Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa sio kosa lake. Uwezo wake wa kufikiri umekuwa wa kiwango cha Josephine Mushumbusi.

Anasema Kikwete haongei na wapinzani wakati Slaa ameonekana mara kadhaa Ikulu akinywa juice. Sasa sijui walikuwa wanakunywa juice kimyakimya!!!

View attachment 105628

Mkuu kamata like zangu
Kama mia hivi...Babu kasahau kuweka akiba ya maneno sasa yamemuishia kawa mropokaji
 
Slaa nae asidandie gari kwa Mbele.Aweke mbele uzalendo,pia afahamu kuwa Rais KIkwete hakutamka nje ya guidance ya sera ya mambo ya nje ya nchi yetu kwa kuwa ameiva ki diplomasia,SLaa si mwana DIplomasia,yeye amekuwa addicted na maandamano.Asubiri karata yake 2015,kuongoza nchi si lelemama.Kwa muda huu ajifunze diplomasia na si against each and every step taken by Mr President.Kwa hili nitamchukia.

Unaifahamu sera ya mambo ya nje ya nchi yetu au unaropoka tu ili kutimiza lengo la kujipatia!kuhalalisha buku saba?
Unamshaurije jirani yako kufanya kile kinachokushinda kufanya ndani ya nyumba yako? Mbona suala dogo tu la Mtwara ametuma batallion ya Jwtz ni kwanini hakwenda kuzungumza na wananchi wa Mtwara? Ushauri wake ulikuwa ni wa kipuuzi ndio maana Rwanda wamemjibu kwa dhihaka na matusi.
 
Kutokana na michango ya wanaJF nimegundua kuwa wengi hawajamuelewa Dk.Slaa.Hii nadhani ni kutokana na kukosa elimu ya falsafa.mtu kama dk.Slaa aliyebobea kwa falsafa unahitaji kutulia ili umuelewe.kwanza dk.Slaa hajaunga mkono matusi ya Kagame.kinachowakasilisha watanzania wengi si kingine zaidi ya kejeli na matusi ya Kagame.
Lakini Slaa hajasema kuwa Kagame alikuwa sahihi kumtusi JK.Tujiulize kama Slaa angesema maneno hayo anayosemekana alitamka na Kagame akiwa hakumtukana JK,je tungekasilishwa na msimamo huu wa Slaa?
 
Hoja ya Dr. Slaa ilikua kwamba Nchi haiwezi kuwa dragged vitani kwa sababu ya kauli ya Kikwete na vile vile akashsuri Kikwete aanze kwanza kukaa na wapinzani wake.

Kweli nimekushusha sana kijana,haya maisha ni mabaya sana ikiwa utaishi kwa kumtegemea mtu,sasa wewe umekuwa kama mtumwa,hupingi chochote toka kwa mabwana zako,hapo nyuma msimamo wako ulikuwa tofauti leo aliekuweka mjini kaenda tofauti umegeuka kweli kinyonga,
Hebu simamam kama kijana mwenye kujitambua,acha siasa za kufuata upepo onyesha kuwa ni mtu uliesimama kwa miguu yako.badilika acha unafiki
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

"Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo," alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE
Nadhani dr. slaa anajua kwamba majeshi ya kagame yaliwafuatilia ntarahamwe huko kongo na kuua laki kadhaa ya raia wa kabila la kihutu wasiokua na hatia yoyote. Pande zote wana mikono iliyojaa damu kwa hiyo kagame asijidai ni msafi. Isitoshe watu karibu milioni 4 raia wa kongo walipoteza maisha kutokana na uvamizi wa kagame kongo. Hakuna damu nzito kuliko nyingine kwa hiyo ushauri wa kuongea watu hawa una mantiki ya kutosha. jk anapaswa kupongezwa badala ya kutukanwa na kagame. Kagame aombe radhi kwa jk, isitoshe ameshusha sana hadhi ya diplomasia ya rwanda. Historia inaonyesha rwanda na tanzania zinapaswa kua na uhusiano mwema wakati wote.
 
Jk anatuabisha tu. Rwanda is just too a small country to argue with. Wote tunaoneka wehu kama wao. what is the difference ?
Mfamaji, as I can see from your statements, I realize that you are very optimistic on the issue. The ability of the country is not judged by her size. Do you remember how Vietnam became a serious threat to US those days? Or can you tell what led to the nuclear bombing of Nagasaki and Hiroshima in Japan those years.

Size doesnt matter, I believe Kagame is well equipped to face Tanzania, that is why he is this much confident that he can hit Kikwete. We should not underestimate the power of any of our enemies when it comes to security issues. By the way, do you know why USA is so hesitant to attack North Korea, despite all her arrogance to USA?
 
Slaa nae asidandie gari kwa Mbele.Aweke mbele uzalendo,pia afahamu kuwa Rais KIkwete hakutamka nje ya guidance ya sera ya mambo ya nje ya nchi yetu kwa kuwa ameiva ki diplomasia,SLaa si mwana DIplomasia,yeye amekuwa addicted na maandamano.Asubiri karata yake 2015,kuongoza nchi si lelemama.Kwa muda huu ajifunze diplomasia na si against each and every step taken by Mr President.Kwa hili nitamchukia.
Kweli dr. unadandia gari kwa mbele. kwa hili kila mtanzania mzalendo hana budi kuwa nyuma ya rais wa jamhuri.
 
mfano wako auendani na mada juu hii, tafuta mwingine, mana JK katoa kauli wakiwa kwenye mkutano kila mtu alikua free kusema. JK ajakosea PK ana matatizo, c angesema tu ckubali ushauri wako basi
 
Kwa hili Babu umepotoka,naona unazeeka vibaya.JK alikuwa sahihi kabisa kusema hilo,Kagame hataki kupambana kwa sababu zake binafsi ni mkweli usiopingika hataki mupinzani nchini kwake ndo maana wapinzani wengi wamefungwa Rwanda na Jenerali Nyamwasa kutaka kuuwwawa na agent wa serikali yake kwa kuanza kumpinga akiwa kama balozi wa nchi ya Rwanda

Serikali ya Tanzania inwapa uhuru nyinyi akina Silaa Uhuru wa kupita kiasi ambao humom kwenu Chadema haupo,nani asiye jua kuwa Kafulila alifukuzwa CDM kwa suala la kuhoji demokrasia,na pia mlitaka kumfukuza ZITO kwa kuwa alitaka kugombea uenyekiti wa CDM

Nini chanzo cha kifo cha Chacha Wangwe ambaye alikuwa amejipanga kugombea uenyekiti wa CDM

Acha hizo,na kwa sasa Tanzania tunahitaji Rais mwenye muono wa mbali kiuchumi na sio mpiga kelele

Naunga mkono hoja.
 
kila siku tuna sema slaa hana uzalendo mnakataa.hawa viongozi wapo kwa ajili ya kutugawa.
sasa majuzi watanzania wote humu jf tulisimama pamoja,kupinga kauli za kagame lakini leo kuna watu wameanza kulegeza sauti eti kisa slaa kaongea.
na anapotugawa inamana anampa nguvu adui.anasahau msemo wa kizaramo genda ubwele.
hata yeye huyo slaa hakutumia busara kumlaumu kikwete wakati hili suala bado ni tete.

Hilo zigo la JK mwenyewe.....yaani nchi iingie vitani kwa ujinga wa raisi!! Mwache akapigane mwenyewe na m.k.e.w.e.!! Mnashabikia vita ya kijinga!!
 
Hoja ya Dr. Slaa ilikua kwamba Nchi haiwezi kuwa dragged vitani kwa sababu ya kauli ya Kikwete na vile vile akashsuri Kikwete aanze kwanza kukaa na wapinzani wake.

Mkuu kikwete katika hotuba yake hakusema kuwa ataingia vitani.. .

Kama kuongea na wapinzani mbona hadi ikulu waliitwa.. ?

Slaa hoja yake hapo ipo wazi.. anapinga ushauri aliotoa jk kwa kagame.. inshort slaa yupo upande wa kagame
 
Slaa nae asidandie gari kwa Mbele.Aweke mbele uzalendo,pia afahamu kuwa Rais KIkwete hakutamka nje ya guidance ya sera ya mambo ya nje ya nchi yetu kwa kuwa ameiva ki diplomasia,SLaa si mwana DIplomasia,yeye amekuwa addicted na maandamano.Asubiri karata yake 2015,kuongoza nchi si lelemama.Kwa muda huu ajifunze diplomasia na si against each and every step taken by Mr President.Kwa hili nitamchukia.
Ulimpenda lini???
 
Dr Slaa Kama kiongozi anahaki ya kutoa maoni hake, sioni wapi issue ya mke wake inaingia hapa, huo ni ushabiki wa kihuni na dalili ya kuishiwa hoja. Issue ya Rwanda na Ntarahamwe ni complicated, kuna kesi za mauji bado zinasikilizwa na baadhi ya viongozi wakuu wa mauji ndiyo pia viongozi wa FDLR na wanatafutwa Kama magaidi, kwa majina Marekani imeweka kitita cha mamiliona ya dola kwa atakayetoa tarifa au kusaidia kukamatwa kwao. Kesi nyingi zimesimama kusikilizwa maana wahusika muhimu waliotoa amri ya kuuwa watu bado wako kwenye kundi la FDLR, hii ni kutoa haki ya utetezi kwa watuhumiwa wa mauji ya 1994. Umoja wa wahanga wa mauaji ya kimbali nao wanafuatilia haki zao kwa ndugu zao walio uliwa ndiyo maana pale Arusha wafiwa na ndugu wa karibu za marehemu walifika kutoa ushahidi. Sometime ushauri mzuri waweza kuonekana mbaya kwa sababu tu haukutolewa mahali sahihi na hii inaeleweka kwa wengi. Imekuwa ni vigumu sana kuendesha kesi za mauwaji hata kwenye mahama zetu, ndiyo maana mtu anayekabiliwa na kosa la kuuwa hapatiwi dhamana. Twaweza kudhani kuwa Rwanda haijafanya jitihada za kumaliza ugomvi wao, ikumbukwe kuwa walianzisha mahakama za kimtaa walizoziita gachacha, hapa msamahama kwa aliye uwa akitubu kosa ni lazima asamehewe. Na baada ya hapo lazima aishi Salama na Ndugu za walio uliwa Ndugu zao! It is not a simple thing. Wengi wanalichukulia tuition la mauwaji Kama ugomvi wa mtu na mke wake au jirani yake. Jiulize mtu akimuua mama yako kwa panga akabaka dada zako na kutwanga mwanao mchanga kwenye kinu na anakataa kukamatwa au kufikishwa mahakamani then jirani yako anakwambia kwanini usikae nae mezani mkayaongea. Naamini Rais kikwete ni mwana diplomasia mkongwe na kiongozi mkubwa afrika, anatabua ukubwa wa tatizo la Rwanda maana alikuwa Waziri wa mambo ya nje baada ya mauji ya kimbali, na migogoro ya maziwa makuu. Mapokeo ya ushauri huo kwa Rwanda alijua hayatakuwa sawa na Uganda for sure. Reaction ya Rwanda tusiidharau lakini hakuna Haja ya Tanzania na Rwanda kupigana vita ingine juu ya hili.
 
Ningejua jinsi yako kama ni ke au me ningejua nikupe tusi gani lakini kwa sasa jichagulie tusi mwenyewe,
unajua nyie warwanda ni watu wajinga sana mlizoe kuingia tanzania na kuishi bila vibari na kufanya uharifu tangu jk kutoa amri msughurikiwe unahaha kama mnataka kutaga,

sasa mwambieni kagame tumewachoka na ujinga wenu pelekeni congo siyo tanzania ushabiki wa kijinga kaa nao kwenu na familia yako jk yuko imara na msimamo wake ni msimamo wa watanzania,koma kabisa .

Acha ujinga wewe!! tukipiga kura leo tunaomuunga KGM Tz tuko wengi mno!!
Go go kagame! chapa hii kitu dhaifu!!
 
Hoja ya Dr. Slaa ilikua kwamba Nchi haiwezi kuwa dragged vitani kwa sababu ya kauli ya Kikwete na vile vile akashsuri Kikwete aanze kwanza kukaa na wapinzani wake.

Dr Slaa as ussual he has once again jumped the gun, what he has said is very un politician. Tanzania has the right to correct the wrongs within the region, either through mediation or advise.

  • Both times when ever in Rwanda or Burundi the Tutsi n Hutu are at their throats trying to destroy each other, Tanzania suffers the most, in terms of law abiding refugees and armed bandits.
  • Our economy goes to shatters due to the influx.
  • Our security is compromised.
  • Land degradation, culture shock, and many other bad elements that destroy our society that is the result of war.
Dr Slaa has failed in this one and has shown political immaturity
 
Unaifahamu sera ya mambo ya nje ya nchi yetu au unaropoka tu ili kutimiza lengo la kujipatia!kuhalalisha buku saba?
Unamshaurije jirani yako kufanya kile kinachokushinda kufanya ndani ya nyumba yako? Mbona suala dogo tu la Mtwara ametuma batallion ya Jwtz ni kwanini hakwenda kuzungumza na wananchi wa Mtwara? Ushauri wake ulikuwa ni wa kipuuzi ndio maana Rwanda wamemjibu kwa dhihaka na matusi.

Sera ya Tanzania ya mambo ya nchi za nje ni oamija na kukuza na kujenga nahusiano mema na majirani.
Pia hatufangamani na uoande wowote. Kufanya nambo ambayo yatasaidia kuimarisha uhusiano kwa maslahi ya nchi zetu.
Rwanda ba Tanzania tupo jtk nahusianio mazuri miaka mingi.
Tumekuwa tukipokea wakimbizi wa rwanda kwa maelfu, tumekywa wapatinishi wa rwanda tangy wkt wa nyerere.
Jk," nilitoa ushauri huo kwa nia njema kabisa kwan naamin kama jambo linaweza kutatulika kwa mazungumzo ya amani basi yafanyike"
Mwita , Mtwara sio kundi la Waasi ndio maana viingozi waandamizi wanaenda mtwara.
 
JK alikuwa sahihi kabisa kutoa ushauri wake,sidhani kama ni sahihi muda wote kutoa ushauri wa kinafiki kama wanaotaka akina Silaa,

Kigoma na Ngara zimekuwa jangwa kwa kupokea wakimbizi ambao wameongeza janga lingine la kuzagaa kwa silaha haramu nchini kwetu

Dr Silaa si kila jambo analofanya Rais lazima wewe ulizungumzie,inaonyesha ni jinsi gani usivyona subira,Mbowe kuitwa Ikulu ugeni wa Obama haikukufurahisha, mimi nadhani ukiwa na uchungu na nchi yako lazima likija jambo la vitisho kuhusu nchi yako liachie wenyewe walinzi wa mipaka JWTZ na Amiri jeshi walizungumze

Au unataka Kagame akusaidie kuingia Magogoni kwa Mtutu baada ya kuona unaangukia pua na kujitahidi kupenyenyeza uongo ili nchi isitawalike

Unalo,na kwa taarifa yako kwenye kula za maoni utaangukia pua 2015,
 
when discussing nation issues political indiferences should not be considered we are all Tanzanians and we are indeed indebted to our national security that is our privilege and not others, what kikwete adviced Kagame and his collegue war-marker Mseveni is true and true only
Kikwete should not be blaimed because always refugees from those countries are trouble marker into our nation.
owing also to internatinal comity we are oblied to pay them residence otherwise it could mean crimes agaist humanity
my concern here is that when it comes to international commitment we must stand as one and show our enemy that we are strong to combat whatever comes negatively into our land otherwise division would mean weaknesses and pay way to them for our destruction.
Dar slaa as a very prominent one in our nation must yes, collect Kikwete but in very joining company rather than being negative to stress where kikwete forgot hence to make the statement clear, that tanzania is strong Rwanda should stop facilitating lebels in neighboring states for for good habitability of great lakes inhabitants.
 
Back
Top Bottom