Dr Slaa na Kuhalalisha Gongo: Kwanini Yupo Sahihi

Status
Not open for further replies.
Lengo la mleta mada anataka tumuone kama yeye ni mccm ambaye yupo tofauti na wenzake kwa kukubali mawazo bila kujali yanatoka wapi.

Sijui kwanini aliamua kudandia hili la pombe wakati yapo mambo mengi ya msingi ambayo wapinzani wanayasimamia kwa mfano kwenye katiba mpya au tume huru.

hamna msingi wowote wa kuruhusu chang'aa hapa kwetu. Hata hizi pombe zilizopo madukani tukisema tuwaulize watanzania najua zaidi ya 70 percent watasema zifutwe sasa sijui Dr Slaa na wewe mlikuwa mnazungumza kwa niaba ya nani.
 
Mchambuzi

Hii hoja inapaswa kuchambuliwa kwa kuangalia mazingira halisi yaliyopo na siyo kutumia nadharia tu.

Gongo ikitengenezwa kwa utaaalamu unaoujengea hoja hapa itakuwa siyo gongo tena bali ni kinywaji tofauti cha chupa kitakachopewa jina la "Gongo"

Nina mashaka kama wapika gongo, wengi wao wakiwa ni walala hoi, watamudu gharama za kununua na kuendesha mitambo hiyo.

Sijui kama hiyo mitambo ya Sido itaendeshwa kwa umeme, mafuta au kuni? Angalia tatizo hapo kwa upana kwa kutilia maanani hali halisi iliyopo sasa huko kwa wapishi wa gongo.

Pia kwa kweli sina uhakika kama mitambo midogo ya Sido inaweza kukidhi mahitaji ya kutengeneza pombe hiyo kitaalamu kwa standard inayotakiwa hasa ukitilia maanani kuwa miongoni mwa ingredients zake ni vinyesi na vitu vilivyooza. Itahitaji pia kuagiza au kutengeneza vifaa vya vipimo vya ubora na madhara ya kiafya kwa viwango vinayakubalika kimataifa na hiyo ni dhahiri itaongeza gharama za utengenezaji wa mitambo hiyo na pia kwa mnunuzi na mteja.

Gongo la kienyeji litaendelea kutengenezwa na inawezekana itakuwa imepatiwa uhalali na kupata njia rahisi kujipenyeza kwenye Baa ndani ya chupa ya gongo iliyohalalishwa. Utapeli bongo ndiyo nyumbani

Warusi wana kinywaji kikali kukaribia gongo,Vodka lakini bado kuna vodka/gongo ya kienyeji "samagon" inashamiri na kuangamiza watu wengi mpaka leo hasa walalahoi.

Pia, issue ya maadili na mtazamo wa jamii ni muhimu sana kama alivyoeleza vizuri sana Bethlehem. Naamini hii ndiyo sababu wengi wanapinga kauli ya Dr. Slaa na siyo kwa sababu za kisiasa. Issue hii sehemu kubwa ya jamii inaiweka kwenye kundi moja na ukahaba, mapenzi ya jinsia moja na madawa ya kulevya.

Kama ulivyofanya wewe, anaweza kujitokeza Mchambuzi mwingine akaweka hapa thesis nzima yenye vielelezo vyilivyobobea kitaalam kwanini ni sahihi kuhalalisha ukahaba, bangi au madawa ya kulevya lakini sidhani Kama sehemu kubwa ya jamii itakuwa tayari kuelewa na kuunga mkono.

Suala hili mimi na wewe tunaweza kulizungumza hadharani na likachukuliwa kama mtazamo binafsi lakini kauli nzito kama hii inapotolewa hadharani na Mwanasiasa mwenye hadhi nzito kama Dr. Slaa inachukuliwa kama ni mtazamo wa taasisi anayoiwakilisha na siyo wake binafsi. Jamii yetu haijawa tayari kuipokea kauli kama hii kama inavyodhirishwa na reaction ya wengi kuhusu kauli ya Dr.Slaa.

Kuwahusisha wanaoipinga na sababu za kisiasa tu ni kutowatendea haki kwa kweli.
Mkuu TZ-kwanza , kunatatizo linalowakabili Watanzania, nalo ni taboo.

Watanzania hawataki kuongelea mambo kwa uwazi hata kama yapo katika jamii.
Leo umalaya unaonekana neno baya sana kuliko nyumba ndogo.

Ukimwi ulipoanza watu waligoma kusema fulani kafariki kwa ukimwi, walisema kapigwa kipapai.
Baada ya jamii kuumia na tatizo, sasa hivi imekubali kwa shingo upande, utasikia marehemu amefariki kwa kisukari cha ghafla, pneumonia hata kama ni TB, kiharusi cha muda mwingi, pressure isiyoshuka kamwe na mambo kama hayo.

Nakumbuka Marehemu Tuntemeke aliwahi kusema bangi iruhusiwe kwasababu kwao inatumika kama sehemu ya mboga za majani.Aliungwa mkono na Marehem Jackson Mwakweta ndani ya bunge la JMT.
Sioni kwanini hili liwe la taasisi na si la mwanasiasa kwasababu la Tuntemeke na Makweta hayakuwa ya taasisi.

Lakini pia nadhani ni hatua nzuri kwa wanasiasa kuwa wa wazi ili tujue wanasimamia wapi na kwanini, wana maono gani na wanapokea vipi hoja wanazokutana nazo huko wanakopita.

Ndani ya bunge la JMT ukiuliza wabunge nini msimamo wao kuhusu mambo ya kitaifa hutapata jibu bali jibu la kichama.
Suala linaloweza kupatiwa jibu la haraka na linalowaunganisha wabunge ni Posho na mishahara yao tu, hilo kila mmoja ataliongelea mwenyewe, ya kitaifa wanajificha nyuma ya vyama vyao.

Haw watu wanaoongoza na hatujui wanasimamia nini ni hatari zaidi kuliko anayesema.
Mfano, Dr Slaa kasema yeye ataiangalia gongo kwa jicho la uhalali kwa msimamo wake.
Niulize nani anajua msimamo wa viongozi wengine wanaotajwa kuhusu suala la gongo? Hata mmoja aliyesimama na kukosoa, hakuna kwasababu hawataki kujulikana wanasimamia wapi.

Hivyo nadhani mjadala wa Dr Slaa si kwamba unavunja taboo za kijinga lakini unatupa msiamamo wake kuhusu mambo ya nchi. Ima ni sahihi au si sahihi hilo linabaki kwa kila mmoja.

Kwa muktadha huo, gongo ipo na inapikwa tena ina walaji kuanzia Dodoma mjengoni hadi vijijini.
Dr Slaa kasema yeye taruhusu iwe halali kwa kuiboresha. Well,reaction ya watu unayoiona si kwasababu amekosea au yupo sahihi ni kutokana na taboo ya kuongelea gongo.

Tena wanaotoa reactions baadhi yao wametoka kupata kichupa cha pepsi kwa mtindo wa netball (kupokezana). Tuue hii taboo na tuongelee issue kama zilivyo.

Kwavile unadhani itakuwa ni gharama na hakuna jinsi ya kuiboresha, je wewe unashauri nini kifanyike.?
Tuendelee kukaa kimya watu wanateketea kwa kuogopa taboo au tujadili na kuona ni vipi suluhisho linaweza kupatikana
 
Lengo la mleta mada anataka tumuone kama yeye ni mccm ambaye yupo tofauti na wenzake kwa kukubali mawazo bila kujali yanatoka wapi.

Sijui kwanini aliamua kudandia hili la pombe wakati yapo mambo mengi ya msingi ambayo wapinzani wanayasimamia kwa mfano kwenye katiba mpya au tume huru.

hamna msingi wowote wa kuruhusu chang'aa hapa kwetu. Hata hizi pombe zilizopo madukani tukisema tuwaulize watanzania najua zaidi ya 70 percent watasema zifutwe sasa sijui Dr Slaa na wewe mlikuwa mnazungumza kwa niaba ya nani.
Maundumula, mbona mCCM number 1 JK anakubali mawazo ya upande wa upinzani?
Kwani kukubali mawazo bila kujali yanatoka wapi ni dhambi?

Nadhani katika watu wanaojadili hayo unayoyasema kwa kina na undani ni huyo unayemsema. Hebu jipe muda upitie nyuzi zake kabla ya kujiridhisha kwa hayo uliyonena.

Aslimia 70 unaipataje ikiwa viwanda vya bia ndio chanzo cha mapato. Soko la pombe limekuwa na ushindani Tanzania, kila siku kama si aina fulani aina nyingine inaingia sokoni.
Hapo usiweke wanywaji wa chang'a, mbege, Chimpumu, Pingu, matap tap, Komoni,mnazi na dengelua kwa uchache.

