Dr Slaa na Kuhalalisha Gongo: Kwanini Yupo Sahihi

Status
Not open for further replies.

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,830
2,000
Sehemu ya Kwanza

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wilbrod Slaa akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Chama Chake mkoani Kigoma alikuja na hoja kwamba, iwapo umma wa watanzania utakiamini Chadema na kukipa ridhaa ya kuliongoza Taifa 2015, kati ya mambo muhimu ambayo Chadema itayafanya ni pamoja na Kuhalalisha Utengenezaji wa Pombe ya Gongo ambapo Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) litapewa jukumu la kutengeneza mitambo ya gongo ili isaidie kuongeza ubora wa pombe hii ili isiwe na madhara kwa wanywaji kama ilivyo sasa. Kwa kumnukuu, Dr. Slaa alisema

Gongo sasahivi ni haramu kwa sababu inatengenezwa katika mazingira machafu, tukishika dola, tutataka SIDO itengeneza mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi

Kwa bahati mbaya sana, mjadala unaoendelea juu ya hili umetekwa na watu waliojaa ujinga (ujinga sio tusi) kuliko werevu, kwani wanaachia "ignorance" kutawala "common sense". Katika hili, ninazungumzia wale wote ambao wanajadiili hoja husika kwa kusukumwa na hisia za kisiasa Zaidi. Ili kulielewa suala husika vyema, kuna umuhimu wa kuweka kando itikadi za vyama. Lakini pengine niseme pia kwamba wapo watanzania wanaosukumwa na imani zao za kidini (Wakristo na Waislamu) ambao kutokana na imani zao, pombe ni kitu haramu, haijalishi ni Jack Daniels, Hennessey, Heineken au GONGO. Ni muhimu tukaheshimu upande huu wa hoja, na binafsi sitatizwi kabisa na upande huu wa hoja, hivyo sitajadili wala kujibu hoja zenye mwelekeo huo. Kinacho nitatiza ni ule upande wa hoja ambao unasukumwa Zaidi kwa hisia za kisiasa kuliko Common sense, hasa katika our socio-economic context

Nianze kwa kusema kwamba - katika hili, Dr Slaa hakukosea, na nichukue fursa hii kumpa pongezi za dhati @Dr. W.Slaa kwani hayo ndio maana ya maamuzi magumu yanayopaswa kufanywa na Kiongozi, maamuzi ambayo Kiongozi wa kweli huwa tayari kuyafanya bila ya kusita na bila ya woga kwamba wengine hawajafanya hivyo, lakini muhimu Zaidi, kiongozi wa kweli yupo tayari kutetea anachokiamini. Nikiwa kama mtanzania ambae nimependezwa na hoja ya msingi ya Dr. Slaa kwa kuona manufaa yake nje ya itikadi za vyama, nipo tayari kumsaidia kuelewesha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa kuhalalisha gongo kama alivyoelezea Dr. Slaa.

Tujiulize – je:
· Maana ya neno "Haramu" ni nini?

Maana yake rahisi ni kitu ambacho kimekatazwa kwa mujibu wa sheria, au by official or accepted rules. Swali linalofuatia ni je:
· Ni sababu zipi ambazo zimepelekea Gongo kuwa unlawful in Tanzania huku pombe nyingine zikiendelea kuwa halali kisheria?

Hili ni swali gumu kidogo kulijibu moja kwa moja, na ni moja ya sehemu muhimu ya hoja yangu ya msingi. Kama tutakavyoona baadae katika mjadala, "uharamu
wa gongo unachangiwa Zaidi na kukosekana kwa juhudi za serikali za kuhalalisha ‘gongo' kwa mtindo ule ule uliotumika kuhalalisha pombe kama "Chibuku", na kuzinyamazia pombe kama "mbege".

