Unyanyasaji ndani ya nyumba za wanandoa

Shining Light

JF-Expert Member
Jan 8, 2024
214
291
Ugomvi ndani ya nyumba ya wanandoa huchukuliwa kama ni jambo la kawaida, Inasikitisha kusikia kwamba ukatili huu unachukuliwa kama jambo la kawaida katika jamii yetu. Watoto huona huu unyanyasaji na kuhishi pia ni jambo la kawaida mpaka wanapo kuwa na kupata ufahamu zaidi na hapo ndio kujua baba alikuwa anakosea sana kumpiga mama.

Jambo hili halimuathiri mama mtu ila pia watoto, linaweza sababisha mtoto wa kiume kukuwa na kuamini ni sawa kupigana au kuwapiga wenza wao ni kitu cha kawaida kabisa ila pia hata mtoto wa kike kuona ni jambo la kawaida kupigwa na mwanaume.

Mara nyingi majeraa makubwa yakitokea, Wanawake hushtaki kwa ndugu wa mwanamme na mara chake kushitaki kwa polisi kwa sababu kuna Imani kuwa anatia aibu familia na kunyanyapaliwa katika jamii kwa kukosolewa kuwa hivyo sivyo unatakiwa kuishi na mumewe au mpenzi wako.

Wanawake ndio huwa waathrika zaidi katika ugomvi wa wanandoa, huteswa na kupigwa na wenza wao. Huwa hupigwa makofi, mateke, kupigwa na vitu tofauti kama mikanda nakutishwa kisu muda mwingine mpaka mapanga.

Vilevile hudhalishwa, tukanwa matusi mazito, na muda mwengine hulazimishwa kufanya tendo la Ndoa bila kujali hali zao au kutaka hidhini yake.

Hii ni changamoto kubwa na ni muhimu sana kuchukua hatua za kurekebisha hali hii ili kuzuia madhara zaidi na kujenga jamii yenye usawa na heshima kwa kila mtu.

Jamii inahitaji kuelimishwa kuhusu madhara ya unyanyasaji wa kijinsia na umuhimu wa kuheshimu na kuthamini kila mwanachama. Elimu hii inapaswa kufanyika kuanzia ngazi ya familia hadi kwenye taasisi za elimu na jamii kwa ujumla. Watoto wanapaswa kuelimishwa mapema kuhusu haki zao na jinsi ya kujikinga na unyanyasaji.

Pia, mfumo wa sheria unapaswa kuimarishwa ili kuhakikisha kwamba wahusika wa unyanyasaji wa kijinsia wanachukuliwa hatua za kisheria. Hii inahitaji uwepo wa sheria zinazolinda haki za wanawake na watoto na utekelezaji wa haki hizo kwa ufanisi.

Zaidi ya hayo, jamii inahitaji kubadili mitazamo yake kuhusu unyanyasaji wa kijinsia. Kuona unyanyasaji wa kijinsia kama jambo la kawaida au la kufumbiwa macho kunahitaji kubadilishwa na badala yake jamii inapaswa kusimama pamoja kupinga unyanyasaji na kusaidia wahanga kupata msaada na haki zao.

Je, Katika Mtazamo wako labda hili jambo unalichukuliaje?
 
Mwanamke huyo huyo anayepigwa akitoka nje amepaka mapoda na anacheka...

Mwanamke ni kiumbe Cha pekee...
 
Mwanamke huyo huyo anayepigwa akitoka nje amepaka mapoda na anacheka...

Mwanamke ni kiumbe Cha pekee...
Duh kumbe ndio mnajijua na kufanana namna hiyoo.

Unapigwa makofi, then unaenda kujiremba usoni, unapaka lipstick mdomoni, unajiseti na nywele zako vizuri, unakimbilia kwenu, then ukifika tu kwenu unafikia kwa kuangua kilio kikubwa na machozi ya kutosha kuwa umepigwa vibaya mno umeumizwa sana, unaongeza na chumvi kuwa umefukuzwa na kutupiwa vitu njee, na akati ukieleza hayo unaeleza huku unalia.

Haa nyie viumbe🙌
 
Back
Top Bottom