Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

naona undergraduate wanapambana kuhusu sheria zao huku nchi ikiendelea kupoteza rasilimali kutokana na mikataba mibovu . ziko wapi elimu zenu mnapozitumia kuzuia upotevu wa rasilimali zetu?
 
Ukisoma michango iliyo humu utajua kwanini Polisi waliuza Taarifa kwa RA na utajua hofu aliyonayo RA na Watawala walionyuma yake hasa Kikwete; inaonekana wanaangaika sana, walichofanya ni kutangaza hiyo taarifa ili wapate muda wakujisafisha haraka naona hata humu JF kuna-vijana wake sijui wanalipwa nini au ni uwezo mdogo wa kufikiri?!

Chakufanya Mwakembe atoe hizi habari Ubalozi wa America na Saudia maana polisi inaonekana wamekwisha nunuliwa, inatakiwa shinikizo la kimataifa na pia ikiwezekana ajiuzuru hiyo kazi, maana watamuua kirahisi akiwa katika cheo hicho kuliko akiwa Raia ikiwezekana aondoke apate hifadhi nje ya nchni.

Yule mama mwenye kifafa inaonekana aliropoka mambo waliyoongea kwenye vikao vyao vya Ushirikina, aliposema CDM wanaletewa fedha kutoka nje ya nchni.

CDM pia nilazima hili swala la kuambiwa ni wa dini sasa walifikishe kwenye meza za Kimataifa kwasababu Serikali ndio wanaliongea wasilipuuze hata kidogo wana haki ya kushtaki UN kuwa CCM inatumia udini kuvuruga kuuwa vyama vya upinzani ushahidi tosha ni maneno yao Maneno ya Kiongozi wa Serikali na Chama tawala ni maneno ya Serikali na Chama chake.

Watanzani huu ndio wakati mgumu sana ikibidi tukubali kufa kwa ajili ya Taifa letu, maana hatuwezi kutawaliwa na hawa wezi tukiwa kimia.
 
profile yako hapa JF inanitatiza hata kutoa comment yangu:
venance aidan
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
  • email.png
    Send Email
Join Date : 19th February 2011
Posts : 2
Thanks0Thanked 0 Times in 0 Posts

Rep Power : 0

.
Kweli mkuu huyu ni TISS aliyejiunga kwa kazi rasmi ya kupropagate madai ya Mwakyembe.
Halafu ukichunguza hawa watu, mkulu, RA, IGP alieyeachilia hii siri kwenye gazeti la RA, sheikh yahya wote hawa ni wale waleee....!!!
Tutafika kweli??? mungu ibariki Tanzania.
.
 
Mimi ntamwamini akijiunga CHADEMA! Anangangania nini CCM?
 
Insu hapa sio uislamu,hiyo imetumiwa tu km propaganda ya kuwashawishi wale wasomali,insu ni mapambano ya kisiasa ndan ya ccm na mtandao wa kugombea urais 2015,watu wote ambao wametajwa hapo wanatakiwa kuuwawa ni tishio kwa nafasi ya mafisad kuchukua nch 2015,huu mtandao umeona lazima 2wapoteze watu wote wanaoonekana kuwa na ushawish,ndio maana ktk hiyo list dr slaa naye yupo,yaan wanajua km slaa atakuwa 015 hata wakipita ndani ya ccm bas slaa atawamwaga ndio maana wametengeneza mtandao wa kuwaangamiza wote.ukichek hata membe anahofiwa kugombea urais na hayupo kwenye mtandao wao ndio maana wanataka kummaliza.na kunasababu ya mashambuliz haya kuanzia songea kwa Nchimbi emanuel mbunge wa jimbo hilo,huyu jamaa yuko kwenye mtandao wa akina Rostam aziz,lowasa na jk,na jana kuna m2 muhimu nilikuwa naongea naye akaniambia jamaa wakiona wameshindwa kujisafisha bas watamuweka bwana Nchimbi et ndio awe mgomea urais kwa maslahi ya mafisad 2015.
<br />
<br />
Ndugu yangu una haki ya kuongea kila kitu lakini huna haki ya kumtuhumu mtu kirahisi hivi,nchimbi ni mbunge wa songea lakini ana kaa dar na toka uchaguzi umekwisha kaenda songea kwa mara ya kwanza last week.ongeeni kwa kutenda haki na si kubuni.
 
Huyu ndio striker wa ccm aliyesimamia mafisadi papa kubigwa chini, ni shujaa wetu wananchi wa tz. Pale shujaa huyu anapokuwa na wasiwasi basi ujue panatisha, wananchi tuwe macho na kumpa ushirikiano; kwani hapa pia inaonekana usalama wa nchi nao ni mdogo!

Kwa uelewa wangu mdogo,hizi taarifa ni za siri; imekuaje gazeti la rosti liziweke hazarani? Au ndio anatuonyesha ukaribu wake na dola? Tuwe makini jamani, hivi vitu tujiulize kwa kina na sio vya kupuuza! Kwani leo ni dr.mwakyembe, na kesho ni wewe..utakimbilia wapi?
 
tumejenga taifa la watu wazushi. Daktari wa phd anazusha. Alizusha mambo mengi akiwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge na uzushi wake unatugharimu hadi leo. Akatuaminisha kwamba richmond na dowans ni moja na kwamba zote zina mikono ya ra na el. Leo hii haya yote yamethibitika kuwa ni uongo na anafanya hivi ili kujiepusha na kitanzi cha uzushi wake.

Ni bahati tu kwamba watanzania ni wavivu wa kukumbuka, tumeshasahau na bado tunamuona mwakyembe shujaa. Mtu huyo huyo kwa sababu ya uzushi wake huo aliposikia tanesco wanataka kuinunua mitambo ya dowans akafanya press conference na kuliambia taifa ni bora nchi iwe gizani kuliko kuinunua mitambo hiyo, sasa hivi tuko gizani na kazi iliyofanywa na kamati yake imeligharimu taifa karibu shilingi bilioni 100, mitambo ipo haiwashwi kisa ni uchochezi dhidi ya nishati ya umeme uliojengwa na mwakyembe na wahuni wenzake.

Mzushi huyu akaja tena na uongo mwingine alipopata ajali ambayo hakuna shaka ilitokana na uzembe wa dereva wake, akadai kulikuwa na lori lililokuwa likitaka kuwagonga na dereva wake alipokwepa ndipo gari likaacha njia na yeye akapata ajali. Uchunguzi wa polisi ulipofanyika ikabainika kwamba wakati ajali ikitokea alikuwa amelala na wala hakuliona lori alilokuwa akilisema...hakika huyu ana phd ya uzushi.

Sasa kazusha jipya eti anataka kuuawa na akaandika barua kutoa ushahidi wa kutunga wa kuunga unga mambo na kuwataja watu na namba za magari mengi akijifanya ana mtandao unaompa taarifa za kila kinachotokea. Ana bahati tu kwamba tuna jeshi la polisi la wasanii ambalo linashindwa kumbana atoe ushahidi wa kina wa maelezo yake ambayo hakuna shaka yatathibitisha kuwa ni ya uzushi.

Anafanya hivi lili el na ra waonekane ni wauaji...ajenda yake ile ile ya kuwazushia na kuwachafua wengine kwa malengo machafu ambayo ufadhili wake unatambulika kuwa ni wa wahuni wachache walio ndani ya idara moja nyeti. Ni aibu kuwa na naibu waziri tena mwenye phd wa kiwango duni kama mwakyembe.

Uzushi wake umelifanya taifa kupiga maktaimu na kujadili hoja moja kwa miaka minne sasa, uzushi wake umeliingiza taifa gizani na sasa anatengeneza uzushi mwingine unaoweza kuligharimu jeshi la polisi, idara ya usalama wa taifa, serikali, chama chake na watanzania kwa ujumla. Mwakyembe ni mtu hatari, ni mtu wa kuogopwa kama ukoma. Huyu mtu ana pepo baya, anapaswa kuangaliwa na kuchungwa sana

wewe kenge kwelikweli
 
<br />
<br />
Ndugu yangu una haki ya kuongea kila kitu lakini huna haki ya kumtuhumu mtu kirahisi hivi,nchimbi ni mbunge wa songea lakini ana kaa dar na toka uchaguzi umekwisha kaenda songea kwa mara ya kwanza last week.ongeeni kwa kutenda haki na si kubuni.

Duh,naona kama hau-sync na habari nzima vile? Rejea usome btn lines..
Anyway,kumbe jamaa ndio juzi tu kaenda songea tokea 2010; eh basi famfa,hatufai
 
Mhhhhhhhhh ....Maoni mengine bwana, naona Rostam tayari amechomeka watu wake humu mtandaoni. Wanatoa maoni ukiyasoma utathani wanachangia tu huja kumbe wanalipwa !! Tutakapo wagundua, Dawa yenu ni kifo tu !!


Umeona eeh! Watu wako kwenye payroll ya ra humu,wanaandika vitu haviclick kichwani kabisa! Ila trust me, watachoka tu; people's power bwana ni mwisho wa yote
 
Namshangaa huyu dr wa sheria kuogopa uchawi,binafsi siamini kama kuna uchawi,sasa msomi wa kiwango cha mwakyembe kutishwa na uchawi,ni aibu,au pengine anajitafutia umaarufu wa kisiasa,,

Jamani ukiangalia vizuri,hii taarifa imeletwa hapa kupitia gazeti la fisadi,kwaio vipaumbele vya habari vimeenda kwenye swala la ushirikina ili msimuelewe dr kama kusudio lao.
Tungejaribu kupata barua halisi aliyoandika dr tuone ukweli wa mambo!

Tusikurupuke jamani, phd huipati ukiwa bingwa wa kukurupuka;huyu ni analyst wa mambo. Sio uDr wa heshima huu. Tafadhali
 
Hi story inashtua sana!!!! Ila nadhani ingekuwa tamu sana kama angemuacha sheikh Y**** atoe 'utabiri' wake wa kupika kwanza.....Then amshushue kwa kutumia evidence......

Hatutafuti evidence kwenye kwenye uhai wa mtu Mheshimiwa!,
 
Tujiulize kama taifa lipo salama kwa kutegemea wanausalama wanaotegemea utabiri na ushirikina kama habari hizi zina ukweli!
Haya yote ni matokeo ya upuuzi na ujinga wa watawala kutegemea nguvu za giza katika zama za sayansi na teknolojia.
Kuna umuhimu wa raia wema kuwasaidia polisi kupeleleza nyendo za wanaodaiwa kuwa kwenye tuhuma hizi, pamoja na kuweka hadharani nyendo zao kama ushahidi kwa wananchi kwa ujumla.
 
Waliosema hivyo kama ni kweli nadhani watakuwa wale lawyers voda fasta ambao hadi sasa ni aibu kwa the legal fraternity.Wakifungua mdomo huwa wanatema upupu na pumba.Wakiandika ndio usiseme maana ni aibu ya kudumu!



lawyers voda fasta ni wapi na inakuaje wawe aibu kwa the llegal fraternity?
 
Mwakyembe anawajua wazi wabaya wake. Anajua wazi kabisa kuwa waasisi wa huu mpango ni baadhi ya viongozi na wananchama wa CCM. Sasa kwa nini bado anang'ang'ania kuwa ndani ya CCM? CCM isn't your mother, get out of it and move on....damn it.
 
Lisemwalo lipo jamani, tukumbuke lile jaribio la kumuua kule Iringa, huyu jamaa bado anawindwa
 
Back
Top Bottom