Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Kama vp mkuu ? maana jambo ambalo litamstaajabisha Mungu halafu binadamu tukaliona la kawaida...
labda tufafanulie..

We hujui Slaa alikula viapo gani mbele ya Mungu halafu akamsaliti LIVE? Tena bila kuona aibu!
 
​siamini kama Slaa anaweza kuongea hii kitu

kila siku tuna sema slaa hana uzalendo mnakataa.hawa viongozi wapo kwa ajili ya kutugawa.
sasa majuzi watanzania wote humu jf tulisimama pamoja,kupinga kauli za kagame lakini leo kuna watu wameanza kulegeza sauti eti kisa slaa kaongea.
na anapotugawa inamana anampa nguvu adui.anasahau msemo wa kizaramo genda ubwele.
hata yeye huyo slaa hakutumia busara kumlaumu kikwete wakati hili suala bado ni tete.
 
Slaa na yeye naona umri unakwenda sasa maana muda mwingine kauli anazozitoa utata mtupu.
 
Kwa nini kikwete asingemwambia privately Paul kagame...au anafikiri kagame hajui kutatua migogoro kwa njia ya amani? Kagame alimuona Jk kama anamfanyia dharau,that is why alimaua kuporomosha matusi.
 
Nadhani Dr. Slaa hapa kakurupuka naye anasema mbona yeye kashindwa kushughulikia mambo yake ya ndani?? Mimi kwa uelewa wangu hii aimzuii kuongelea amani ya east afrika...mimi nadhani si kila kitu tupinge usalama wa east afrika una maana usalama wa tanzania...

J.K alikua sawa tu mtutu ukishindikana haina budi kurudi mezani.

I stand to be corrected

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

kakurupuka kabisaa, mbona yeye dr ameshindwa kumaliza ya ndani ya chama chake na familia yake lkn amamtaka jk amalize ya tz na wapinzani
 
Kwa nini kikwete asingemwambia privately Paul kagame...au anafikiri kagame hajui kutatua migogoro kwa njia ya amani? Kagame alimuona Jk kama anamfanyia dharau,that is why alimaua kuporomosha matusi.

Kwhaiyo mkutano uliitishwa kwa ajili ya nini?
 
Hapo Katibu Mkuu anatia aibu kama kweli kasema maneno hayo, hata Zitto recently akichangia kwenye mjadala huu katika twitter aliweza kusema kiukweli kuwa sio FDLR wote walihusika na genocide, wapo waliozaliwa ukimbizini na wapo ambao wakati huo 1994 walikuwa watoto wadogo lakini kwa sasa wanakuwa forced na reality kushika silaha...! Pia sio wote katika FDLR ni FOCA
point said so kikwete was right , majitu mengine bwana unaichukulia hoja kijuu juu tu kama kuku anataka kutaga , basi na slaa angeenda kumshauri kikwete kabla ya kusema ili atuambie alivyomshauri
 
Nyerere alifanya kazi katika wakati mgumu zaidi maana kuzima upinzani kulizalisha silent rebellion na ni hatari zaidi.Kumbuka utekelezaji wa azimio la Arusha lililoambatana na displacement ya watu lilitengeneza hasira ya kitaasisi na kabla ya hapo tayari Nyerere alishakumbana na Uasi takribani miaka 10 nyuma huku akina Kambona wakiwa exile kama potential threats(Ingawa hoja ya kuwa kama Kambona alikua Hero au Villain ni subject of debate).Upinzani uliopo unatambulika kisheria na kitaasisi na ni rahisi kufanya dialogue au compromise on issues.JK yupo kwenye wakati mzuri zaidi wa kufanya dialogue na wapinzani wanaotambulika kitaasisi kuliko Nyerere ambaye muda wote alikua alert but still he managed to cooordinate the forces against common enemy!Unasemaje hapo?

Nyerere alichafanya ni kila aliyemuona tishio kisiasa, "he was either liquidated or exiled". Baada ya hapo ilikuwa haiwezekani ku-organise uasi dhidi ya nyerere kwa sababu kuanzia padri, shehe, mwalimu mkuu mpaka daktari wa muhimbili alikuwa ni askari kanzu wa nyerere. Na hii ndiyo maana ya "authoritarian government". Nyerere hakufanya maamuzi kwa kuwashinda watu kwa hoja kwa sababu wenye hoja m-badala walikufa au walifukuzwa. Na kila mtanzania wa kawaida aliyekuwa na mawazo tofauti aliogopa kuyasema mawazo yake. Na ndiyo maana Nyerere aliwahi kuitwa "haambiliki".
Kuhusu JK kukutana na wapinzani, anafanya hivyo na kuna ushahidi wa hilo. Tatizo ni kwamba wapinzani wakishakutana na JK wanataka JK afanye wanayoyataka wapinzani. Kama yana maslahi kwa taifa JK anatakiwa afuate mawazo ya wapinzani. Na kama yana maslahi kwa chama fulani, JK anayo haki ya kuyakataa mapendekezo ya wapinzani.

Sasa nakuuliza wewe Ben Saanane: nini mtazamo wako binafsi kuhusu huu mgogoro wa Tanzania na Rwanda? na jee mtazamo umebadilika kutokana na kauli ya Dr. Slaa? au umebaki ule ule wa awali.
 
You should tackle first thing first!.
Even if the outside influence might cause more damage to an already existing problems, isn't that the same as mopping the rain that comes from the roof leakage; which is the real problem in the long between the two?
 
Kinadharia ushauri wa Kikwete unaweza kuonekana kama mzuri lakini haukuwa na action plan au road map ya utekelezaji kushauri bila action plan ni sawa na kuropoka hasa unapomshauri mkuu wa nchi nyingine.

Kama Kikwete ataanzisha vita na Kagame binafsi nitakuwa wa mwisho kwenda vitani, kwa sababu naamini Kikwete hakuwa sahihi kuwaambia Rwanda wakutane na waasi alichotakiwa ni ku-mediate mkutano kwa kuwakutanisha mahasimu na sio kuwaambia wakutane, kwanza wakutane wapi na nani awe mlalamikaji na mlalamikiwa.

Utawakutanishaje ikiwa upande mmoja haujakubali kuzungumza? Alichokifanya JK ni kutaka upande huo ulegeze msimamo wake ili wakubali kuongea na maasimu wao. Na kwa tabia ya PK huwezi kulifanya hili kwa usiri unamwambia sehemu ambayo atajua kuwa kila mtu amesikia ushahuri huo.
 
Kwa nini kikwete asingemwambia privately Paul kagame...au anafikiri kagame hajui kutatua migogoro kwa njia ya amani? Kagame alimuona Jk kama anamfanyia dharau,that is why alimaua kuporomosha matusi.

mbona slaa hakumshauri kikwete privately.yeye haoni kwamba anahatarisha msimamo wa taifa.
au ndio kakosa la kuongea.
sio kila mgogolo ndio ufanye ngazi ya kupandia kisiasa. huo ndio upimbi.
 
===>> Heee... I can't imagine ...Dr. Slaa as of this moment, day... to me ur USELESS, Mnafiki mkubwa.. hufai hata kuwa kiongozi of which anyway u hv never been... hujui UTAIFA NI NN...uko just to score political cheap popularity...

==> Slaa uliondoe BORITI kwanza ktk jicho lako ndipo uliondoe jicho la mwezio... kweli nyani ni nyani....hee...huyu ndio Slaa au..??

===>> Ntakudharau na kukuona mjinga sana kwa hili na nimejua ur inner most part.... poor Slaa...

===>> Kumbe ww Slaa wajiona UNAFAA SANA..MWEMA SANA...BORA SANA...WAJUA SANA...HODARI SANA... UNAJIDAI UNAFANYA RESEARCH B4 U SPEAK.... I*m rounding u to ZERO...0 KABISA... I will be against u to death for all in all...

===>> hv unaumwa nn Slaa..!!?? Rais wa nchi YAKO ANATUKANWA....ANATISHIWA NA MUUAJI KAGAME TENA PUBLICLY UNATHUBUTU TO OPEN UR DIRTY MOUTH NA KUSEMA JK KAKOSEA KUWAPA USHAURI....JUST A PIECE OF AN ADVICE... ww ushindwe kuweka utaifa mbele unaleta HYPOCRICY MBELE....

==>> Hapa umechemsha kupindukia...na utafeli ushangae.... sikukudhania uko hovyo hivyo Slaa...

===>> ooohh God... I knew Upadri hujakushindwa bure.... ni Mipango ya Mungu...alikujua....

===>> Narudia Watz wazalendo wanaojua kupima mambo kwa kina TUTAKUDHARAU UTASHANGAA...

===>> Hv ww Slaa ww JK kwako hafanyi jema hata moja....ukome..uchu wa madaraka utakumaliza.... unapenda sana sifa ww...

===>> I dought perhaps ur thinking & reasoning capacity has gone with age....


===>> I*m against u Slaa... to me ur a failure to hell....

ww si Mzalendo hata tone.... Aisee... ptuuuu....!!!
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE


Sidhani kama hiyo kauli ha[o kwenye RED imetoka kwa Dr Slaa, kama ndivyo basi mzee wetu anazeeka vibaya. Hivi repercussion ya kauli hiyo si ndiyo ingekuwa mara mbili zaidi ya hii ya kuwataka wao wenyewe wapatane? Umwambie Kagame njoo Tanzania nikupatanishe na FDLR atakuelewa kweli???
 
point said so kikwete was right , majitu mengine bwana unaichukulia hoja kijuu juu tu kama kuku anataka kutaga , basi na slaa angeenda kumshauri kikwete kabla ya kusema ili atuambie alivyomshauri

Of course, ni kuwa Dr. Slaa kama amesema hayo nae pia kateleza......! Hili suala kwa kweli sio la Kikwete ni la Tanzania na huo ndio msimamo wa nchi yetu, msimamo usio na kificho
 
Ni kweli! huwezi kuongea na wauaji mkiwa wawili..kinachotakiwa ni kupatanishwa..Ingawa siungi mkono matusi ya Kagame!
 
ila naye Slaa sasa naona ameshaanza kuzeeeka awachie sasa wengineyaani siasa zetu za ndani utafananishaje na RwANDA pLS Dr sio Kila kitu Lazima Ukiongelee mambo engine Yaache Yapite Na huko unakoenda nahis utahariaribbisa Yanii nahis hata motto mdogo atakushinda coz mtu unapotoa ushauri si lazima mtu aupokeee sasa na wewe mzee upeo nahisi kadri siku zinavyokwenda unapungua pls pls Dr Usikurupuke
 
UNAFIKI mbaya jamani.

Huyu mzee uroho wa pesa na madaraka unampeleka kubaya sana kiasi kwamba anawalaghai wafuasi wa chadema waache kuomba Mungu!

Huyu ndio anasema Kikwete haongei na wapinzani?!!!

View attachment 105632[/QUOTES
SLAA kwa hili amenikera mnoo,inaelekea ameropoka hapa,kwani ukiwa mpinzani kila kitu ndio uwe unapinga tu,watu wana uelewa sana siku hizi,hatutaki kudanganywa kipuuzipuuzi,tunataka ujipange kwa sera zako,SASA NAANZA KUFIKIRIA KUCHANGANYA AKILI ZA MBAYUWAYU NA ZANGU MWENYEWE ILI NIFANYE UAMUZI SAHIHI,MAANA NIKIMTEGEMEA MBAYUWAYU MOJA KWA MOJA AHADI ZAKE SI ZA KWELI ATANITUMBUKIZA MTONI
 
Kwani dk slaa kwa madhambi yote aliyonayo naye anamkosoa mtu,yeye kama kagame ni ngugu yake aende akaishi naye.
 
Back
Top Bottom