Dr Slaa na Kuhalalisha Gongo: Kwanini Yupo Sahihi

Dr Slaa na Kuhalalisha Gongo: Kwanini Yupo Sahihi

Status
Not open for further replies.
Kwenye hili kwanza ungekuwa mstaarabu na kusema ukweli kuwa umetoa maneno hayo kutoka kwa prof. Shivji. Ulichokifanya hapa kinaitwa plagiarism.

Kama ungekuwa unanisoma elsewhere, hii sio mara ya kwanza kuja na maneno haya ambapo nilisema source ni nini;nakumbuka ulikuwa na kitabu hiki;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mipangomingi, hebu jaribu kuwa wazi ueleweke, tatizo letu eti tukishapenda...kupenda nini? Hapa hoja ni kinywaji cha gongo kuhalalishwa ili iweze kutengenezwa katika mazingira safi na salama kwa wanaoitumia. Mpaka hapo kuna tatizo gani? Huo upunguani wetu ni upi na ukweli unaouongelea ni upi? Kwamba gongo pamoja na kupigwa marufuku haipo? Kumbuka Tanzania imezaliwa mwaka 1964 ikaikuta gongo ipo, hadi leo ipo na itaendelea kuwepo. Kwa hali ilivyo sasa ni kwamba inatoa mwanya kwa vyombo vya dola na viongozi wala rushwa kuzidi kuneemeka kwa njia haramu kuwakamua eti wanaokamatwa na gongo. Gongo ni pombe kama pombe zingine; tofauti ni mazingira ya utengenezaji tu.

Hakuna mada yoyote aliyochambua ZeMarcopolo kisomi labda unitajie. Kwamba gongo inaathiri kibiolojia? Kisaikolojia? Kiuchumi? Kijamii? Ni pombe gani haina athari hizi; bia? konyagi? vodka? gin? whisky? Captain Morgan (rum)? Kwa nini gongo. Na tukiongelea mazingira; hata soda ikitengenezwa kwenye mazingira machafu inaweza kuleta madhara makubwa!
Nimesema kama tatizo ni pombe, basi ZeMarcopolo angeeleweka kama angeunga mkono upigwaji marufuku wa aina zote za pombe.

Asante sana Mipangomingi, ubarikiwe sana.

ZeMarcopolo uchambuzi wake anasema hivi; kwa sasa hivi Tanzania kuna Gongo inayotengenezwa kitaalamu yaani kwa viwango vya kikemia na mazingira na Gongo isiyotengenezwa kwa kutofuata viwango vya kikemia na afya. Hiyo ya mwanzo inaitwa Konyagi na asili yake ni kutoka kwa hao wanaotengeneza kienyeji waiuze kiwandani ili ikidhi viwango. Gongo hii ni halali na inauzwa hadharani. Hiyo ya pili ni ile inayotengenezwa kienyeji bila kiwango, na jina lake limeendelea kuwa Gongo, na hairuhusiwi kutengenezwa wala kuuzwa wala kunywa. Sasa mnapokuja na hoja ya kuhalalisha Gongo, tunawauliza ni ipi?

Hoja ingeeleweka kama ingekuwa kurejea utaratibu wa zamani wa kuwaambia hao akina mama chaudibe wapeleke Gongo lao kiwandani (kitu ambacho ni kigumu) au ku-extend kiwanda cha Konyagi kiwe kila Kijiji ili kutengeneza Gongo ya viwango ambayo mtaita jina mlitakalo!! Na zaidi, madam hao local brewers wana utaratibu na ujuzi wa kuitengeneza na wateja wakaikubali na kununua, wataendelea tu kuitengeneza kwa vyovyote ilivyo kwani raha ya gongo inywewe kwa uficho eti, huku bei itakuwa hata kwa kizibo unapimiwa. Tuwe wakweli, Dr. Slaa anataka kuhalalisha Gongo au anataka ku-extend shughuli za TDL mpaka vijijini? Kama kuhalalisha Gongo, narudia tena ni ipi? Na ikishahalalisha, Je hiyo sheria ya kuhalalisha Gongo itazungumzia pia isiyo halali? Kama itazungumzia Gongo isiyo halali itakuwa ni ipi hiyo? Majibu Tafadhali cc@Zemarcopolo
 
