Me nina 30 nimeshaenda kuzimu na kurudi hapa hapa duniani, yani cha moto nimekiona.
Kwa kifupi hakuna pigo halijanipiga, kutoka kila kona. Si magongjwa, si uchumi, si mahusiano, labda kifo tu nimeepushwa sijafa, sijafiwa lakini watu hao hao walio hai wanakufanya uone bora ukalale njaa kwenye mti kuliko kuwa karibu nao.
Nikimuangalia Ayubu najiona mimi kabisa.
Maumivu yangu yamenipeleka kwa MUNGU wangu.
Kadri navyoona uovu ndivyo navyouona uso wa MUNGU: yeye ni kinyume kabisa uovu.
Najua kwasababu alishajifunua kwenye sheria zake na kupitia YESU.
Muangalie aliyekuumiza kwa hakika ameenda kinyume na MUNGU alivyoagiza.
Possibly na wewe ushaenda kinyume mara nyingi na umeumiza wengine, na MUNGU alikuacha.
Kwahiyo hii Neema / Rehema uliyoonyeshwa, ielekeze na kwa wengine.
Hawajui walitendalo.
Badala ya kumnyooshea MUNGU kidole, wewe tubu ya kwako,
na kumuomba akuokoe kutoka kwenye hali ngumu / akuondoe kutoka kwa watesi wako.
Utauona mkono wa MUNGU.
"Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.
Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake."
Psalm.24.4-5.NENO