Vipi kama ungemjibu kwa hoja ili nawe tusikie una maoni gani juu ya kupigwa marufuku? ni sababu zipi unazodhani na njia ipi itumike?
 
Lengo la mleta mada anataka tumuone kama yeye ni mccm ambaye yupo tofauti na wenzake kwa kukubali mawazo bila kujali yanatoka wapi.

Sijui kwanini aliamua kudandia hili la pombe wakati yapo mambo mengi ya msingi ambayo wapinzani wanayasimamia kwa mfano kwenye katiba mpya au tume huru.

hamna msingi wowote wa kuruhusu chang'aa hapa kwetu. Hata hizi pombe zilizopo madukani tukisema tuwaulize watanzania najua zaidi ya 70 percent watasema zifutwe sasa sijui Dr Slaa na wewe mlikuwa mnazungumza kwa niaba ya nani.

Mwongozo wa ccm(1982) unaposema kwamba kukosoa na kukosoana ni silaha ya mapinduzi maana yake ni nini kama sio kuruhusu mawazo mbadala? Mwongozo unaonya wanachama kama wewe na viongozi kutohamaki wanapokosolewa bali kushiriki katika mijadala na kutafuta ufumbuzi; Tatizo lako na wenzako ni kwamba mnaishi kwa mtindo wa zidumu fikra sahihi za mwenyekiti, sasa mwenyekiti huyo huyo kawaambia majuzi dodoma kwamba msipokuwa waangalifu, mtafanya chama kipoteze uchaguzi 2015 na kuwaeleza kwamba kelele za "wembe ule ule" wembe utawakata wenyewe; baadae kidogo, kinana akaomba msamaha kwa wananchi kwa kusema ccm imefanya mambo ya maana lakini kuna mengine mengi imefanya ya ovyo sana ambayo yameathiri wananchi, akataja suala na ubinaifishaji n.k;masuala aliyojadili kikwete na kinana ni yale yale ambayo mimi ndani ya ccm na wengine wengi ndani na nje ya ccm wamekuwa wakiyajadili, na badala ya kuona hoja, mnatuita kila aina ya majina; kwa vile ni kinana na kikwete, mnakenua meno na kupiga makofi; Sasa kwa kutumia maneno yako hapo juu Je - Mwenyekiti wako Kikwete na Katibu Mkuu wako kinana kusema waliyosema, je how do they fit in katika kauli yako hii kwamba:

Lengo la mleta mada anataka tumuone kama yeye ni mccm ambaye yupo tofauti na wenzake kwa kukubali mawazo bila kujali yanatoka wapi
.

Tatizo lenu ni unafiki na utomvu wa mawazo kutokana na kudhania kwamba shughuli za ccm ni shughuli binafsi kama vile azam, ipp, METL n.k ambapo mkikosolewa mnaona kama ni wivu wa kibiashara;ccm ni mali ya Wanachama ambayo kupitia kwake, wanachama na wasio wanachama wameipa dhamana ya kuongoza na kuendesha nchi kupitia kodi zao;kama ikishindwa, ipishe wengine, hakuna haja ya kutetea mabovu yanayoumiza wananchi huku hapo hapo ukijiendesha kwa kutumia kodi zao;

Ccm itakufa kutokana na wanafiki kama wewe ambao hawaelewi kwamba sifa moja wapo ya kiongozi ni kukubali mawazo mazuri hata kama ni ya mpinzani wako; isitoshe, ccm inatekeleza mengi ya mawazo ya upinzani baada ya kuona umuhimu wake, kwa mfano suala la katiba ambalo unasema silijadili wakati profile yangu imejaa mada kibao juu ya katiba mpya;

Amka toka usingizini, acha ujinga (hili sio tusi)/ignorance, tumia fursa yako kujenga nchi hata kama itabomoa maslahi ya wanaokutuma Lumumba; anza kwa kujadili hoja ya gongo iliyopo mbele yetu na uchague upande na kuchambua kwa HOJA; hoja yako kuhusu 70% ya watanzania watasema pombe zote zifutwe ni hoja hafifu sana na ya kujaribu kuyeyusha hoja mbele yetu ambapo serikali hii hii imehalalisha chibuku, inanyamazia kimya mbege, na ni bingwa wa kukusanya kodi kubwa kubwa kutoka kwenye vilevi badala ya kubuni vyanzo vipya vya kodi; narudia tena, punguza ujinga/ignorance, hii ni miaka 52 ya uhuru;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wazee wa viroba na gongo+akili za kibavicha=?

Hivi mnajua kiasi gani wanasiasa wa ccm waliopo bungeni leo wananunua madebe ya gongo kununua kura wakati wa uchaguzi? Hadi ushahidi wa video upo; na kwa 2015 wengi wenu mtakuwa ni wapambe wa wagombea wa ccm kwenda kuhonga wapiga kura gongo; acheni unafiki, tuungane kuokoa afya za watanzania;

Cc ZeMarcopolo, ifweero, FaizaFoxy, Maundumula, Ritz, chama, MSALANI, Dr.W.Slaa, Nguruvi3 NasDaz

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi you've played your part well.tatizo hapa ni kwamba wengi wana mitizamo ya kiitikadi na wengine pia wana allergy na mtu aitwaye Dr.Slaa.
 
Lengo la mleta mada anataka tumuone kama yeye ni mccm ambaye yupo tofauti na wenzake kwa kukubali mawazo bila kujali yanatoka wapi.

Sijui kwanini aliamua kudandia hili la pombe wakati yapo mambo mengi ya msingi ambayo wapinzani wanayasimamia kwa mfano kwenye katiba mpya au tume huru.

hamna msingi wowote wa kuruhusu chang'aa hapa kwetu. Hata hizi pombe zilizopo madukani tukisema tuwaulize watanzania najua zaidi ya 70 percent watasema zifutwe sasa sijui Dr Slaa na wewe mlikuwa mnazungumza kwa niaba ya nani.

Badilika ndugu usiwaze buku 7 tu.
 
Hivi mnajua kiasi gani wanasiasa wa ccm waliopo bungeni leo wananunua madebe ya gongo kununua kura wakati wa uchaguzi? Hadi ushahidi wa video upo; na kwa 2015 wengi wenu mtakuwa ni wapambe wa wagombea wa ccm kwenda kuhonga wapiga kura gongo; acheni unafiki, tuungane kuokoa afya za watanzania;

Cc ZeMarcopolo, ifweero, FaizaFoxy, Maundumula, Ritz, chama, MSALANI, Dr.W.Slaa, Nguruvi3 NasDaz

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi,
Hii issue ni debatable subject tena yenye economical interest kwa nchi na watu. Lakini kwa bahati mbaya Dr.W.Slaa aliishusha hii subject kisiasa sana...hata hivyo, kutokana na nafasi yake, cjui angeiwakilisha vipi hoja yake hii ili isionekane ya kisiasa.
Rose Mayemba alipoileta hii mada hapa jamvini alianza vizuri na kuonekana ni ya mada inayozingatia weledi kitaalamu. Kwa bahati mbaya, kama walivyo wataalamu wetu wengine; panapo politics, hawaoni taabu kujia hamnazo. Ingawaje alianza kuiwasilisha mada kitaalamu na kutoa nuru, baadae akajitoa ufahamu na akaingiza siasa kiasi cha kuwaona wale wanaopinga ni kama watu wasio na akili wakati suala la uharamu na ama uhalali wa gongo ni suala la kitaalamu zaidi kuliko kufikia kutoa conclusion nyepesi. Matokeo yake, hoja yake yote ikapoteza msingi wa kitaalamu na kuonekana ni kama iliyolenga kuja kumtetea Dr. Slaa na kuwaponda wale ambao na hoja ya Dr. Slaa.

Sina shaka hata kidogo na uwezo wako Mchambuzi katika kuchambua na kuyaelezea mambo! Kwa bahati mbaya nawe ukafanya kosa lile lile alilofanya Rose. Ulifanya haraka kuileta mada yako na kuwataka watu wasubiri hoja za msingi kuhusu mada yenyewe. Kwavile ulifanya haraka, matokeo yake nawe ukaleta hoja zenye msingi ule ule; wa kisiasa huku mambo mengine ya msingi ukiwa umeacha kipolo! Kwa bahati mbaya, watu hawawezi kujadili kijacho ambacho hakuna anayekifahamu zaidi ya wewe mwenyewe. Kutokana na ombwe hilo, watu hawana budi kujadili hoja yako iliyo mezani ambayo haina tofauti kubwa sana na ile ya Dr. Slaa na hitimisho la Rose.

Hivyo basi, badala ya kuwadhihaki akina Marcopolo, chama, @FaizaFoxy and the like kwa kuona wanaingiza siasa za CCM na CHADEMA; ningekushauri wewe kwanza ulete zile hoja za msingi na za kisayansi kuhusu ni namna gani hii dangerous gongo ya leo inaweza kuwa safe gongo at minimal cost for the advantage of poor Tanzanians; not only brewers but also end users! Lakini ikiwa analysis yako itaishia kugundua kwamba, in order to make gongo safe, it'll no longer be cheap in terms of production and end users; usione taabu hapa ku-conclude na kusema wazi kwamba "Wazo la Dr. Slaa ni zuri lakini haliwezi kuwa na msaada kwa watu maskini bali litasaidia sana kuongeza wigo wa mapato ya kodi coz' it can attract large or middle level investors; whether local or foreign." Kinyume chake, tuache watu wenye political interests waingize politics coz' mada zenyewe zinawakilishwa kisiasa siasa!!
 
Nimekusoma mkuu; ni kwamba tu nilikuwa mbali kidogo kukamilisha sehemu ya pili na pengine nilikosea kutoweka sehemu ya kwanza na ya pili katika bandiko moja; naomba muda kidogo pilika pilika za xmas zitulie halafu ntamalizia hoja;
Wakati mkinisubiri, kuna hoja muhimu sana za Nguruvi3 ambazo ningependa kusikia mawazo yenu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Sehemu ya Kwanza

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wilbrod Slaa akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Chama Chake mkoani Kigoma alikuja na hoja kwamba, iwapo umma wa watanzania utakiamini Chadema na kukipa ridhaa ya kuliongoza Taifa 2015, kati ya mambo muhimu ambayo Chadema itayafanya ni pamoja na Kuhalalisha Utengenezaji wa Pombe ya Gongo ambapo Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) litapewa jukumu la kutengeneza mitambo ya gongo ili isaidie kuongeza ubora wa pombe hii ili isiwe na madhara kwa wanywaji kama ilivyo sasa. Kwa kumnukuu, Dr. Slaa alisema

Kwa bahati mbaya sana, mjadala unaoendelea juu ya hili umetekwa na watu waliojaa ujinga (ujinga sio tusi) kuliko werevu, kwani wanaachia "ignorance" kutawala "common sense". Katika hili, ninazungumzia wale wote ambao wanajadiili hoja husika kwa kusukumwa na hisia za kisiasa Zaidi. Ili kulielewa suala husika vyema, kuna umuhimu wa kuweka kando itikadi za vyama. Lakini pengine niseme pia kwamba wapo watanzania wanaosukumwa na imani zao za kidini (Wakristo na Waislamu) ambao kutokana na imani zao, pombe ni kitu haramu, haijalishi ni Jack Daniels, Hennessey, Heineken au GONGO. Ni muhimu tukaheshimu upande huu wa hoja, na binafsi sitatizwi kabisa na upande huu wa hoja, hivyo sitajadili wala kujibu hoja zenye mwelekeo huo. Kinacho nitatiza ni ule upande wa hoja ambao unasukumwa Zaidi kwa hisia za kisiasa kuliko Common sense, hasa katika our socio-economic context

Nianze kwa kusema kwamba - katika hili, Dr Slaa hakukosea, na nichukue fursa hii kumpa pongezi za dhati @Dr. W.Slaa kwani hayo ndio maana ya maamuzi magumu yanayopaswa kufanywa na Kiongozi, maamuzi ambayo Kiongozi wa kweli huwa tayari kuyafanya bila ya kusita na bila ya woga kwamba wengine hawajafanya hivyo, lakini muhimu Zaidi, kiongozi wa kweli yupo tayari kutetea anachokiamini. Nikiwa kama mtanzania ambae nimependezwa na hoja ya msingi ya Dr. Slaa kwa kuona manufaa yake nje ya itikadi za vyama, nipo tayari kumsaidia kuelewesha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa kuhalalisha gongo kama alivyoelezea Dr. Slaa.

Tujiulize – je:
· Maana ya neno "Haramu" ni nini?

Maana yake rahisi ni kitu ambacho kimekatazwa kwa mujibu wa sheria, au by official or accepted rules. Swali linalofuatia ni je:
· Ni sababu zipi ambazo zimepelekea Gongo kuwa unlawful in Tanzania huku pombe nyingine zikiendelea kuwa halali kisheria?

Hili ni swali gumu kidogo kulijibu moja kwa moja, na ni moja ya sehemu muhimu ya hoja yangu ya msingi. Kama tutakavyoona baadae katika mjadala, "uharamu
wa gongo unachangiwa Zaidi na kukosekana kwa juhudi za serikali za kuhalalisha ‘gongo' kwa mtindo ule ule uliotumika kuhalalisha pombe kama "Chibuku", na kuzinyamazia pombe kama "mbege".

Sehemu kubwa ya watanzania wanaombeza Dr. Slaa ni wale ambao wamelelewa kutofikiri nje ya boksi (out of the box) kwani kimsingi ilitakiwa wafanya yafuatayo:
· Aidha kumpinga from a policy and regulation perspective kwa nia ya kumhoji Zaidi ili waone kama hoja ya Dr. Slaa ina mashiko, au kama sio hivyo, basi
· Wampe pongezi Dr. Slaa kwa kuwa mbunifu wa kutafuta njia za kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Binafsi nipo kwenye kundi la pili kwani nina uelewa tosha wa policy and regulatory implications za suala husika, hivyo, nichukue fursa hii kumpongeza Dr. Slaa kwa kuja na maamuzi magumu ambayo wanasiasa wengi wangeogopa kuja nayo kwani wengi wao hawana uwezo wa kusimamia wanachokiamini, lakini mbaya Zaidi, hawatumii akili zao kubuni njia za kutatua matatizo ya wananchi, badala yake, wanatumia muda mwingi kubuni njia za kuboresha matumbo na familia yao ‘at the expense of the poor', hasa wale wale wanaojitafutia rizki zao vijijini kupitia biashara kama hizi za gongo kwa maisha kama ya ‘kuku wa kienyeji' kwani, nje ya kuwanyonya kupitia uzalishaji wa mazao ya chakula to feed the urban elites na mazao ya biashara for exports to fund the bureaucracy, serikali imewatupa kwa miaka Zaidi ya 50.

Iwapo wapo viongozi ambao wanapinga hoja ya Dr. Slaa, basi wajitokeze mbele ya umma na wafafanulie umma kwanini Dr. Slaa hayupo sahihi. Vinginevyo ukimya wao maana yake ni kwamba hawana hoja kwani kwa hili wamezidiwa kete. Kilichobakia ni wao kukaa kimya na kutegea wana "CCM maslahi" kumshambulia Dr. Slaa juu ya hili kwa kupotosha mantiki ya hoja nzima. Mimi kama mtanzania kwanza, mwana CCM baadae nimeona mashiko makubwa ya hoja ya Dr. Slaa na nina amini kwamba, mawazo yake yakifanyiwa kazi kikamilifu, yatakuwa na tija kwa uchumi wa wahusika pamoja na afya za wanywaji.

Kwa wale wote mnaombeza Dr. Slaa katika hili, ni muhimu mtambue kwamba mataifa mengi makubwa duniani ambayo yamepiga hatua katika suala zima la viwanda vya bidhaa mbalimbali yalianza uzalishaji kupitia mbinu za kienyeji (traditional methods) ambapo wazalishaji waliendesha shughuli zao majumbani au karibia na makazi yao. Mifano ni mingi – kuanzia the blue brothers waliokuja na wazo la kutengeneza ndege ya abiria, na viwanda vingine vingi vikubwa duniani ambavyo vinatengeneza goods for direct consumption. Hata utengenezaji wa pombe katika jamii hizi haukuwa tofauti na haya kwani brands za pombe zinazotambulika duniani leo (beers, whiskies, brandy, gins, wines etc), utengenezaji wake ulianzia majumbani na vilabuni. Ni baadae sana utengenezaji wa pombe hizi ukaingia ‘on an industrial scale'. Hoja ya msingi katika hili ni kwamba serikali za mataifa makubwa leo – badala ya kuwakwaza wabunifu na wazalishaji, wao walikuja na interventions (policy and regulatory wise) ambapo walianzisha udhibiti, safety standards and regulations, kwa lengo la kumwinua mzalishaji na kumlinda mnywaji. Uwepo wa vyombo kama Food and Drugs Association nchini marekani ni matokeo ya serikali kujali kuwekeza katika juhudi hizi.

Tanzania ni nchi huru (kisiasa) kwa miaka 50, lakini kiuchumi ni nchi tegemezi, na utegemezi huu unachangiwa sana na Serikali kutokuwa inward oriented na kunyayua wazalishaji wa ndani na pia kuja na policy interventions zinazolenga kuwekeza katika ‘innovation capabilities' za wananchi, suala ambalo lingesaidia nchi kuwa na consumption ya home made goods (na pengine exports) ambazo kitendo cha serikali kuzitambua na kusaidia kuzikuza kungesaidia sana wananchi kujenga Utamaduni wa kuthamini bidhaa zao. Badala yake, kutokana na serikali kukosa umakini wa kusimamia ipasavyo suala zima la Utamaduni katika Nyanja ya uchumi, vitu vingi vinavyotengenezwa Tanzania vinaendelea kutambulika kama ‘haramu', ‘chini ya viwango', na ‘havifai' mbele ya macho ya watanzania walio wengi. Bidhaa ya mtanzania maskini ambayo inaonekana kuwa ni ya maana mbele ya serikali ni mazao ya chakula to feed the urban elites na pia mazao ya biashara (kahawa, chai, n.k) ambayo yanaisaidia serikali kupata fedha kuendesha bureaucracy yake, huku matokeo kwa mkulima wa mazao ya biashara yakiwa ni sifuri in terms of improvement of livelihoods kwa watanzania walio wengi (vijijini). Ni aibu na inasikitisha kuona kwamba miaka 52 baada ya uhuru, serikali inatawala wananchi wenye kuabudu bidhaa na Utamaduni wa nje kuliko vya kwao, huku serikali yao ikiendelea kuabudu Zaidi wawekezaji na mitaji ya nye bila ya kujali kwamba watanzania wana mitaji mikubwa kuliko hiyo ya wawekezaji (ubunifu na pia rasilimali za nchi kama vile madini, n.k).

Kwa wale wanaombeza Dr. Slaa katika hili la kuhalalisha ‘gongo', ni muhimu wakatambua pia kwamba – wazo la kuhalalisha gongo liliwahi kujadiliwa wakati wa utawala wa Baba wa Taifa - Mwalimu Nyerere (mwanzo mwa miaka ya 1970s) ambapo serikali ilikuja na wazo la kuhalalisha utengenezaji wa gongo kwa njia ya kuboresha viwango n.k. Kilichositisha zoezi hili ilikuwa ni pamoja na matokeo ya utafiti ambayo yalionyesha kwamba kwa hali za watanzania wa wakati ule (miaka kama kumi baada ya uhuru), watanzania wengi wasingeweza kumudu bei ya pombe hii kufuatia impact of ‘regulating and licensing' of the product. Uamuzi wa kuhalalisha pombe ya gongo ulikwama miaka ya sabini, lakini katika mazingira ya sasa ambayo socio-economic profile ya watanzania wengi imebadilika, serikali ikiamua kufufua mkakati huu, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mafanikio.

Kwa wale wote wanaombeza Dr. Slaa katika hili, kutokana na haya yote, mna haja ya kuelewa kabla ya kupinga hoja ya Dr. Slaa, hivyo kuendelea kutambua pombe ya gongo kama haramu, tujifunze kwa wenzetu ambao badala ya kukwaza wazalishaji wa pombe, waliamua kwanza kuwekeza katika juhudi za kuinua wazalishaji na kulinda afya za wanywaji kupitia taasisi mbalimbali za udhibiti wa viwango kama nilivyokwisha jadili. Ni pale tu udhibiti unaposhindikana ndio serikali inatakiwa kuja na mpango wa kupiga marufuku, sio utengenezaji wa pombe tu, bali chochote ambacho mzalishaji amelenga kwa ajili ya matumizi ya binadamu, huku akijipatia rizki yake.

Kwa wale wote wanaombeza Dr. Slaa katika hili, ni muhimu mkatambua kwamba linapokuja suala la pombe ya gongo, tatizo la msingi sio gongo ‘per se', bali mchakato wa utengenezaji wa gongo, lakini hasa ukosefu wa specifications pamoja na quality control ambayo ni routine and scientific, hali ambayo inapelekea pombe za kienyeji kama gongo kuendelea kuwa unpredictable in terms of the right quality and right quantity. As a result, pombe kama gongo huishia kuwa na constituents ambazo hazitakiwi kuwepo ndani ya kilevi, kitu ambacho ni hatari kwa afya za watumiaji (nitajadili hili kwa undani baadae). Muhimu pia ni kwamba tofauti na pombe nyingine zinazotengenezwa na kuwa packaged kisasa Zaidi, pombe kama gongo haina "long shelf life" (baada ya kutengenezwa), na matokeo yake ni - increased concentration of toxic constituents (tutalijadili kwa undani baadae).

Kwa kumalizia sehemu hii ya kwanza – niseme tu kwamba badala ya kumbeza Dr. Slaa katika hili, na badala ya serikali kuendelea kupiga marufuku utengenezaji wa pombe ya gongo kwa miaka 52 ya uhuru, kuna haja ya serikali kuzinduka kutoka usingizini na kuja na mkakati wa kuboresha mazingira ya utengenezaji, sio tu wa pombe ya gongo, bali pombe zote za kienyeji zinazotengenezwa chini ya kiwango kama historia inavyotueleza kuhusiana na mataifa yaliyoendelea. Vinginevyo kama nchi hizi zingeendelea kupiga marufuku pombe katika karne za huko nyuma badala ya kuingilia kwa kumwinua mzalishaji na kumlinda mnywaji, makampuni makubwa kama SABMiller, Heineken, Guinness na mengineyo leo yasingekuwao. Hivyo basi, badala ya kuendelea kumbeza Dr. Slaa katika hili, huku serikali nayo iking'ang'ania na mtazamo wake kwa miaka 52 kwamba "Gongo ni haramu", kuna haja ya Serikali sasa kuja na regulations, safety and standard procedures ambazo zitasaidia kuwanyanyua wazalishaji huku pia ikiwalinda wanywaji.

Baada ya sehemu hii ya utangulizi, katika sehemu ya pili ya mjadala, nitakuja na uchambuzi wa kina juu ya pombe hii ya gongo, hasa kwa kuifananisha na pombe nyingine za kienyeji kama vile mbege, pombe ya mananasi, na Kibuku. Katika hili, tutaona jinsi gani serikali ilivyokuwa na double standards kwa kuhalalisha Chibuku na kwa kunyamazia Mbege. Pamoja na athari zinazoendana na matumizi ya Gongo, udhibiti wa athari hizi upo ndani ya uwezo wa serikali kupitia vyomba kama vile TBS, TFDA na taasisi nyinginezo (sio polisi), lakini only if there is "Political Will."

Itaendelea…

Cc Chakaza, Ericus Kimasha, Daudimtwale, Dr.W.Slaa, Ritz, ifweero

wahurumie vijana wengi wanaosoma sasa st.marys/mathewe nk wengi ni spoonfeeding, hivyo baadhi yao hawawezi kufikiri nje ya boksi, ww jiulize mbona tembo(pombe ya mnazi) imeruhusiwa na inauzwa na kwa taarifa ya vijana ambao hamjawahi kunywa hii ni pombe hatari kuliko gongo. tofauti ya tembo na gongo ni mazingira ya utengenezaji. pombe ya mnazi process yake ni fupi lakini ni hatari kuliko gongo

hivi watu wanajua viroba na konyaji ni hatari kuliko gongo lakin mbona zinatumiwa. kama unabisha waulize walevi kwann wanalazimika mara nyingi kuchanganya na pombe nyingine ndipo wanywe. kunywa mfululizo peke yake halafu uone kitakachokupata.

tangu gongo imekuwa haramu upishi na uuzaji wake katika mazingira machafu umekithiri. kwa bahati mbaya watumiaji wakubwa ni maskini ambao hata uwezo wa kula vizuri haupo.matokeo yake tumepoteza nguvu kazi kubwa ya taifa kwa kuendelea kuifanya kuwa haramu. la msingi bora iharalishwe ili iwekewe viwango na kupunguzwa alcoholic content vinginevyo tutaendelea kuua watu. gongo haina tofauti na matumizi ya kondomu, tangu watu wameambiwa kondomu ni kinga wamekuwa wazinzi na waasherati kuliko hata wanyama, ndio maana hata maambukizi ya ukimwi yanatisha kwa sasa. usiangalie takwimu za hospitali think beyond the box, utajua ukweli. vinginevyo basi uzinzi na uasherati uwe haramu kisheria na watu wafungwe wakikamatwa wanafanya nje ya ndoa

gt jitahidi kuwaelimisha labda watakuelewa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom