Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

mbona baba wa taifa alizika hoja ya g55 ya serikali tatu na leo imeibuliwa na chadema na inashika nafasi?
ni suala la muda tu. kama mmeshindwa kuwapiga basi ungana nao mjenge rwanda.
jk is right at the moment and slaa will ve right if time persist.
Huku ni kufanya siasa mkuu swala la serikali tatu limeletwa na tume wewe unatwambia chadema haya mkuu,lakini hili la tamko la slaa ni kukosa uzalendo kupindukia rais alishatamka na ukawa ni msimamo wa taifa zima yeye slaa anatuletea nini hiki.
 
## Ur sick of unknown infections... ww una viroja* huna hoja* kuhusu hili....shukuru Mungu CDM gave u job... utamlamba Slaa hata masab..rii....

== Kwa hili Slaa ni KIHIYO, HOVYO, BURE like his hawara Josephine.... huwezi ona au sikia wazi wazi Rais anatukanwa na Nyani toka nje ... na nyie MNAKENUA TU... na I heartly & physically embarassed & touched with Slaa na Kagame anayemsapoti....basi Slaa aende Rwanda anafanya nn hapa..??

Hasira zako haziwezi kuzuia tusitoe mawazo yetu. Sijui huko wapi na unafanya nini lakini unaproke vita with no justfiable reasons. Matusi yaliyotelewa na Mohamund wa Iraki na Chaves wa Venuzuela dhidi ya Rais wa Marekani wamarekani wangelikuwa wameingia vitani nao miaka mingi.
 
By RUTASHUBANYUMA: Vita vya maneno kati ya JK na Kagame vinaasharia jinsi ambavyo Kagame haoni kama JK ana ushawishi au hata ufahamu wa historia ya Rwanda na hivyo kumkejeli jinsi ambavyo anaona inafaa. Kagame ameahidi kumvutia pumzi JK na akipata mwanya atamzabua kofi kutokana na JK kumshauri Kagame kukaa mezani na waasi wa Rwanda.

Kagame ni vigumu kuthamini ushauri wa JK kwa sababu zifuatazo:-

1) JK haifahamu vizuri historia ya Rwanda ambayo imejengwa kwa damu. Watutsi ambao ni wachache wametumia damu kuwatawala wahutu ambao ni wengi na jinsi ya kuwawezesha wengi (Wahutu) bila kuathiri haki za wachache (Watutsi) ndani ya Rwanda imeshindikana hadi leo.
Mfupa uliomshinda Mzee fisi je JK atauweza kwa utendaji huu tunaoufahamu hapa nchini?


a) JK kushauri mahasimu hao wakae meza moja bila ya kujua ajenda na mikakati ya kufanikisha vikao tajwa kwa Kagame anaona ni upuuzi ambao mjenga hoja -JK- lazima azabuliwe kofi ili aache kujiingiza kwenye mambo yasiyomhusu.

b) JK katika masuala ya Muungano na kero zake amekuwa akiendelea kutegemea kamati ya viongozi wa kitaifa watokanao na chama chake cha CCM tu bila ya kutafuta wapinzani katika kushauriana nao. Hivyo aidha ni unafiki au usahaulifu tu kumshauri Kagame afanya yale ambayo yeye mwenyewe JK hana mpango wa kuyafanya.
Charity always begin at home.................

c) JK katika uundaji wa kamati ya marekebisho ya katiba katumia ubabe wa uwingi wa wabunge wa CCM Bungeni katika kupitisha sheria ambayo imempa yeye madaraka ya kurekebisha Katiba atakavyoona inafaa na ushirikishwaji wa wananchi ni changa la macho tu. Sasa yawaje amshauri Kagame kujenga mazingira ya ushirikishwaji wa mahasimu wake jambo ambalo yeye mwenyewe JK hayuko tayari kulifanya. Tena hapa nchini ingelikuwa ni rahisi zaidi kwa JK kwani hakuna umwagaji wa damu katika wananchi kudai haki zao za kimsingi zaidi ya ukatili wa polisi ambao anayo mamlaka ya kuwakemea na wala hana mpango wa kufanya hivyo..

d) Katika kero za Muungano, JK aliwahi kudiriki kusema kamati ya kushughulikia kero tajwa na kuundwa na chama kimoja tu cha CCM wawe wanakutana angalau mara nne kwa mwaka hata kama hawana la kujadili ikimaanisha tu yeye JK anacheza mchezo wa siasa wa kuonyesha raia kazi inafanyika hata kama hakuna linaloendelea! Mbali ya hilo, JK hana mkakati wa kuzimaliza kero za Muungano nje ya CCM na ndiyo maana hawezi kufiria muundo mbadala wa kutafuta ufumbuzi wa kero za muungano nje ya chama chake sasa iwaje amtarajie Kagame atafute ufumbuzi wa kero za Rwanda nje ya chama chake cha RPF?

e)
JK hana taswira ya kuutetea na kulinda utawala bora na ndiyo maana katika kipindi chake mauaji yanayofanywa na polisi hadi leo yanazidi yale yaliyofanywa na maraisi wote waliomtangulia. Pia, katika historia ya nchi yetu kamwe Waziri Mkuu hajawahi kutamka hadharani kuwa ni sahihi kwa polisi kupiga raia wanaodai haki zao. Hadi wa leo, JK yuko kimya na wala hajamchukulia Pinda hatua yoyote ile ikiashiria anaafiki udhulumaji wa haki za kimsingi kabisa za binadamu! Hivi kwa kisa kipi Kagame amsikilize JK ambaye hana rekodi yoyote ile ya kuheshimu utawala bora?

2)
Chaguzi ya Uraisi 2010 kuna utata mkubwa kati yake na Dr. Slaa ni nani alishinda Uraisi kutokana na Tume ya uchaguzi kufanya kazi kwa minajili ya kulinda masilahi ya CCM huku ikishirikiana na Idara ya Usalama pamoja na serikali za mitaa. Kagame pamoja na faulo zake kibao, hakuna anayemtilia mashaka ya uhalali wa chaguzi zote zilizomsimika madarakani. Kwenye mazingira ya namna hii, ni JK au Kagame ambaye anastahili kuwekwa darasani na mwenzie juu ya utawala bora?

3) Viongozi wengi wa TZ hususani CCM hukimbilia kutatua matatizo ya nje ya chi yetu na kutumia sarakasi hizo kufunika matatizo ya hapa nchini lakini wasichojua ni kuwa ili waheshimike ndani na nje ya mipaka ya nchi hii ni pale watakapoanza kutatua kwa dhati matatizo ya hapa ndani na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu bila ya kujali masilahi ya muda mfupi ya vyama vyao.

4) Kwa karata hizi ni dhahiri Kagame yuko sahihi kabisa kumbeza JK kwa kumtishia na kunuia kumzabua kofi kwa kile ambacho ni
"kiherehere" cha JK kujiingiza katika tanuru la moto la wengine wakati hapa nyumbani moshi unafukuta kila mahali na JK haonyeshi hata dalili kujua majibu ya kero zetu yako katika nyanja ipi.
 
Hivi historia ya Kikwete na Kagame inaeleweka vizuri??Hawa jamaa hawana issue nyingine baina yao ambayo labda sisi wengine hatuijui?

Inawezekana wana ugomvi wao mwinngine wa siku nyingi?Kushauri kuongea na waasi ndio iwe sababu ya haya ypte?Fanyeni uchunguzi hapa si bure!
 
Sawa kabisa mkuu umenena mimi nimemfuatilia sana Ben Saanane kuhusu hii issue ya Kagame na Kikwete.

Mwanzo alikuwa ana msapoti sana Kikwete sasa hivi kaja na lugha nyingine lakini mimi hanisumbui nishamuelewa

yeye ni "double face" kaja mkuu wake wa kazi kabadilika ninacho mshauri awe na mawazo huru upinzani sio kupinga

kila kitu ni hayo tu.

Waalimu wako walipata kazi sana shuleni.Onyesha ni wapi nilikobadili msimamo.Myopic...!
 
Wanasiasa kama slaa wanatakiwa maombi rasmi sasa kunamzee mmoja naye kila siku analalamika bila kutoa suruhu hawa watu ni hatari sana ni wanafiki wazuri tu.
 
Khaa!!! Ninamuheshimu Dr. Slaa, lakini kama kumkosoa JK ni kama hapa kwenye red na blue basi safari yetu hadi tufikie demokrasia ya kweli bado ndefu sana. Sidhani kama ni sahihi kwa kuwa ni chama upinzani basi maana yake kupinga kila jambo linalofanywa na serikali iliyopo madarakani. Ndiyo maana wakati mwingine tunakuwa tunalalamikia mambo mengine yasio ya msingi ilimradi tuwe tunapingana na serikali. Kwa akili yangu ndogo sana nadhani si sahihi. Nadhani si vyema kuwa na mawazo ya kupinga kila jambo eti tu kwa sababu ni wapinzani. :bored:

Tatizo mnataka tukubaliane na nyinyi kwa kila kitu,Mbona CCM hamko tayari kuyasikiliza malalamiko ya Wapinzani ila tu pale mnapoelemewa na tatizo ndipo mnapowakumbuka Wapinzani kama Watanzania wenzenu?
 
huyu mzee ni pimbi.
hivi kweli cdm imekosa washauri wa kumshauri huyu babu.
hivi kweli chama makini kinaweza kuwa na katibu kama huyu.
nimegundua pesa za msaada wa siri zinatoka kwa wale jamaa wenye hiyo nembo.na lengo lake ni kunywa damu.
sasa tutakufungasha wewe na kagame wako kama utaendelea na ujinga.
we unafurahia wanajeshi wetu wanavyo uwawa darfur na watu wasio julikana.wewe una ajenda binafsi.
 
Huwezi kutenganisha HELLEN KIJO BISIMBA na RWANDA na Vile vile huwezi kutenganisha huyu mama na SLAA , kwa hiyo siwezi kushangaa anamkosoa JK

Hellen Kijo Bisimba ni sawa na mama yako mzazi. Uwe na adabu unapo mjadili. Mbona mama yako mzazi hana tofauti na Bi Chau na hatusemi?
 
Huku ni kufanya siasa mkuu swala la serikali tatu limeletwa na tume wewe unatwambia chadema haya mkuu,lakini hili la tamko la slaa ni kukosa uzalendo kupindukia rais alishatamka na ukawa ni msimamo wa taifa zima yeye slaa anatuletea nini hiki.

uncle deo ww na mm tunakiri limeletwa na tume lakini tume imepata maoni toka kwa wa tz.
chadema tunasema hoja ya serikali 3 ni yetu.
kama hujawasikua top leaders wetu n bahati mbaya sana.
yote kwa yote kila jambo jema lina wakati wake.
dr kumkosoa jk n mtazamo wake awe amekosea au yuko sahiihi yy n mtu mzima atapima reactions za watu humu.
atabaki bro ben na wengine ambao kwao zidumu fikra za dr ndio msimamo wao.
 
Hizi siasa tu, hakuna lolote. Yaani siasa za bongo kwa watu kama kina slaa ni kupingana na serikali kwa kila jambo!!!!!
 
Boko haramu wangekuja bongo ningefurahii saaaaannnnaaaaaa
 
Hapo Katibu Mkuu anatia aibu kama kweli kasema maneno hayo, hata Zitto recently akichangia kwenye mjadala huu katika twitter aliweza kusema kiukweli kuwa sio FDLR wote walihusika na genocide, wapo waliozaliwa ukimbizini na wapo ambao wakati huo 1994 walikuwa watoto wadogo lakini kwa sasa wanakuwa forced na reality kushika silaha...! Pia sio wote katika FDLR ni FOCA
mi nakumbuka kipindi hicho mambo yalikua shwari na wala hakukua na genocide.Habyarimana alikua amekuja dar,kwaajili ya kufanya mazungumzo na waasi wa rwanda wa kikundi cha RPF kama sikosei.kisha asubuhi moja nasikia habari ya kutunguliwa kwa ndege ilikua imembeba rais wa rwanda na wa burundi kipindi wanatokea dar kwenye mazungumzo.

Kumbe watusi waliamua kumuua habyarimana rais mhutu.
Genocide iliyofuata ni reaction ya wahutu baada ya kuuliwa habyarimana,na kumbe kina kagame waliplan,baada ya kumuua habyarimana wakasonga mbele na kunyakua madaraka kwa nguvu.
Kwahiyo kagame ndo mhusika mkuu wa kilichotokea.
 
Tatizo mnataka tukubaliane na nyinyi kwa kila kitu,Mbona CCM hamko tayari kuyasikiliza malalamiko ya Wapinzani ila tu pale mnapoelemewa na tatizo ndipo mnapowakumbuka Wapinzani kama Watanzania wenzenu?

kadhia ya kigali sio ya ccm wala kikwete.ni la watanzania wote
 
Kwa vyovyote ule ulikuwa ushauri, nae Kagame alikuwa na haki ya kuudharau kama rais nae alivyodharau ushauri wa kumuwajibisha kamanda aliesababisha mauaji ya Mwagosi (RIP). Tatizo liliopo kwa sasa ni ujuwaji wa kagame na matusi kwa watanzania na kwa rais wake, hili halikubaliki kabisa. Ushauri pokea au kata, huwezi kulazimisha ushauri utakaoupenda. Sioni tafauti ya kuwaita awapatanishe na ile kuwaambia wakae wazungumze, kwa kagame na attitude yake against ushauri wowote wa kutafuta suluhisho la kudumu usingezuia aggressive behaviour yake kwa wataomshauri. Yeye mwenyewe binfasi ni miongoni mwa watuhumiwa according to evidence zilizopo. jengine la kusema Kikwete hakutani na wapinzani ni political immaturity, tumeona jopo Zima la chadema lilipokutana na rais kuhusu mchakato wa katiba na kuyasikiliza matashi yao, tumeona juzi pia kakutana na mwenyekiti wa CUF, huwezi kumlinganisha na Kagame asietaka hata kukaa nao pamoja akaweka foundation ya kudumu. Taliban hivi sasa wanazungumza na US kutafuta suluhisho itakuwa hawa ndugu? Si mpenzi wa Kikwete na serikali yake, lakini ningelipendelea kuwe ukweli katika matamshi ya viongozi sio propaganda na political opportunism.
 
AHAAAA hapo mkuu ndiyo hasa nilikuwa namaanisha yaani mtelezo kwa mtelezo sasa sijui nani atamtelezea mwenzake, msimamo umeshatoka wa nchi na raisi alisema hayo mbele ya hadhara ya waheshimiwa , kingine ambacho ni ziada ya hili ni kuwa usije ukakuta muheshimiwa ana ajenda na mataifa mengine kwa rwanda. nalisema hili nikiwa na hoja moja kagame tangu siku nyingi alikataa kuwa pamoja na hao FDRL ki masikilizano na baadhi ya mataifa yalimuunga mkono akiwamo baba wa taifa , iweje leo mtu anafufua kitu kilichozikwa siku nyingi , hapo ndipo naanza kuikubali hoja ya dr.slaa kwa upande mwingine utofauti wa kikwete na kagame usije kutuingiza katika vita. lakini kama nchi tuwe wamoja kwa hili

Mkuu nikueleweshe tu kuwa taarifa zilizopo kwenye publica domain sasa kuhusu mauaji ya Rwanda ni tofauti ya zile zilizokuwepo wakati ule wa 1990s. Mengi yaliyokuwa yamefichwa sasa yako wazi, hata Gen. Romeo aliyekuwa kamanda wa UNAMIR amekiri kwenye speech zake na kitabu chake kuwa alikuwa 'fooled' na propaganda za RPF, lakini amekuja ku-realize nao ni wauaji tu. FDLR-FOCA ilianzishwa 2000, ingawaje wapiganaji wake wengine walikuwa ni ex-FAR.

