Dr. Slaa Vs Lowassa Urais 2015

Nani unaona anafaa kuwa Rais kati ya Wawili hawa?

  • Edward Lowassa

    Votes: 103 13.0%
  • Dr. Willibrod Slaa

    Votes: 640 80.6%
  • Wote hawafai/sijaamua

    Votes: 51 6.4%

  • Total voters
    794
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Willbrord Slaa
Ni kiongozi ambae ameweza amethubutu kutoka azarani na kuzivumbua shida za. Watanzania na kueleza shida kero na matatizo yaliojificha yanayowakabili Watanzania Kitu ambacho. Lowasa atokiweza kwa sababu tayari ana Kashfa nyingi za. Ufisadi Kwa Slaa Watanzania wote tuseme anaweza. Yes we can
 
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi ne...nda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa.
Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa mgombea wetu."
- Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995
Aya sasa wapiga Debe ninyi mnasemaje?

Yaan sawasawa ufananishe Mlima Kilimanjaro na Kichuguu
Lowassa Mlima na Padri ni Kichuguu
 

Kwan 2nahtaji kiongoz wa kutuhubiria matatizo yetu kila cku?? 2nahtaji mtatuaji sio mtangazaji
 

Mh kwa hali hii mbona 2takosa kiongozi??
 
kuna watu wanaroho ngumu, bado slaa anagombea tu
 
Aisee hivi hatuchoki. Si tupumzike kidogo hadi angalau mwezi wa pili tuanze tena.
 

Tusiruhusu Chama Cha Upinzani Kuingia madarakani hata kidogo kwani CCM ni chama kinachojitoshereza sanaaaaaaaaaaaaa,,,wanaokiharibu ni wale wasiokitakia chama maendeleo mazuuuri lakin chama kitabaki pale pale kuwa ni chama imara sanaaaaa bali watu wachache waliomo katka chama ndo wanakiweka katika wakati mgumu kidogo.


CHA MSINGI NI KUWAJIBIKA NA WALE WACHACHE WALIOKO NDANI YA CHAMA WANAOKIHARIBU HIKI CHAMA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE.
 
JF, kama mtandao unaoheshimika nchini na kwingineko, ilifanya utafiti juu ya nafasi ya Dr. Wilbrod Peter Slaa na Edward Ngoyai Lowassa katika Urais wa nchi hii hapo 2015. Hakuna haja ya kufutilia tafiti za Twaweza na wengineo tukaacha tafiti yetu wenyewe.


Katika tafiti ya JF iliyoanzishwa na Mkuu Salary Slip katika uzi wa URAIS 2015: Dr. Willibrod Slaa vs Edward Lowassa, Dr. Slaa amemuacha mbali sana Lowassa. Natoa rai kwa wana-JF kujenga mazoea ya kuthamini ya kwetu kwanza. Matokeo kwa kifupi yalikuwa hivi:

Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa 720. Dr. Slaa amepata kura 597 sawa na asilimia 82.92%. Lowassa alipata kura 81 sawa na asilimia 11.25%. Kura 42 sawa na asilimia 5.83% zilikuwa za wote hawafai/sijaamua
 

Hujaeleweka kwenye statistical data zako mkuu. Pangilia vizuri hayo matokeo ili yasomeke vizuri nani kapa nini.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…