anavyosema
2. Endapo Hillary atashinda (assumption) taratibu zitakazofuata zitakuwa impeachment
3. Hillary akishindwa tayari Comey ataonekana ku influence uchaguzi

Kisiasa
Kwa uzito wa suala hili, kampeni ya Clinton imetoka na kumtaka Comey aweke wazi kila kitu
Hili ni katika kuruidhsa Imani na kuzuia uharibifu Zaidi unaoweza kutokana na hilo

Unaweza kuona walivyomweka Comey katika mazingira magumu

Tunaendelea kufuatilia
 
Nguruvi3
nimekuelewa.. nadhani uchaguzi wa U.S.A hauna tofauti na wa Tanzania. Maana hawako fair hata kidogo na chama kilichopo madarakani kinatumia kila njia kibaki madarakani, mfano mpaka Michelle Obama naye eti anakuja kukinusuru chama
uchaguzi uliopita Obama alimuita H. Clinton kuwa ni kiongozi dhaifu, why sasa anampigia kampeni namna hiyo?

Na hizo poll za marekani hazina utofauti na zile tafiti za TWAWEZA, ni uzushi mtupu tu
Mkuu mimi nadhani tukubali kuwa wenzetu "wametuzidi " kwenye demokrasia. Ebu fikiria "the any former First Lady " wa nchi yetu ateuliwe kuwakilisha chama kugombea urais nyakati hizi!! Hivi patakalika kweli hapa, na aina ya opposition parties tulionao!? Katika hili nadhani 'wametutangulia '.
 
Ni kweli wako mbali kidemokrasia
 
Nguruvi3
nimekuelewa.. nadhani uchaguzi wa U.S.A hauna tofauti na wa Tanzania. Maana hawako fair hata kidogo na chama kilichopo madarakani kinatumia kila njia kibaki madarakani, mfano mpaka Michelle Obama naye eti anakuja kukinusuru chama
uchaguzi uliopita Obama alimuita H. Clinton kuwa ni kiongozi dhaifu, why sasa anampigia kampeni namna hiyo?

Na hizo poll za marekani hazina utofauti na zile tafiti za TWAWEZA, ni uzushi mtupu tu

mkuu kwenye hili jukwaa nenda kwa step....soma zaidi ya kuandika
 
Trump kasema hao wanawake wanamsingizia, na ameahidi kuwa shughuli za uchaguzi zikiisha lazima awafungulie mashtaka. Mpaka hapo, hilo suala kasha limaliza...hata wakitokea wengine...hawatakuwa na impact. Ni kwa sababu hii ya Trump hao evangelical christians...wamerejesha imani kwa Trump; nao wanaona kasingiziwa, vinginevyo hasingetishia kwenda mahakamani.

Kumbuka kuwa kesi hizi zimepata uzito baada ya kuibuka kwa ile audio clip ambapo Trump amesikika akikiri wazi wazi kuwa amekuwa akiwatomasa maungo kinamama jinsi atakavyo. Hii haiwezi kufutika kirahisi kwa yeye kutoa tamko na kutishia kuwashitaki watuhumu wake.
 
Mkurugenzi wa FBI kwa namna moja au nyingine sasa anaanza kuangaliwa kwa jicho tofauti kwamba anafanya kazi kwa kufuata shinikizo la republicans. Kulingana na matokeo ya uchunguzi wake yatakavyokuwa mwisho wa siku inaweza kumjenga au kummaliza. Sina hakika kama kwa kipindi kifupi kilichobaki kabla ya uchaguzi ataweza kukamilisha uchunguzi wake ili kuufunga mjadala huu once and for all na akishindwa kupata uthibitisho wa kumtia hatiani Clinton basi kibao kitamgeukia yeye kwamba amekuwa akifanya kazi kwa shinikizo la republicans ambao yeye pia ni mwanachama wake!
 
Mkuu Mwalimu usitishwe na hayo maneno ya wanasiasa. Hiyo janja ya kuinasua kampeni ya bi clinton ambayo iko dhoofulihali kwa sasa!! Malalamiko hayo ni kawaida na hayana tofauti na yale ya Republican,pale FBI waliposema hawakuona kosa ktk zile emails za awali. Republican na aliyekuwa mgombea wa Democrat Bernie sanders walililamikia uamzi huo.

James Comey hatishwi na kauli za viongozi wa Democrat yeye anafanyakazi yake kwa mujibu wa sheria. Hiki ndo kitanzi cha Bibi,ikulu imeshaota mbawa na atashitakiwa tu atake asitake!!
 
Bado ni mapema mno kuhitimisha matokeo kutokana na uchunguzi huu ambao bado unaendelea ambapo matokeo yake ndio yataamua hatima ya uchaguzi. Endapo uchunguzi utamkuta Clinton ana hatia then hii itabadilisha uelekeo kwa kiasi kikubwa kwa faida ya Trump, lakini endapo uchunguzi hautamkuta Clinton na kosa lolote then Comey atakuwa amejitwisha gunia la misumari. Mpaka pale uchunguzi utakapokamilika na matokeo kuwekwa hadharani ndipo tunaweza kusema kwa hakika kwa nani anasimama kwenye nafasi nzuri.

Pia kumbuka kwamba wagombea hawa wawili wana kundi kubwa la wafuasi wanaowaunga mkono ambalo bila kujali misukosuko inayoendelea wako tayari kuendelea kuuunga mkono wagombea wao. Kwa jinsi ile ile ambayo watu wa Trump wameendelea kumuunga mkono mtu wao pamoja na tuhuma za unyanyasaji kingono ndivyo hivyo watu wa Clinton wanaamuunga mkono mtu wao pamoja na tuhuma hizi za email.
 
Back
Top Bottom