Baada ya genocide ya Rwanda, pia kwa kutumia taarifa ambazo ni biased, Kagame alijinufaisha na genocide kupata misaada na kutumia kama fimbo kuwanyamazisha wapinzani wake nje na ndani ya Rwanda. Alipoingia Congo kwenye vita ya kumtoa Mobutu, Tanzania pia tulihusika, lakini baada ya Kabila kuwa madarakani ilidhirika kuwa dhamira ya Rwanda ni tafauti. Ukumbuke kuwa wanajeshi wa Tanzania walikuwa Congo ili kufundisha jeshi jipya la taifa hilo (hii haikuwa ishara nzuri kwa Rwanda, kwa vile walitaka waache wanajeshi wao wabaki Congo kwa wingi kwa vile uchumi wao haukuweza kubeba gharama zao). Kwa mara ya kwanza hapo, Tanzania na Rwanda zilipishana misimamo. Pili wahutu wengi sana waliuawa kwa kisingizio cha kuwatafuta ex-FAR.

Baada ya Kabila kutoa tamko la kufukuza wanyarwanda wote jeshini (hii ilitokea wiki chache tangu Tanzania kuondoa wanajeshi wake Congo, kwa vile inteligencia ilionesha hali kuwa sio shwari, upepo mbaya ulikuwa ukivuma ndani ya jeshi la Congo). Kilichofuatia unakijua, ambapo ni kufukuzwa kwa kina James Kaberebe na akina Bizima Karaha. Kabarebe akamkalia kooni Kagame ili wampindue Kabila, lakini Kabila akatumia utu uzima kutafuta marafiki wapya ikiwemo ex-FAR, na makundi mengine ikiweo ALiR I na ALiR II ili kupigana na Rwanda. Njama za Rwanda zikashindwa ingawaje wakafanikiwa kumuua Kabila binafsi. Tanzania haikuunga mkono jambo hilo.

Mambo mengi hayo yako kwenye public domain, labda nije direct kwenye swali lako. Ni kuwa mtizamo wa amani mashariki ya Congo umebadilika, ndio maana nchi za maziwa makuu, AU pamoja na SADC wamesema sasa basi. Jaribu kufikiri, ikiwa FDLR ingekuwa na shida na ukweli ungekuwa wazi kwanini UN Intervention Brigade kwenye mandate yao wasiambiwe wa-deal na FDLR badala yake M23 ndio wametajwa wakati wengine wamekuwa mentioned in general?
 
Dah! apa Dr Slaa full kutokota! lazima ajue AU marais walienda kufanya nini ? nasidhani km walienda kunong'oneana hapana nikuongea na kushauri...Pili Dr Slaa nadhani hana huelewa na mahakama za GACHACHA nini kazi yake? Kazi kuu ya gachacha ni kusuluhisha na kupatanisha kati ya wahutu na watusi ata km waliua baba au mama yako mbele ya macho yako mnatakiwa kusamehana na kuanza maisha mapya thats all Je uko sio KIKWETE anachomaanisha? Pia lazima Uelewa hawa wanazid kuzaliana na vita haitaisha
 
Waalimu wako walipata kazi sana shuleni.Onyesha ni wapi nilikobadili msimamo.Myopic...!

Bro Ben, " simkubali kikwete na serikali yake lakini kwa hili la kagame namuunga mkono nakubaliana na kauli yake"
Sasa baba kesha onyesha msimamo tofauti unategemea mtoto atafanyaje"
 
mbona baba wa taifa alizika hoja ya g55 ya serikali tatu na leo imeibuliwa na chadema na inashika nafasi?
ni suala la muda tu. kama mmeshindwa kuwapiga basi ungana nao mjenge rwanda.
jk is right at the moment and slaa will ve right if time persist.
may be let's wait and see
 
umechemka mkuu hata kama ugonvi mkubwa kiasi gani mazunguzo ndio msingi wa kuleta amani,na kikwete alishauri tu kama hawakutaka ushauri wake basi wangekaa kimya sio kukmtukana rais wetu, wewe huwa hutoi ushauri hata kwa ndugu zako?wakikitukana utafurahi? niko pamoja na kikwete
 
Back
Top Bottom