Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Wapendwa wana JF, nimebahatika kutembelea nchi ya Rwanda kwa siku tatu kuanzia tarehe 2/8/2013- 5/8/2013. Nikiwa kwenye ziara yangu nilibahatika kufika miji ya Nyakarambi, Ruchira, Gituku, Kibungo, Kabarondo, Kayonza na Rwamagana.
Nikiwa huko nimeweza kujifunza kuwa wanyarwanda wanamchukia sana Kikwete lakini wanawapenda sana watanzania. Nilibahatika kuongea na watu tofauti wakiwemo raia wa kawaida, viongozi na wanajeshi.

Nilichogundua ni kwamba kila nyarwanda hata aliyeko kijijini anataarifa kuhusu mgogoro wa Kagame na kikwete kwani baada ya kujua mimi ni mtanzania walianza kurusha shutuma kwa Kikwete alivyo mjinga kuingilia masuala ya Rwanda na kujikomba Umoja wa mataifa bila kwanza kumshirikisha kagame mwenyewe au Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wa raia wanadai wanaipenda sana Tanzania na watanzania wote isipokuwa wanamchukia Kikwete kwa tabia ya kupenda kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi tofauti na ilivyokuwa enzi za mwalimu. Wanasema Kikete hakuwa na haja ya kuyaongelea masuala ya Rwanda akiwa Ethiopia badala yake angetumia busara hizo kwanza kukaa na kagame akamshauru wakiwa wawil au angetumia jumuiya ya Affrika masharikia kutoa ushauri wake.

Kwa upande wa viongozi wa serikari niliobahatika kuongea nao wanadai kitendo alichokifanya kikwete akiwa Ethopia hakikuwa cha kiungwana kwani kule hakukuwa sehemu muafaka ya kuongelea jambo hilo na wanaongeza kuwa wanaimani kuwa hayo hayakuwa mawazo ya watanzania bali yalikuwa mawazo ya Kikwete binafsi na hawawezi kuwacghukia watanzania wote kwa sababu ya kikwete.

Tukiwa kwenye burudani tunapata kalinya nilibahatika kuongea na Mwanajeshi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mbalanga, ambaye pia hakuwa tofauti sana na raia pamoja na viongozi wa serikali. Yeye alisema Kikwete hawataki wanyarwanda na wanyarwanda hawamtaki kikwete lakini wanajua watanzania wanawapenda sana wanyarwandwa hivyo uhususiano baina ya watanzania na wanyarwanda hauwezi kuvunjika kwa mtazamo wa mtu mmoja, Ingawa kitu kilichonishtua ni pale aliposema tumajenga kwa kasi sana bandari yetu ya nchi kavu pale Rusumo kwa ajili ya kuweka vifaa vya kujilinda na kweli pale Rusumo upande wa Rwanda wanajenga bandari kubwa ya nchi kavu. Mwanajeshi huyo haukuishia hapo alisema pamoja na hayo Presdent ameshatwambia tukae tayari kwa lolote na tunajua udhaifu wa watanzania. Tunaweza kuwa ni rahisi kuwagawa na kutumia udhaifu huo kuwapiga.

Mwisho nilimalizia Benako kituo kodogo cha magari makubwa kilichoko kilometer 15 kutoka mpakani ambapo nilifanikiwa kuongea na nyarwanda wa ngara mwenye uraia wa Tanzania.
Mama huyo alisema baada ya agizo la kikwete la kuwataka wahamiaji wote haramu aidha warudi kwao au watumie taratibu za kupata uraia, serikali yake imetumia nafasi hiyo kuwanyanyasa na kuwatishia kwani hata kama mtu una uraia wa Tanzania ulioupata kihalali miaka zaidi ya ishirini iliyopita unaambiwa wewe ni mhamiaji halamu, Hivyo unalazimishwa kutoa rushwa vunginevyo unaorodheshwa kama mkimbizi au mhamiaji halamu.

Nawasilisha
 
Inaonekana Slaa anataka mpaka apangishwe chumba magogoni wakae na Mushumbusi ndio aone kwamba Rais wetu ni mwanasiasa wa kisasa anayeongea na mtu wa itikadi yoyote kwa lengo la kufikia makubaliano ya amani bila shuruti.

Hivi Slaa haoni aibu kusema UONGO at his age?
Uroo wa pesa na madaraka unampeleka kubaya sana Slaa...

View attachment 105629
Hiyo ndio dalili ya mvua hivi inakuwaje mtu unagombea urais kwa miaka ishirini haushindi kwa nini usiwape wengine nao wajaribu! maana ukiona haushindi sio chama ni wewe kuwa nyota yako haishawish watu kukuchagua hiyo ndio demokrasia? kweli CCM ina mapungufu lakini ni mara mia CCM iendelee kuwa madarakani kuliko mtu kama slaa na mbowe wapewe nchi si kuiuza huko. Huku wanajiita demokrasia lakini akitokea mtu mwingine kuwa anataka kugombea wanakuja juu demokrasia ya kinafiki zaidi.

Kuna kipindi nilisema huyu mzee hana sera anaendeshwa zaidi na matukio na hisia yaani kama hakuna tukio linagusa public attention basi huwa ameishiwa kabisa that why every day he is talking about the past. Hana jipya wala njia mbadala kusema hawa wameshindwa hivi sisi tufanye hivi ukimtazama unaona uroho alionao lakini si uchungu na uzalendo. si aghalabu tukisikia ndio wanaotumiwa na kagame kuhatarisha amani ya nchi ili wawasingizie CCM. Ni vyema akazane kutela maedeleo kalatu maana uzalendo ulisha mshinda baba paroko. Miaka yote aliyokuwa mbunge kalatu bado imelala na aliyepo ni hivyohivyo kutwa kucha maandamano.
 
Wapendwa wana JF, nimebahatika kutembelea nchi ya Rwanda kwa siku tatu kuanzia tarehe 2/8/2013- 5/8/2013. Nikiwa kwenye ziara yangu nilibahatika kufika miji ya Nyakarambi, Ruchira, Gituku, Kibungo, Kabarondo, Kayonza na Rwamagana.
Nikiwa huko nimeweza kujifunza kuwa wanyarwanda wanamchukia sana Kikwete lakini wanawapenda sana watanzania. Nilibahatika kuongea na watu tofauti wakiwemo raia wa kawaida, viongozi na wanajeshi.

Nilichogundua ni kwamba kila nyarwanda hata aliyeko kijijini anataarifa kuhusu mgogoro wa Kagame na kikwete kwani baada ya kujua mimi ni mtanzania walianza kurusha shutuma kwa Kikwete alivyo mjinga kuingilia masuala ya Rwanda na kujikomba Umoja wa mataifa bila kwanza kumshirikisha kagame mwenyewe au Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wa raia wanadai wanaipenda sana Tanzania na watanzania wote isipokuwa wanamchukia Kikwete kwa tabia ya kupenda kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi tofauti na ilivyokuwa enzi za mwalimu. Wanasema Kikete hakuwa na haja ya kuyaongelea masuala ya Rwanda akiwa Ethiopia badala yake angetumia busara hizo kwanza kukaa na kagame akamshauru wakiwa wawil au angetumia jumuiya ya Affrika masharikia kutoa ushauri wake.

Kwa upande wa viongozi wa serikari niliobahatika kuongea nao wanadai kitendo alichokifanya kikwete akiwa Ethopia hakikuwa cha kiungwana kwani kule hakukuwa sehemu muafaka ya kuongelea jambo hilo na wanaongeza kuwa wanaimani kuwa hayo hayakuwa mawazo ya watanzania bali yalikuwa mawazo ya Kikwete binafsi na hawawezi kuwacghukia watanzania wote kwa sababu ya kikwete.

Tukiwa kwenye burudani tunapata kalinya nilibahatika kuongea na Mwanajeshi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mbalanga, ambaye pia hakuwa tofauti sana na raia pamoja na viongozi wa serikali. Yeye alisema Kikwete hawataki wanyarwanda na wanyarwanda hawamtaki kikwete lakini wanajua watanzania wanawapenda sana wanyarwandwa hivyo uhususiano baina ya watanzania na wanyarwanda hauwezi kuvunjika kwa mtazamo wa mtu mmoja, Ingawa kitu kilichonishtua ni pale aliposema tumajenga kwa kasi sana bandari yetu ya nchi kavu pale Rusumo kwa ajili ya kuweka vifaa vya kujilinda na kweli pale Rusumo upande wa Rwanda wanajenga bandari kubwa ya nchi kavu. Mwanajeshi huyo haukuishia hapo alisema pamoja na hayo Presdent ameshatwambia tukae tayari kwa lolote na tunajua udhaifu wa watanzania. Tunaweza kuwa ni rahisi kuwagawa na kutumia udhaifu huo kuwapiga.

Mwisho nilimalizia Benako kituo kodogo cha magari makubwa kilichoko kilometer 15 kutoka mpakani ambapo nilifanikiwa kuongea na nyarwanda wa ngara mwenye uraia wa Tanzania.
Mama huyo alisema baada ya agizo la kikwete la kuwataka wahamiaji wote haramu aidha warudi kwao au watumie taratibu za kupata uraia, serikali yake imetumia nafasi hiyo kuwanyanyasa na kuwatishia kwani hata kama mtu una uraia wa Tanzania ulioupata kihalali miaka zaidi ya ishirini iliyopita unaambiwa wewe ni mhamiaji halamu, Hivyo unalazimishwa kutoa rushwa vunginevyo unaorodheshwa kama mkimbizi au mhamiaji halamu.

Nawasilisha
Jambo la kwanza ni kwamba sijaridhika na maamuzi ya mods kuunganisha hii topic ya Omulangira na hii ya slaa amkosoa Jk. Kulikuwa na haja ya kuwa na mjadala ambao ni independent katika hoja aliyoileta Omulangira. Hizi majuzi nilileta hoja inayofanana na hii ya Omulangira kwamba Kikwete azungumze na Kagame. Naamini haya yanayoendelea hivi sasa ni kati ya Kikwete na Rwanda na si katika ya Rwanda na Tanzania. Sasa kauli binafsi za Kikwete zisiiponze nchi. Akubali alikosea, amuombe msamaha mwenzake ili yaishe. Hatutaki vita. Nimesisitiza kwenye thread hii: https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/499266-kikwete-zungumza-na-kagame.html
 
Last edited by a moderator:
Nini cha kumkosoa? sijaona ubaya alioufanya Kikwete kuhusu Rwanda au wewe umeuona?
Kosa linalolalamikiwa na wanyarwanda alilofanya Kikwete ni kitendo cha kutoa ushauri wake hadharani alipaswa atambue Kagame ni rais kama yeye anastahili heshima kama yeye anavyostahili.

Alichotakiwa ni kum-face Kagame in person then angepima mwitikio wa Kagame baadae angewauzia viongozi wengine wa EAC ushauri wake, mbali ya ushauri Kikwete alitakiwa pia aje na action plan tofauti na alivyouacha ukielea.

Kitu kingine ambacho kingeonekana kizuri ni kujitolea yeye kama yeye Kikwete kuwa msuluhishi, mediator.
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.

CHANZO: NIPASHE

wewe slaa inaonekana akili zako nusu sasa,yaani nilivyokuwa nakukubali wewe na chadema yako leo unaweza kuongea upuuzi kama huu? au huwa unapata ushauri kutoka kitandani kabla ya kuja kuropoka? wewe na mwigulu mnafanana...
 
slaa amenogewa na utamu wa juice ya ikulu aliyobahatika kuipata kipindi kile naona anatafuta mbinu tena ya kualikwa kupitia mgongo wa kagame.
 
Dr. Slaa sio kosa lake. Uwezo wake wa kufikiri umekuwa wa kiwango cha Josephine Mushumbusi.

Anasema Kikwete haongei na wapinzani wakati Slaa ameonekana mara kadhaa Ikulu akinywa juice. Sasa sijui walikuwa wanakunywa juice kimyakimya!!!

View attachment 105628

Haya twende na akili yako ya kushikizwa hapo wanaongea au kila mtu yuko kivyake?
 
Kinadharia ushauri wa Kikwete unaweza kuonekana kama mzuri lakini haukuwa na action plan au road map ya utekelezaji kushauri bila action plan ni sawa na kuropoka hasa unapomshauri mkuu wa nchi nyingine.

Kama Kikwete ataanzisha vita na Kagame binafsi nitakuwa wa mwisho kwenda vitani, kwa sababu naamini Kikwete hakuwa sahihi kuwaambia Rwanda wakutane na waasi alichotakiwa ni ku-mediate mkutano kwa kuwakutanisha mahasimu na sio kuwaambia wakutane, kwanza wakutane wapi na nani awe mlalamikaji na mlalamikiwa.

Akili zako za kufikiri ndiyo zimeishia hapo. Nashindwa kuelewa kama kuna Mtanzania anaweza kuwa against statement ya Rais Kikwete. Action plan ipi? Kwanza kubali idea au kataa ndipo action plan inafuata. Kikao kile hakikuwa cha kutoa action plan. Watanzania tuna utajiri wa action plans.Uliza Kenya kilitokea nini baada ya Koffi Annan kuona yanazidi kumshinda. Uliza uhuru wa Mozambique, Zimbabwe, Namibia, SA. Jamani katika masuala ya kitaifa kama haya, tuache siasa.
 
Dr.Slaa anaweza kuongea hivyo kwa sasa. Lakini hata Dr. Slaa angekuwa Rais wa nchi,maisha yake binafsi na mipaka ya nchi yake ikitishiwa,angeanza kwanza ku deal na wanaotishia mipaka ndipo angekuja kutatua ya ndani.

Ukiwa unagombana na mkeo/mumeo ndani,ukasikia watu wanataka kuvunja gate wavamie kwako,cha kwanza utaenda kupambana na wanaivunja gate lako ukisha wasambaratisha ndio utarudi ndani kupatana na mkeo/mumeo.

Sawa sawa.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wazee wa wilaya ya Karagwe walimtaka Kikwete kuacha choko choko zake na Kagame kwani hazina faida yoyote zaidi ya kuwaumiza wao pindi vita itakapotokea.

Katika barua waliomwandikia walisema hawajui walichotofautiana lakini vyovyote vile hakina masarahi kwa nchi. "Mwaka 1978 tulijitolea kupigana na ndugu na jamaa zetu walikufa wakipigania kuikomboa sehemu ya nchi yetu iliyokuwa inakaliwa na nduri Idd Amini. Mh rais leo tukikuuliza tuna faida gani na hizi chokochoko?"

Walisema wao waliifadhi wakimbizi wa Rwanda na wanajua athari za vita tokea hata wakati wa Amin hivyo hawako tayari kuona tena vita kwenye ardhi uao. Zaidi walisema hawaoni sababu ya rais Kikwete kumlazimisha Kagame kuongea na waasi maana wananchi wa Rwanda na rais wao ndiyo wanajua uzito wa suala hili.

Barua hiyo sijui kama ni busara kuiweka hapa maana ina mambo mengine hayahusiani na na hili. Lakini kwa ujumla wazee wanasema bif binafsi hazitakiwi kuingiza nchi vitani na wao ndiyo watakuwa wahanga maana wanaishi mpakani.
Hao wazee bilashaka watakua ni wanyarwanda. namaanishwa hao (wazee) ndio walee alio wafichua Mtikila
 
Kumekuwa na majibishano kwa muda sasa, majibishano ambayo ni matokeo ya ushauri uliosomwa na rais Kikwete, ushauri ambao hakuutoa binafsi, bali ni makubalioano ya Viongozi wa AU, waliokutana kujadili masuala ya amani na changamoto zake huko Addis Ababa, Ethipia.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo kama briefing kwa viongozi wa AU juu ya waliyokubaliana.
Tangu hapo kumeibuka mfululizo wa mashambulizi kutoka upande mmoja dhidi ya Rais Kikwete. Kwanza ieleweke kuwa alichokifanya rais Kikwete ni makubaliano ya viongozi wa mataifa hayo katika kikao kilichowakutanisha pamoja. Kumlaumu kwa kauli hiyo aliyoisoma ni kumuonea tu, wa kulaumiwa ni viongozi hao kwa umoja wao.

Tufanye kuwa ushauri ulitolewa na Rais Kikwete.
Hapa ndipo nilishangazwa na kauli iliyotolewa na Dr. Slaa.
Dr. Slaa alipinga ushauri uliotolewa na rais Kikwete na kuuita kuwa si wa busara (?)
na kauli yenyewe ni hii
Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi
.
Dr. Slaa anaweza kuwa na hoja katika maelezo yake, (hasa katika reference zake) lakini alikosea sana kuupinga ushauri ule, ni ukweli usiopingika kuwa Jamii haitaacha kumuangalia Dr. Slaa kwa historia yake, aliwahi kuwa Padri na anatambua nguvu ya msamaha pia nguvu ya upendo kwa mustakabali wa jamii za wanadamu(Kama kweli ana amini). Ushauri wake haukuwa mbaya, bali upinzani wake, ushauri wake ulitakiwa uwe ni nyongeza, ulitakiwa kuwa ushauri mbadala ikiwa ule wa rais Kikwete ungekuwa mgumu kutimizika. Badala yake yeye ameshauri njia moja tu, ambayo ni Kikwete kuwaita kwa lengo la kuwapatanisha (si ushauri mbaya).

Upinzani wa kupinga kila kitu hautatufikisha popote kama taifa, hatuwezi tukapinga kila kitu kama ambavyo hatuwezi kukubali kila kitu. Dr. Slaa anatakiwa aitambue nafasi yake katika jamii, na matarajio ya jamii juu yake hivyo ni wajibu wake kuandaa mazingira ambayo yatawaunganisha watu na kusimama kama taifa huko tuendapo, na ambayo hayatampa shida.
Ni vizuri kukosoa na kushauri, lakini mambo mengine tunaweza kuishia kuchangia kushauri tu.
Ni kweli kuwa siku za hivi karibuni, serikali imetuponyoka na sasa imekuwa serikali inayo operate kwa manufaa ya makundi fulani ya ndani na nje ya nchi, imekuwa ya kikatili sana kwa raia wake, haijali tena imetugawa na tumegawanyika. lakini hayo yasitufanye vipofu wa kuona na viziwi wa kusikia. Tuendelee kutambua mazuri na mabaya pia, Kama tunaonglea mapambano na mapinduzi za kifikra ni lazima akili zetu ziwe wazi na active, mioyo yetu pia isizongwe na hisia za chuki na kukata tamaa, bali matumaini na dhamira.
Matatizo ya Rwanda yatamalizwa kwa nguvu ya msamaha na Upendo baada ya pande hizo kukutana.
Kwa kumalizia, naomba Dr. Slaa atafute na kuangalia Film iitwayo Amish Grace.
 
Seen and digested, upo sahihi iwapo tu uliyo yasema kuhusu Dr slaa ni ya kweli, maana hakuna mahala nipofanikiwa kuthibitisha kwamba amepinga ushauri wa Kikwete kwa muuaji Kagame
 
Inawezekana dr. slaa aliongea haraka bila kuwaza matokeo ya matamshi yake.
Hiyo ya dr. slaa kuwa kiongozi wa dini siyo kifungo, na ndo maana akajitoa kwa kuwa aliona ni kugumu.

Nazidi kusimamia msimamo unaosema kuwa tuwaheshimu walioko madarakani kwa kuwa wamewekwa na Mungu mwenyewe.

copy: chama
 
Last edited by a moderator:
Binafsi sishangai maneneno hayo kutolewa na Slaa, sababu itambulike wazi huyo mzee (Slaa) haitakii mema nchi yetu. Tukiwa watu wazuri wakutunza kumbumbu hatuwezi sahau kauli aliyo ibwabwaja kua "Nchi haita tawalika" akimaanisha yukotayari kuona kwagharama yoyote Nchi haitawaliki, iwekwakulianzisha yeye na chamachake au kuwaunga mkono watu mfano wa PK.
 
Wapendwa wana JF, nimebahatika kutembelea nchi ya Rwanda kwa siku tatu kuanzia tarehe 2/8/2013- 5/8/2013. Nikiwa kwenye ziara yangu nilibahatika kufika miji ya Nyakarambi, Ruchira, Gituku, Kibungo, Kabarondo, Kayonza na Rwamagana.
Nikiwa huko nimeweza kujifunza kuwa wanyarwanda wanamchukia sana Kikwete lakini wanawapenda sana watanzania. Nilibahatika kuongea na watu tofauti wakiwemo raia wa kawaida, viongozi na wanajeshi.

Nilichogundua ni kwamba kila nyarwanda hata aliyeko kijijini anataarifa kuhusu mgogoro wa Kagame na kikwete kwani baada ya kujua mimi ni mtanzania walianza kurusha shutuma kwa Kikwete alivyo mjinga kuingilia masuala ya Rwanda na kujikomba Umoja wa mataifa bila kwanza kumshirikisha kagame mwenyewe au Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wa raia wanadai wanaipenda sana Tanzania na watanzania wote isipokuwa wanamchukia Kikwete kwa tabia ya kupenda kujipendekeza kwa mataifa ya magharibi tofauti na ilivyokuwa enzi za mwalimu. Wanasema Kikete hakuwa na haja ya kuyaongelea masuala ya Rwanda akiwa Ethiopia badala yake angetumia busara hizo kwanza kukaa na kagame akamshauru wakiwa wawil au angetumia jumuiya ya Affrika masharikia kutoa ushauri wake.

Kwa upande wa viongozi wa serikari niliobahatika kuongea nao wanadai kitendo alichokifanya kikwete akiwa Ethopia hakikuwa cha kiungwana kwani kule hakukuwa sehemu muafaka ya kuongelea jambo hilo na wanaongeza kuwa wanaimani kuwa hayo hayakuwa mawazo ya watanzania bali yalikuwa mawazo ya Kikwete binafsi na hawawezi kuwacghukia watanzania wote kwa sababu ya kikwete.

Tukiwa kwenye burudani tunapata kalinya nilibahatika kuongea na Mwanajeshi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mbalanga, ambaye pia hakuwa tofauti sana na raia pamoja na viongozi wa serikali. Yeye alisema Kikwete hawataki wanyarwanda na wanyarwanda hawamtaki kikwete lakini wanajua watanzania wanawapenda sana wanyarwandwa hivyo uhususiano baina ya watanzania na wanyarwanda hauwezi kuvunjika kwa mtazamo wa mtu mmoja, Ingawa kitu kilichonishtua ni pale aliposema tumajenga kwa kasi sana bandari yetu ya nchi kavu pale Rusumo kwa ajili ya kuweka vifaa vya kujilinda na kweli pale Rusumo upande wa Rwanda wanajenga bandari kubwa ya nchi kavu. Mwanajeshi huyo haukuishia hapo alisema pamoja na hayo Presdent ameshatwambia tukae tayari kwa lolote na tunajua udhaifu wa watanzania. Tunaweza kuwa ni rahisi kuwagawa na kutumia udhaifu huo kuwapiga.

Mwisho nilimalizia Benako kituo kodogo cha magari makubwa kilichoko kilometer 15 kutoka mpakani ambapo nilifanikiwa kuongea na nyarwanda wa ngara mwenye uraia wa Tanzania.
Mama huyo alisema baada ya agizo la kikwete la kuwataka wahamiaji wote haramu aidha warudi kwao au watumie taratibu za kupata uraia, serikali yake imetumia nafasi hiyo kuwanyanyasa na kuwatishia kwani hata kama mtu una uraia wa Tanzania ulioupata kihalali miaka zaidi ya ishirini iliyopita unaambiwa wewe ni mhamiaji halamu, Hivyo unalazimishwa kutoa rushwa vunginevyo unaorodheshwa kama mkimbizi au mhamiaji halamu.

Nawasilisha
Mkuu upuuzi huo warudishie walio kutuma (wanyarwanda wenzio)
 
duh..mjadala unakolea...

umeongea point ya ukweli...Katibu wangu mkuu DR WP Slaa ambaye ni mzazi na tegemeola taifa ana mgogoro mkubwa na wazandiki wa CCM....tunajua hata roho yake kimsingi kaiweka rehani kwa ajili ya tanzania mpya... kwani kama ni kitumbua cha CCM kweli kakitia mchanga......

therefore, msongo huu unaomkabili Dr Slaa nahisi umemfanya ateleze kauli na kureflect state of mind ya what is actualy happening at home......i think this was just a mere accident....

kwa hili mimi binafsi ninaomba tu nimuombee msamaha.......na pia kumwomba kuwa mara zote ni vema akumbuke kuwa yeye ni raisi mbadala wa tanzania..na pengine ndiye raisi ajaye..... machinery haitamwelewa asipokuwa makini kutofautisha levels na orientations za reactions...
 
matatizo ya kukariri kua, ukishakua mpinzani kila kitu unakipinga ndio haya...inanipa mashaka kuwa na kiongozi mwenye hulka za kidikteta, kiongozi ambaye hana msahama, wala asiyependa reconciliation ni hatari, Mungu mwenyewe anasamahe...ingawa tunamkosea kila siku...bahati mbaya Chadema kuwa na viongozi wenye hulka hatarishi kama hawa..
 
Mtaongea sana kuhusu suala hili kwa mapenzi yenu ya CCM na CHADEMA lakini ukweli utabaki kuwa alichosema Dr. Slaa ndiyo jibu. Nitafafanua kuhusu hilo: Huwezi kusuruhisha pande 2 zinazozozana au kupigana bila kuzikutanisha, kwanza unasikiliza madai ya kila upande ukiwa peke yako au ujumbe wako. Kila mmoja atatoa malalamiko yake na ukishapata hoja zao basi unawaita sehemu ambayo wewe utaona ni safe kwako na wao pia. Utasikiliza tena malalamiko yao wakiwa pamoja harafu utatoa usuluhishi, na siku zote usuluhishi ni kuwapatanisha ili waishi kwa amani na upendo kama mwanzo. Na baada ya kuwapatanisha na wao wakakubaliana na wewe basi utawaomba wapeane mikono kuonyesha kwamba wamekubaliana na busara zako, mtapiga picha za pamoja na kuanza maisha mapya. Hii inatokea hata kwenye level ya familia, majirani, vijiji nk.
Lakini leo nashangaa mtu ambaye mnapigana tena mmeshikana mashati anakuja mtu anakuambia kaeni naye mpatane? inawezekana kweli? Acheni unafiki, tufate kanuni na taratibu za kuishi.
 
Tutafanya makosa sana Wa TZ Kama Nchi tukimkabidhi huyu jamaa (Slaa) asie itakia mema Nchi hii. Yeye kwake upinzani nikupinga kila kitu.
 
Back
Top Bottom