Dunia ijadili chanzo cha ugaidi sio matokeo yake

Dunia ijadili chanzo cha ugaidi sio matokeo yake

Usiongozwe na hamaki, soma nilichoandika vizuri.
Sijakutisha bali ilitokea. Nimeweka mfano wa majangili waliokuwa wanauaa Arusha watu na wanyama pori.
Sekta ya utalii nchini iliingia doa kama ilivyokuwa ya Kenya.
Hatuongei kwa nadharia, tuna mifano na huo ni mmoja wapo.

Ukishakubali kuwa alshabaab wana haki ya kuteka meli, wana haki ya kuteka watalii utakataa vipi siku watakapodai haki yao ya kumiliki tembo Arusha? Umeelewa dhana nzima?

Ukishakubali kuwa Alshabaab wana haki ya kutungua ndege Mombasa, utawanyima vipi haki yao ya kutungua ndege JNIA?
Huu ni uovu usiohitaji certificate au diploma kuulani. Ni vitendo vya uhayawani kwanini tuvipe promotion?
Wameingia mall na kuua hadi watoto, bado tunadhani upo umuhimu wa kuwasikiliza.
Miaka 20 hawajaweza kusikilizana wao wenyewe kwa wenyewe wakiwa na kila sababu za kijamii kuwa taifa moja, vipi unadhani wataweza kuisikiliza dunia?

kwa taarifa yako wale wateka meli sio al shabab, bali ni waharifu wa kawaida kama waharifu wengine hakuna hata tukio moja la utekaji meli alshabab walosema wamehusika. Wale ni maharamia tu
 
Nguruvi3 umenena, lakini mambo ya ngoswe kwanini hatuwaachii ngoswe wenyewe waelewane? Al-shababu iliitwaa Somalia, wakadhibiti vitendo vyote vya kihuni na uharamia baharini na kwa majirani zake kama Kenya. Chakushangaza watu wasio Wasomali wakaukataa utawala wa al-shababu kwa hoja kwamba sio wa Kidemokrasia na wakatumia majirani wa Somalia (Kenya, Uganda, Rwanda, etc.) kwa njia moja au nyingine katika harakati za kuwaondoa al-shababu. Hivi kipimo cha democrasia ni kipi? Hivi Rwanda, Uganda, Tanzania, na Kenya kuna demokrasia gani zaidi ya ukabila, utawala wa mabavu na rushwa? Hata kule Marekani hakuna Demokrasia ila kuna vyombo vya ukandamizaji (kama jeshi, polisi, mahakama) vingi vyenye nguvu, watu wengi na vifaa vya kisasa vya kuwabaini na kupambana na watu wakorofi wanaolipinga dola na matajiri. Marekani kutumia ardhi ya Kenya kuwapiga al-shababu ni kosa kwa Wasomali kama vile Uganda ingetumia ardhi ya Tz kuipiga kenya.
 
Nami naheshimu sana rai za wengine.
Tumeshahu matukio ya kuteka watalii yalivoathiri sekta ya utalii Kenya? Kenya ingakaa mbali kwa mtazamo upi? Kwamba iwaache tu waendelee na shughuli zao hata kama ina athiri uchumi wao. Haki ya kujilinda inakuwa wapi?

Na sisi tuliwafundisha Polisi wa Somalia kwa nia njema tu. Tukiruhusu Alshabaab watishe basi hakuna aliye salama.
Nakumbusha kuwa majangili nao walikuwa wanatishia kama Alshabaab.
Kwa jinsi Somalia ilivyo haya majina ya Alshabaab kuwa vijana ni ulaghai tu. Viongozi wao ni wazee wengine miaka 50 na 60. Kuna kijana wa umri huo.

Hoja yangu ni kuwa watu wasishabikie matukio ya maafa kama haya. Hili ni tatizo lipo ukumbini kwetu.
Watu wasitafute sababu za kuwapa Alshabaa sababu kwa kusema tujadili uhalifu.
Ugaidi ni uovu tu bila kujali kafanya nani.

Kuna vitu vya kujadili lakini hawa Alshabaab wanaopita mitaani na 'plaizi' na kung'oa meno watu wenye meno ya dhahabu kwa kisingizio cha dini, kugawana mitaa ili kuchukua kodi na hata kuteka meli maana watekaji ni vijana (Alshabaab) leo tujiulize kwanini wanfanya hayo! serious! Tujadili chanzo cha watu walioshindwa kuelewana wakiwa na kila sababu za kuwaunganisha kijamii.
Real! Tujadili hadi upumbavu ili tupate jibu la matokeo! real!

Leo tukimbie na kukubaliana na vitisho vyao badala ya kufikiria kupambana nao.
Kukimbia ni kuwapa ushindi na hawataachi hapo watadai zaidi kwasababu wanajua tunawaogopa.

Nani anajua makombora ya Kenya yameua watu wangapi na wa aina gani huko Somalia? Je, hawa watekaji hawana wazazi ama ngugu waliouawa na makombora ya Kenye huko kwao?
 
na bado hawa alkaida wanaopewa silaha syria siku wakija kuuziwa na wanaowasapiti dunia itawaka moto
 
MMM, labda nifunguke kuwa kinachofanyika hapa ni spinning za kutaka kuhalalisha tukio la Nairobi na kukwepa ukweli kuhusu tukio.
Inatafutwa njia ya kuingiza mataifa ya magharibi ili ujengeke uhalali wa uovu.

Watu wanashindwa kujiuliza ni vipi Wasomali ambao kijamii ni jamii iliyo na ufungamano washindwe kuishi kwa amani miaka 20? asilimia 99.9 ni waislam na lugha moja, hawana kabila wana koo na tamaduni zao ni sawa.
Hili ni nyongeza ya swali mleta mada atusaidie ili kutoa mwelekeo wa majadiliano.