Mnajitahidi sana kulazimisha umma uamini kwamba gongo ilishakuwa legalized kupitia konyagi;hoja hii ya ZeMarcopolo ni hoja hafifu sana;nitaijadili kwenye sehemu yangu ya pili ambayo itajikita zaidi katika utaalam wa kutengeneza vilevi hivi;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Wewe jamaa kumbe sometimes ukiiweka akili yako vizuri una hoja nzuri sana tu zinazoweza kufanya watu mkajadiliana kistaarabu kabisa kwa hoja eti eeh!!??. Hapa nimekupenda mkuu na Pingana tu na Dr Slaa kwa hoja naamini hata yeye atakuheshimu sana kwa hilo. Hatukatai kwamba kuna wakati mijadala inayohusu watu binafsi pia katika mazingira flani huja na huyo mtu hujadiliwa ktk uelekeo huo,but for this Dr Slaa has point for GT na Mchambuzi na wengine wengi wameilewa. Na mimi naungana na hao.

Anyway najua na kutambua fika kuwa hata wewe umeelewa lakini hukubaliani na Dr Slaa kwa sbb unahisi huyu bwana ana re-invent kitu ambacho tayari sheria na taratibu za nchi yetu zinaruhusu utengenezaji wa pombe/vilevi aina zozote (na hii ndiyo hoja yako kiukweli).....lakini wakati huo huo sheria hizohizo zinaharamisha hii inayoitwa Gongo (hili ndilo tatizo la msingi tunalolijadili na ndiyo msingi wa mleta hoja na Dr Slaa) ndiyo maana akasema wao CHADEMA wakifanikiwa kushika dola "wataihalalisha Gongo kisheria" . Kilicho kibaya ni kuwa kuna watu wanamshambulia aliyeleta mjadala huu Dr W.P. Slaa yeye kama yeye kwa kumuita majina ya ajabu kama vile huyo bau kalewa gongo,na wewe kuna post yako hapa juu umesema siku ile anatoa hoja hii alikuwa "amepigwa kipapai" bila ya kuichambua na kuipinga hoja yake kwa hoja ...........ila leo(wewe) umekuja vizuri!!.

Sasa hebu twende kwenye hoja zako. Mimi natofautina naa wewe kwa kiwango kikubwa kwa sababu bado naamini na nitaendelea kuamini kuwa this Mzee Dr Slaa na huyu Mchambuzi wako sahihi;

Kabla sijakujibu naomba usome Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010 - 2015 Sura ya Tatu inayohusu Sekta za Uzalishaji Mali Kifungu cha 50 (a) - (g).

Kinachopingwa ni pombe yenye madhara kwa binaadamu.

Katika mjadala huu wote tuko upande mmoja isipokuwa Dr. Slaa tu. Tumekubaliana kuwa pombe isiyokidhi viwango iwe haramu na wanaotengeneza au kuuza wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. Mwenzetu Mchambuzi amependekeza itumike sheria ya bidhaa bandia. Lengo lake naamini ni kumlinda mnywaji. Hii ni sahihi kabisa.

Slaa yeye anataka polisi waache hii pombe isiyokidhi viwango iuzwe na polisi wasiwabudhudhi wauzaji. Hapo ndipo mimi na Mchambuz tunapotofautiana na Slaa.

Mjadala hapa umeisha, tunajadili nyepesinyepesi tu za Christmass.

Nikutakie Christmass njema.
 
Kama ungekuwa unanisoma elsewhere, hii sio mara ya kwanza kuja na maneno haya ambapo nilisema source ni nini;nakumbuka ulikuwa na kitabu hiki;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu Mchambuzi, hebu pia mpongeze japo kidogo Ze Marco, kitendo tuu cha kuweza kumsoma Shivji na kukumbuka ni hatua!. Kwa walio wengi Shivji ni mwiba!, halafu kunahitaji level fulani ya uelewa kumsoma na kumuelewa na sio tuu kumkariri!.
Pasco
 
Maelezo ya NasDaz hayajahitimisha hoja hii kama unavyopenda iwe;sehemu yangu ya pili na mimi nitakuja na maelezo ya kitaalamu kama ya nasdaz, nilichofanya kwenye #1 ilikuwa ni kuanza na theory kwanza; nipo mbali kidogo na PC ndio maana inaniwia vigumu kumalizia sehemu yangu ya pili;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
am waiting, and don't forget to conclude if it'll still be possible for existing local poor distillers to participate in that business or it it'll eventually turns into opportunity to people with money and industrial know how. Nakubaliana 100% na maelezo ya Mipangomingi kwamba, kama kuwawezesha basi ni kutafuta soko la gongo hii isiyo salama kwa existing modern distillers like Konyagi....yaani kwamba gongo iwe ni semi-finished processed product ambayo inapelekwa kwa distillers for final processing...final processing ambayo am afraid kwa local poor distillers hawataiweza due to lack of capital and technology. Tusisahau, this's not all about kupata mitambo salama ya bati and similar materials inayoweza kuundwa na kutengenezwa na SIDO, this includes proper chemistry; proper chemical formulation.
 
Last edited by a moderator:
Sawasawa mkuu,

Hii post yako ungempa copy FaizaFoxy angefurahi sana. Yeye amesema huwa anatumia hiyo kitu lakini sio kwa njia ya kuvuta. Hajasema kwa njia ipi!

Hahahaha haha, niliwahi kusema natumia kwa njia ipi, lakini nadhani post zangu nyingi zilifutwa wakati nilipokuwa na ban ya maisha kabla Obama hajaja kuniombea niwachiwe.

Mimi natumia bangi kwa njia mbili, moja ni kwenye oud (udi) wa kujifukiza, huwa nikitengeneza udi wangu, ili kupata harufu "unique" huwa nnachanganya na majani ya bangi kwa mbali, hupendelea zaidi kuchanganya na majani mabichi ya bangi ili yakaukie kwenye udi, nikikosa mabichi huwa nnanunua sigara za bangi kwa fundi viatu (si mbali na kwangu) nnachanganya na oud wangu na nnajifukiza.

"Oud" nnaouchanganya na bangi huwa na harufu nzuri sana na ya pekee. Na Gozi langu siku hiyo huhamasika vibaya sana. Kidogo lakini, ataejaribu asizidishe manjonjo.

Na namna nyingine, huwa nnairoweka bangi kwenye maji, kwa saa 24, halafu nnaichemsha, halafu nnaichuja, halafu hayo maji yake nnachanganya kwenye shampoo ya kuoshea nywele na kwenye "liquid soap" ya kuogea, naongeza kidogo na vimanukato nivijuavyo, basi naaam, utatafuta dunia nzima hupati sabuni na shampoo kama hiyo. Ni unique, ukitoka hapa huna haja hata ya kutia perfume mwilini.

Hayo ndio matumizi yangu ya bangi kwa ufupi.

Mpaka sasa nimefanya ka research kadogo ka mtandaoni na nje, sijaona haswa sababu za bangi kukatazwa isipokuwa ni watu fulani fulani waliokuwa na mashamba ya bangi walitaka monopoly ya kuwauzia viwanda vya vya madawa wakitaka biashara yao isife na wao walikuwa na influence basi wakaifanya ipigwe marufuku (hawa ni ma settlers wa America).

By the way, Gozi langu linapiga kama kawaida likiwa nyumbani, na likiishiwa linaniuliza kama nnayo "stock". Na mara kwa mara Gozi langu likienda mikoani kwenye shughuli zake huwa nnaliagiza bangi mbichi ya kutengenezea vipodozi vyangu. kwi kwi kwi teh teh teh.

Legalize It.

cc Pasco, lara 1
 
Last edited by a moderator:
Mnajitahidi sana kulazimisha umma uamini kwamba gongo ilishakuwa legalized kupitia konyagi;hoja hii ya ZeMarcopolo ni hoja hafifu sana;nitaijadili kwenye sehemu yangu ya pili ambayo itajikita zaidi katika utaalam wa kutengeneza vilevi hivi;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Wewe, gongo ilishawahi kuhalalishwa kilipojengwa kiwanda cha Konyagi, tena sio kimya kimya ilitangazwa kabisa, "wanaopika gongo sasa wakauze kiwandani", na hizo zilikuwa enzi za Nyerere Rais na Songambele akiwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani (hii Dar ilikuwa ni Mkoa wa Pwani enzi hizo).

Wanyamwezi na Wasukuma, ndio ilikuwa dili yao kubwa wakati huo kwani walikuwa wakiletwa na wenyeji kuwalimia mashamba yao na baada ya kazi ya mashambani walikuwa wanajitafutia kipato cha ziada kwa kutengeneza gongo, hususan la mapapai mabovu. Nnalijuwa hili kwa sababu hata shambani kwetu Kigamboni walikuwepo na ndio ilikuwa kazi yao.

Waliokuwa wanaipika kule Kigamboni na sehemu zingine zingine kama vile Sinza, Mabibo (siku hizo huko kote mashamba madogo madogo tu, si mji kama sasa) ilikuwa utawakuta wako msururu na baiskeli zao na madumu na machupa yao wakiiuza pale kiwanda cha Konyagi Mbozi Road, Chang'ombe, labda siku hizo ulikuwa bado ni mdogo sana au hujazaliwa. Hili nimeliona kwa macho yangu na si la kuhadithiwa.

Kisutu pale unapoona DIT kwa sasa, ilikuwa ndio sehemu kubwa ya wanywaji gongo enzi hizo kabla hapaja-bomolewa, upo hapo ulipo?

Hilo zoezi likashindwa na likafa kama yalivyoshindwa mambo mengi ya Nyerere. Mzowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.

Tuulize wenyeji wa zamani tukujuze mambo haya, bado tupo na tuna mengi ya kuwafaidisha.
 
Hahahaha haha, niliwahi kusema natumia kwa njia ipi, lakini nadhani post zangu nyingi zilifutwa wakati nilipokuwa na ban ya maisha kabla Obama hajaja kuniombea niwachiwe.

Mimi natumia bangi kwa njia mbili, moja ni kwenye oud (udi) wa kujifukiza, huwa nikitengeneza udi wangu, ili kupata harufu "unique" huwa nnachanganya na majani ya bangi kwa mbali, hupendelea zaidi kuchanganya na majani mabichi ya bangi ili yakaukie kwenye udi, nikikosa mabichi huwa nnanunua sigara za bangi kwa fundi viatu (si mbali na kwangu) nnachanganya na oud wangu na nnajifukiza.

"Oud" nnaouchanganya na bangi huwa na harufu nzuri sana na ya pekee. Na Gozi langu siku hiyo huhamasika vibaya sana. Kidogo lakini, ataejaribu asizidishe manjonjo.

Na namna nyingine, huwa nnairoweka bangi kwenye maji, kwa saa 24, halafu nnaichemsha, halafu nnaichuja, halafu hayo maji yake nnachanganya kwenye shampoo ya kuoshea nywele na kwenye "liquid soap" ya kuogea, naongeza kidogo na vimanukato nivijuavyo, basi naaam, utatafuta dunia nzima hupati sabuni na shampoo kama hiyo. Ni unique, ukitoka hapa huna haja hata ya kutia perfume mwilini.

Hayo ndio matumizi yangu ya bangi kwa ufupi.

Mpaka sasa nimefanya ka research kadogo ka mtandaoni na nje, sijaona haswa sababu za bangi kukatazwa isipokuwa ni watu fulani fulani waliokuwa na mashamba ya bangi walitaka monopoly ya kuwauzia viwanda vya vya madawa wakitaka biashara yao isife na wao walikuwa na influence basi wakaifanya ipigwe marufuku (hawa ni ma settlers wa America).

By the way, Gozi langu linapiga kama kawaida likiwa nyumbani, na likiishiwa linaniuliza kama nnayo "stock". Na mara kwa mara Gozi langu likienda mikoani kwenye shughuli zake huwa nnaliagiza bangi mbichi ya kutengenezea vipodozi vyangu. kwi kwi kwi teh teh teh.

Legalize It.

cc Pasco, lara 1

Interesting indeed,

Hapa mpenda chemistry Rose Mayemba nitamuomba atuchambulie kama njia ya "oud" ina tofauti na kuvuta. Ninachokiona mimi kwa harakaharaka ni tofauti ya dose tu or more specifically, number of molecules inhaled. Ile kujisikia bomba ndio euphoria yenyewe.

Siku hizi Slaa kakimbia JF. Ningefurahi sana kusikia maoni yake juu ya bangi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi, hebu pia mpongeze japo kidogo Ze Marco, kitendo tuu cha kuweza kumsoma Shivji na kukumbuka ni hatua!. Kwa walio wengi Shivji ni mwiba!, halafu kunahitaji level fulani ya uelewa kumsoma na kumuelewa na sio tuu kumkariri!.
Pasco

Upo sahihi mkuu;nakumbuka ZeMarcopolo alikuwa na kitabu hiki kama sikosei 2010;
Pasco & ZeMarcopoloco, Kitabu cha prof issa kinaitwa:
Let the People Speak: Tanzania Down the Road to Neo Liberalism,
ISBN:2-86978-183-0

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Wewe, gongo ilishawahi kuhalalishwa kupitia Konyagi, na wale Wanyamwezi na Wasukuma, ndio ilikuwa dili yao kubwa wakati huo kwani walikuwa wakiletwa na wenyeji kuwalimia mashamba yao na baada ya kazi ya mashambani walikuwa wanajitafutia kipato cha ziada kwa kutengeneza gongo, hususan la mapapai mabovu. Nnalijuwa hili kwa sababu hata shambani kwetu Kigamboni walikuwepo na ndio ilikuwa kazi yao.

Waliokuwa wanaipika kule Kigamboni na sehemu zingine zingine kama vile Sinza, Mabibo (siku hizo huko kote mashamba madogo madogo tu, si mji kama sasa) ilikuwa utawakuta wako msururu na baiskeli zao na madumu na machupa yao wakiiuza pale kiwanda cha Konyagi Mbozi Road, Chang'ombe, labda siku hizo ulikuwa bado ni mdogo sana au hujazaliwa. Hili nimeliona kwa macho yangu na si la kuhadithiwa.

Kisutu pale unapoona DIT kwa sasa, ilikuwa ndio sehemu kubwa ya wanywaji gongo enzi hizo kabla hapaja bomolewa, upo hapo ulipo?

Tuulize wenyeji wa zamani tukujuze mambo haya, bado tupo.

Hapo ndipo unaponimalizaga FF!!!

Btw huu mjadala aliumaliza Mchambuzi mwenyewe. Kakiri kuwa gongo isiyokidhi viwango ipigwe marufuku.

Sasa hivi kwenye hii thread tuko kiChristmass zaidi...
 
Hapo ndipo unaponimalizaga FF!!!

Btw huu mjadala aliumaliza Mchambuzi mwenyewe. Kakiri kuwa gongo isiyokidhi viwango ipigwe marufuku.

Sasa hivi kwenye hii thread tuko kiChristmass zaidi...

Usipotoshe umma kwa kujificha nyuma ya hoja mufilisi kwamba gongo halali ni konyagi;kuwa na subira nitulie na kumalizia sehemu yangu ya pili;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Sehemu ya Kwanza​

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wilbrod Slaa akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Chama Chake mkoani Kigoma alikuja na hoja kwamba, iwapo umma wa watanzania utakiamini Chadema na kukipa ridhaa ya kuliongoza Taifa 2015, kati ya mambo muhimu ambayo Chadema itayafanya ni pamoja na Kuhalalisha Utengenezaji wa Pombe ya Gongo ambapo Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) litapewa jukumu la kutengeneza mitambo ya gongo ili isaidie kuongeza ubora wa pombe hii ili isiwe na madhara kwa wanywaji kama ilivyo sasa. Kwa kumnukuu, Dr. Slaa alisema

Kwa wale wote wanaombeza Dr. Slaa katika hili, kutokana na haya yote, mna haja ya kuelewa kabla ya kupinga hoja ya Dr. Slaa, hivyo kuendelea kutambua pombe ya gongo kama haramu, tujifunze kwa wenzetu ambao badala ya kukwaza wazalishaji wa pombe, waliamua kwanza kuwekeza katika juhudi za kuinua wazalishaji na kulinda afya za wanywaji kupitia taasisi mbalimbali za udhibiti wa viwango kama nilivyokwisha jadili. Ni pale tu udhibiti unaposhindikana ndio serikali inatakiwa kuja na mpango wa kupiga marufuku, sio utengenezaji wa pombe tu, bali chochote ambacho mzalishaji amelenga kwa ajili ya matumizi ya binadamu, huku akijipatia rizki yake.

Cc Chakaza, Ericus Kimasha, Daudimtwale, Dr.W.Slaa, Ritz, ifweero

Maelezo yako ni mazuri sana lakini sijui kama ulifanya uchunguzi na kujua kuwa kinywaji cha Konyagi ambacho ni Spirit of the nation na ambayo ni product ya Tanzania inatokana na nini.... kwangu mimi naona ni maneno ya kujaribu kuzima hoja.... ila naomba uwafafanulie watanzania wenzangu na wasiojua kama mimi Konyagi ni zao la pombe gani kwanza kabla ya sehemu ya pili...
 
Attachments

  • Konyagi.jpg
    Konyagi.jpg
    8.5 KB · Views: 130
Administrator! Naomba post yangu juu ya mjadala wa Dr. Slaa iwekwe hadharani nimechoka kujibiwa inbox...
 
Mchambuzi:

Labda nianze kwa kusema context ya kisiasa kwenye hoja hii imeleta utata. Ungefanya vema kumtoa Dr. Slaa na dhamira yake katika hili

GONGO ni neno linalosimama kwa niaba ya: pombe haramu, isiyo na viwango, ya bei nafuu, inayopatikana kirahisi, iliyoshindwa kudhibitiwa na serikali, inayochochea rushwa kwa polisi na yenye madhara makubwa kwa binadamu.

Sasa basi;
Endapo pombe hiyo itahalalishwa katika misingi ya kufanya mabadiliko katika sifa zote nilizozipata hapo juu basi itakuwa siyo gongo tena. Ni vema ukathibitisha kwamba yote hayo yakifanyika tutafanikiwa kufuta gongo haramu. Maana tunaweza kutengeneza mfumo halali na bado ule haramu ukaendelea kuwepo.

Kushindwa kudhibiti tatizo siyo msingi wa kulihalalisha, tunaweza kujenga hoja ya kuhalalisha utoaji mimba au hata rushwa kwa hoja hiyo hiyo ya kushindwa kwetu kudhibiti.

Ni kweli kwamba hata sigara na pombe zingine zinaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya ya binadamu, ila kwenye gongo tofauti ni ukubwa wa tatizo kwenye jamii. Siyo sahihi kulinganisha konyagi na gongo, Serikali kupandisha kodi kwenye vileo na sigara ni namna mojawapo ya kudhibiti madhara, kama konyagi ingekuwa bei ya gongo nadhani tungekuwa tunazungumza lugha tofauti kabisa.
 
Siungi mkono kwa maana ile anayosema Dr. Slaa kwavile hoja yake naona imekaa kisiasa zaidi hasa inapoelekea kumaanisha kwamba atafanya hivyo kwa ajili ya watengeneza gongo maskini....kwamba hawa watengeneza gongo maskini wa leo, wakiwezeshwa basi watakuwa na uwezo wa kutengeneza gongo iliyo salama. Endapo hoja itajikita kwenye kutengeneza gongo salama bila kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa local gongo brewers, then I can bet on it coz' I know at industrial level, percentage methanol can be reduced to acceptable rate and remain with only methanol necessary to neutralize Ethyl Ethanol. This's very important to me coz' as I stated earlier, to make it safe. production costs itaongezeka maradufu na kuwa si kwa ajili ya watengeneza gongo wa leo tena bali ni kwa ajili ya big investors. Kwahiyo, ikiwa hoja ni kuwafanya watengenezaji wa leo wa-survive kiuchumi basi ni bora kuwaachia kama ilivyo kuliko kuhalalisha wakati unafahamu fika hawatakuwa na ubavu wa kukidhi vigezo, not only financially but also technically. Nitaunga mkono hoja iwapo msingi wa kuhalalisha gongo utakuwa ni ku-attract modern investment ili serikali ipate kodi na sio hivi inavyozungumzwa sasa!

Tuendelee!

  1. Duuh, jamaa (Dr Slaa) kawakamata baadhi ya watu mpaka baaasi!!...Eti nini? Umesema kwamba huungi mkono kwa sababu "maana ya hoja yake imekaa kisiasa". What is your problem exactly hata ushindwe kutambua kuwa ktk nchi yetu kila kitu kinakuja kisiasa kutoka kwa wanasiasa???...Wanasiasa ni wajanja sana,wana control kila kitu wewe,mimi,yule, fedha,mamlaka(dola) nk nk na hii ni popote pale duniani,nenda hata UK,Marekani!!.Hapa nina maana moja tu hatuwezi kuacha kujadili yanayokuwa moved out na wanasiasa kwa sababu haya ndiyo maisha tunayoishi!!.
  2. Ktk bold red; ungekuwa wewe ndiye mtawala na mwanasiasa mwenye mamlaka na maamuzi (kama alivyo Kikwete leo na serikali yake na chama chake CCM) utawasaidiaje watengeneza gongo wa leo na kuepuka hili uliloli - raise la Cost of production kuwa kubwa?
  3. Unasema wazalishaji wa gongo waachwe tu kama walivyo kwa sababu ni wazi hawawezi kumudu gharama za uzalishaji gongo kisasa financially and technically? Unaamaanisha nini hapa? Kwani ktk mfumo wa uendeshaji wa nchi na wananchi who is responsible kuwawezesha watu katika haya?.....Jibu ni rahisi sana; Ni hawahawa wanasiasa kupitia chombo kinachoitwa serikali kwa kutoa sera,sheria,kanuni,miongozo na taratibu zilizowafanya wakubalike kwa wananchi hata wakaambiwa nyie undeni serikali na tusimamieni sisi wananchi!!
  4. Defenetely,walioko madarakani sasa ni wanasiasa wa CCM halafu huku nje ndiyo wako kina Dr Slaa na CHADEMA na wanavizia hiyo nafasi ya kuunda serikali iwapo sera na miongozo za hawa waliopo sasa zitaendelea kushindwa hata kuwajali wapika na wanywa gongo. Jamaa ni lazima watatumia madhaifu ya hawa ili wao kupenya na ktk hili LA KUHALARISHA GONGO,kwa mtazamo wangu Dr Slaa ameamusha mjadala ambao ni sensitive sana unaogusa mamilioni ya watanzania wa kipato cha chini vijijini na mijini ambao ni wapenzi na watumiaji wa kinywaji hiki cha asili ambacho chini ya serikali ya chama cha mapinduzi "kimeharamishwa" lakini kinatengenezwa na kunywewa hivyohivyo kiharamuharamu na watu na sidhani hili kama litakoma!!
  5. Hiyo ktk BLUE BOLD mbona sikuelewi? Kwani Dr SLAA na CHADEMA wanaposema wataandoa uharamu wa gongo kwa kuihalalisha wewe unaelewaje?...iHivi "Modern investment" hapa ina maana gani kwako labda? Wazungu toka Canada kama wale wa Anglo Barrick Mines kule Geita,Tarime na Kahama wanaochimba dhahabu yetu au?.......
  6. Na hapa ndiyo maana mimi nikasema sometimes siasa ni ujanja na kuangalia hitaji la jamii pana(watengenezaji na wanywa gongo ni jamii pana mno ya watu wa kipato cha chini kila kona ya nchi) na hapa maana yake ni kutengeneza kura kwa wanasiasa wajanja. DR SLAA na CHADEMA yake wakiicheza na kui - deliver vizuri hii na ikaeleweka kwa walaji, wanapasua. Wengi wa wanaopingana na sera hii mpya ya CHADEMA badala ya kuipinga kwa hoja wanamtukana matusi ya nguoni. Soma post za mtu anaitwa Chama(huyu ni wazi ni mwana CCM,nafikiri) humu utathibitisha hili.....Kuwapuuza wapika gongo na watumiaji na kufikiri juu ya BIG INVESTMENT ni kosa kubwa la kisiasa!!......Mimi nasema Gongo ihalalaishwe,itengenezwe ktk viwango na katika hali ya usafi na iitwe hivyohivyo 'GONGO TANZANIA BRAND"
 
Hakuna aliymkamata Dr. Slaa. Mleta mada wa awali(ambae ali-include chemical formular ya Gongo) nimemuuliza maswali ya msingi hadi sasa hajajibuingawaje ni karibu wiki sasa! Mchambuzi amesema atayajibu baadae....nasubiri majibu yake manake sitaki hoja za kisiasa kama zilivyoletwa na Dr. Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom