Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Nadhani . waaa hapa kakurupuka naye anasema mbona yeye kashindwa kushughulikia mambo yake ya ndani?? Mimi kwa uelewa wangu hii aimzuii kuongelea amani ya east afrika...mimi nadhani si kila kitu tupinge usalama wa east afrika una maana usalama wa tanzania...

J.K alikua sawa tu mtutu ukishindikana haina budi kurudi mezani.

I stand to be corrected

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Hatuwezi kusikia chochote kizuri anachokifanya JK, toka mdomoni mwa Dr Slaa.
Na hapa anajionyesha alivyo na upeo mdogo wa usalama wa nchi kitaifa.

Tatizo Slaa hajapita JKT wala mgambo, aangalie wenzake wa upinzani Uingereza hata Marekani.
Inapokuja usalama wa nchi, support yote Ipo kwa amiri jeshi mkuu.
 
Hivi huyu babu ana matatizo ya kumbukumbu? au ni unafik tu?

juice-ilikuwepo.jpg

slaa-lissu-kikwete.jpg
Sijaona connection yeyote hapo. Just because alikutana na Kikwete kwa hiyo asimkosoe kuhusu Rwanda?
 
hakuna utetezi wowote unaoweza kondoa ukweli kwamba JK ni mpuuzi tu. watu makini kama DR.slaa wanampa ushauri adhimu aukatae tu. alafu tutajua nani yuko sahihi kati ya JK na DK. tatizo Jk anachachawa sana mbele ya maraisi wenzie, sijui anatumia na nchi za magharibi?? au ana maslahi na migogoro. kama ana busara si aombe awe msuluhishi??, dk waukweli SLaa uko makini
 
Sijaona connection yeyote hapo. Just because alikutana na Kikwete kwa hiyo asimkosoe kuhusu Rwanda?

Nini cha kumkosoa? sijaona ubaya alioufanya Kikwete kuhusu Rwanda au wewe umeuona?
 
hakuna utetezi wowote unaoweza kondoa ukweli kwamba JK ni mpuuzi tu. watu makini kama DR.slaa wanampa ushauri adhimu aukatae tu. alafu tutajua nani yuko sahihi kati ya JK na DK. tatizo Jk anachachawa sana mbele ya maraisi wenzie, sijui anatumia na nchi za magharibi?? au ana maslahi na migogoro. kama ana busara si aombe awe msuluhishi??, dk waukweli SLaa uko makini
Una pepo la Slaa, Ibilisi wa amani!
 
Tutapambana na nyie mamluki mliomwagwa hapa kwa fujo na kila siku mnachonga IDs chungu nzima ili kuvuruga mijadala muhimu. Miaka ya nyuma kulipokuwa na wanachama wachache kulikuwa na kuheshimiana sana hata kama watu hawakubaliani, lakini tangu nyie mamluki wa buku 7 kuja hapa uwepo wenu umechangia sana kushusha viwango vya mijadala maana mkiona mjadala muhimu tu dhidi ya Serikali au CCM basi mtashuka hapa na IDs zenu 50 50 ili kuandika kejeli, kashfa na hata matusi ili tu kuvuruga mijadala kiasi ambacho baadhi ya wanachama wasiku nyingi kutotaka tena kuingia kuchangia lolote lile. Kwa taarifa yenu tumechoshwa na vitendo vyenu vya kukubali kutumika kama mamluki kwa ujira mdogo sana ili kuvuruga majadiliano muhimu hapa. Serikali na vyombo vyake vya dola itunyanyase na nyinyi mamluki hapa JF mtunyanyase na kuvuruga mijadala. Kama hamna cha maana cha kuandika zaidi ya kashfa, matusi na kejeli basi kaeni kimya vinginevyo tutapambana nanyi ili kuhakikisha JF inaendelea kuwa na hadhi na heshima yake kama miaka ya nyuma. Nyie wote wote akina Ritz, chama, scramble, Faiza Foxy, Bukyanandi, wabuyaga, Hamida, Utaifa kwanza, Zemarcopolo, lizaboni, leomimi na mambulula wengine wa buku 7 mnaochonga IDs mpya kutwa kucha ni sumu kali sana ya future ya JF. Kama hamuwezi kuandika cha maana zaidi ya pumba zenu basi tafuteni sehemu nyingine ya kuandika pumba zenu hapa tumezichoka zinatuharibia ukumbi wetu. Inawezekana kabisa kuwa na wanachama hata milioni na bado watu kuandika bila kashfa, kejeli au matusi. Habari ndiyo hiyo na kwa taarifa yako si kila mtu anataka vyeo vya kubabatizwa kama unavyodhani.

Mr. Man nimekupata hasa. na nimefurahi kusikia mawazo yako ambayo yanaonyesha kuwa hatuko tofauti sana ingawa kama nilivyosema mwanzoni tatizo ni IQ yako. nikiwa na maana kuwa kutokana na comments zako za mwanzo ni moja kwa mojo inaonyesha wewe una IQ finyo: Angalia mr. Man, hivi inakuja kabisa kiongozi wa nchi ambaye ameshindwa kuheshimu mienendo ya demokrasia nchini kwake lakini yeye anakuwa mtu wa kutoa njia ya kusuruhisha migogoro ya nchi nyingine! Tusiangalie wewe ni wachama gani au mimi ni wachama kipi, tuangalie facts! Je ni kweli inakuja kabisa? kiongozi ambaye anakuwa na kigugumizi kwa vitu ambavyo viko wazi na ambavyo ni muhimu kwa nchi yetu eti bado anataka kuwapatanisha maadui wa nchi nyingine, huu ni unafiki na kutafuta sifa za bure! Tumechoka na tutaendelea kukataa unafiki wa namna hii pamoja na kutafuta sifa ambazo watu hawatakiwi kuwa nazo. Mr. Man kama wewe unaitakia nchi yetu amani anzia hapa kutatua matatizo ya watu wetu. Hawa wanyarwanda kama wakitaka kutuchokoza kwa sababu zao ni kiasi cha siku mbili tunamaliza matatizo yao! Wewe na viongozi wenu si wazalndo kwani Tanzania imepoteza sifa zake mble ya mataifa mengine kutoka na uzembe wenu na kutaka sifa bila kuzifanyia kazi. Madawa ya kulevya, passport zinauzwa kama maembe ya dodo nk. shame on you na badirikia
 
yeye kafeli darasani wewe na babako mmefeli maisha.

Nani kakudanganya nimefeli maisha? Kwa akili zako kama za KITIMOTO unafikiri kufanikiwa maisha ni kukaa IKULU tu? Poor you! Hayo ni makao ya muda tu sawa na mpangaji tu kwenye nyumba yoyote ambayo itafika muda fulani lazima tu mtatoka, au mmeshajimilikisha IKULU?
 
Nguruvi3,

Siyo mchangiaji wa mambo ya Kisiasa hasa za Tanzania siku hizi. Nachangia tu hapa kwa sababu ni swala linaloenda nje ya mipaka ya Tanzania. M-mbabe kanisaidia hapa kwa jibu safi ambalo sitaki niongeze wala kupunguza maana ndiyo mawazo yangu. Hakuna anayepinga ushauri wa Kikwete. Kama mataifa yote yanajua, kuna haja gani kusema hapo? Kama PK hataki, si muitieni USA waje na Drone zao waanze kuiharibu Rwanda kama walivyofanya Libya na mwisho wanaleta tu Risiti za gharama ya vita yao kumuondoa Kagame?

PK anafanya kile mataifa ya West yalifanya miaka ya 60 na 70. Kwa Tanzania kwa sasa hawawezi kuja kwa sababu Tanzania ni mali ya USA na China. Hata Banda lazima aufyate ila PK anabaki anasemea pembeni. Ndiyo maana hasemi vita ila anasema "akipata kamwanya sehemu, basi atamtandika...." Vita haihitaji mwanya ila kuondoka na kulianzisha.
kukubali au kukataa ushauri siyo hoja niliyoi-raise mimi.
ushauri hata ukiwa mzuri kiasi gani, ukitolewa ambavyo sivyo lazima kuwe na backlash.

tatizo langu liko kwenye approach ya JK (sina tatizo na nia yake) kwenye hii issue ya Kagame. ilihitaji ka-HEKIMA kadogo tu.

JK akubali tu kuwa ali-goof kwenye approach, licha ya nia nzuri iliyomo ndani ya ushauri wake!
 
hakuna utetezi wowote unaoweza kondoa ukweli kwamba JK ni mpuuzi tu. watu makini kama DR.slaa wanampa ushauri adhimu aukatae tu. alafu tutajua nani yuko sahihi kati ya JK na DK. tatizo Jk anachachawa sana mbele ya maraisi wenzie, sijui anatumia na nchi za magharibi?? au ana maslahi na migogoro. kama ana busara si aombe awe msuluhishi??, dk waukweli SLaa uko makini

well articulated,guy!!! Whoever has a fully developed brain knows about this.how dare u advise your counterparty to have seated in a circle of argument with people condemned to be manslayers or liquidators as a part and parcel of reaching resolution so far? There must be something wrong with jk in his mind in particular. I anticipated him and his counterparties to come up with an ideal idea of drawing a road map and strategic plan on the way forward that could actually see all x-combantants who are now termed as rebel groups become abducted and face trials(ictr & gacaca) in regards to their accusations as the only means suggested and adhered to by different elites in and outside the conflict area.
Kagame knows exactly what is going through right from the beginning where he set and asserted for an action that ended up bringing harmony and peace in his territory within a period of not less than nine years.He is focused,he is a man of sight and missions and he knows exactly where he is heading to.No need of an empty headed person,who sees nowhere come out and drive him on the proper way of dealing with the matters in the end while he had never set a peaceful plan right from the beginning.Jk derseves nothing to contribute on this saga rather than giving credit to a smart president PK for his outstanding endeavor of bringing the situation the way now it is.That is to say, Rwanda is in a state of tranquillity as compared to a couple of few years past.Bravo Kagame.
U are in the right truck,keep moving on!!!
 
Nini cha kumkosoa? sijaona ubaya alioufanya Kikwete kuhusu Rwanda au wewe umeuona?

Bibie,
Kikwete anataka Kagame azungumze na wauaji wake. Ni kama vile kuwaambia Wayahudi wazungumze na Wanazi wa Hitler. Wewe unaona hilo limekaa vizuri? Kikwete anapaswa kwanza kuzungumza na watu wa Mtwara kuhusu gesi yao.
Siyo kutumia mabavu.
 
Jasusi,

..kuna FDLR ambao hawakushiriki wala kupanga mauaji ya 1994. Hao ndiyo JK alipendekeza Paul Kagame azungumze nao.

..wale FDLR waliopanga au kushiriki ktk mauaji wanatafutwa kwa warrant za kimataifa na wakitokea popote pale wanakamatwa. Kwa msingi huo hao hawawezi kukaa ktk meza ya mazungumzo na Kagame. Mwezi Julai wakati Kagame akiendelea kuporomosha matusi kwa JK yuko mtuhumiwa alikuwa transfered toka Arusha kwenye Kigali.

..Mwisho, mbona Frelimo walifanya mazungumzo na Renamo? Mbona MPLA walifanya mazungumzo na UNITA? Mbona Wapalestina wanazungumza na Waisraeli? Mbona Wacongo wanazungumza na Wanyarwanda?

..Hivi vita vimeendelea kwa karibu miaka 20 sasa. Wacongo zaidi ya milioni 3 wamepoteza maisha. When are going to say enough is enough??
 
Last edited by a moderator:

jokaKuu,
Hao ambao hawakushiriki kwenye genocide walishakaribishwa warudi. Hata wale walioshiriki pia. Ndio sababu Rwanda ilianzisha Gacaca. FDLR wana agenda ambayo inakinzana na maslahi ya serikali ya Kagame na utulivu wa nchi kwa ujumla. They can participate in the country as long as they are not tribalistic, lakini hawa wanataka kurudi in power by military means. Frelimo walifanya mazungumzo na Renamo baada ya source of support for Renamo---South Africa and Rhodesia--- kukauka. MPLA walifanya mazungumzo na UNITA baada ya Savimbi kuwa kaput. Kill the head of FDLR and I will join the chorus to want Kagame to talk.
 
Hoja ya Dr. Slaa ilikua kwamba Nchi haiwezi kuwa dragged vitani kwa sababu ya kauli ya Kikwete na vile vile akashsuri Kikwete aanze kwanza kukaa na wapinzani wake.

