Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

1. Nakubaliana na hoja yako ya kwanza kwamba kushinda vita kunahitaji umoja wa kitaifa.
2. Kuhusu nyerere na ushawishi wa ndani; tukumbuke kwamba wakati wa nyerere hakukuwa na chadema wala CUF. Fikra za nyerere zilikuwa ni "fikra sahihi" kwa hiyo hakuhitaji kumshawishi mtu yoyote kwenda vitani. Alichofanya ni kutoa amri tuu na amri ikatekelezwa. JK anafanya kazi katika mazingira tofauti na yale ya JKN. Miongoni mwa wapinzani kuna wazalendo na pia kuna "unscrupulous, machiavellian, opportunist characters ". Hili kundi la pili ndilo kundi la hatari sana kwa taifa letu. Wasi wasi wangu ni kwamba Slaa yuko kwenye hili kundi la pili, na kama haya yaliyoandikwa humu ni maoni yake kweli; basi chadema wana kila sababu ya kuutazama upya uongozi wao kama kweli wanajali maslahi ya taifa letu.

Hakuna maslahi yoyote tutakayoyapata huko Congo hapa kuna jambo zito limejificha hasa Marekani anapojihusisha na huu mgogoro.Akina JK wameshaahidiwa pepo tayari.Huu ni mgogoro wa kimaslahi.
 
You should tackle first thing first!.

Huku ndio kunaitwa kupamba maandishi tu, kama kasema hivyo kweli anaji expose tu as vuvuzela. Ina maana Dr.Slaa aliomba kazi kwa watanzania ya kuwaongoza bila ya kujua job description, can we really afford another learn as you go leader in our politics.

Kuna wakati inabidi ajue the meaning of national interest politics na si kila kitu kupinga tu kama mwanasiasa mwenye kiwewe. Naanza kuichukulia kwa umakini sana kauli ya mchungaji Mtikila ya kuwa Kagame katupandikizia wanyarandwa tayari, na huko ndani ya CDM naona waanze mchakato wa kuangalia historia za watu wanaowapa nafasi za kutoa ushauri kwa viongozi wajuu.

Maana with Slaa and Mbowe both without clear national visions and already are willing to take advise from members in the social media. What it shows there are not many brains in that party, no wonder majimbo, majimbo my foot.
 
Kushinda vita kunahitaji umoja wa kitaifa.Uzalendo ni kigezo kimojawapo katika sababu za kushinda au kushindwa.Kiongozi mkuu wa Nchi ni lazima aunganishe taifa dhidi ya common enemy ambaye ni adui wa nje.Wahenga walisema kamba hukatika......!

Uongozi wa JK na brutality dhidi ya wapinzani wa serikali yake unaliweka taifa katika precarious situation.Nyerere alishinda vita ya Kagera kutokana na ushawishi wa ndani.Rais anatakiwa amfanye mtanzania ajisikie proud anaposimama mbele ya raia wa mataifa mengine.Pride na national values ndizo zinazolitofautisha taifa kubwa na dogo.We have what it takes to make Tanzania a giant Nation in Africa and beyond![/QUOTE
leo umegeuka? tulikuwa wote kule nyuma kumshambulia kagame leo silaha kasema
uko naye.
 
Naungana na Dr Slaa na watanzania wote wanaopenda amani na majirani zake. Aidha, sikuiona busara ya Rais Kikwete kumtaka hadharani Rais Kagame na Rwanda kuzungumza na wauaji wale. Wengi wetu humu hamjui uzito wa kilichotokea mwaka 1994 ambapo mpaka leo watu 1 millioni wahakuweza kuwa accounted for. Katika nchi yenye watu 10 million, hiyo ni idadi kubwa mno na ni kubwa hata hivyo kwa standard yoyote. Nadhani Rais wetu angeweza tu kuongea na Kagame kwenye mikutano yao ya ndani uwezekano wa kukaa na wale nk. Rwanda ni nchi ndogo sana na Tanzania ambapo pia wanaishi Wanyarwanda wengi tu mpaka ndani ya seriklai na majeshini, hakuna haja ya ugomvi. Tofauti ingekuwa kama wanataka meter kadhaa ya ardhi yetu. Nadhani Rais wetu ashughulike zaidi na matatizo ya ndani Tanzania na umasikini wa watanzania walio wengi kuliko hilo la Rwanda. Kwangu anaona ni ku divert attention juu ya matatizo ya ndani na serikali yetu kuwa adiu wa raia wake. Kwangu adui ni Malawi anayetamani ziwa letu la Nyassa. Hakuna haja ya Tanzania kuwa na uadui na jirani. Ukimgusa Kagame, unamgusa Museveni. Hilo yujue. Kenya atasimamia pale maslahi yake yatakapokuwa pindi vurugu zikitokea. Congo na wacongo wala haitabiriki na kwa hiyo sio wa kutilia maanani sana. Kule Congo kuna Wanyarwanda kama milioni 5, na Rais Joseph Kabila pia ni Mnyarwanda kwa hiyo lolote laweza kutokea. Watanzania tuwe waangalifu sana na ukanda huu wa maziwa makuu. Kuna mambo mengi yaliyojificha. Tujenge Tanzania na tudumishe ujirani wetu. Kama Kikwete binafsi na tatizo na Kagame binafsi wayamalize wenyewe. Vita ya Kagera 1979 bado inaumiza Tanzania na sio jambo jema kupigana bila sababu. Wamarekani wasitutumie kwa maslahi yao. Asanteni.

Naona watu hamna historia nzuri ya mauaji ya kimbari ya Rwanda.......Naona hamfahamu kabisa hata huyu Kagame naye kwa kiasi kikubwa anahusika na yale mauaji ya Rwanda...someni tena historia vizuri then mje kivingine.......Anakataa kuzungumza na wauaji wakati yeye pia ni muuaji mkubwa pia.....acha hicho kikosi chake cha mauaji anachokitumia kuwa Assasinate wapinzani wake...this guy is full of blood on his hands....ajifanya eti haongei na wauaji...damn him
 
1. Nakubaliana na hoja yako ya kwanza kwamba kushinda vita kunahitaji umoja wa kitaifa.
2. Kuhusu nyerere na ushawishi wa ndani; tukumbuke kwamba wakati wa nyerere hakukuwa na chadema wala CUF. Fikra za nyerere zilikuwa ni "fikra sahihi" kwa hiyo hakuhitaji kumshawishi mtu yoyote kwenda vitani. Alichofanya ni kutoa amri tuu na amri ikatekelezwa. JK anafanya kazi katika mazingira tofauti na yale ya JKN. Miongoni mwa wapinzani kuna wazalendo na pia kuna "unscrupulous, machiavellian, opportunist characters ". Hili kundi la pili ndilo kundi la hatari sana kwa taifa letu. Wasi wasi wangu ni kwamba Slaa yuko kwenye hili kundi la pili, na kama haya yaliyoandikwa humu ni maoni yake kweli; basi chadema wana kila sababu ya kuutazama upya uongozi wao kama kweli wanajali maslahi ya taifa letu.

Nyerere alifanya kazi katika wakati mgumu zaidi maana kuzima upinzani kulizalisha silent rebellion na ni hatari zaidi.Kumbuka utekelezaji wa azimio la Arusha lililoambatana na displacement ya watu lilitengeneza hasira ya kitaasisi na kabla ya hapo tayari Nyerere alishakumbana na Uasi takribani miaka 10 nyuma huku akina Kambona wakiwa exile kama potential threats(Ingawa hoja ya kuwa kama Kambona alikua Hero au Villain ni subject of debate).Upinzani uliopo unatambulika kisheria na kitaasisi na ni rahisi kufanya dialogue au compromise on issues.JK yupo kwenye wakati mzuri zaidi wa kufanya dialogue na wapinzani wanaotambulika kitaasisi kuliko Nyerere ambaye muda wote alikua alert but still he managed to cooordinate the forces against common enemy!Unasemaje hapo?
 
Slaa ameshafanya vitu vingi sana ambavyo watu na hata Mungu hakutegemea kama angevifanya...

Slaa is a man of surprises (Bad surprises)...
Kama vp mkuu ? maana jambo ambalo litamstaajabisha Mungu halafu binadamu tukaliona la kawaida...
labda tufafanulie..
 
Dr.Slaa anaweza kuongea hivyo kwa sasa. Lakini hata Dr. Slaa angekuwa Rais wa nchi,maisha yake binafsi na mipaka ya nchi yake ikitishiwa,angeanza kwanza ku deal na wanaotishia mipaka ndipo angekuja kutatua ya ndani.

Ukiwa unagombana na mkeo/mumeo ndani,ukasikia watu wanataka kuvunja gate wavamie kwako,cha kwanza utaenda kupambana na wanaivunja gate lako ukisha wasambaratisha ndio utarudi ndani kupatana na mkeo/mumeo.

good comment!!kuna mijitu mingine kaz yao ni kupinga tu hata mambo ambayo hayahitaji kupingwa!
 
