Mfano mimi huyo Mungu nimemkosea kiasi gan hata nistahili haya? Nina 27yrs lakin hakuna langi sijaona nimezaliwa nikakuta familia isioeleweka ,iliyojaa migogoro ,nikaozeshwa nikiwa bado mdogo kwa mwanaume ambaye hata sikua namjua kwa namna yoyote na hata sikumpenda ,ndoa nayo ikawa chungu familia iliyonilazimisha kuolewa haina msaada wowote watu hapo ni kwa kifupi ,kosa langu ni lipi hasa ?hii dunia imelaaniwa na haina faida kama kifo ni suruhu kher nijifie taratibu mamaeee
Me nina 30 nimeshaenda kuzimu na kurudi hapa hapa duniani, yani cha moto nimekiona.
Kwa kifupi hakuna pigo halijanipiga, kutoka kila kona. Si magongjwa, si uchumi, si mahusiano, labda kifo tu nimeepushwa sijafa, sijafiwa lakini watu hao hao walio hai wanakufanya uone bora ukalale njaa kwenye mti kuliko kuwa karibu nao.
Nikimuangalia Ayubu najiona mimi kabisa.
Maumivu yangu yamenipeleka kwa
MUNGU wangu.
Kadri navyoona uovu ndivyo navyouona uso wa
MUNGU: yeye ni
kinyume kabisa uovu.
Najua kwasababu
alishajifunua kwenye
sheria zake na kupitia
YESU.
Muangalie aliyekuumiza
kwa hakika ameenda kinyume na MUNGU alivyoagiza.
Possibly na wewe ushaenda kinyume mara nyingi na umeumiza wengine, na MUNGU
alikuacha.
Kwahiyo hii
Neema / Rehema uliyoonyeshwa, ielekeze na kwa wengine.
Hawajui walitendalo.
Badala ya kumnyooshea MUNGU kidole, wewe
tubu ya kwako,
na kumuomba
akuokoe kutoka kwenye hali ngumu /
akuondoe kutoka kwa watesi wako.
Utauona mkono wa MUNGU.
"Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.
Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake."
Psalm.24.4-5.NENO