Watu wanasahau kuwa Kenya ilishambuliwa katika sekta za utalii na Alshabaab licha ya manshambulizi mengine yaliyotangulia kule Mombasa. Leo equation imegeuzwa wanaambiwa Kenya wanaonekana wabaya

Watetezi wa Alshabaab wana hoja moja inayowasumbua.
Wao wanadhani Alshabaab inapigana vita ya dini dhidi ya watu wa imani nyingine.
Kwasababu au kutoelewa facts na kuzikwepa zingine kwa spinning mara nyingi hujikuta wakiwa mahali pabaya zaidi.

Hakuna dini katika hizi tuzijuazo inayohubiri mauaji na ukatili. Hakuna! kama ipo nitajiwe moja.
Alshabaab wanatafuta sympathy ya kidini na bahati mbaya wasiojua dini wamewaunga mkono na kujikuta wanapaka dini matope. Huu ndio ukweli hata kama utauma. Huwezi kutetea Alshabaab kwa dini na dini ikabaki katika hadhi na heshima yake(Nina maana kufungamanisha dini na Alshabab ni kuichafua dini ambayo haisemi lolote kuhusu Alshabab)

Alshabaab wanasema jino la dhahabu ni haram kidini. Wanapita waking'oa kwa plaizi halafu wanauza meno hayo!!
Alshabaab wanasema ni harama kuangalia soka, wakati huo huo wanaangalia TV kusikia Marekani wanasema nini.
Wanasema ni haramu kutumia vifaa vya magharibi, wanatoa Tanganzo hilo wapo juu ya gari lililotengenezwa magharibi.
Alshabaab wanasema ni haram kutumia msaada wa FAO, wanakusanya magunia ya misaada wanakwenda kuuza nchi nyingine.
Wamefikia mahali wanazuia watu wasitumie mbolea, watumie kilimo cha zamani, njaa ikiuma wanawakimbia watu kwasababu wao wana pesa haram na uwezo wa kujikomboa.

Sasa anapotokea mtu na kudhani tunapaswa kujadili hawa wapuuzi ili tujue chanzo cha hasira zao inasikitisha.
Katika hayo hapo juu kipi unaweza kukiweka mezani ukasema kina mashiko.

Alshabaab si watetezi wa dini. Ni wahuni na wapuuzi wachache, kuwaunga mkono ni upuuzi kuliko upuuzi wao.
Hawana sababu ya kuulizwa wana chuki gani kwasababu hawana hata moja bali wamejaa ujinga na upumbavu.

Al-shababu ilianza kwa kuishambulia Kenya na kuvuruga sekta ya utalii, hii ni sawa wamefanya makosa. Lakini, je, wanasiasa wa Kenya waliwaeleza Wakenya sababu za kushambuliwa na Al-shabab? Kenya imefanya nini kwa Al-shabab hata wafikirie kuharibu sekta ya utalii wa Kenya kwa mashambulizi? Siku zote wanasiasa hawatuelezi ukweli wa makosa yao hata kidogo. Mfano, Tz hatujaambiwa ukweli hasa wa kwanini tulipigana na jirani zetu Uganda. Sababu tulizopewa ni mbovu mbovu tu, eti Amin kateka eneo la Kagera, lakini chanzo cha Amini kuteka Kagera hakisemwi. Lakini tulikuwa tunajua kuwa Obote (adui wa Amin) alikuwa TZ baada ya kupinduliwa na Amin. Hata hapa Marekani wakati wa tukio la September 11 wako Wamarekani wasiojua sera yao ya Mambo ya nje waliowauliza wanasiasa kwanini Osama anatushambulia hivi? Wasiasa wakawajibu 'wanatuonea wivu kwasababu ya ustaarabu wetu' Hivi ni kweli ustaarabu wa Wameraki ndiyo sababu ya kuandamwa na Al-Qaeda? Tusikeshe tukishughulikia matokeo bali chanzo. Dunia kwanini haitaki negotiation na 'magaidi' ili kutambua madai yao?
 
Kwanza kabisa naomba nitamke sipo hapa kuwatetea alshabaab wala sipo hapa kuwaunga mkono serikali ya kenya,

….unipe uthibitisho ya kwamba hao wanaohusika na utekaji nyara wa meli,uharamia na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ni Alshabaab,naomba kama uthibitisho unao,uweeke hapa na kama hauna basi nami nachelea kusema kwamba unazungumzia watu wawili tofauti,

Wasomali ni wasomali,wapo waumin wa dini mbali mbali,ikiwemo christians,muslims na kadhalika,

Hoja kuu ya alshabaab katika miaka hii ya enzi zao za kuchomoza kwao ni kutaka ufreee katika ardhi yao kuish kwa namna ambayo wao wanaona ni bora kuishi nayo,na kutokuingiliwa kwa jumuiya ya mataifa kwa interest zingine ambazo si kweli kwamba ni kwa minajili ya kwenda kurudisha aman,mi na wewe tutakubaliana kabisa kabisa kwamba America hawez kutia mguu sehem yyte bila ya kuwa na maslahi yake kwa namna moja ama nyingine,hilo liko wazi.

Mimi naungana na mtoa mada,

Umeona hapo juu ni kwa jins gani baadhi ya watu walipokuja kuushutumu uislam moja kwa moja ya kwamba waliofanya ivyo wamechochewa na uislam pamoja na mafundisho ya iman yao,kitu ambacho si cha kweli,

Sote tunajua alqaeda ni nani,na nani kaianzisha na ni vipi uhusiano ulikuwapo baina ya osama na marekani kabla ya kuhitilafiana.
Sote tunafaham nani ni TALIBAN,ALIKUWA ANAFANYA NIN AFGHANSTAN hadi marekani kawavamia na kuwaita magaid ili hali kwa sasa amerudi nyuma na kumwambia ahmed karzai akae.

Hiyo ya kusema Alshabaab kutungua ndege mombasa ushasema ni tetes na sio kweli,na hilo la kusema la uharamia na utekaji nyara pia sio kweli,wao wako na mission maalum na wako wazi especially pale yanapofanyika mashambuliz moja kwa moja huwa wanakuja kutoa tamko ya kwamba wao wamehusika,

Kwa mantik hiyo basi,mimi naweza kusema kwamba propagnda ziangaliwe vizuri na iman ziangaliwe kwa umakini,na pale tunapoamua kukemea umwagaji wa damu tukemee kote kote bila ya kuangalia wapi unafanyika uovu huo,

Alshaabab wanasema kwamba wao wana vita na kenya kwa kuwa kenya kapeleka majesh yake katika ardhi ile,na ile ni ardhi yao,we unasema kwamba kenya imekwenda kule kwa kuwa alshabaab walikuwa wanatishia usalama na biashara ya utalii ukanda wao,uthibitsho uko wapi ya kwamba wanaofanya ivo ni wao??wapo wasomali wengi ambao kwa namna moja ama nyingine hujihusisha na uharamia na vita vya kikabila,lakini kwakuwa anaefahamika kwa ukanda huo ni alshabaab basi propaganda zinajengwa kuonesha wao ni wahalifu,sawa,kwa namna yyte ile iwavyo tuzungumze nin chanzo cha hayo yote,
Hoja ni kwamba mauaji mengi yanafanyika huko somalia,kina mama na watoto wanauwawa na serikali za ushirika na kenya yakiwemo majesh yao,lakini huwez kuiskia BBC & CNN wakilielza hilo,ila sasa kwakua pale WASTEGATE waliouwa ni wengi wakiwemo na wazungu na raia wa nchi mbali mbali wao lazima walipoti,

Nadhani umeiona ile list ya wale vijana waliofanya shambuliola utekaji kuwa ni vijana kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo kenya,uingereza,marekani na kadhalika,umejiuliza ni kwa nini??

Tusipokuwa makin media zinaweza kutufanya tuwachukie wasiostahili kuchukiwa na kuwapenda wanaostahili kuchukiwa,
Au kwa kuwa wanaoish kule asilimia kubwa ni watu wa iman flan ambayo inasemekana wamezoea sana vurugu vurugu??

TUNAPOJADILI MAMBO YANAYOUMIZA KAMA HAYA,TUEPUKA KUJADILI KUHUSU OUTCOMES,TUJADILI SANA CHANZO CHA HAYO YOTE.
Mkuu The Big, kwanza nikuhakikishie kuwa tunazungumza kiungwana, kiraia na kindugu kama Watanzania kama ulivyosema hata kama tutakuwa na mitazamo tofauti, ndio tija ya mjadala.

Pili, hao vijana unaosema wametoka mataifa mbali mbali ni Wasomali waliopewa ukimbizi na nchi hizo.
Mwaka huu mwezi wa 3 Marekani imechukua wakimbizi wa Somnalia 240 kwa gharama zao, kuwapa hifadhi na haki ya ukaazi moja kwa moja.
Ndivyo ilivyo kwa Sweden, Norway n.k. Ni mradi endelevu kwa miaka mingi

Hakuna nchi yoyote ya kiarabu ikiwemo Saudi Arabia iliyofikiri kuwachukua hata kama wanatenganishwa na km 80 za maji ya bahari ya sham. Huu ni ukweli mchungu lakini ndio ukweli wenyewe. Hakuna aliyewaona kama wanadamu, jirani au waislam. Hakuna!

Hivyo vijana hao wamepata hati za kusafiri kama raia wa nchi husika lakini haiondoi ukweli kuwa ni wasomali. Hakuna suala la kutoka mataifa mbali mbali, ni wasomali waliotokea mataifa mbali mbali na kutumia fursa walizopewa kwa njia chafu na ovu. Walikuwa na option ya kubaki Mogadishuwakakataa sasa tunawaona ''mashujaa''! jamani!

Tatu, Watalii walitekwa na Alshaabaab wakitaka wapewe pesa ili wawaachie. Sijui unataka ushahidi gani zaidi ya huo.
Ndege ya Mombasa ilinusurika kutunguliwa, Alshabaab walidai kuhusika kisa ni ndege ya Israel.

Nne, Mharamia ni vijana ambao kwa jina lao halisi ni Alshabaab. Hata kama si wao bado suala linabaki ni wasomali.
Kwenye maeneo ya mapambano ya makabila yapo mengine salama kama Baidoa, Putland, na kidogo Hergesa. Sehemu kubwa ya vurugu za Mogadishu ni Alshabaab.

Nne, hakuna anayewakataza wasiishi kama wanavyotaka. Kinachokataliwa ni wao kutaka kuingilia mambo ya nchi nyingine. Haiwezekani waishi Isleigh Kenya, wafanye vurugu Kenya eti waachwe kwasababu wanataka nchi yao.

Wameachiwa nchi yao miaka 20,sasa inatawaliwa kwa kata hata kabla ya majeshi hayajaingia.
Hawa si watu wanaosimamia masilahi ya Somalia ni makundi yenye interest zao. Huwezi kuamini kuwa wanaoendesha shughuli ni matajiri wakubwa na hawataki amani kwasababu kupitia vurugu wao wanafaidika.

Tano, kuhusu kulaumiwa na kuhusishwa kwa dini hapa lazima Waislam wajilaumu wenyewe.
Sikubaliani na dhana ya kutuhumu dini na wanaofanya hivyo mara nyingi uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana.

Nasema waislam lazima wajilaumu kwasababu wamekuwa wanakwepa ukweli kwasababu rahisi.
Kuuhusisha uislama ili kukidhi haja za magaidi ni jambo la kawaida kwa magaidi.
Bahati mbaya waislam wanaingia katika mtego kwa kutokuwa tayari kukemea maovu kwavile tu wameonewa huruma na waovu na waovu wana majina yanayofanana nao na wanatumia maandiko vibaya, who cares! muhimu wanajua aya hata kama wana 'misuse au abuse'' maandiko matakatifu. Utasikia ni wenzetu, ni ndgu zetu! n.k.

Alshabaab wameua sana, wanafanya hivyo kwa mgongo wa dini na waislam wanaonekana kama wameridhika.
Ni ukweli lazima usemwe. Hakuna anayesema maovu wanayofanya kwa kutumia dini, kila mmoja yupo bize kuwatetea kwasababu wana majina tu yanayoonyesha imani fulani.

Nimetoa mifano ya uhalifu wa Alshabaab, hutasikia hata siku moja waislam wakilaani kinyume chake utawasikia wakitetea kwa njia za ajabu na kusikitisha. Hapa jamvini ni mfano mzuri, hakuna anayekataa niliyoorodhesha kama uhalifu wa Alshabaab, zinatafutwa njia za kutetea uhalifu huo.

Hili si kwa Alshabaab ni sehemu kubwa ya EAC na pengine dunia.
Ni kosa kubwa kwasababu waislam wanaingizwa katika mitego isiyohusisna na dini na wanaingia bila sababu kwa kutojua au hofu isiyo na mantiki.

Mathalan, znz, aliwahi kutoa maneno Sophia Kawawa.

Hayakuwa mazuri asilani lakini yalizua tafrani sana.
Leo watu wanaumizwa kwa Tindikali umememshikia nani akialaani,sababu ni tofauti ya Iman kitu ambacho hakipo katika uislam. Watu wanakubali uhalifu kwa kuhusisha na dini hata kama wanajua si sahihi, kinyume chake wanahamaki na kurukia mambo yasiyo na mantiki.

Ukiuliza unaambiwa kuna aya so and so ambayo haina uhusiano na upuuzi au uovu bali kujenga tu mazingira ya kutetea uovu kwa kutumia dini. Matumizi haya mabaya ndiyo mtego ambao watu wameingia na kuingiza dini bila sababu za maana. Tukumbuke kuna watu wanaoamini dini na kuna dini, hivi ni vitu viwili tofauti kabisa

Ustadh alisema Qisas kimerhusiwa, ''tafuta…kata kichwa kwa siri''.

Leo watu wanamwagiwa tindikali hilo linaonekana sawa na watu wamekaa kimya.

Wakati huo huo watu wameandamana kwasababu mkuu wa Wilaya mwenye jina la Amina kavuliwa hijabu hata kama hakuwa mwislam.

Hoja yangu ni kuwa magaidi na waouvu wengine wanatumia dini ''kuwateka '' waislam kisaikolojia wakijua huo ndio mtego unaonasa kwa urahisi.

Waislam wanatetea uhalifu kwa kutumia dini bila kujua kufanya hivyo ni kutoitendea haki dini.
Inakuwa rahisi dini kuhusishwa kwasababu ya matumizi mabaya yasiliyolingana na maandiko au mfunzo.

The Big, nimalizie kwa swali moja, hivi inakuwaje Somalia yenye 99.9 Waislam washindwe kutumia imani yao kuwaleta pamoja na watumie imani hiyo hiyo kulaani kinachotokea kwingine.

Kwanini waislam wadhani kuna uhalifu uliofanyika Libya kwa akina mama na watoto wasifikirie miaka 20 ya uhalifu kama huo Somalia?

Naomba unipe shule na elimu kidogo.
Hivi kusema hili jambo ni baya na ovu kunamuondoa mtu katika imani au kunamwimarisha?
Hivi mtu ana qualify vipi kiiimani, anaposimamia haki na ukweli au anapotumia imani kuficha haki na ukweli?

Je kama chanzo ni tofauti za kiimani utaweza kutoa solution? Je kama ni dini fulani inafundisha watu wake ugaidi na kuchukia wakristo utaweza kubadili wanachoamini?

Viongozi wa 'magaidi' wanafahamika mbona wanatafutwa wauawe badala ya kuwapeleka the Huge? kaseme kwanini wanaendesha ugaidi. kwanini UN haitaki kusulisha mzozo huu kwa njia ya majadiliano mezani?
 
First of all,you have to define terrorism properly,

What is terrorism???Who is a terrorist??

What is islam??Who is Muslim??What does islam say concerning terrorism??

You have to define it properly,

Who started the first world war??muslims??

Who started the second world war??muslims??

Who killed about 20 milions of Aborigines in Australia?muslims??

Who sent the nuclear bombs of hiroshima and nagasaki??muslims??

Killed more than 100 millions of indians in north america?muslims??

Who killed more than 50 millions of indians in south america?muslims??

Who took more than 180 millions of african people as slaves and 88% of them died and were thrown in Atlantic ocean?muslims??

Who is fighiting the war with the lord resistance army in uganda??muslims??

NO,NOT MUSLIMS...!!

So,you have to define terrorism properly,

If a non muslim does something bad,it is crime,but if a muslim commits the same is a terrorist...

Pata tano. Hoja iko pale pale dunia tuketi chini na kukinyooshea vidole chanzo halisi cha ugaidi, tusitoe majibu mepesi
 
Chanzo ni chuki baada ya kuona hawapati kitu duniani na mbinguni hawatapata kitu. Kwa hiyo wanaamua kuua wale wanaoelekea kupata baraka ndo maana uhalifu wao hufanywa kwa siri dhidi ya watu wasio na hatia
 
First of all,you have to define terrorism properly,

What is terrorism???Who is a terrorist??

What is islam??Who is Muslim??What does islam say concerning terrorism??

You have to define it properly,

Who started the first world war??muslims??

Who started the second world war??muslims??

Who killed about 20 milions of Aborigines in Australia?muslims??

Who sent the nuclear bombs of hiroshima and nagasaki??muslims??

Killed more than 100 millions of indians in north america?muslims??

Who killed more than 50 millions of indians in south america?muslims??

Who took more than 180 millions of african people as slaves and 88% of them died and were thrown in Atlantic ocean?muslims??

Who is fighiting the war with the lord resistance army in uganda??muslims??

NO,NOT MUSLIMS...!!

So,you have to define terrorism properly,

If a non muslim does something bad,it is crime,but if a muslim commits the same is a terrorist...

Mkuu nakubaliana na hoja yako ya kuwa Ugaidi na wafanya Ugaidi haviendani na dini ya uislam tatizo lililopo ni
1. Wanaotenda Ugaidi kwa wingi wao ni Waislam, ni kwa nini waislam wanaingia humu ndio hoja ya msingi mimi na wewe inatakiwa tujue waislam karibu duniani kote hawapendi kusoma mambo ya Duniani tunajikita zaidi kwenye Quran na hapa tunakuwa na upeo mdogo wa kuelewa mambo ya kidunia hivyo hawa wapanga Ugaidi ambao wengi wao wapo Marekani wanawatumia waislam kama watakavyo ili kuendeleza wanachokitaka ambacho ni kuifanya dunia isiwe na amani kwani imani itakapokuwepo hapa duniani hawatauza silaha zao wanazozitengeneza.

2. Mfano wa pili wa kutumika kwa waislam katika mambo mabaya yasiyompendeza mungu ni katika Biashara ya madawa ya Kulevya tuangalie katika nchi yetu wengi ya wanaosikika kufanya biashara hii au kusafilisha na kukamatwa wengi ni waislam tunatakiwa sisi waislam tujitafakari kwa nini tunatumika hovyo na kujiingiza katika mambo ya hovyohovyo wakati misimamo na misingi ya uislam ni amani na mambo yote yanayompendeza mungu.
 
Terrorists hata siku moja hawawezi kukosa sababu ya kufanya ugaidi... shetani ni shetani tu,hata umpe nini itabaki kuwa shetani tu ... terrorism is an evil spirit,no way you can negotiate with devil ...

Mkuu nakuunga mkono 100%
 
Viongozi wa 'magaidi' wanafahamika mbona wanatafutwa wauawe badala ya kuwapeleka the Huge? kaseme kwanini wanaendesha ugaidi. kwanini UN haitaki kusulisha mzozo huu kwa njia ya majadiliano mezani?

Tatizo ni Marekani kwani Gaidi atakapokamatwa na kupelekwa kushitakiwa katika mahakama ya wahalifu wa kivita NK watatoa ushuhuda jinsi Marekani inavyojishughulisha na Ugaidi ndio maana Marekani inafanya kila iwezavyo kuwasaka na kuwaua hawa viongozi wa Ugaidi hapa Duniani.
 
Mkuu The Big, kwanza nikuhakikishie kuwa tunazungumza kiungwana, kiraia na kindugu kama Watanzania kama ulivyosema hata kama tutakuwa na mitazamo tofauti, ndio tija ya mjadala.

Pili, hao vijana unaosema wametoka mataifa mbali mbali ni Wasomali waliopewa ukimbizi na nchi hizo.
Mwaka huu mwezi wa 3 Marekani imechukua wakimbizi wa Somnalia 240 kwa gharama zao, kuwapa hifadhi na haki ya ukaazi moja kwa moja.
Ndivyo ilivyo kwa Sweden, Norway n.k. Ni mradi endelevu kwa miaka mingi

Hakuna nchi yoyote ya kiarabu ikiwemo Saudi Arabia iliyofikiri kuwachukua hata kama wanatenganishwa na km 80 za maji ya bahari ya sham. Huu ni ukweli mchungu lakini ndio ukweli wenyewe. Hakuna aliyewaona kama wanadamu, jirani au waislam. Hakuna!

Hivyo vijana hao wamepata hati za kusafiri kama raia wa nchi husika lakini haiondoi ukweli kuwa ni wasomali. Hakuna suala la kutoka mataifa mbali mbali, ni wasomali waliotokea mataifa mbali mbali na kutumia fursa walizopewa kwa njia chafu na ovu. Walikuwa na option ya kubaki Mogadishuwakakataa sasa tunawaona ''mashujaa''! jamani!

Tatu, Watalii walitekwa na Alshaabaab wakitaka wapewe pesa ili wawaachie. Sijui unataka ushahidi gani zaidi ya huo.
Ndege ya Mombasa ilinusurika kutunguliwa, Alshabaab walidai kuhusika kisa ni ndege ya Israel.

Nne, Mharamia ni vijana ambao kwa jina lao halisi ni Alshabaab. Hata kama si wao bado suala linabaki ni wasomali.
Kwenye maeneo ya mapambano ya makabila yapo mengine salama kama Baidoa, Putland, na kidogo Hergesa. Sehemu kubwa ya vurugu za Mogadishu ni Alshabaab.

Nne, hakuna anayewakataza wasiishi kama wanavyotaka. Kinachokataliwa ni wao kutaka kuingilia mambo ya nchi nyingine. Haiwezekani waishi Isleigh Kenya, wafanye vurugu Kenya eti waachwe kwasababu wanataka nchi yao.

Wameachiwa nchi yao miaka 20,sasa inatawaliwa kwa kata hata kabla ya majeshi hayajaingia.
Hawa si watu wanaosimamia masilahi ya Somalia ni makundi yenye interest zao. Huwezi kuamini kuwa wanaoendesha shughuli ni matajiri wakubwa na hawataki amani kwasababu kupitia vurugu wao wanafaidika.

Tano, kuhusu kulaumiwa na kuhusishwa kwa dini hapa lazima Waislam wajilaumu wenyewe.
Sikubaliani na dhana ya kutuhumu dini na wanaofanya hivyo mara nyingi uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana.

Nasema waislam lazima wajilaumu kwasababu wamekuwa wanakwepa ukweli kwasababu rahisi.
Kuuhusisha uislama ili kukidhi haja za magaidi ni jambo la kawaida kwa magaidi.
Bahati mbaya waislam wanaingia katika mtego kwa kutokuwa tayari kukemea maovu kwavile tu wameonewa huruma na waovu na waovu wana majina yanayofanana nao na wanatumia maandiko vibaya, who cares! muhimu wanajua aya hata kama wana 'misuse au abuse'' maandiko matakatifu. Utasikia ni wenzetu, ni ndgu zetu! n.k.

Alshabaab wameua sana, wanafanya hivyo kwa mgongo wa dini na waislam wanaonekana kama wameridhika.
Ni ukweli lazima usemwe. Hakuna anayesema maovu wanayofanya kwa kutumia dini, kila mmoja yupo bize kuwatetea kwasababu wana majina tu yanayoonyesha imani fulani.

Nimetoa mifano ya uhalifu wa Alshabaab, hutasikia hata siku moja waislam wakilaani kinyume chake utawasikia wakitetea kwa njia za ajabu na kusikitisha. Hapa jamvini ni mfano mzuri, hakuna anayekataa niliyoorodhesha kama uhalifu wa Alshabaab, zinatafutwa njia za kutetea uhalifu huo.

Hili si kwa Alshabaab ni sehemu kubwa ya EAC na pengine dunia.
Ni kosa kubwa kwasababu waislam wanaingizwa katika mitego isiyohusisna na dini na wanaingia bila sababu kwa kutojua au hofu isiyo na mantiki.

Mathalan, znz, aliwahi kutoa maneno Sophia Kawawa.

Hayakuwa mazuri asilani lakini yalizua tafrani sana.
Leo watu wanaumizwa kwa Tindikali umememshikia nani akialaani,sababu ni tofauti ya Iman kitu ambacho hakipo katika uislam. Watu wanakubali uhalifu kwa kuhusisha na dini hata kama wanajua si sahihi, kinyume chake wanahamaki na kurukia mambo yasiyo na mantiki.

Ukiuliza unaambiwa kuna aya so and so ambayo haina uhusiano na upuuzi au uovu bali kujenga tu mazingira ya kutetea uovu kwa kutumia dini. Matumizi haya mabaya ndiyo mtego ambao watu wameingia na kuingiza dini bila sababu za maana. Tukumbuke kuna watu wanaoamini dini na kuna dini, hivi ni vitu viwili tofauti kabisa

Ustadh alisema Qisas kimerhusiwa, ''tafuta…kata kichwa kwa siri''.

Leo watu wanamwagiwa tindikali hilo linaonekana sawa na watu wamekaa kimya.

Wakati huo huo watu wameandamana kwasababu mkuu wa Wilaya mwenye jina la Amina kavuliwa hijabu hata kama hakuwa mwislam.

Hoja yangu ni kuwa magaidi na waouvu wengine wanatumia dini ''kuwateka '' waislam kisaikolojia wakijua huo ndio mtego unaonasa kwa urahisi.

Waislam wanatetea uhalifu kwa kutumia dini bila kujua kufanya hivyo ni kutoitendea haki dini.
Inakuwa rahisi dini kuhusishwa kwasababu ya matumizi mabaya yasiliyolingana na maandiko au mfunzo.

The Big, nimalizie kwa swali moja, hivi inakuwaje Somalia yenye 99.9 Waislam washindwe kutumia imani yao kuwaleta pamoja na watumie imani hiyo hiyo kulaani kinachotokea kwingine.

Kwanini waislam wadhani kuna uhalifu uliofanyika Libya kwa akina mama na watoto wasifikirie miaka 20 ya uhalifu kama huo Somalia?

Naomba unipe shule na elimu kidogo.
Hivi kusema hili jambo ni baya na ovu kunamuondoa mtu katika imani au kunamwimarisha?
Hivi mtu ana qualify vipi kiiimani, anaposimamia haki na ukweli au anapotumia imani kuficha haki na ukweli?

Sub'hana ALLAH..
Mkuu Nguruvi3 umekuja na hoja maridhawa sana,

Na mara nyingi huwa naburudika sana kujadiliana na wewe kwani huwa naenjoy hasa pale napokusoma kwa undan hisia zako,kama vile nakuona vile,insha allah na tuendelee...

Nakujibu swali lako linalosema ya kwanba

1.INAKUAJE SOMALIA YENYE WAISLAM 99.9% WASHINDWE KUTUMIA DINI YAO KUWALETA PAMOJA BALI WANATUMIA IMANI YAO KULAANI KILICHOTOKEA SEHEMU ZINGINE??

JIBU;

Somalia ya kusema kwamba wako 99.9% muslims washindwe kuungana unaweza ukawa una hoja kubwa katika hilo jambo mimi naomba nilizungumze kwa muktadha wa kipekee kidogo,

Ukiona watu wa iman moja na asili moja,wanashindwa kuelewana na kuungana lazima ujiulize swali la uhalisia sana,ya kwamba kuna nini kinawapelekea kuwa ivo??

Nin chanzo cha migogoro yao??iman yao au nin haswa??

Uislam kama uislam ni mfumo wa maisha unaohubiri amani na upendo,

Uislam ni mfumo unaojipambanua katika nyanja mbali mbali ikiwemo za kifamilia mfano ndoa,mirathi,n,k
Kibiashara,kibenk,kiulinzi,na kadhalika,kwa ufupi ni mfumo ulioweka namna ya kuendea kila kitu kinachomgusa mwana damu na maisha yake,na yule ambae anausoma na kuufuata kikamilifu huwez kumskia anaangukia kwenye hali ya mtafaruku na vurugu kwa namna moja ama nyingine,

Uislam pia haujampa muislam unyonge wa kutokujitetea pale anapoona anadhulumiwa na kuhatarishiwa maisha yake bila makosa ya aina yoyote,umemruhusu mwanadam kujilinda na kujitetea uhai wake pale anapohis unachukuliwa bila kudhuru nafsi za watu wasio husika na wasio na makosa,

Pia uislam unaruhusu kisas kuwa ni haki lakini kwa kuangalia mipaka yake,na inaruhusu pia kusamehe ni bora zaid kwani mungu ndie mwenye hekima zaid(SAMAHANI KWA KUKUHUBIRIA DINI KIDUCHU)

Kwaiyo sasa,hoja ya kusema kwanin wasomali 99.9% ni waislam wanashindwa kutumia iman yao kuwaunganisha,mimi nakujibu kwamba kipo kitu kinawapelekea kuwa ivo,either kutofuata mafundisho na kuusoma uislam unataka nini,ama kugawanywa na kutawaliwa na watu wa nje wenye interest na ardhi yao kama kulivofanywa miaka 20 iliyopita,

Pia nguruvi3 al akhiy,unakosea sana unaposema ya kwamba Marekani kaondoka pale sasa yapata miaka 20..!!,suala si kuondoka,suala ni kwamba kaacha nin baada ya kuondoka,na alipakuta vipi wakati anaenda au palikuwa vipi kabla hajaenda,NAONA HAPO UMEFANYA TENA KOSA LA KUDISCUSS OUTCOMES...!!

WAISLAM KUFIKIRIA UHALIFU UNAOFANYWA NCHI MFANO WA LIBYA NA KUTOFIKIRIA ULE ULIOFANYWA SOMALIA MIAKA 20 ILIYOPITA SIO HOJA SANA NGURUVI3,

Hoja hapo ni kwamba nin chanzo cha uhalifu huo??ni uislam au watu husika??

Kimfano kama wasomali wanapigana vita vya koo kwa koo,ni kusema kwamba uislm ndio umewaamrisha ivo au ubinadam wao??waislam si wasomali peke yao dunian,na haukuanza huko somalia,kwaiyo waangaliwe kwa muktadha huo.

Concerning non violence,its a crime kuwaambia watu wasichukue tahadhari kwa pale wanapoona wanakuwa victims of constant brutal attacks kutoka kwa jamii ya watu wengine,,

Hilo la Tindikali zanzibar na sehemu zingine,mfano umefanya case study yako hapa TANZANIA,MIMI KAMA MUISLAM NAWEZA KULIPANGUA KUWA ATAFUTWE MCHAWI katika HILO,na mchawi uislam,

Kwan zanzibar kumekuwa na makanisa na ukristo kwa miaka mingi sana,na waislam na wakristo wamekuwa wanaish kwa aman kwa miaka mingi sana,haya mbona tunakuja kuyaskia leo?yametoka wapi??

Ni uislam umebadilika kimafunzo au kuna jambo lipo nyuma ya camera??

Uislam ni ule ule,haujabadilika tokea zama hizo,hauna versions,haya yametokea wapi??

Needless to say,sio tuh wakristo wamekutwa na dhahama hiyo,hata masheikh wameshawahi mwagiwa tindikali,lakin hakuna alieamua kunyooshea kidole iman ya mtu mwingine kwa kuwa tunajua fika iman zetu hazifundishi ivo,sasa kwanin mchawi asitafutwe tuishie kunyoosheana vidole??

Ndio kwa maana siku zote mimi nasema kwamba tusome iman zetu,tuyafanyie kazi mafundisho yetu,na tujifunze kuvumiliana katika jamii yetu,

PIA KABLA YA KUTAFUTA SULUHU YA MAMBO TUSIKIMBILIE KUANGALIA TU OUTCOMES,BALI TUANGALIE PIA NIN CHANZO??

TAREJEA BAADENI UKINIHITAJI,SHUKRANI.
 
Last edited by a moderator:
First of all,you have to define terrorism properly,

What is terrorism???Who is a terrorist??

What is islam??Who is Muslim??What does islam say concerning terrorism??

You have to define it properly,

Who started the first world war??muslims??

Who started the second world war??muslims??

Who killed about 20 milions of Aborigines in Australia?muslims??

Who sent the nuclear bombs of hiroshima and nagasaki??muslims??

Killed more than 100 millions of indians in north america?muslims??

Who killed more than 50 millions of indians in south america?muslims??

Who took more than 180 millions of african people as slaves and 88% of them died and were thrown in Atlantic ocean?muslims??

Who is fighiting the war with the lord resistance army in uganda??muslims??

NO,NOT MUSLIMS...!!

So,you have to define terrorism properly,

If a non muslim does something bad,it is crime,but if a muslim commits the same is a terrorist...

Don't come up with cheap propaganda!It's impossible to seperate TERRORISM from ISLAM!
The difference is that you have no proof that those people killed in name of CHRISTIANITY but we have proof that terrosts kill with praise in their mouth(ALLAHU AKBAR).

Also BIBLE doesnt teach people to kill but KORAN has 109 verses which emphasize ISLAM believers to kill non believers,Jews and Christians.

Kwa hiyo mkuu acha propaganda ambazo tumeshazichoka zinazodai Uislamu ni dini ya amani wakati sivyo na kuja na visingizio vile vile mnavyotumia duniani kote kuhalalisha ugaidi.

ISLAM was never religion of PEACE and will never be!

ACHENI UGAIDI!
 
Ziko wapi hizo verses zinazosema hivo??

We unadhan niko hapa kuutetea uislam?nipo kuelezea uhalisia,

Uislam hauna kosa ulilolfanya linalohitaji kutetewa kwa namna yoyote,wewe kama unadhani nipo hapa with full mission ya kuusafisha uislamyou better think twice,

Siko hapa kubishana wala kutetea jambo lolote lile kuhusu uislam,hauhitaji utetez wowote na haujafanya crime ya aina yoyote,

Na hayo unayoyasema hayatuzuiii sisi kuendelea kuuabudu na kuufuata uislam wetu.