Sehemu kubwa ya watanzania wanaombeza Dr. Slaa ni wale ambao wamelelewa kutofikiri nje ya boksi (out of the box) kwani kimsingi ilitakiwa wafanya yafuatayo:
· Aidha kumpinga from a policy and regulation perspective kwa nia ya kumhoji Zaidi ili waone kama hoja ya Dr. Slaa ina mashiko, au kama sio hivyo, basi
· Wampe pongezi Dr. Slaa kwa kuwa mbunifu wa kutafuta njia za kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Binafsi nipo kwenye kundi la pili kwani nina uelewa tosha wa policy and regulatory implications za suala husika, hivyo, nichukue fursa hii kumpongeza Dr. Slaa kwa kuja na maamuzi magumu ambayo wanasiasa wengi wangeogopa kuja nayo kwani wengi wao hawana uwezo wa kusimamia wanachokiamini, lakini mbaya Zaidi, hawatumii akili zao kubuni njia za kutatua matatizo ya wananchi, badala yake, wanatumia muda mwingi kubuni njia za kuboresha matumbo na familia yao ‘at the expense of the poor', hasa wale wale wanaojitafutia rizki zao vijijini kupitia biashara kama hizi za gongo kwa maisha kama ya ‘kuku wa kienyeji' kwani, nje ya kuwanyonya kupitia uzalishaji wa mazao ya chakula to feed the urban elites na mazao ya biashara for exports to fund the bureaucracy, serikali imewatupa kwa miaka Zaidi ya 50.

Iwapo wapo viongozi ambao wanapinga hoja ya Dr. Slaa, basi wajitokeze mbele ya umma na wafafanulie umma kwanini Dr. Slaa hayupo sahihi. Vinginevyo ukimya wao maana yake ni kwamba hawana hoja kwani kwa hili wamezidiwa kete. Kilichobakia ni wao kukaa kimya na kutegea wana "CCM maslahi" kumshambulia Dr. Slaa juu ya hili kwa kupotosha mantiki ya hoja nzima. Mimi kama mtanzania kwanza, mwana CCM baadae nimeona mashiko makubwa ya hoja ya Dr. Slaa na nina amini kwamba, mawazo yake yakifanyiwa kazi kikamilifu, yatakuwa na tija kwa uchumi wa wahusika pamoja na afya za wanywaji.

Kwa wale wote mnaombeza Dr. Slaa katika hili, ni muhimu mtambue kwamba mataifa mengi makubwa duniani ambayo yamepiga hatua katika suala zima la viwanda vya bidhaa mbalimbali yalianza uzalishaji kupitia mbinu za kienyeji (traditional methods) ambapo wazalishaji waliendesha shughuli zao majumbani au karibia na makazi yao. Mifano ni mingi – kuanzia the blue brothers waliokuja na wazo la kutengeneza ndege ya abiria, na viwanda vingine vingi vikubwa duniani ambavyo vinatengeneza goods for direct consumption. Hata utengenezaji wa pombe katika jamii hizi haukuwa tofauti na haya kwani brands za pombe zinazotambulika duniani leo (beers, whiskies, brandy, gins, wines etc), utengenezaji wake ulianzia majumbani na vilabuni. Ni baadae sana utengenezaji wa pombe hizi ukaingia ‘on an industrial scale'. Hoja ya msingi katika hili ni kwamba serikali za mataifa makubwa leo – badala ya kuwakwaza wabunifu na wazalishaji, wao walikuja na interventions (policy and regulatory wise) ambapo walianzisha udhibiti, safety standards and regulations, kwa lengo la kumwinua mzalishaji na kumlinda mnywaji. Uwepo wa vyombo kama Food and Drugs Association nchini marekani ni matokeo ya serikali kujali kuwekeza katika juhudi hizi.

Tanzania ni nchi huru (kisiasa) kwa miaka 50, lakini kiuchumi ni nchi tegemezi, na utegemezi huu unachangiwa sana na Serikali kutokuwa inward oriented na kunyayua wazalishaji wa ndani na pia kuja na policy interventions zinazolenga kuwekeza katika ‘innovation capabilities' za wananchi, suala ambalo lingesaidia nchi kuwa na consumption ya home made goods (na pengine exports) ambazo kitendo cha serikali kuzitambua na kusaidia kuzikuza kungesaidia sana wananchi kujenga Utamaduni wa kuthamini bidhaa zao. Badala yake, kutokana na serikali kukosa umakini wa kusimamia ipasavyo suala zima la Utamaduni katika Nyanja ya uchumi, vitu vingi vinavyotengenezwa Tanzania vinaendelea kutambulika kama ‘haramu', ‘chini ya viwango', na ‘havifai' mbele ya macho ya watanzania walio wengi. Bidhaa ya mtanzania maskini ambayo inaonekana kuwa ni ya maana mbele ya serikali ni mazao ya chakula to feed the urban elites na pia mazao ya biashara (kahawa, chai, n.k) ambayo yanaisaidia serikali kupata fedha kuendesha bureaucracy yake, huku matokeo kwa mkulima wa mazao ya biashara yakiwa ni sifuri in terms of improvement of livelihoods kwa watanzania walio wengi (vijijini). Ni aibu na inasikitisha kuona kwamba miaka 52 baada ya uhuru, serikali inatawala wananchi wenye kuabudu bidhaa na Utamaduni wa nje kuliko vya kwao, huku serikali yao ikiendelea kuabudu Zaidi wawekezaji na mitaji ya nye bila ya kujali kwamba watanzania wana mitaji mikubwa kuliko hiyo ya wawekezaji (ubunifu na pia rasilimali za nchi kama vile madini, n.k).

Kwa wale wanaombeza Dr. Slaa katika hili la kuhalalisha ‘gongo', ni muhimu wakatambua pia kwamba – wazo la kuhalalisha gongo liliwahi kujadiliwa wakati wa utawala wa Baba wa Taifa - Mwalimu Nyerere (mwanzo mwa miaka ya 1970s) ambapo serikali ilikuja na wazo la kuhalalisha utengenezaji wa gongo kwa njia ya kuboresha viwango n.k. Kilichositisha zoezi hili ilikuwa ni pamoja na matokeo ya utafiti ambayo yalionyesha kwamba kwa hali za watanzania wa wakati ule (miaka kama kumi baada ya uhuru), watanzania wengi wasingeweza kumudu bei ya pombe hii kufuatia impact of ‘regulating and licensing' of the product. Uamuzi wa kuhalalisha pombe ya gongo ulikwama miaka ya sabini, lakini katika mazingira ya sasa ambayo socio-economic profile ya watanzania wengi imebadilika, serikali ikiamua kufufua mkakati huu, ni dhahiri kwamba kutakuwa na mafanikio.

Kwa wale wote wanaombeza Dr. Slaa katika hili, kutokana na haya yote, mna haja ya kuelewa kabla ya kupinga hoja ya Dr. Slaa, hivyo kuendelea kutambua pombe ya gongo kama haramu, tujifunze kwa wenzetu ambao badala ya kukwaza wazalishaji wa pombe, waliamua kwanza kuwekeza katika juhudi za kuinua wazalishaji na kulinda afya za wanywaji kupitia taasisi mbalimbali za udhibiti wa viwango kama nilivyokwisha jadili. Ni pale tu udhibiti unaposhindikana ndio serikali inatakiwa kuja na mpango wa kupiga marufuku, sio utengenezaji wa pombe tu, bali chochote ambacho mzalishaji amelenga kwa ajili ya matumizi ya binadamu, huku akijipatia rizki yake.

Kwa wale wote wanaombeza Dr. Slaa katika hili, ni muhimu mkatambua kwamba linapokuja suala la pombe ya gongo, tatizo la msingi sio gongo ‘per se', bali mchakato wa utengenezaji wa gongo, lakini hasa ukosefu wa specifications pamoja na quality control ambayo ni routine and scientific, hali ambayo inapelekea pombe za kienyeji kama gongo kuendelea kuwa unpredictable in terms of the right quality and right quantity. As a result, pombe kama gongo huishia kuwa na constituents ambazo hazitakiwi kuwepo ndani ya kilevi, kitu ambacho ni hatari kwa afya za watumiaji (nitajadili hili kwa undani baadae). Muhimu pia ni kwamba tofauti na pombe nyingine zinazotengenezwa na kuwa packaged kisasa Zaidi, pombe kama gongo haina "long shelf life" (baada ya kutengenezwa), na matokeo yake ni - increased concentration of toxic constituents (tutalijadili kwa undani baadae).

Kwa kumalizia sehemu hii ya kwanza – niseme tu kwamba badala ya kumbeza Dr. Slaa katika hili, na badala ya serikali kuendelea kupiga marufuku utengenezaji wa pombe ya gongo kwa miaka 52 ya uhuru, kuna haja ya serikali kuzinduka kutoka usingizini na kuja na mkakati wa kuboresha mazingira ya utengenezaji, sio tu wa pombe ya gongo, bali pombe zote za kienyeji zinazotengenezwa chini ya kiwango kama historia inavyotueleza kuhusiana na mataifa yaliyoendelea. Vinginevyo kama nchi hizi zingeendelea kupiga marufuku pombe katika karne za huko nyuma badala ya kuingilia kwa kumwinua mzalishaji na kumlinda mnywaji, makampuni makubwa kama SABMiller, Heineken, Guinness na mengineyo leo yasingekuwao. Hivyo basi, badala ya kuendelea kumbeza Dr. Slaa katika hili, huku serikali nayo iking'ang'ania na mtazamo wake kwa miaka 52 kwamba "Gongo ni haramu", kuna haja ya Serikali sasa kuja na regulations, safety and standard procedures ambazo zitasaidia kuwanyanyua wazalishaji huku pia ikiwalinda wanywaji.

Baada ya sehemu hii ya utangulizi, katika sehemu ya pili ya mjadala, nitakuja na uchambuzi wa kina juu ya pombe hii ya gongo, hasa kwa kuifananisha na pombe nyingine za kienyeji kama vile mbege, pombe ya mananasi, na Kibuku. Katika hili, tutaona jinsi gani serikali ilivyokuwa na double standards kwa kuhalalisha Chibuku na kwa kunyamazia Mbege. Pamoja na athari zinazoendana na matumizi ya Gongo, udhibiti wa athari hizi upo ndani ya uwezo wa serikali kupitia vyomba kama vile TBS, TFDA na taasisi nyinginezo (sio polisi), lakini only if there is "Political Will."

Itaendelea…

Cc Chakaza, Ericus Kimasha, Daudimtwale, Dr.W.Slaa, Ritz, ifweero
 

CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
7,032
2,000
Ngoja waje wale wajinga, Chang'aa ya kenya ni zaidi ya Gongo lakini ilifika mahari wakaona ihalalishee, Pamoja na Gongo kutokutambulika kisheria wanywaji hawajawahi i miss hata siku moja. Ni sawa na Bangi hakuna mtumiaji wa bangi aliye shindwa kuvuta, bangi zipo kila siku Gongo ipo kila siku mirungi ipo na inaliwa kila siku.
 

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,605
2,000
Ndugu Mchambuzi Mimi jambo hili naliangalia zaidi katika muktadha wa kisiasa kuliko muktadha wa kiuchumi kwa mazingira ya Tanzania. Dr.Slaa ni kiongozi wa kisiasa, Lengo lake kuu ni kupata uungwaji mkono na jamii ya walio wengi kabla ya kitu chochote kile.

Ndugu Mchambuzi unapotaja neno gongo katika mazingira ya tanzania kutokana na kanuni za kimaadili na kiutamaduni ni neno lisilo na mvuto kwa jamii ya walio wengi. Kwa hiyo jambo hilo likishupaliwa, watu hawataliangalia katika misingi ya kiuchumi nakiafya bali kimaadili na hivyo kufanya mwanasiasa anayesimamia hiyo ajenda kupotezakukubalika.Anayekataa na ajaribu aone.Ni sawa na concept ya kuhalalisha ukahaba (kumradhi) anayetaka na ajaribu kuja na ajenda hii aone kama atapata uungwaji mkono na jamii ya kitanzania.Suala kwa hoja za aina hii si uchumi wala Afya; ni kanuni za kimaadili za jamii.
 
Last edited by a moderator:

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,830
2,000
Ndugu Mchambuzi Mimi jambo hili naliangalia zaidi katika muktadha wa kisiasa kuliko muktadha wa kiuchumi kwa mazingira ya Tanzania. Dr.Slaa ni kiongozi wa kisiasa, Lengo lake kuu ni kupata uungwaji mkono na jamii ya walio wengi kabla ya kitu chochote kile.
Naunga mkono hoja lakini pia ni muhimu uelewe kwamba kazi ya mwanasiasa ni pamoja na kubaini kero za wananchi na kuzifanyia kazi. Suala la gongo limekuwa kero kwa muda mrefu na nimejaribu kufafanua hapo juu kwanini nadhani sasa ifikie wakati kero hii ipatiwe ufumbuzi, bila ya kujalisha itikadi za kisiasa;

Ndugu Mchambuzi unapotaja neno gongo katika mazingira ya tanzania kutokana na kanuni za kimaadili na kiutamaduni ni neno lisilo na mvuto kwa jamii ya walio wengi. Kwa hiyo jambo hilo likishupaliwa, watu hawataliangalia katika misingi ya kiuchumi nakiafya bali kimaadili na hivyo kufanya mwanasiasa anayesimamia hiyo ajenda kupotezakukubalika.Anayekataa na ajaribu aone.Ni sawa na concept ya kuhalalisha ukahaba (kumradhi) anayetaka na ajaribu kuja na ajenda hii aone kama atapata uungwaji mkono na jamii ya kitanzania.Suala kwa hoja za aina hii si uchumi wala Afya; ni kanuni za kimaadili za jamii.

Kwahiyo una maana gongo ingeitwa jina lingine kama vile "punguza kiu" n.k, suala la maadili lisingekuwa na uzito? Vinginevyo naona msingi wa hoja yako, lakini kama ulinisoma vyema kwenye bandiko namba moja hapo juu, nilijadili kwamba hoja zozote zinazoendana na masuala ya kimaadili na kitamaduni zina mashiko yake, na nitaheshimu hoja zote za namna hiyo, hivyo sitazijadili hizo. Badala yake, hoja yangu itajikita zaidi katika kuchambua juu ya umuhimu wa serikali kuhalalisha gongo kwa manufaa ya uchumi wa mtengenezaji, afya ya mnywaji, pamoja na multiplier effect ya kuhalalisha pombe za namna hii katika uchumi wa taifa, hasa katika nchi ambayo serikali yake inatambua vilezi vingine vya kienyeji kama kama vile mbege, chibuku, chimpumu, lakini vile vile vinywaji vya kigeni ambavyo ni moja ya vyanzo vikuu vya kodi ya serikali. Tanzania ingekuwa ni nchi ambayo imepiga marufuku vilevi vyote kwa mujibu wa sheria, hoja yangu na ile ya Dr. Slaa zingekosa mashiko.
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013
2,000
Umeandika maneno meeeeeeeengi lakini kumbe hata hujui Dr. Slaa alisema nini!

Anza kwanza kusoma alichosema Dr. Slaa halafu kafanye correction ya kile ulichoandika.

Slaa alisema anahalalisha gongo ili wauza gongo wasikamatwe na polisi ambao huchukua rushwa kwa wauza gongo.

Gongo iwapo itaboreshwa, gharama yake lazima itaongezeka na wanywaji watashindwa kuinunua pombe ya gharama kubwa. Pombe bora zipo lakini hawazinunui kwa sababu ya gharama wanaopt kunywa gongo.

This is to say that wazalishaji wa pombe ya gongo isiyokidhi viwango lazima wataendelea kuwepo. Swali ulilopaswa kujiuliza ni je, polisi wasiwakamate hawa ambao wataendelea kuuza hii pombe isiyokidhi viwango?

Pili, fikiria kwa mapana zaidi. Gongo inasababisha magonjwa ya ini yaani cirhosis pamoja na liver cancer. Economic barden ya kumhudumia mgonjwa mmoja wa kansa ya ini haipungui shilingi milioni tano. Ukijumlisha na indirect barden ya watu wanaomuuguza kushindwa kwenda kazini, watoto wake kushindwa kuconcentrate na masomo kwa sababu baba au mama mgonjwa etc utagundua kuwa mtu anayeshabikia kuruhusu biashara ya gongo ishamiri either ana upeo mdogo au hana nia njema na nchi yetu.

Taarifa nilizopata ni kwamba Slaa alipigwa "kipapai". Lengo lake lilikuwa kuongea kuhusu katiba mpya lakini akajikuta anaongea kuhusu gongo.
 

KIng TAY

Member
Jan 31, 2013
13
0
Miongoni mwa jitihada kubwa zaid zinazofanywa na asasi mbalimbali za kiafya ni upigaji vita wa matumizi ya vilevi hasa unywaji pombe na uvutaji sigara.
Tafiti mbalimbali znaonesha madhara mengi yanayosababishwa na ulevi kuanzia ngazi ya familia, jamii mpaka Taifa. Ulevi umeleta madhara makubwa katika nyanja za kiuchumi,kiafya,nk.
Magonjwa mengi yasiyoambukiza mfano KISUKARI, HIGH BLOOD PRESSURE, OBESITY, CANCERS, ALCOHOL FETAL SYNDROME yameletwa na unywaji wa pombe pamoja na uvutaji sigara.
Pato la mwananchi wa kawaida limezd kudidimia kutokana na utumizi wa pombe, migogoro na utengano katika familia zetu hutokana na ulevi wa pombe ..
Nadhani Dr.Slaa inabidi apitie tafiti mbalimbali ili aweze kujua madhara yatokanayo na pombe katika nyanja za KIUCHUMI, KIAFYA nk..
Siasa nyepesi ni mbaya kama madhara ya pombe kwa mama mjamzito..
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013
2,000
Halafu unaposema kuwa gongo iruhusiwe kwa sababu jamii zote zilianza kwa kuwa na viwango duni unakuwa TOO low. Hiyo ni sawa na kusema watu wawe wanavaa vibwaya mpaka siku watakatengeneza kiwanda chao cha nguo.

Teknolojia ikishagunduliwa ukikataa kuitumia kwa sababu eti wenzako nao walianza chini unakuwa unajichelewesha mwenyewe kuendelea. Unaona Dar es Salaam jiji limejaa magari kibao lakini hakuna hata moja lililobuniwa au kutenenezwa Tanzania. Kwanini kwenye gongo ndio tusisitize kwamba iendelee kunywewa mpaka tutakapobuni njia zetu?

Hivi unajua kwanini wanasayansi wanafanya conferences? Well, lengo kuu ni kupeana uzoefu mbalimbali wa taarifa mpya. Ukishaipata ile taarifa kama wewe ni mtu unayependa maendeleo unaitumia kuboresha viwango vya kazi unazofanya. Sio sahihi kusema utaendelea na njia duni mpaka pale utakapogundua mwenyewe.
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,422
2,000
Ni upuuzi kuhalalisha Gongo....
Ni Ujinga kuchangia hoja kwa jambo usilolijua... kama pombe ni haramu basi zipigwe marufuku zote tu na kama si haramu basi zote ziwe huru ila ziwe katika hali ya usalama zaidi... navyojua kama Pombe unaiweza kuitawala basi si kosa na kama huiwezi basi ni kosa kuitumia
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,422
2,000
Inawezekana Gongo inapendwa kwa sababu ya hali yake ya uchafu na watumiajai wake wengi ni wachafu
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,935
2,000
jadili...

Ifike mahali tuwaze mambo ya msingi zaidi. Kama vinywaji vikali vipo varieties za kutosha kabisa, watanzania hawana shida ya vilevi. Changamoto zinazomkabili Mtanzania, hili la kukosa kilevi cha bei rahisi halipo.
 

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,830
2,000
Umeandika maneno meeeeeeeengi lakini kumbe hata hujui Dr. Slaa alisema nini!

Anza kwanza kusoma alichosema Dr. Slaa halafu kafanye correction ya kile ulichoandika.

Slaa alisema anahalalisha gongo ili wauza gongo wasikamatwe na polisi ambao huchukua rushwa kwa wauza gongo.

Gongo iwapo itaboreshwa, gharama yake lazima itaongezeka na wanywaji watashindwa kuinunua pombe ya gharama kubwa. Pombe bora zipo lakini hawazinunui kwa sababu ya gharama wanaopt kunywa gongo.

This is to say that wazalishaji wa pombe ya gongo isiyokidhi viwango lazima wataendelea kuwepo. Swali ulilopaswa kujiuliza ni je, polisi wasiwakamate hawa ambao wataendelea kuuza hii pombe isiyokidhi viwango?

Pili, fikiria kwa mapana zaidi. Gongo inasababisha magonjwa ya ini yaani cirhosis pamoja na liver cancer. Economic barden ya kumhudumia mgonjwa mmoja wa kansa ya ini haipungui shilingi milioni tano. Ukijumlisha na indirect barden ya watu wanaomuuguza kushindwa kwenda kazini, watoto wake kushindwa kuconcentrate na masomo kwa sababu baba au mama mgonjwa etc utagundua kuwa mtu anayeshabikia kuruhusu biashara ya gongo ishamiri either ana upeo mdogo au hana nia njema na nchi yetu.

Taarifa nilizopata ni kwamba Slaa alipigwa "kipapai". Lengo lake lilikuwa kuongea kuhusu katiba mpya lakini akajikuta anaongea kuhusu gongo.

Mkuu ZeMarcopolo,

All that said and done, suala la msingi hapa ni jinsi gani Dr. Slaa has stimulated my thinking; Swali linalofuatia kwako ni je:
· Kuna haja ya kuhalalisha gongo au hakuna haja?

Binafsi naamini kwamba kuna haja ya kuhalalisha gongo, na nikaenda mbali na kujadili kwanini nafikiri hivyo na nipo katika maandalizo ya sehemu ya pili ya mada yangu. Tumuache Dr. Slaa kwa sasa, badala yake, mimi na wewe tuingie katika mjadala ambao umekuja baada ya Dr. Slaa kusema neno moja tu la msingi kwamba kuna haja ya kuhalalisha gongo, hoja ambayo nimeiendeleza kama ulivyokwisha soma #1 . Nadhani kwa mtindo huo, tutaacha kujadili personality (DR. Slaa) na kujadili ISSUE (whether to legalize or continue to ban Gongo).

Nimejadili kwamba ndio ipo haja, na kwa ufupi (rejea kwa kirefu bandiko namba moja), nimejikita zaidi katika kuchambua juu ya umuhimu wa serikali kuhalalisha gongo kwa manufaa ya uchumi wa mtengenezaji, afya ya mnywaji, pamoja na multiplier effect ya kuhalalisha pombe za namna hii katika uchumi wa taifa, hasa katika nchi ambayo serikali yake inatambua vilezi vingine vya kienyeji kama kama vile mbege, chibuku, chimpumu, lakini vile vile vinywaji vya kigeni ambavyo ni moja ya vyanzo vikuu vya kodi ya serikali. Tanzania ingekuwa ni nchi ambayo imepiga marufuku vilevi vyote kwa mujibu wa sheria, hoja yangu na ile ya Dr. Slaa zingekosa mashiko.

What are your counter arguments katika hili? Kumbuka hata Serikali ya TANU chini ya Nyerere ilifikiria kuhalalisha pombe hii kwa hoja inayofanana sana na ya Dr. Slaa miaka 30 baadae; Kilichoikwamisha TANU ni gharama kwa mnywaji kutokana na regulation and licensing effects on the producer. Kwa vile suala hili ni more socio-economic, huku siasa ikiwa ni daraja tu la kuitekeleza au kutoitekeleza kupitia sera na udhibiti, political spinning haina nafasi hapa, tulijadili bila ya kujali itikadi za vyama.
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,935
2,000
Ni Ujinga kuchangia hoja kwa jambo usilolijua... kama pombe ni haramu basi zipigwe marufuku zote tu na kama si haramu basi zote ziwe huru ila ziwe katika hali ya usalama zaidi... navyojua kama Pombe unaiweza kuitawala basi si kosa na kama huiwezi basi ni kosa kuitumia

Gongo ni Pombe Haramu, serikali ilishafanya utafiti na kujiridhisha kuwa ni hatari kwa Mtanzania kutumia Pombe hii kali inayotengenezwa kienyeji, Serikali kwa kuwapenda wananchi wake ikapiga marufuku kinywaji hiki.
 

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
11,422
2,000
Gongo ni Pombe Haramu, serikali ilishafanya utafiti na kujiridhisha kuwa ni hatari kwa Mtanzania kutumia Pombe hii kali inayotengenezwa kienyeji, Serikali kwa kuwapenda wananchi wake ikapiga marufuku kinywaji hiki.

Imeruhusu pombe zipi ambazo ni Salama? wajua Gongo haina tofauti na Konyagi? na konyagi ukinywa nyingi unakufa! ndio na gongo vile vile nyingi una ndei
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom