Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

The crux of the matter here ni hii kitu inayoitwa HEKIMA.

mathalani, jirani yako akiwa ana ugomvi na mkewe. ukiambiwa kumshauri, wewe utafanyeje?

1. je, utasimama barabarani na kuanza kutangaza ushauri kwa jirani yako?

AU

2. utamfuata jirani yako nyumbani kwake (au hata kumwita kwako) na kumshauri?


Je ndugu yako akikuulia mke wako, watoto wako, mama yako na baba yako , alafu jirani yako akakushauri mkae na ndugu yako myamalize ! utakuwa mwenda wazimu kukubali ushauri huo
 
Mkuu Nguruvi, msome Mfamaji......

Kuna uwezekano Jk anatafuta vita ili aendelee kukaa ikulu?

I perfectly know what I mean. Kama JK angekuwa na busara hata chembe asinge bwabwaja huko Adis. Wanakutana kila mara EAC na njia nyingine za masasiliano zipo. Otherwise JK is a perpetrator of the whole unfounded saga. Sio kwamba JK hakumjibu. Alimjibu baada ya kumchokoza. WW vip huoni?

Hapo A: napaacha kama palivyo kwasababu panajitosheleza.

B: Kwa maneno mengine FJM anasema kauli za Paul kumdhuru Rais wa Tanzania na nchi kwa ujumla ni kubwa kuliko mambo mawili yaliyobaki i.e Ushauri na suala la Intarahamwe.

Rais wa nchi yoyote ni alama ya taifa. Sisi Watanzania tuna haki ya kumuongelea rais kwa madhaifu au mapungufu yake kwasababu ndio waajiri wake na si raia au kiongozi wa taifa jingine.
Tishio la kumdhuru Rais ni tishio la taifa na hilo tu linatuunganisha bila kujali itikadi zetu za kisiasa.

Dr.W.Slaa
alipaswa kuliona kama kiongozi kwanza na Kauli ya kwanza ilipaswa kulaani matishio ya Paulo dhidi ya viongozi (akiwemo yeye) na nchi . Hakulaani kauli za Paulo akaliona la JK, kuna tatizo!!

C: Hapa ndipo watu wengi ima wanapakwepa au hawajui kuwa ni sehemu muhimu sana ya mtafaruku huu.
Jk hakutoa kauli zile Washington au Abuja wakati PK akiwa hayupo,ameitoa kauli mbele ya PK na Museveni akiwepo na kuunga mkono. Paulo Kagame hakusema lolote.

Aliporudi Kigali akutuma mawaziri na wala si yeye kusema pamoja na kuwa alikuwa na nafasi hiyo.
Mawaziri wakaanza kuiongelea kwa ushabiki wa ajira bila kujua hata kilichosemwa katika mkutano.
Kagame akamalizia kwa kuita wanajeshi na baadaye kutoa kauli za vitisho

Na kuonyesha kuwa PK hakujua ajibu nini na kwanini na wapi, yeye na mawaziri wake walianza kuongelea barua ya Mtikila na kumhusisha JK bila kufuatilia au kujua Mtikila mi mtu wa aina gani.

Hoja ilipokosa mashiko wakaamua kuvamia diplomasia kwa njia ya kauli za zisizo na chembe ya ustaarabu.
Kwani PK angesema hakubali ushauri wa JK katika mkutano au kuita press conference kingeharibika nini?

Tukirudi kwa Dr Slaa, ni lazima ajue kuwa zipo domestic na international politics.
Wanachama na mashabiki wa chadema walisimamam kidete na kusema uwepo wa Mbowe katika hafla ya Togwa na Obama ulikuwa ni sehemu ya Utaifa, na kutetea kuwa mambo ya kitaifa ni lazima utaifa kwanza.

Leo nauliza je, hili la kutishiwa viongozi na nchi si suala la taifa? na je, Dr Salaa hakupaswa kusimama kidete na kauli za kutishiwa kwetu kama alivyosimama kidete na utaifa wa Mbowe katika Togwa na Obama.

Lakini pia lazima wanchama wa CDM na mashabiki wao waelewe kuwa CDM ni chama cha upinzani na ni mbadala wa serikali iliyopo madarakani kama wananchi wakiamua. CDM wanapaswa kujipanga na kuhakikisha kauli zao katika majukwaa ya kimataifa zinapimwa na kuchujwa vema.

Ni kwa vile CCM kumebaki vichwa wazi, kama kungekuwa na vichwa vizuri suala hili lingerudi katika domestic politics na kuwaumiza sana Chadema.

Hivi leo hii mtu wa Karagwe, Ngara na Kagera anayepata adha kutokana na ujambazi wa Wanyarwanda pamoja na tishio la Kagame na kumbu kumbu ya Idd Amin atajisikiaje akisikia kuna kiongozi anyesimama pamoja na PK dhidi ya taifa hili?

Leo mwanasiasa akienda na kufanya spinning kuwa Chadema inaunga mkono PK na Rwanda, nafasi ya CDM maeneo hayo ni ipi? Je, tutawaulaumu wananchi kutokana na mkanganyiko huu

Na mwisho, Watanzania! tunajua hatuna natural leader kama tuliokuwa nao.
Hawa waliopo ni wa kupika na kutengeneza, tuna wajibu wa kuwa ''grill na groom' kabla hawajaingia magogoni ili wakifika huko wawe wameiva tayari.

Hakuna sababu za kuoneana haya wala kuleta ushabiki wa Simba na Yanga katika masuala serious kama haya. Akikosea JK tunampa za uso akikosea Slaa tunampa za uso kwa manufaa ya Tanzania. Period

cc JokaKuu Jasusi @Dr Kitila Mkumbo
 
wewe si mtanzania ni wale watoto wa haramu wa kinyruanda mliofadhiliwa nchini kwetu
Siku 14 kurudi makwao,
basi atoe siku 14 kwa watanzania wanaoishi nje illegally kurudi Bongo
(hasa watoto wao hao vigogo waliopo Ulaya na US). JK ni mtu mbaya sana,
amechafua Tanganyika na sasa nje, after 2015 atakwenda wapi?
 
Manazi walioua Waisrael walisakwa na bado wanasakwa mmoja mmoja na kuangamizwa . Nterahamwe ni lazima wasakwe na kuangamizwa sio watu ni mijitu.
watu wanaoishi mikoa ya jirani na Rwanda walishuhudia ushetani uliofanywa na hawa watu.
Mh. Kagame yupo sahihi kabisa sio watu wa kukaa na kusema yaishe. Jamani tusicheze na maumuvu ya watu , wengi hawawezi kusamehe . Mbona na sisi sheria zetu ziko wazi , anayeua naye auawe
 
Rwanda na Uganda hawana kitisho chochote kwa Tanzania acheni kukuza haya mambo.Naamini kijeshi tupo vizuri zaidi kuliko hao majirani zetu.Na kwa taarifa yenu hakuna watu wenye misimamo mikali katika siasa za nje kama tulioko CHADEMA.Kagame asingethubutu kutoa matusi anayoyatoa kwa JK kama Slaa angekuwa Rais.Angeanzaje kwanza?Ili kwenye ukweli lazima tuseme Rais wetu amechemsha na hili halihusiani na Uzalendo kabisa.
Mark my word - jamaa hawa ni tishio kweli kweli katika ukanda wetu wa Africa Mashariki na kati, mimi ni mwenyeji wa mipakani mwa nchi hizi mbili najua ninacho zungumza hapa. Wewe umewahi kusikia wapi RAIS anamtishia maisha Rais mwenzake, is this normal? Watu wasio wajuwa jamaa hawa wanawachukulia kijuu juu, 'am telling you hawasemi kitu bila ya kukifanyia kazi - repeat hawana UTANI!! Leo naona kuna baadhi ya Watanzania wenzangu wanao leta itikadi za vyama wanasahau kabisa kuzungumzia USALAMA wa Taifa na Rais wetu wanafikili ni business as usual sio kweli, namuheshimu sana Dr.Slaa lakini katika hili simuhungi mkono amekosea sana akumbuke inapokuja suala la USALAMA wa TAIFA letu tunapashwa kuwa na mshikamano i.e tusahu tofauti za kitikadi kwa muda. Kama jamaa hawa wanaweza kuwavarisha wanajeshi nguo za kike na kuwapenyeza DRC ili waendeleze vurugu na mauuaji watashindwaje kuwavarisha wanajeshi/commandos wao nguo za janjaweed - AKILI KICHWANI MWAKO.
 
Slaa MNAFIKI sana, ndio maana hata goti lake hawezi kulikunja!!!

View attachment 105631
996882_559275840803081_1767920150_n.jpg

Mkuu hawa Vodacom si wangempa na yeye Track-suit na raba, maana wanaleta ubaguzi mpaka anaona anatengwa na hashirikishi kwa kila kitu yaani hata Vita tukichokozwa nao washirikishwe
 

Attachments

  • Jamii f 1.jpg
    Jamii f 1.jpg
    29.1 KB · Views: 62
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

"Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo," alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE

Hapo kwenye rangi ya blue ninapaunga mkono sana!!! Mh. Rais Jakaya Kikwete ni mahiri wa kupatanisha nakumbuka vizuri alipowapatanisha ghafla Kibaki na Odinga, wakaishia kushikana mikono. Tatizo lililopo kati ya Kagame na JK ni Kagame mwenyewe. Kwanini kama ni ushauri tu mtu ukurupuke na kutoa matusi. Ikiwa JK angekuwa alitoa kauli hizo akiwa analengo baya wala nisingetoa maoni haya ningetoa toa maoni tofauti na haya kwa kumkosoa Mh Rais.

Nilishangaa sana kauli za Kagame alizozitoa mbele ya vijana "Makuruta" akiwa anatamba utadhani anatangaza vita na "kijinchi" Wakati alikuwa anatangaza vita na Baba yake Mzazi. Kama Kagame angeitisha mkutano wa Wazee wa Kinyarwanda nigemuona ni mtu mwenye busara sana kwani katika kauli zake bila shaka angepata mawazo ya Wazee hao. Kawakusanya Makuruta akawa anatamba akitembea toka upande huu kwenda upande mwingine huku akimtusi Rais Halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kitendo cha Mh Rais kuwafutia vibali wale wote wanaoishi kule Kagera na sehemu nyinginezo isichukuliwe ni kauli iliyokuja baada ya sakata hili hapana bali ni kwasababu ya matukio ya ujambazi wa muda mrefu. Namuunga mkono Mh Rais tena naongezea kusema tangazo hili lilichelewa sana. Kwa kusisitiza ningemuomba Mh Rais atangaze rasmi jukumu la mabalozi wetu wa nyumba kumi la kila balozi kuwa na orodha za wakazi wake kila balozi ili tuwadhibiti hawa wanaokuja bila mapembe toka kwao na kuja kuyaoteshea katika ardhi ya Tanzania. """Tanzania bila wahamiaji haramu, inawezekana!!!"""
 
Jk anatuabisha tu. Rwanda is just too a small country to argue with. Wote tunaoneka wehu kama wao. what is the difference ?
ebu tupe wazo lako?how we can argue this stupid thing with rwanda
 
mbulula wewe nani kakwambia nautaka udc? Natetea nchi yangu toka kwa mafisi kama nyie ambao mmekosa kabisa uzalendo na kutumiwa na maharamia wanaoisaliti nchi kwa kulipwa ujira mdogo sana. Mmemwaga hapa hamna cha maana mnachoandika zaidi ya upuuzi katika kutetea maharamia na magaidi.
Mr. Man inaonyesha unautaka tu kwani kutokana na IQ yako sioni kama una mahali pengine pakwenda zaida ya hapo tu. Au ukubali kubakia Lumumba.
 
wewe si mtanzania ni wale watoto wa haramu wa kinyruanda mliofadhiliwa nchini kwetu
Ukiona mtu mzima anatumia lugha ya maudhi kuwasilisha hoja, amefilisika kimawazo. Mkimbizi anajulikana kwa Kiswahili chake kibaya
 
ni kinyume cha mambo kwa slaa kumpinga jk kwanza hamna sababu ya kupigana zingine ni tabia mbaya tu,
 

Hapo kwenye rangi ya blue ninapaunga mkono sana!!! Mh. Rais Jakaya Kikwete ni mahiri wa kupatanisha nakumbuka vizuri alipowapatanisha ghafla Kibaki na Odinga, wakaishia kushikana mikono. Tatizo lililopo kati ya Kagame na JK ni Kagame mwenyewe. Kwanini kama ni ushauri tu mtu ukurupuke na kutoa matusi. Ikiwa JK angekuwa alitoa kauli hizo akiwa analengo baya wala nisingetoa maoni haya ningetoa toa maoni tofauti na haya kwa kumkosoa Mh Rais.

Nilishangaa sana kauli za Kagame alizozitoa mbele ya vijana "Makuruta" akiwa anatamba utadhani anatangaza vita na "kijinchi" Wakati alikuwa anatangaza vita na Baba yake Mzazi. Kama Kagame angeitisha mkutano wa Wazee wa Kinyarwanda nigemuona ni mtu mwenye busara sana kwani katika kauli zake bila shaka angepata mawazo ya Wazee hao. Kawakusanya Makuruta akawa anatamba akitembea toka upande huu kwenda upande mwingine huku akimtusi Rais Halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kitendo cha Mh Rais kuwafutia vibali wale wote wanaoishi kule Kagera na sehemu nyinginezo isichukuliwe ni kauli iliyokuja baada ya sakata hili hapana bali ni kwasababu ya matukio ya ujambazi wa muda mrefu. Namuunga mkono Mh Rais tena naongezea kusema tangazo hili lilichelewa sana. Kwa kusisitiza ningemuomba Mh Rais atangaze rasmi jukumu la mabalozi wetu wa nyumba kumi la kila balozi kuwa na orodha za wakazi wake kila balozi ili tuwadhibiti hawa wanaokuja bila mapembe toka kwao na kuja kuyaoteshea katika ardhi ya Tanzania. """Tanzania bila wahamiaji haramu, inawezekana!!!"""

unaunga mkono hata mambo ya hovyo naanza kuamini kuwa yawezekana mzee kweli ameanza kuchoka jk siyo mpatanishi wa rwanda,awaite yeye kama nani kitu amabacho jk alifanya nikutoa maoni yake kwa mada ambayo ilikuwa mbele yake ambayo kila mjumbe alikuwa na uhuru wa kutoa maoni yake kama alivyofanya jk.
 
Dr. Slaa sio kosa lake. Uwezo wake wa kufikiri umekuwa wa kiwango cha Josephine Mushumbusi.

Anasema Kikwete haongei na wapinzani wakati Slaa ameonekana mara kadhaa Ikulu akinywa juice. Sasa sijui walikuwa wanakunywa juice kimyakimya!!!

View attachment 105628

Dr Slaa namheshimu sana, ila hii tabia ya kukosoa kila jambo sikubaliani nayo. Wakati tafakari, unashusha hadhi tuliyokupa watanzania wengi.. Wewe ni raisi wa wengi nchi hii. Kikwete was right.
 
Kwa alichoshauri Kikwete kiko wazi na kinahitimishwa na kufafanuliwa vizuri na yeye mwenyewe katika Hotuba aliyoitoa mwisho wa mwezi uliopita,Kiukweli kabisa Mh Rais katika Hutuba yake ameongea mambo mengi sana ya msingi na kwa HUTUBA yake hiyo nzuri,mimi nadhani ilitosha kuondoa hali ya sintofahamu na kujibu maswali mengi ya kwanini Kagame ana mtukana!sasa Utagundua kitu kimoja tu!kwamba Kagame ni mkaidi na hata Kikwete angetumia Lugha za malaika bado Kagame angeonyesha dharau tu,na Kwa alichofanya Mh Kikwete naamini alikuwa sawa Kabisa..Kwa Slaa anachojaribu kufanya maarifa tu..kwani siasa ni maarifa inategemea uta m-catch on guard wapi mpinzani wako then you jump on it.
 
Mr. Man inaonyesha unautaka tu kwani kutokana na IQ yako sioni kama una mahali pengine pakwenda zaida ya hapo tu. Au ukubali kubakia Lumumba.

Tutapambana na nyie mamluki mliomwagwa hapa kwa fujo na kila siku mnachonga IDs chungu nzima ili kuvuruga mijadala muhimu. Miaka ya nyuma kulipokuwa na wanachama wachache kulikuwa na kuheshimiana sana hata kama watu hawakubaliani, lakini tangu nyie mamluki wa buku 7 kuja hapa uwepo wenu umechangia sana kushusha viwango vya mijadala maana mkiona mjadala muhimu tu dhidi ya Serikali au CCM basi mtashuka hapa na IDs zenu 50 50 ili kuandika kejeli, kashfa na hata matusi ili tu kuvuruga mijadala kiasi ambacho baadhi ya wanachama wasiku nyingi kutotaka tena kuingia kuchangia lolote lile. Kwa taarifa yenu tumechoshwa na vitendo vyenu vya kukubali kutumika kama mamluki kwa ujira mdogo sana ili kuvuruga majadiliano muhimu hapa. Serikali na vyombo vyake vya dola itunyanyase na nyinyi mamluki hapa JF mtunyanyase na kuvuruga mijadala. Kama hamna cha maana cha kuandika zaidi ya kashfa, matusi na kejeli basi kaeni kimya vinginevyo tutapambana nanyi ili kuhakikisha JF inaendelea kuwa na hadhi na heshima yake kama miaka ya nyuma. Nyie wote wote akina Ritz, chama, scramble, Faiza Foxy, Bukyanandi, wabuyaga, Hamida, Utaifa kwanza, Zemarcopolo, lizaboni, leomimi na mambulula wengine wa buku 7 mnaochonga IDs mpya kutwa kucha ni sumu kali sana ya future ya JF. Kama hamuwezi kuandika cha maana zaidi ya pumba zenu basi tafuteni sehemu nyingine ya kuandika pumba zenu hapa tumezichoka zinatuharibia ukumbi wetu. Inawezekana kabisa kuwa na wanachama hata milioni na bado watu kuandika bila kashfa, kejeli au matusi. Habari ndiyo hiyo na kwa taarifa yako si kila mtu anataka vyeo vya kubabatizwa kama unavyodhani.
 
The crux of the matter here ni hii kitu inayoitwa HEKIMA.

mathalani, jirani yako akiwa ana ugomvi na mkewe. ukiambiwa kumshauri, wewe utafanyeje?

1. je, utasimama barabarani na kuanza kutangaza ushauri kwa jirani yako?

AU

2. utamfuata jirani yako nyumbani kwake (au hata kumwita kwako) na kumshauri?


Una akili sana, ukweli Kikwete jamaa hajakosea kumwita kimbele front "fore bee" unajua mwenye busara angemwita jamaa na kumshauri kama option ya pili hapo juu! Alimkosea sana jamaa, hata hivyo walimtaka aombe msamaha kama aliteleza akagoma sasa busara yake iko wapi mnatetea bila kuona ukweli!!!!!!!
Japo sasa kwa sasa lilipo fika hata kama kakosea tunapaswa kuungana kuilinda nchi yetu sote hata mimi niko tiari kwenda vitani kwa makosa ya JK kuilinda nchi si kumlinda JK la hasha nchi yangu kwanza, Kagame pia si mstaarabu alipaswa kumuelimisha mwenzie kama hakuona makosa yake ili kuomba msamaha. Kingine hawa wakubwa huwa wanadanganywa sana kwani hakuna mshauri anaye wambia ukweli kuwa hapa unakosea husuport mawazo yao bila kujali kakosea au yuko sahihi!!!!!!!!!
 
Mkuu Nguruvi, msome Mfamaji......
Mkuu Sikonge , kwanza niheshimu mawazo na mtazamowa wa Mfamaji kuhusu sauala hili.

Pili, sikubaliani naye kuwa JK anatafuta njia za kuanza vita ili abaki madarakani.
Endapo angependa iwe hivyo mbona Joyce B alishaingia kwenye ulingo?
Ukizingatia tuna mpaka bado ni rahisi sana kulianzisha na Rwanda pengine zaidi ya nchi nyingine.

Lakini pia kwa hali ilivyo ni wazi JK keshachoka kukaa hapo Ikulu na angependa mwingine achukue jukumu la kuendeleza umasikini huu ambao kwakwe ni failure kubwa sana.

Unaweza kuliona taifa lilivyo kama ushahidi wa kukata tamaa na imebaki bora liende.
Nieleze kipi kinampa faraja kukaa magogoni? Tension kubwa ya kila jambo unalolifikiri , kwa mtazamo wa kuwa wewe ndiye yeye.

Tatu, kuhusu kuwasiliana na PK kwa njia nyingine, nadhani katika EAC limefanyika at least kwa ushahidi tulio nao tena kuanzia Mkapa n.k. Moja kati ya mambo yaliyomchagiza PK kusema makao makuu EAC yahamie Nairobi ilikuwa ni kutaka kuiadhibu Tanzania kwa misimamo yake juu ya waasi a.k.a wanyarwanda ndani ya DRC. Utakumbuka neno great lakes region limetokana na vikao vya EAC kuhusu DRC. Kwa msimamo wa Paulo akisaidiwa na Kaguta ushauri haukukubalika the least to say na suala hilo likahamia rasmi SADC.

Kikao cha Nairobi kati ya Koffi Annan, Obasanjo, Mkapa na PK kilimwambia amkamate Laurent Nukunda kwasababu alijua yuko wapi . PK akafanya hivyo haraka sana. Hii maana yake alikuwa anashauriwa.

Suala lilipotua SADC PK alipinga sana uwepo wa majeshi akijua Tanzania itapeleka askari.
PK alikuwa na wajibu wa kuongea na mwenzake kuhusu hilo na si wajibu wa JK kuongea naye tu.

PK ni nani wa kubembelezwa na si kuambiwa?Yeye amefanya jitihada gani za ku address suala la DRC au kuwasiliana na wenzake ndani ya EAC zaidi ya kukataa jitihada za kimataifa?
Nini ni solution ya PK kuhusu DRC ambapo yeye ni sehemu ya tatizo?

Je, kuuunga mkono kura ya maoni ya Kivu kujitoa DRC ndiyo solution ya Kagame? Tumesahau kuwa Wanyarwanda waliopo Kagera wanaweza kuanza katatizo ili nao waungwe mkono kujitenga kama Kivu. Tukubali tu na kumuonea haya katika hatari inayoonekana wazi.

Ni nini solution ya PK kuhusu DRC? naomba nifahamishwe

Suala la Rwanda si siri, mataifa yanajua chanzo na nani yupo nyuma ya ghasia hizo. Kuliongea Adis Ababa sioni tatizo tena wakiwepo viongozi wa EAC. Museveni aliunga mkono kauli ya JK, je hakuona umuhimu wa kuliongea EAC?

Paulo angekuwa na busara angemwambia JK kuhusu wapi waliongelee au kufanya approach ya kumsihi mwenzake njia bora za kuwasiliana kama zilikuwepo ingawa naami zilishakwisha.

Bado PK angeweza kuliongelea kwa spirit ya EAC badala ya matusi na vitisho.
Labda niambieni katika suala hili ni sehemu gani nzuri ya PK aliyoifanya? (the best part of PK)
 
Last edited by a moderator:
Je ndugu yako akikuulia mke wako, watoto wako, mama yako na baba yako , alafu jirani yako akakushauri mkae na ndugu yako myamalize ! utakuwa mwenda wazimu kukubali ushauri huo

kukubali au kukataa ushauri siyo hoja niliyoi-raise mimi.
ushauri hata ukiwa mzuri kiasi gani, ukitolewa ambavyo sivyo lazima kuwe na backlash.

tatizo langu liko kwenye approach ya JK (sina tatizo na nia yake) kwenye hii issue ya Kagame. ilihitaji ka-HEKIMA kadogo tu.

JK akubali tu kuwa ali-goof kwenye approach, licha ya nia nzuri iliyomo ndani ya ushauri wake!
 
Hoja ya Dr. Slaa ilikua kwamba Nchi haiwezi kuwa dragged vitani kwa sababu ya kauli ya Kikwete na vile vile akashsuri Kikwete aanze kwanza kukaa na wapinzani wake.
Boss, kwani sisi tuna waasi? System tulizonazo inclusion iko automatic, tunga Bunge! Wapinzani na chama tawala wanajadiliana. Tuna taasisi ile ya vyama vienye wabunge bungeni inayoongozwa na Mh. Mbatia kote huko vyama vyote vinashiriki vinavyotaka.

Tuna majukwaa ya kisiasa ambapo kila mtu au chama viko huru kuongea lolote?


Tuko kwenye mchakato wa Katiba vyama vyote vinashiriki na CDM ifika mahali ikaenda ikulu...

Swali: Mnamtuhumu Kikwete kwamba haongei au hashirikishi wapinzani, niambieni mnatakiwa kufanyiwa nini?
 
Back
Top Bottom