Kama wewe unaumia kwa sisi kuwa waislam,sisi hatuumii kwa wewe kuwa muamin wa dini nyingine.

Hilo halitakuja litokee,wewe amini unachokiamin na sisi tunaamin kile tunachokiamin...

Ila usidhan eti ya kwamba tunaweza kukaa kimya kuacha watu sampuli yako muje na hoja za kushikiza shikiza huku ukitarajia sisi tutakaa kimya bila kueleza uhalisia ulivo.
 
Mkuu,mimi sio mnafiki na huwa sina tabia ya kumsifia mtu anapoharibu eti ili asikwazike!I always tell the facts!

Kuhusu ni verse zipi;Wewe ni muislamu hivyo unazijua!Kama huzijui nenda google search Koran Satanic verses utazipata!

Kuhusu Uislamu hauitaji utetezi wowote kwani hauna kosa;Hoja yako ilikuwa kuwa Uislamu usihusishwe na matukio ya kigaidi yanayotokea lkn nikakuhakikishia kuwa Koran ina mafundisho yanayochochea ugaidi sasa utasemaje uislamu usihusishwe?

Hayo unayosema hayatuzuii sisi kuwa waislamu;Mkuu mimi sijasema msiwe waislamu,nilichosema ni kuwa aminini dini zenu lkn muheshimu dini za wengine!haiwezekani kamwe wakristo wakalazimishwa kuwa waislamu tena chini ya mtutu wa bunduki!huku mkiua watoto wao na kubaka wake zao mbele Yao!HAIWEZEKANI!
Nyie njooni mtu-convince tubadilike bila kutishana,kushikiana mapanga wala kulipuana mabomu!UZENI SERA!Maana ukristo wa sasa si ule wa 'akupigaye shavu la kulia mpe la kushoto' ni Ukimuua MAMA yangu namuua BABA yako!

Wewe unaumia na sisi kuwa waislamu;Mkuu,dini zote zinazohubiri UPENDO ndio ambazo ningependa kuwa muumini.Lkn samahani kwa kusema hata WAHINDU wanaoabudu ktk ng'ombe wana upendo kuliko nyie mnaoabudu kwa huyo mungu wenu.

Kuuelezea uhalisia;Ni uhalisia upi hapo uliouelezea,unataka kusema kuwa UISLAMU usihusishwe na UGAIDI wakati kila siku watu wanauawa huku mungu wako akisifiwa?Unataka kusema wale walioteka watu WESTGATE MALL si waislamu na hawakuua watoto na wanawake na kuwabaka?Unataka kusema hizo verse za kuhamasisha mauaji haziko kwenye KORAN?Unataka kusema wakristo 109 waliowawa kanisani pale Pakistani huku waislamu wakisema 'allahu akbar' ni usanii wa Aljazeera?

Sina haja ya kukwambia uache imani yako lakini nakuhakikishia utakutana na MUNGU wako Jehanamu.
 
Watu wetu wengi wasio na hatia wanapoteza maisha na viungo vyao kutokana na ugaidi, hii inauma, lakini inauma zaidi kuona dunia iko kimya kujadili chanzo halisi cha ugaidi duniani, badala yake tunalia na matokeo ya ugaidi tu. Hii ni ngoma ya 'do me do you', kama Marekani yenye nguvu ilishindwa vibaya huko Somalia enzi zile, je, Kenya? al-shababu na 'magaidi' watasambaratisha maisha yetu na chumi zetu tusipokuwa waangalifu na ugaidi. Tunacheza ngoma tusizozijua vema. kenya ondoka Kenya, vinginevyo uchumi wako utasambaratika kabisa kama Uchumi wa marekani unavyoyumba sasa kwa kuwasaka magaidi duniani.

Kwanini chanzo cha ugaidi hakisemwi huko the Huge?

The Heague inaweza kubadili maandiko matakatifu?
 
Osama ni nadharia iliyotengenezwa na Mmarekani kuteleza hujuma zake dhidi ya uislamu.

Marekani hawana hujuma na uislam. Ingekuwa wana hujuma na uislam wangeanza kuhujumu nchi ya Saudi Arabia ambapo ndio kitovu cha uislam, badala yake marekani ni marafiki wakubwa wa Saud Arabia, na hizo nchi mbili huwa zinasaidiana sana.

Marekani wana hujuma na nchi zenye kutoa mafuta kwa sababu wanayataka hayo mafuta. Kwa bahati mbaya au nzuri nchi hizo zinakaliwa na waislam, matokeo yake hata nchi kama afghanistan and the like wanaingilia kati wakidhani kuwa mmarekani anavita na uislam, wakati ukweli sio huo.

Na ukiangalia utaona kwenye zile nchi za kiislam ambazo hakuna mafuta(mengi) hata wakichapana waislam wao kwa wao marekani haingilii, lakini waislam wa nchi zinazotoa mafuta mengi wakichapana kidogo tu marekani anakimbilia kupeleka majeshi.
Si unaona hata Syria wameanza siku nyingi mno kuuana lakini marekani alikuwa hana mpango wa kwenda, mpaka baada ya malalamiko mengi ndio mmarekani akaanza kujiuliza aende au asiende.

Venezuela majority ni waKristo marekani walipeleka chokochoko kujaribu kushawishi watu walete machafuko ikashindikana kwa sababu watu wa venezuela sio mburula mburula, vinginevyo moto pia ungewaka.

Hii ishu mnavyoitazama kwa nje haifanani kabisa na undani wake, inabidi tuwe makini na tusiwe wavivu wa kushughulisha ubongo wetu.
 
Back
Top Bottom