Dunia imejaa watu waongo

Dunia imejaa watu waongo

Me nina 30 nimeshaenda kuzimu na kurudi hapa hapa duniani, yani cha moto nimekiona.

Kwa kifupi hakuna pigo halijanipiga, kutoka kila kona. Si magongjwa, si uchumi, si mahusiano, labda kifo tu nimeepushwa sijafa, sijafiwa lakini watu hao hao walio hai wanakufanya uone bora ukalale njaa kwenye mti kuliko kuwa karibu nao.

Nikimuangalia Ayubu najiona mimi kabisa.

Maumivu yangu yamenipeleka kwa MUNGU wangu.

Kadri navyoona uovu ndivyo navyouona uso wa MUNGU: yeye ni kinyume kabisa uovu.

Najua kwasababu alishajifunua kwenye sheria zake na kupitia YESU.

Muangalie aliyekuumiza kwa hakika ameenda kinyume na MUNGU alivyoagiza.

Possibly na wewe ushaenda kinyume mara nyingi na umeumiza wengine, na MUNGU alikuacha.

Kwahiyo hii Neema / Rehema uliyoonyeshwa, ielekeze na kwa wengine.

Hawajui walitendalo.

Badala ya kumnyooshea MUNGU kidole, wewe tubu ya kwako,

na kumuomba akuokoe kutoka kwenye hali ngumu / akuondoe kutoka kwa watesi wako.

Utauona mkono wa MUNGU.

"Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.

Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake."

Psalm.24.4-5.NENO
Kiwango cha maumivu ninayopitia nina hakika 💯 sijawahi kuumiza mtu yoyote kwa kiwango hicho
 
Eti umeenda kuzimu na kurudi 🤣🤣
Hayo ni matatizo ya afya ya Akili mkuu.

Yale yale mnakuja ooh nimeonana na Mungu ameniambia hivi na vile 🤣 🤣
Uchizi mtupu
 
Mtu yuko zake hapa anavuta hewa ya bure ya MUNGU,

Akitoka anenda kula zake kitimoto wa MUNGU, anashushia na wine iliyotengezwa zabibu za MUNGU,

Kisha Anaenda kwa demu wake aliyeumbwa na MUNGU,

Anapiga zake kimoja kilichodizainiwa na MUNGU,

Anaenda zake kuoga na maji ya MUNGU,

Kisha analala kwenye godoro lake la kunesanesa lilotengezwa na mazao na vyuma vya MUNGU,

Akiamka full kuperuzi jf na vifaa vilivyotengenzwa na malighafi za MUNGU,

kupost kumdhihaki MUNGU.
 
Mkuu jaziliza madini kwenye andiko lako tupate point za kuunga mkono hoja
 
Pamoja na yote hayo mkuu anakuja mtu anakwambia Maisha yetu yote Mungu anajua mwanzo na mwisho, yaani Mungu ameshapanga tutazaliwa vipi mpaka kifo chetu kitakuwaje.
Kwahiyo matatizo yote unayopitia Mungu alishapanga uyapitie 🤣🤣 Mungu amekupangia upate joto la jiwe mpaka useme 🤣
we acha tu yaan
 
Kiwango cha maumivu ninayopitia nina hakika 💯 sijawahi kuumiza mtu yoyote kwa kiwango hicho
Relax mkuu, usione kwamba Mateso au hali unayopitia ni kwamba Kuna watu uliwaumiza.

Kuna watoto wachanga wanazaliwa wakiwa na Kansa, hawajamkosea yeyote ila ni magonjwa ambayo yapo tu.

Uwe mwema, uwe mbaya, matatizo au shida haibagui mtu.

Uwe unashinda kanisani,
Uwe unashinda Misikitini,
Au uwe unashinda bar unalewa na malaya,
Matatizo hayachagui yoyote.

Pamoja na changamoto zote kwenye maisha, Kuna furaha kidogo Sana Huwa unaipata, itumie hiyo nafasi kufurahia maisha.
 
Shukran
 
Mkuu nimeishiwa power nisaidie kujazia
Unafeli sana jamaa wewe ndio yaliyokukuta ulipaswa kumwaga shuhuda humu nasi tupate kujifunza lakini unakuja na thread ya kulalamika bila kuonyesha source ya kulalamika kwako inakuwa haileti maana
 
Mtu yuko zake hapa anavuta hewa ya bure ya MUNGU,

Akitoka anenda kula zake kitimoto wa MUNGU, anashushia na wine iliyotengezwa zabibu za MUNGU,

Kisha Anaenda kwa demu wake aliyeumbwa na MUNGU,

Anapiga zake kimoja kilichodizainiwa na MUNGU,

Anaenda zake kuoga na maji ya MUNGU,

Kisha analala kwenye godoro lake la kunesanesa lilotengezwa na mazao na vyuma vya MUNGU,

Akiamka full kuperuzi jf na vifaa vilivyotengenzwa na malighafi za MUNGU,

kupost kumdhihaki MUNGU.
Kwahiyo unakubali Vyakula na vinywaji ameleta Mungu ?
Uko na safari ndefu mkuu.
Mpaka hewa unasema ni hewa ya Mungu 🤣 Hivi unajua mazingira ni nini?
 
Kama kwenda kuzimu na kurudi ni msemo tu Tukiamua kutumia Akili, basi hata mbinguni si sehemu halisi kama tukitumia akili
I cannot tolerate you anymore honestly, pls stop quoting me.

MUNGU anataka kupendwa.

Kupendwa ni hiari.

Maadam umemkataa achana naye.

Sasa mtu umemkataa unapoteza muda kumjadili wa nini! !

Kwanini unapoteza muda kujadili kitu ambacho hakipo? ?
 
Back
Top Bottom