Kushinda vita kunahitaji umoja wa kitaifa.Uzalendo ni kigezo kimojawapo katika sababu za kushinda au kushindwa.Kiongozi mkuu wa Nchi ni lazima aunganishe taifa dhidi ya common enemy ambaye ni adui wa nje.Wahenga walisema kamba hukatika......!

Uongozi wa JK na brutality dhidi ya wapinzani wa serikali yake unaliweka taifa katika precarious situation.Nyerere alishinda vita ya Kagera kutokana na ushawishi wa ndani.Rais anatakiwa amfanye mtanzania ajisikie proud anaposimama mbele ya raia wa mataifa mengine.Pride na national values ndizo zinazolitofautisha taifa kubwa na dogo.We have what it takes to make Tanzania a giant Nation in Africa and beyond![/QUOTE
leo umegeuka? tulikuwa wote kule nyuma kumshambulia kagame leo silaha kasema
uko naye.

Nimegeuka wapi?Hapa tunajadili internal coordination of forces mzee.
 
Slaa nae asidandie gari kwa Mbele.Aweke mbele uzalendo,pia afahamu kuwa Rais KIkwete hakutamka nje ya guidance ya sera ya mambo ya nje ya nchi yetu kwa kuwa ameiva ki diplomasia,SLaa si mwana DIplomasia,yeye amekuwa addicted na maandamano.Asubiri karata yake 2015,kuongoza nchi si lelemama.Kwa muda huu ajifunze diplomasia na si against each and every step taken by Mr President.Kwa hili nitamchukia.

Uzalendo?????you are jocking!!
Wezi wa EPA.Meremeta,Richmond ,Watu wa madawa ya kulevya nao utawaita Wazalendo kuliko Slaa!
 
jk alitoa ushauri ilikuwa kwenye mkutano tena ulio rasmi na ilikuwa ni kila mtu anatoa ushauri wake suala ilikuwa kuufuata au kuuacha.sasa kagame anataka vita mpaka atapokufa hitimisho lake na waasi ni lipi maake wanatuletea sisi wakimizi tu.kwa suala la dkt slaa sishangai kwasababu vyama vyetu huwa havina sera za nje zaidi ya kuwa na mahusiano na vyama vya nje lakini sera za kimataifa hamna kitu ila jk kwa suala la diplomacy amejitahidi sana huyu baba shida yake ni uchumi tu ila mengine tunamuonea
 
Hakuna maslahi yoyote tutakayoyapata huko Congo hapa kuna jambo zito limejificha hasa Marekani anapojihusisha na huu mgogoro.Akina JK wameshaahidiwa pepo tayari.Huu ni mgogoro wa kimaslahi.

Kwa hiyo hudhani kwamba kama taifa kubwa katika ukanda wa maziwa makuu tuna majukumu ya kuhakikisha wa-congo wanaishi maisha yao kwa amani?
 
Kumbe hata Slaa ni mwanasiasa kiasi hiki hovyooooo kweli
 
Dr Slaa Yuko na point,
Kwetu sisi si rahisi hata kuwaruhusu wapinzani watoe hoja mbadala kwa serikari,kuikosoa inapelekea serikari inaagiza watu wapigwe.
sisi tuko mbele kusukuma wenzetu pataneni na adui zenu.
kwa lugha rahisi sisi na raisi wetu Ni wanafiki, wapenda sifa tu.
 
Inaonekana Slaa anataka mpaka apangishwe chumba magogoni wakae na Mushumbusi ndio aone kwamba Rais wetu ni mwanasiasa wa kisasa anayeongea na mtu wa itikadi yoyote kwa lengo la kufikia makubaliano ya amani bila shuruti.

Hivi Slaa haoni aibu kusema UONGO at his age?

Uroo wa pesa na madaraka unampeleka kubaya sana Slaa...

View attachment 105629

hahahaha!!mtumishi wa mungu lakin mzandiki aliekubuhu!!duuuh!!
 
jk alitoa ushauri ilikuwa kwenye mkutano tena ulio rasmi na ilikuwa ni kila mtu anatoa ushauri wake suala ilikuwa kuufuata au kuuacha.sasa kagame anataka vita mpaka atapokufa hitimisho lake na waasi ni lipi maake wanatuletea sisi wakimizi tu.kwa suala la dkt slaa sishangai kwasababu vyama vyetu huwa havina sera za nje zaidi ya kuwa na mahusiano na vyama vya nje lakini sera za kimataifa hamna kitu ila jk kwa suala la diplomacy amejitahidi sana huyu baba shida yake ni uchumi tu ila mengine tunamuonea

Uko obsessed na bibi wa Slaa!Kama wengi humu waki attack vimada wa viongozi wa magamba,mod ataban halaka
 
Back
Top Bottom