Utachaguaje Sasa wakati ujazaliwa eti
Kiranga huyu jamaa vipi unawezaje kichagya uzaliwe au usizaliwe wakati hujui HATA kama Kuna KITU kinaitwa ubongo.
Naamini mtoa MADA hajaelewa ila
Kiranga namsubiri
Mimi nimemuelewa mtoa mada kaongea hoja ya kidhahania ya falsafa kubwa sana
Kwamba.
Ingekuwa maisha ni kama mkataba wa kazi, unapewa kuusoma na kuelewa hii kazi ina wajibu huu na huu, na mshahara huu, asingekubali kusaini mkataba ule na kukubali hiyo kazi.
Kwamba, kama maisha yangekuwa na option ya kukubali au kukataa kuzaliwa kabla mtu hajazaliwa, asingekubali kuzaliwa.
Kuna kitabu kizuri sana kinachambua haya mambo kifalsafa kinaitwa "The Human Predicament : A Candid Guide To Life's Biggest Problems" cha David Benatar, kinaongelea haya mambo kisomi sana.
Nilitaka kukiweka hapa, lakini nikaona bora nisikiweke, kitabu kina mambo mazito sana kinaweza kumfanya mtu ajiue na nisingependa kusababisha hilo.
Kimsingi mtoa mada yuko karibu sana na ukweli kwenye point zake zote, nilikuwa naipitia point moja baada ya nyingine, nikasema kuwa mimi nipo optimistic zaidi yake, lakini hilo linawezekana kuwa linatokana na privilege niliyoipata maishani na mchango wangu kwa watu.
Mfano, mwaka huu nimesomesha watoto wanne chuo. Hawa ni wa kwenye extended family tu hawana support. Nimemkopesha mtu tu nimekutana naye mitandaoni $2,000 kwa mwaka mzima bila riba na wala sina hakika kama atanirudishia. Vimizinga mizinga hivi vya $100 mpaka $500 ndiyo imekuwa kama kawaida. Sasa najiuliza, ningekataa kuzaliwa, hawa waja nani angewasaidia?
Wengine ukiwaambia huna kitu wanakwambia kabisa kuwa General you are the last man standing ukishindwa wewe huku tumeanguka vibaya sana.
So, it's like that movie "It's A Wonderful Life" kwangu mimi. Kama hujaiona itafute.
Kama alivyosema rais J.F Kennedy, mimi sijiulizi dunia itanifanyia nini, najiuliza mimi nitaifanyia nini dunia.
Najua waja wa dunia wana mengi, wengine hata kwenye birthday yako badala ya kukuuliza wakuoe zawadi gani ya birthday wataanza kukuuliza kioande chao cha keki ya birthday kiko wapi?
Ila mtoa maada namuelewa vizuri sana na hizi hoja zake nilizifikiria sana mpaka nikasoma hicho kitabu zimeandikwa kifalsafa zaidi. Mtoa mada kama kaandika kwa hisia raw, anaonekana kama ana hasira yu. Lakini ana hoja za kifalsafa nzito sana.
Nilitaka ku push back point yake ya mwisho namba 8 kuwa hawezi kuchukia kila kitu, kuna vitu atakuwa anavipenda tu. Yani hata hapa JF alipokuja kujieleza, hata kama kuna sehemu anapachukia, lakini hawezi kuchukia mpaka nafasi aliyopata kujieleza na kuona kumbe kuna Kiranga anayaelewa haya mawazo na kashayasoma yameandikwa na wasomi kifaksafa kabisa katika vitabu.
So niliona namba 8 kuna pushback fulani inawezekana kufanyika. Na hiyo oushback ndiyo inayoweza kutumika kuwa hooeful kuwa kuna sehemu ya maisha ambayo ni nzuri bado. Maisha ni bike unavyojipanga kuishi, maisha hayako hapa kukupendelea wewe.
So there is some pushback, especially kuanzia hapo namba 8. Lakini nikaona that is a value judgement statement na yeye ana haki ya kusema hivyo kama yeye.