Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA | Page 29 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Jul 19, 2016.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Jul 19, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,219
  Likes Received: 7,338
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi Marekani

  UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI

  Baada ya kumalizika chaguzi za ndani ya vyama, kilichopo ni uchaguzi mkuu wa Marekani
  Wagombea ni Donald Trump wa Republican na Hillary Clinton wa Democrat

  Uzi huu utakuwa mwendelezo hadi uchaguzi utakapomalizika.

  Kabla hatujaendelea na mijadala, tuangalie lililopo mbele kwa sasa.

  Mkutano mkuu wa Republican ulioanza leo
  Mkutano ni wa kumtihibitisha mgombea kiutaratibu wa vyama, na kuweka sera za vyama mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu.

  Mkutano mkuu wa GOP upo Cleveland
  Kwasasa mkutano umeanza na wazungumzaji kadhaa wameshaongea.

  Agenda kubwa ya leo ni ulinzi na usalama wa Taifa.

  Hii ni nguzo katika chama cha Republican. Kwamba, huitumia katika katika chaguzi.

  Katika waongeaji wa leo, mmoja ni Lt Gen mstaafu Michael Flynn, Director of Intelligence Agency kabla. Mwingine ni Joni Ernest seneta wa Iowa, ambaye naye pia ni mstaafu

  Mayor wa zamani wa New York, Rudi Gulian aliongea akiambatanisha hotuba yake na mambo ya ulinzi wa ndani, akiwazungumzia Polisi na walinzi wengine.

  Wiki moja iliyopita Rudi alihoji mauaji ya askari kutokana na kile kinachoitwa black lives matter. Gulian alisema, iweje kundi lisisimame kwa mauaji ya vijana kule South Chicago.

  Rudi Gulian anaonekana kama alama ya 9/11 kutokana na kuwa meya wakati huo.
  Hivyo kuongea kwakwe kunafungamishwa na suala la ulinzi na usalama.

  Kinachoonekana kwa siku ya kwanza, ni suala la ulinzi hasa ugaidi.

  Hili linafungamanishwa na Hillary Clinton na emails(Benghaz).

  Kuna wakati Lt Gen Michael alimshambullia Obama kwa uwepo wa ISIS na Osama.
  Gen alikosea kwani kuingiza Osama na Obama ni kutoa point kwa Democrat

  Mkutano mkuu ulianza kwa kupingwa na makundi nje, hata hivyo hali imetulia.
  Jambo moja ni kuonekana kwa baadhi ya watu mashuhuri kama Gav wa Texas Rick Perry

  Hata hivyo, safu kubwa ya viongozi nguli kama Familia ya Bush, Mitt Romney, John McCain haipo katika mkutano mkuu na kupunguza hamasa kwa kiasi Fulani

  Mbinu wanayotumia GOP ni kutisha Wamerekani kuwa hawapo salama.

  Mbinu ya pili ni kumshambulia Clinton, wakitambua kumshambulia Obama ambaye approval rate yake ipo katika 50% italeta tabu.

  Tutaendelea kila wakati kutokana na yanayojiri
   
 2. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #561
  Nov 8, 2016
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,767
  Likes Received: 2,668
  Trophy Points: 280
  Earlier she (HRC) said in a radio interview that if she won she would call Mr Trump and hoped he would play a "constructive role" in helping to bring the country together.
  Source :BBC
  =====
  She's backing off too, uh!!
  ------
  'Mama' kaona nini mbele?
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #562
  Nov 8, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,219
  Likes Received: 7,338
  Trophy Points: 280
  No Tujitegemee,let be honest.

  Hii kauli aliitoa baada ya mdahalo wa pili alipoulizwa kama atakubali Trump akishinda

  In fact hata Obama amesema kabla, atamkabidhi ofisi wananchi wakiamua Trump ndiye mshindi

  Hii kauli inakuja kufuatia kauli ya Trump kuwa 'ameweka suspense' kauli ya kukubali matokeo

  Si kauli ngeni na ndiyo inayotumika kumhukumu Trump kwa kukataa kukubali matokeo

  Nayasema haya kwasababu yapo katika rekodi na tujaribu kuwa wakweli

  Kauli yake si mpya na haielezi chochote kuhusu matokeo unless kuna habari nyingine
   
Loading...