Dr Slaa na Kuhalalisha Gongo: Kwanini Yupo Sahihi

Dr Slaa na Kuhalalisha Gongo: Kwanini Yupo Sahihi

Status
Not open for further replies.
Achana na hawa wa Lumumba, subiri wale great thinkers wanaojadili hoja, hawa ni magolikipa wa Lumumba hata ukilegeza kiatu na kuwarushia golini wanataka wakidhani ni mpira.

wewe hoja huna, unabwabwaja tu. bora umedhihirisha upumbavu wako kwa kutukana kalale sasa
 
Nchi zilizoendelea sasa hivi zinapamba na ulevi wanapunguza matangazo ya pombe na matumizi ya pombe.

Nchi kwetu viongozi wanapambana kuongeza walevi na kupoteza nguvu kazi.

Kiongozi anayataka kuruhusu gongo leo tunasema amechukua maamuzi sahihi.
 
Hiyo pombe yenyewe hata pato la taifa mchango wake haujulikani.
Pili pombe kimaadili hairuhusiwi si na dini tu bali hata jamii ya watanzania. Sasa mtu kama Slaa aliyepitia upadri iweje leo atangaze kuhalalisha gongo? Manake akija na hoja ya kuhalalisha Ndoa za kijinsia moja kwa kuhakikisha kuna wodi za kuwawezesha wanaume kupata mimba na kujifungua kina mchambuzi nae atakuja kuliunga mkono? Ushabiki wa kisiasa ni mbaya sana. Huyu anatetea alichokisema Slaa kimahaba ya kisiasa tu lakini ajua ubaya wa gongo. Huyu ndio rais mtarajiwa. Kweli CCM ni dume la mbegu na ina hazina ya wanasiasa wenye uweledi sana. Ni mtanzania gani atakubali uvunjwaji huu wa maadili ya mtanzania?
 
Kitu gani sasa hivi kinachomfanya muuza gongo na mnywa gongo kuchagua "option" hiyo wakati kuna safer options? This is the central question...

Hapana, the key questions are:

*Kwanini serikali ilihalalisha chibuku ambayo kimsingi ni traditional brew?
*Kwanini mbege inaendelea kutumika kihalali wakati na yenyewe ni pombe ya kienyeji kama gongo?
*Kwanini serikali ya TANU ilitaka kuhalalisha gongo miaka ya sabini? Je, mazingira ya kuachana na mpango ule bado yapo relevant leo?
*Kwanini viongozi wa CCM hawajitokezi to criticize Dr. Slaa juu ya hili?(Najua utajibu nini katika hili).

Pia kwanini mnapotosha ukweli kwamba moja ya kazi kubwa za SIDO ni pamoja naku organize small scale industrialization nchini, hivyo ina nyenzo na uwezo wa kusimamia suala tunalojadili kupitia its stakeholders iwapo serikali itaona kuna haja ya kufanya hivyo katika kuhalalisha pombe hii kwa hoja nilizojadili awali? Hauoni kwamba katika mamno kama haya, effectiveness ya SIDO ndio itaonekana zaidi?

Na kuhusu affordability ya mitambo, kwanini mnakimbilia bei kwa watengenezaji badala ya kujadili jinsi gani wazalishaji wanaweza kusaidiwa hata kupitia mikopo ambayo itarudisha tu fedha kwani pombe ni biashara yenye faida? Kumbuka, kujadili kwenu bei ya mitambo ni kutapatapa kihoja kwani ilitakiwa msimamie hoja kwamba come what may, kuhalalisha gongo sio sawa;

Mwisho, kwanini kwenye mambo mengine kama yale ya ulaji wa mabilioni ya kikwete ambayo tulidanganywa yalienda kusaidia wafanyabiashara, hatuoni faida zake? Fedha hizi zingeenda kwenye masuala kama haya ya mitambo ya pombe za kienyeji hivi mnajua multiplier effect ambayo ingezaliwa? Kwa jinsi serikali yetu ilivyokuwa bingwa wa kujiendesha kupitia kodi za vilevi na sonyo, muda sio mrefu itaamka katika hili.

Mkuu @zemarcopoli, ipo siku CCM italijadili hili, na nitakuhoji kama nilivyokuhoji mengine baada ya uongozi wa ccm kusema mambo ambayo awali ulinipinga vikali na mimi, na baadae nikikumbusha na kukuita tujadili upya hoja, ni kawaida yako kutoweka;mfano ni hoja ya JK kwa watendaji wa chama nchini kwamba ccm 2015 itapoteza dola iwapo wataendela na siasa zao uchwara za kujiamini na nyimbo za wembe ni ule ule huku wananchi wakitahabika, wembe ambao JK akasema bila ya uangalifu, utawakata wenyewe;sisi tulisema, mkatuita kila aina ya majina, JK au Kinana akisema, mnakenua na kuwapigia makofi;

Katika hili la pombe za kienyeji, ZeMarcopolo, historia itajirudia - kaa chonjo, siku hiyo inakuja;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Huu mjadala wa gongo unathibitisha kuwa nchini kwetu kuna tatizo kubwa sana katika somo la hesabu.

This is very SIMPLE mathematics lakini inawashinda watu wenye masters degree kung'amua! Hili ni janga kwa taifa...

Labda niwape very simple example ili muelewe. Lakini mtaelewa iwapo tu mmedhamiria kuelewa.

Mfikirie kijana anatefanya biashara ya bodaboda. Unapomwambia kijana huyo kwamba ile biashara yake ya bodaboda utaiboresha kwa kumuuzia kihiace ili aweze kubeba abiria wengi kwa mpigo, unakuwa unazungumzia biashara nyingine kabisa na sio ile ya bodaboda.

Hapo hauboreshi biashara ya bodaboda ila unaanzisha biashara mpya ya kihiace ambayo mtaji wake, running costs, risks zake ni tofauti kabisa na bodaboda.

It is extremely NAIVE to presume kwamba waendesha bodaboda nchi nzima watakubaliana na kuyamudu mabadiliko hayo.

Likewise, it is extremely NAIVE to presume kwamba wauza gongo nchi nzima watanunua mitambo ya SIDO.

Hakuna mtu anayewakatalia SIDO kufanya ubunifu wowote wa kuboresha maisha ya watu. It will be excellent kama watabuni mtambo wa miujiza ambao unatengeneza gongo safi na salama kwa gharama ileile.

Hata hivyo swali linabaki palepale, je wale ambao hawatanunua mitambo hiyo na kuendelea kuuza pombe yenye sumu, sheria iseme nini juu yao?

Kumbukeni kuwa vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu vilikuwa vunagawiwa BURE. Lakini wapo watu walivikataa kwa imani kuwa vinapunguza nguvu za kiume. Kwahiyo hata mitambo ya SIDO ikitolewa bure, it is NAIVE to presume that they will be positively perceived everywhere by everyone.

Hatuwezi kuweka sheria ya kumbana mtu anayekataa kutumia chandarua, je tuache pia kuweka sheria kwa watu wanaouza sumu?
 
Tusichoke kuwaelimisha

Mngekuwa very effective iwapo Lumumba ingewafundisha KUELIMISHA, lakini kwa bahati mbaya, mnafundishwa kukosoa, kukashifu na kutukana;hadi sasa haujaja na counter arguments kwanini gongo ihalalishwe au isihalalishwe kwa hoja;pengine ni kwasababu signature yako tayari ilishamkebehi DR. Slaa and little did you know kwamba tupo wachache wenye uelewa juu ya umuhimu wa hoja hiin tumewachambulia, mnajiuma uma tu; hilo ndio tatizo la 'kuchambuliwa'; jifunze kuchambua mambo rationally and objectively, msijadili mtu, jadili hoja;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hapa unakosea. Thinking ya namna hii haiwezi kutufikisha popote. Unajua mtu anaweza kufa hata kwa kula ugali iwapo ataula hovyo. Au soda, hivi mtu akinywa soda non stop, atakuwa salama? Tukiuendesha mjadala kwa design hii tutapoteza mwelekeo. Kama unataka gongo iruhusiwe kwa sababu unadhani gongo na konyaji ni vinywaji sawa, basi inabidi turudi hatua nyingi sana nyuma kabla hatujaanza kujadili kuhalalishwa au kutokuhalalishwa kwa gongo.
@ZeMarcoplo, kiwango duni cha uelewa unachouonesha katika huu mjadala unaniacha mdomo wazi! Kwa mada iliyopo mbele yetu kwa nini ujikite katika kuelezea athari za ulevi kama vile athari hizo ni kwa pombe ya gongo tu na si vilevi vingine? Ni pombe gani haina athari za kibiolojia, kisaikolojia, kiuchumi na kijamii kwa kutumia maneno yako? Ningekuelewea kama ungekuwa unataka pombe za aina zote zipigwe marufuku...hapo labda ningekuelewa ingawa hicho ni kitu unachojua fika kuwa katu hakiwezekani, not now not ever. Hakuna nchi yoyote iliyofanikiwa kutokomeza ulevi wa aina yoyote ile ingawa zipo zinazojidanganya kwamba zimeweza...sana sana zimejikuta zikikabiliwa na athari za ulevi uliojificha wenye athari kuliko ulevi wa wazi.

ZeMarcopolo said:
Halafu unaposema kuwa gongo iruhusiwe kwa sababu jamii zote zilianza kwa kuwa na viwango duni unakuwa TOO low. Hiyo ni sawa na kusema watu wawe wanavaa vibwaya mpaka siku watakatengeneza kiwanda chao cha nguo.

Teknolojia ikishagunduliwa ukikataa kuitumia kwa sababu eti wenzako nao walianza chini unakuwa unajichelewesha mwenyewe kuendelea. Unaona Dar es Salaam jiji limejaa magari kibao lakini hakuna hata moja lililobuniwa au kutenenezwa Tanzania. Kwanini kwenye gongo ndio tusisitize kwamba iendelee kunywewa mpaka tutakapobuni njia zetu?
Katika post zote za kipuuzi nilizowahi kuzisoma jamvini, this one takes the prize! Kwa hiyo ubunifu out the window! Kwa nini tulitafuta uhuru? Kwa nini tuhangaike na elimu? Kwa nini tuhitaji wataalam wetu? Tulipoteza tamaduni zetu, tukapoteza imani zetu, tukapoteza majina yetu, tukapoteza uzalendo wetu...sasa tunataka kupoteza na utu wetu...sasa tutabakiwa na nini? Utumwa? Uzezeta? Tutakuwa na tofauti gani na wanyama wa kufugwa. ZeMarcopolo, Dr Slaa alisema hivi;
Dr. Slaa said:
Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi.
Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.
Kama vile umezinduka usingizini ZeMarcopolo unaongezea hii inayoonekana kupingana na dhana yako ya awali kama ulivyoelezea hapo juu;
ZeMarcopolo said:
Hivi unajua kwanini wanasayansi wanafanya conferences? Well, lengo kuu ni kupeana uzoefu mbalimbali wa taarifa mpya. Ukishaipata ile taarifa kama wewe ni mtu unayependa maendeleo unaitumia kuboresha viwango vya kazi unazofanya. Sio sahihi kusema utaendelea na njia duni mpaka pale utakapogundua mwenyewe.
ZeMarcopolo, je unajua kwamba mpaka sasa wananchi wanaoathirika kwa unywaji wa maji yasio salama ni maradufu ya wanaoathirika na unywaji wa "gongo" usio salama? Je kuna ubaya wowote akitokea mtu na kupendekeza kuchukuliwa kwa hatua kuhakikisha mafi safi na salama yanapatikana? Je "gongo" salama? Hata hivyo wapo wengi waliofikia hapo walipo, thanks to utengenezaji/unywaji wa pombe.

Yawezekana kwako wewe pombe ni haramu lakini kubali usikubali, hapa nchini hata wewe unafaidika sana tu na biashara ya pombe kwani ni moja katika njia zinazoiingizia serikali mapato. Biashara ya "gongo" kama ilivyo biashara ya vinywaji vingi vya ulevi kama bia, whisky, vodka rum n.k. imeweza kuboresha maisha ya watu wengi tu na kuwawezesha wengine kufika hapo walipo.Kwa jirani zetu Kenya pombe ya chang'aa ambayo ni jina pacha la gongo iliruhusiwa kwa watu walio tayari kuzingatia viwango na kanuni kama zilivyoorodheswa na serikali.

th

Hii ni bar mojawapo hapo Dar es Salaam. Bishara ya pombe haitaweza kupigwa marufuku jijini/nchini.
​

Duh, ZeMarcopolo, jaribu kuacha unafiki, kweli huoni hoja katika hili bandiko la Mchambuzi? je huoni faida yoyote ya uboreshaji katika utengenezaji wa kinywaji chochote cha burudani kama gongo? Huoni kwamba unazoita athari za gongo, ambazo hazina tofauti na pombe zozote zingine zile, zitapungua kama itatengenezwa katika mazingira salama? Huna hata huruma na Watanzania wenzako?
 
Ningekuona mwerevu sana kama ungenisaidia kuandika lihadithi langu refu kwa hiyo mistari miwili au mitatu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Hivi mwenyewe ndio umejitutumua kutetea gongo kwa maandiko mareeeefu. Rudi ukasome post yangu #71 , ina mistari 7 imeelezea maudhui nne tofauti na zote zinaeleweka na to the point.

Wewe umeandika jikitabu zima maudhui moja na haueleweki.
 
Dr. Slaa yuko sahihi kama mazingira ya utengenezaji wa gongo yakiboreshwa haitokuwa haramu tena, wanaokereka na hilo jina watapendekezwa jina jingine baada ya chadema kshika dola
 
Si kwamba sikusoma bandiko lako hili, honestly sikuona cha maana ambacho kiliamsha akili yangu nikujibu;
Hayakuanza leo hayo, Nyerere alijaribu na kiwanda cha konyagi yakamshinda.
hauelezi nyerere na konyagi walishindwana wapi na kwanini, wakati mimi nilijadili kwanini kuhalalisha gongo haikuwezekana miaka 30 na kitu iliyopita;lakini muhimu, haujadili kwanini leo chini ya serikali ya JK, pombe kama chibuku na mbege ni halali lakini sio gongo;
Sasa hivi mitaani kuna viroba ambavyo amma bei sawa au chini ya bei ya gongo, lakini wapenzi wa gongo uzi uleule.
Hakuna kinachoeleweka hapa;

Alozowea vya kuchinja vya kunyonga haviwezi.
Hii ni mipasho;
Kwa hili la gongo Babu kachemsha. Ni bora angesemea bangi ningemuelewa na ningemuunga mkono.
Nimejadili kwanini namuunga mkono Dr. Slaa lakini badala na nyie kuja na counter arguments, mnasingizia uzi mrefu, au mnakimbia hoja na kuanzisha mijadala ya bodaboda kama ZeMarcopolo;

Kitu kingine ambacho babu angesema chenye maana ni kuwa encourage walipike kwa wingi zaidi na kulifanya gongo kuwa mafuta mbadala ya gari (kama economics za kwetu zinalipa) kama ilivyo Brazil, hapo ningemuelewa lakini hili la kuhalalisha iwe kinywaji halali, kalishindwa Nyerere ataweza babu?
Haujibu swali langu kwamba je mazingira ya kushindwa miaka 30 na kitu iliyopita ni yale yale ya leo?

Vinginevyo hoja juu ya matumizo ya gongo kama mafuta ya gari ni mjadala tofauti lakini muhimu zaidi, hapa tunaongelea kuhalalisha kitu ambacho tayari kipo, kina soko, na kina "economics" zake if I may borrow your term, (gongo as an alcoholic beverage sio kipya kama wazo la alternative fuel), safety issues na regulations kadhaa ambazo zinakuja na political will kama kwa suala la chibuku litamaliza matatizo husika kwani tatizo la gongo sio gongo per se bali mchakato wa utengenezwaji wake;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
@ZeMarcoplo, kiwango duni cha uelewa unachouonesha katika huu mjadala unaniacha mdomo wazi! Kwa mada iliyopo mbele yetu kwa nini ujikite katika kuelezea athari za ulevi kama vile athari hizo ni kwa pombe ya gongo tu na si vilevi vingine? Ni pombe gani haina athari za kibiolojia, kisaikolojia, kiuchumi na kijamii kwa kutumia maneno yako? Ningekuelewea kama ungekuwa unataka pombe za aina zote zipigwe marufuku...hapo labda ningekuelewa ingawa hicho ni kitu unachojua fika kuwa katu hakiwezekani, not now not ever. Hakuna nchi yoyote iliyofanikiwa kutokomeza ulevi wa aina yoyote ile ingawa zipo zinazojidanganya kwamba zimeweza...sana sana zimejikuta zikikabiliwa na athari za ulevi uliojificha wenye athari kuliko ulevi wa wazi.

Katika post zote za kipuuzi nilizowahi kuzisoma jamvini, this one takes the prize! Kwa hiyo ubunifu out the window! Kwa nini tulitafuta uhuru? Kwa nini tuhangaike na elimu? Kwa nini tuhitaji wataalam wetu? Tulipoteza tamaduni zetu, tukapoteza imani zetu, tukapoteza majina yetu, tukapoteza uzalendo wetu...sasa tunataka kupoteza na utu wetu...sasa tutabakiwa na nini? Utumwa? Uzezeta? Tutakuwa na tofauti gani na wanyama wa kufugwa. ZeMarcopolo, Dr Slaa alisema hivi;

Kama vile umezinduka usingizini ZeMarcopolo unaongezea hii inayoonekana kupingana na dhana yako ya awali kama ulivyoelezea hapo juu;
ZeMarcopolo, je unajua kwamba mpaka sasa wananchi wanaoathirika kwa unywaji wa maji yasio salama ni maradufu ya wanaoathirika na unywaji wa "gongo" usio salama? Je kuna ubaya wowote akitokea mtu na kupendekeza kuchukuliwa kwa hatua kuhakikisha mafi safi na salama yanapatikana? Je "gongo" salama? Hata hivyo wapo wengi waliofikia hapo walipo, thanks to utengenezaji/unywaji wa pombe.

Yawezekana kwako wewe pombe ni haramu lakini kubali usikubali, hapa nchini hata wewe unafaidika sana tu na biashara ya pombe kwani ni moja katika njia zinazoiingizia serikali mapato. Biashara ya "gongo" kama ilivyo biashara ya vinywaji vingi vya ulevi kama bia, whisky, vodka rum n.k. imeweza kuboresha maisha ya watu wengi tu na kuwawezesha wengine kufika hapo walipo.Kwa jirani zetu Kenya pombe ya chang'aa ambayo ni jina pacha la gongo iliruhusiwa kwa watu walio tayari kuzingatia viwango na kanuni kama zilivyoorodheswa na serikali.

th

Hii ni bar mojawapo hapo Dar es Salaam. Bishara ya pombe haitaweza kupigwa marufuku jijini/nchini.
​

Duh, ZeMarcopolo, jaribu kuacha unafiki, kweli huoni hoja katika hili bandiko la Mchambuzi? je huoni faida yoyote ya uboreshaji katika utengenezaji wa kinywaji chochote cha burudani kama gongo? Huoni kwamba unazoita athari za gongo, ambazo hazina tofauti na pombe zozote zingine zile, zitapungua kama itatengenezwa katika mazingira salama? Huna hata huruma na Watanzania wenzako?
Tatizo lenu mkishapenda then mnakuwa mfu kabisa katika kusimamia ukweli na kuwatoa upunguani wenzenu. ZeMarcopolo amechambua mada hii kisomi zaidi sjui kwanini mmekuwa vilaza hivi kuelewa anachomaanisha. Endeleeni kujijaxa ujinga tu.
 
Last edited by a moderator:
Hapana, the key questions are:

*Kwanini serikali ilihalalisha chibuku ambayo kimsingi ni traditional brew?
*Kwanini mbege inaendelea kutumika kihalali wakati na yenyewe ni pombe ya kienyeji kama gongo?
*Kwanini serikali ya TANU ilitaka kuhalalisha gongo miaka ya sabini? Je, mazingira ya kuachana na mpango ule bado yapo relevant leo?
*Kwanini viongozi wa CCM hawajitokezi to criticize Dr. Slaa juu ya hili?(Najua utajibu nini katika hili).

Pia kwanini mnapotosha ukweli kwamba moja ya kazi kubwa za SIDO ni pamoja naku organize small scale industrialization nchini, hivyo ina nyenzo na uwezo wa kusimamia suala tunalojadili kupitia its stakeholders iwapo serikali itaona kuna haja ya kufanya hivyo katika kuhalalisha pombe hii kwa hoja nilizojadili awali? Hauoni kwamba katika mamno kama haya, effectiveness ya SIDO ndio itaonekana zaidi?

Na kuhusu affordability ya mitambo, kwanini mnakimbilia bei kwa watengenezaji badala ya kujadili jinsi gani wazalishaji wanaweza kusaidiwa hata kupitia mikopo ambayo itarudisha tu fedha kwani pombe ni biashara yenye faida? Kumbuka, kujadili kwenu bei ya mitambo ni kutapatapa kihoja kwani ilitakiwa msimamie hoja kwamba come what may, kuhalalisha gongo sio sawa;

Mwisho, kwanini kwenye mambo mengine kama yale ya ulaji wa mabilioni ya kikwete ambayo tulidanganywa yalienda kusaidia wafanyabiashara, hatuoni faida zake? Fedha hizi zingeenda kwenye masuala kama haya ya mitambo ya pombe za kienyeji hivi mnajua multiplier effect ambayo ingezaliwa? Kwa jinsi serikali yetu ilivyokuwa bingwa wa kujiendesha kupitia kodi za vilevi na sonyo, muda sio mrefu itaamka katika hili.

Mkuu @zemarcopoli, ipo siku CCM italijadili hili, na nitakuhoji kama nilivyokuhoji mengine baada ya uongozi wa ccm kusema mambo ambayo awali ulinipinga vikali na mimi, na baadae nikikumbusha na kukuita tujadili upya hoja, ni kawaida yako kutoweka;mfano ni hoja ya JK kwa watendaji wa chama nchini kwamba ccm 2015 itapoteza dola iwapo wataendela na siasa zao uchwara za kujiamini na nyimbo za wembe ni ule ule huku wananchi wakitahabika, wembe ambao JK akasema bila ya uangalifu, utawakata wenyewe;sisi tulisema, mkatuita kila aina ya majina, JK au Kinana akisema, mnakenua na kuwapigia makofi;

Katika hili la pombe za kienyeji, ZeMarcopolo, historia itajirudia - kaa chonjo, siku hiyo inakuja;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Katika post yako hii naona umebadilisha lugha. Hutumii neno gongo, unasema "pombe za kienyeji".

Nimewaomba MODs waunganishe hizi threads kwa sababu mambo mengi nimeyaeleza kwenye threads nyingine. Hapa naona kama tunaanza upya.

Kuhusu CCM na rushwa nimeshasema kwamba simjui kiongozi hata mmoja aliyeshinda uchaguzi ndani ya CCM bila kutoa rushwa. Mtu yeyote anayejua chaguzi za CCM hawezi kukataa hili.

Kwa vile umeleta diversion, naomba na mimi nilete diversion kidogo.

Wewe Mchambuzi unajitambulisha kama mwana CCM lakini kutwa kazi yako ni kutetea sera za Chadema na Dr. Slaa huku ukiponda kila kitu about CCM. Remind me the last time you wrote anything good about CCM. Kuna kitu alikwambia Pasco may be you should consider it.

Ndugu yangu Mag3 kwanza nikutakie Christmass njema. Pili, hoja zako nyingi nimekuwa nikizijibu kwa wiki sasa kwenye thread zilizotangulia. Tafadhali ukipata fursa pitia huko for my position on this issue. I have been very consistent on what I advocate.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo pombe yenyewe hata pato la taifa mchango wake haujulikani.
Pili pombe kimaadili hairuhusiwi si na dini tu bali hata jamii ya watanzania.

Duh!

Inamaana hujuhi Mchango wa waleve lwenye pato la taifa ?

Na ndio maana wanataka Kuboresha kisha kuirasimisha Gongo ili ichangie kama Konyagi na Kibuku.

Maadili yapi? Mbona Kanisani Mnakunywa pombe? Hivi Ule mkate si una Divai ? Divai si Gongo iliyochakachuliwa tu au ?
 
*Kwanini serikali ya TANU ilitaka kuhalalisha gongo miaka ya sabini? Je, mazingira ya kuachana na mpango ule bado yapo relevant leo

Serikali ya TANU ilipiga vita mfumo wa vyama vingi. Kwa minajili hiyo ya kuona kila kilichosemwa na TANU ni alfa na omega, utasema tupigr vita mfumo wa vyama vingi.
 
Kibuku sio pombe kali. Haina methanol.
Haitumii decomposed products kutengeneza.

This comparison is not relevant.

You are very wrong;nitajadili na kufafanua zaidi kwenye sehemu yangu ya pili;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Serikali ya TANU ilipiga vita mfumo wa vyama vingi. Kwa minajili hiyo ya kuona kila kilichosemwa na TANU ni alfa na omega, utasema tupigr vita mfumo wa vyama vingi.

Umekimbia hoja;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
*Kwanini viongozi wa CCM hawajitokezi to criticize Dr. Slaa juu ya hili?(Najua utajibu nini katika hili).

Kila kitu na wakati wake.

Kipindi cha kushindanisha sera ni kipindi cha uchaguzi. Hapo ndio huwa kuna haja ya kila hoja kujibiwa na hoja.

Hiki ni kipindi cha kila chama kupanga safu yake ready for 2014 and 2015. Kama Slaa ameona kupanga safu yake ni kutetea gongo, shauri yake. Si kazi ya CCM kumjibu.

Vyama viko vingi, ukiendekeza kujibu utajikuta kuanzia asubuhi mpaka jioni unajibu wanasiasa tu. CCM ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi sio kujibu wanasiasa.

Kama Slaa aliongea ili CCM imjibu basi amebugi. Na kama anahitaji jibu basi ninaweza kumpa in advance.

Sheria za nchi zinatungwa Bungeni. Iwapo wananchi wanaona kipaumbele chao cha maendeleo ni kuruhusu biashara ya gongo ishamiri, wajenge hoja na kuwapa wabunge wao wapeleke Bungeni. Hakuna mtu mmoja anayeweza kuahidi kubadili sheria, mtu wa namna hiyo ni muongo.
 
*Kwanini mbege inaendelea kutumika kihalali wakati na yenyewe ni pombe ya kienyeji kama gongo?

Ukisoma posts zilizotangulia nimekuuliza, kama unaona hizi pombe nyingine ni sawa na gongo, kwanini usipiganie nazo zipigwe marufuku, badala yake unapigania gongo ihalalishwe?
 
Tatizo lenu mkishapenda then mnakuwa mfu kabisa katika kusimamia ukweli na kuwatoa upunguani wenzenu.
Mipangomingi, hebu jaribu kuwa wazi ueleweke, tatizo letu eti tukishapenda...kupenda nini? Hapa hoja ni kinywaji cha gongo kuhalalishwa ili iweze kutengenezwa katika mazingira safi na salama kwa wanaoitumia. Mpaka hapo kuna tatizo gani? Huo upunguani wetu ni upi na ukweli unaouongelea ni upi? Kwamba gongo pamoja na kupigwa marufuku haipo? Kumbuka Tanzania imezaliwa mwaka 1964 ikaikuta gongo ipo, hadi leo ipo na itaendelea kuwepo. Kwa hali ilivyo sasa ni kwamba inatoa mwanya kwa vyombo vya dola na viongozi wala rushwa kuzidi kuneemeka kwa njia haramu kuwakamua eti wanaokamatwa na gongo. Gongo ni pombe kama pombe zingine; tofauti ni mazingira ya utengenezaji tu.
ZeMarcopolo amechambua mada hii kisomi zaidi sjui kwanini mmekuwa vilaza hivi kuelewa anachomaanisha.
Hakuna mada yoyote aliyochambua ZeMarcopolo kisomi labda unitajie. Kwamba gongo inaathiri kibiolojia? Kisaikolojia? Kiuchumi? Kijamii? Ni pombe gani haina athari hizi; bia? konyagi? vodka? gin? whisky? Captain Morgan (rum)? Kwa nini gongo. Na tukiongelea mazingira; hata soda ikitengenezwa kwenye mazingira machafu inaweza kuleta madhara makubwa!
Nimesema kama tatizo ni pombe, basi ZeMarcopolo angeeleweka kama angeunga mkono upigwaji marufuku wa aina zote za pombe.
Endeleeni kujijaxa ujinga tu.
Asante sana Mipangomingi, ubarikiwe sana.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom