Mkuu Pasco hizo color hapo zinapokuwa connected ndipo bila shaka unadondoka JF na kumwaga "Likes" kwa kwenda mbele!! Manake ile kitu mi naijua, ukishakuwa mjani, unakuwa mtu wa peace & Love, hakuna husuda wala roho mbaya! Masela kitaa utasikia, "jealous people never win!" Hadi sasa umemwaga "Likes" 29,913 jamvini; sidhani kama kuna anayekukaribia achilia mbali kukufikia! I bet by December 31,2013 midnight; utakua ushagonga 30,000!Mkuu Ze Marco, ninachokukubali ni jinsi unavyokuwa king'ng'anizi on what you believe in, kitu ambacho ni kizuri kwenye debate as debate na sio lazima kiwe kweli ni kizuri in reality!.
La bangi nililisemea na nimeishajiribu nilipokuwa Tambaza, nikaijaribu tena nilipokuwa Ilboru, ila mimi inanituma vibaya!, na siku ninapoamua kukubali mwenyewe initume hivyo vibaya, huwa nashtua juzi, jana, leo na kesho!. Haina sumu ya nicotine kama sigara, yenyewe ina canabis tuu!, haileti cancer kama sigara etc. Baadhi ya hospital imekubaliwa na kwa hapa nchini naomba nikupe taarifa rasmi, kosa sio kuvuta bangi bali kukutwa ukivuta hadharani!, kama ilivyo kufanya mapenzi sio dhambi bali kufanya hadharani ni jinai!. Jinai ya bangi ni kukutwa na bangi na sio kuvuta!.
Enzi Walter Rodney akiwa mwalimu UD alikuwa anaipiga hiyo kitu kisawasawa!. Kuna lecture mwingine Mjamaica, alikuwa akiipiga hadharani, wanafunzi waliokereka wakamlipua akashikwa, akashitakiwa, akakiri na kulipishwa faini, utawala wa chuo ukamuita kumuonya na kusema wazi hiyo kitu na sehemu ya maisha yake, ama bangi ama afungashe!. Akakubaliwa kuendelea kuipiga lakini kwa masharti, asiipige tena akiwa darasani au kwenye maeneo ya wazi, ajipigie jani lake akiwa nyumbani kwake!. Marastafarai kibao wanakula hiyo kitu na kuna hadhi waheshimiwa wabunge wetu wanapata hiyo kitu wengine ikiwatuma vizuri, wengine ikiwatuma vibaya ila wapataji wanapata!.
Siungi mkono ndoa za jinsia moja ila niko very accomodative na situation yao haswa wale wanaojikuta huko kwa anatomical reasons and not by choice!. Kuna baadhi yao wamezaliwa na ulemavu huo na ni kama ulemavu mwingine wowote!, ni watu wa kuhurumiwa, kusaidiwa na sio kushangaliwa, kubezswa, kudhihakiwa na kutengwa!.
Merry Chrismass!.
Pasco
Last edited by a moderator: