Mkuu nguruvi3 me nashangaa unapata shida ya nn hapa..! James comey yuko sahihi kwa sababu bi clinton akipatikana na makosa,kosa lake ni la kijinai. Hiyo sheria ya hatch act ingawa sijaisoma lkn kwa vyovyote haiwezi kuzuia makosa ya kijinai kuchunguzwa hata km ni ndani ya siku 60 zilizotajwa.
Lkn lingine mkuu
Nguruvi3 HC hatakiwi marekani, hili limefanyika ili kupunguza hayo makali yake ili iwe Rahisi kwa trump kushinda bila mizengwe! National poll kwa sasa ni :Clinton 46%+1 na trump 45. Mpaka jtano naamini trump ataongoza mpaka siku ya uchaguzi yenyewe!!!
Mkuu suala la kupata tabu linatoka wapi?
Nimeeleza tangu mwanzo, hatuna influence yoyote kwa uchaguzi wa Marekani na tupo takribani km 13,000 kutoka sanduku la kura, kwanini unadhani tunapata tabu na ili iweje!
Nadhani hujafuatilia nyuzi hii kwa undani na nyingine zilizotangulia.
Dhima yetu si jingine bali kujadiliana katika upana na kuweka scenario na perspective mbali mbali ili wasomaji waokote kimoja au viwili. Hilo tu
Mathalan, hukujua Hatch act na sasa unaweza kufuatilia na kuijua ili kesho ukija utupe kile tusichokiona au kile unachokiona tofauti. Hivyo ndivyo mijadala inavyokuwa.
Mbona hatukupata tabu kueleza process nzima ya uchaguzi wa Marekani kuanzia primaries hadi sasa?
Pengine kwa kutoangalia mambo kwa upeo mpana, na kuongozwa kwa ushabiki kuliko hoja, tayari unasema kuna 'criminal offense' Hebu tueleze chombo gani kimesema hayo?
Lini investigation ikawa 'crime' na hayo ndiyo aliyosema Comey?
Jiulize kama ni simple hivyo, kwanini vyombo vyote Marekani vimegeuza Comey kuwa subject?
Sasa kama Trump au Clinton hatakiwi US hayo ni maoni yako na tunayaheshimu, siyo facts
Ukisoma mabandiko mawili hapo juu, hakuna mahali nimesema Comey yupo wrong.
Zipo sehemu nimeuliza, na hiyo ni njia ya kuleta fikra kwa msomaji bila kumwekea maoni.
Ni vema kama ungalikuja na 'rebuttal' ukishambulia hoja moja hadi nyingi kwa mtazamo na faida yetu sote
Sipendi kabisa kusema haya baadhi wameeleza kwa lugha laini, lakini tulipofikia pengine ni muhimu kusema. Nadhani upo katika wrong forum
Ahsante