Ben Saanane
Mm nafkiri wewe na Bavicha wote + Padre Slaa munapenda maigizo zaidi tu.
Sasa unataka rais akae vipi na Upinzani tena mbona juzi tu Mbowe katoka kula batta Ikulu kule..
Kampatia ubunge Mbatia,
Na Padre si ndio alisema kama hamtambui Rais sasa atakaaje nan mtu ambae hamtambui?
Sasa alipoenda Mbowe ikulu watu walieka zogo sana kumbe Padre na yeye anataka akatembee haya Mr. President ameshasikia kilio cha Padre kwenda kutembea Ikulu nafkiri atapata mualiko wa Eid asijali.
Ila musiwe na akili za kitabu tu changanya na za kuzaliwa nyinyi pasua kichwa kweli
 
Slaa MNAFIKI sana, ndio maana hata goti lake hawezi kulikunja!!!

View attachment 105631

ZeMarcopolo nilishakwambia una uwezo mdogo wa kufikiri,kujenga hoja na hata kujitetea kisiasa..kwa mfano ulichoandika hapo juu kina uhusiano gani na topic inayoendelea? Kuna mahusiano gani ya mwili wa mtu na hoja yake? Au ndo ujinga wenu wa kuchagua watu kwa muonekano wa sura zao? Au ndo unatuaminisha kuwa wewe ni mbaguzi wa watu wenye kasoro za viungo vya mwili? Sitaki nijibu ujinga uliosema lakini dr Slaa angekuwa na tatizo la goti ungeweza tembea kwa miguu kweli? ZeMarcopolo 0.5(5)^10 KB thinking capacity.
 
Hatuwezi kusikia chochote kizuri anachokifanya JK, toka mdomoni mwa Dr Slaa.
Na hapa anajionyesha alivyo na upeo mdogo wa usalama wa nchi kitaifa.

Tatizo Slaa hajapita JKT wala mgambo, aangalie wenzake wa upinzani Uingereza hata Marekani.
Inapokuja usalama wa nchi, support yote Ipo kwa amiri jeshi mkuu.

Obama kapitia jeshi lipi?Mbona anaweza kumudu issue zinazohusu usalama wa nchi yake?Tatizo lenu ndio hilo,kwa nini hamuheshimu maoni ya mtu?hayo ni maoni yake na nyie toeni yenu!Mmezoea ile karne ya 'zidumu fikra za mwenyekiti',kuwa kiongozi ni kama mungu,akisema amesema.Slaa ni binadamu kama binadamu wengine,hayo ni maoni yake na yameeleweka sana tu!!!
 
Mshaurini mkuu wenu arudi kwenye mimbari kuhubiri, siasa zimemshinda.
Usalama wa nchi yoyote si suala la kupiga domo kama anavyofanya.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wazee wa wilaya ya Karagwe walimtaka Kikwete kuacha choko choko zake na Kagame kwani hazina faida yoyote zaidi ya kuwaumiza wao pindi vita itakapotokea.

Katika barua waliomwandikia walisema hawajui walichotofautiana lakini vyovyote vile hakina masarahi kwa nchi. "Mwaka 1978 tulijitolea kupigana na ndugu na jamaa zetu walikufa wakipigania kuikomboa sehemu ya nchi yetu iliyokuwa inakaliwa na nduri Idd Amini. Mh rais leo tukikuuliza tuna faida gani na hizi chokochoko?"

Walisema wao waliifadhi wakimbizi wa Rwanda na wanajua athari za vita tokea hata wakati wa Amin hivyo hawako tayari kuona tena vita kwenye ardhi uao. Zaidi walisema hawaoni sababu ya rais Kikwete kumlazimisha Kagame kuongea na waasi maana wananchi wa Rwanda na rais wao ndiyo wanajua uzito wa suala hili.

Barua hiyo sijui kama ni busara kuiweka hapa maana ina mambo mengine hayahusiani na na hili. Lakini kwa ujumla wazee wanasema bif binafsi hazitakiwi kuingiza nchi vitani na wao ndiyo watakuwa wahanga maana wanaishi mpakani.
 
Back
Top Bottom