During your life never stop dreaming. No one can take away your dreams

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
1,328
3,691
"During your life never stop dreaming. No one can take away your dreams"
- Tupac.

NDOA ni chanzo kimoja wapo kilichochangia kiasi kikubwa cha kutokomeza kama sio kuua kabisa ndoto za watu wengi katika jamii. Watu walikuwa na malengo na kumiliki biashara kubwa, kuwa wanasheria mashughuli na kada kadha wa kadhaa.

Lakini malengo yao na ndoto zao zimefifia baada ya kufunga ndoa kwani wamekutana na sheria na miiko mbalimbali katika ndoa hizo.

Wengi wao mfano, wanawake wamekuwa kwenye ndoa kwa nafasi ya kulea watoto na kuhudumia kazi za nyumbani. Sababu wanakutana na upinzani mkali kutoka kwa wenza wao wasio penda walishughulishe kwa chochote nyanja ya kiuchumi.

Pia baadhi ya wanaume wanasema usije oa mwanamke wanasheria, nesi na taasisi zifananazo na hizo kwa sababu tofauti tofauti wanazozijua wao. Hivyo imechangia kiasi kikubwa cha Kuua ndoto za wenza wao badala ya kuwa sapoti.

Jamii imelifanya jambo la kuoa kama ni lazima sababu ya umasikini kwenye jamii zetu hususani afrika. Unakuta msichana anakatishwa kuendelea na masomo sababu ya uchu, tamaa na umasikini kwa wazazi wakitegemea mahari baada ya kumlazimisha mtoto wao kuolewa.

Somewhere in Tanzania kuna mzazi aliyesababisha vifo vya watoto wake wawili wakike baada kuwa achisha shule na kuforce kuwa peleka kwa mganga wa kienyeji ili wapewe dawa ya kuotesha maziwa(chuchu) hili awapeleke wakaolewe, sababu ni umasikini na tamaa za Mali.

Leo hii watu mbalimbali wamepoteza maisha sababu ya kadhia mbalimbali wanazokumbana nazo katika ndoa zao.

Wazazi wanawapangia na kuwachaguli watoto wao wenza kuangalia kigezo cha unafuu wa maisha na kupelekea kuwanyima haki za msingi za watoto wao za kuchagua mtu sahii wa kuishi nae.

Kwa kumalizia nasisitiza KATAA NDOA, kwasababu ni mfumo usio rasmi unaotetewa na jamii kwa maslahi yao binafsi, na kutokomeza matarajio ya watu kuwa vile wanavyotaka wawe.
 
Back
Top Bottom