Na hao wanaompinga Mungu usiwape nafasi, sio ukisikia tu njaa ndio ukamlaumu Mungu hajakuletea lunch, jiulize we umeshamfanyia nini huyo Mungu unaemlalamikia mara zote? Unataka kufanyiwa tu bila kuwa na juhudi yoyote? Yaani ufaulu tu mtihani bila kusoma? Hauwezi kunywa sumu eti kwa sababu tu unahisi kiu!
Amini tu kama ubaya upo basi na wema upo! Kama shetani yupo basi na Mungu yupo! Usiruhusu mtu aliyeingiwa na ushetani akutenganishe na Mungu, usitafute dhambi ya kukufuru bila sababu! Kila mmoja anajua shetani anatafuta wa kwenda nao, hii ni mitandao kila mmoja ana lengo lake humu! Usiwe na uhakika sana kuwa wote ni watu! Mambo ni mengi mamaake..
Mfano huu;
UELEWA KATIKA MAANDIKO NI KWELI UNAMHITAJI ROHO MTAKATIFU.
Kuna mtumishi aliwahi kunikataza kuua mbu nilipokuwa kwake, eti kwa sababu katika amri kumi za MUNGU, moja wapo inasema, "USIUE" akasema kuwa, Mungu hakuainisha usiue nini, yeye kasema usiue, hivyo hatupaswi kuua cho Chote.
Mtumishi alitaka ning'wate na 🦟 halafu nimshukuru MUNGU, kwa sababu andiko linasema, "Shukuruni kwa kila jambo, maana hayo ni mapenzi ya MUNGU" yaani mimi kung'wata na 🦟 ni mapenzi ya Mungu... 😃😃😃😃😃
UELEWA
Nb; doing the same thing over and over expecting different results is insanity..
So try changing how you look at things mate, or else..utalaumu mpk nguo unazovaa!